Katiba ya CCM na Vyombo vya Dola

Katiba ya CCM na Vyombo vya Dola

Hata hao Tiss wakijitenga na ccm bado sana wapinzani kupewa nchi hii siyo ya majaribio wewe watu gani hawaeleweki wanasimamia nini ili mradi tu kuenenda na matukio
kujaribu ni Maendeleo kujaribu ni sayansi, Huwezi kupata kitu sahihi bila kujaribu kwanza, acha umbumbu.
 
Daaaa....kudos mkuu, inekuwa Mzee wa facts &data. Mwenye kushindwa kuelewa itabidi tumpime malaria.
Wapuuzi! Mtu keshanza kutukana! Ukimuuliza TISS ni nini hajui....

Kazi za TISS hajui ...hajui inafanyaje kazi zake...

Afu hapo hapo wanataka nchi...?

Ipo kazi sana...!
 
Ukweli ccm amejiunganisha na hizo taasisi za ulinzi na usalama kiasi ambacho wanazitumia kisiasa pia hii ni hoja ya msingi kuzingatia.
Huenda taasisi yetu tiss ni imara na haiyumbishwi ndio maana tuko salama, lakini muundo wake ni wa chama kimoja na mfano ni pale mkuu wa mkoa kama bashite anapokuwa m/kiti wa ulinzi na usalama wa mkoa wakati huo huo ni mjumbe wa ccm anapokea maagizo toka idodomia au Lumumba b7.
 
Ungejua unyeti na umuhimu wa hao mabwana wa mstari , hakika usingekuja kubwabwaja maneno mbofu mbofu hapa jamvini namna hiyo.

Kukaa kwako , kulala kwako, kusatehe kwako, kujikuna kwako, kubarizi kwako, kusoma kwako, kuuza kwako genge, kuingia kwako JF muda wowote , kuangalia kwako taarifa ya habari saa 2 usiku, kwenda kwako msibani, harusini, n.k koooteeeee huko kunafanikishwa na kazi iliyotukuka ya hao mabwana either direct or indirect , either in a visible or invisible manner. Siku ukiwakosa wazalendo kama hawa hakika utalia na kusaga meno.

Ila kwasababu Watanzania ni watu wa style ya kinyonga , leo hii tutawaona kama hawafahi ila siku wakiingia hao wengine mnao dhani watakuja kuwaletea maziwa , asali na siagi. ndipo mtajuuuuta kukutwa na bwana pepsi na kubaki kusema " Tungejua......" .

Asiye sikia la mkuu .
Yote mema unayoona wanafanya ni wajibu wao, hawafanyi kwa hisani. Hao ni waajiriwa Sawa na watumishi wengine wa umma, wanalipwa na kuishi kwa gharama za wananchi kupitia kodi wanazolipa, lasilimali , na dhamana mbalimbali za nchi. Hawa si watumwa wa chama chochote cha siasa, wanakiuka viapo vyao.

Tanzania hii yenye watu zaidi ya milioni 45 ni aibu chombo mhimu kama hiki kutumikia/kuegemea chama chenye wanachama wasiofika ha milioni 8. Tunajua wrote kuwa was Tanzania karibu 75% si wanachama wa vyama vya siasa. Hao CCM wanao lindwa na TISS ni kama 17.8% tu ya wa Tanzania wote.

Watu wa msimamo wako wa ku specialize watumishi wa umma ndio mnasababisha baadhi yao wajione Miungu watu
 
Wapuuzi! Mtu keshanza kutukana! Ukimuuliza TISS ni nini hajui....

Kazi za TISS hajui ...hajui inafanyaje kazi zake...

Afu hapo hapo wanataka nchi...?

Ipo kazi sana...!
Kazi za TISS ni kutengeneza tension za hovyo ktk jamii zinazoibeba CCM?
Kazi za TISS ni kuilinda CCM isiondoke madarakani?
Kazi za TISS ni kuwakandamiza upinzani kwa maelekezo ya CCM?
 
Hata hao Tiss wakijitenga na ccm bado sana wapinzani kupewa nchi hii siyo ya majaribio wewe watu gani hawaeleweki wanasimamia nini ili mradi tu kuenenda na matukio
Ssa si mtenganishe na muweke tume huru..... afu mnavyosema BADO KUPEWA NCHI kwani according to NEC nani huwa anampa ccm nchi?? si wananchi?? ssa wananchi kma waliwapa ukawa kura mamilion kipi kinakufanya usiamini ukawa hawawezi ingia ikulu??

Dah such comments zinakera kweli.....
 
Tukubaliane kitu kimoja, upinzani mmeshudwa kuwashawishi TISS, Jeshi, Polisi hata umaa kwa ujumla kama mko tayari kubeba mzigo wa Tanzania, hili sio jambo lililo fichika. TISS ina majukumu mengi, moja kati ya majukumu yao, ni kulinda ustawi wa hii nchi. Leo hii nchi ya amani na utulivu, ichukuliwe na watu wasiojielewa mwisho wa siku hakuna Tanzania wala amani. Jipangeni kwanza ndio muaminiwe.
kwahiyo TISS wanaona ni sawa nchi iongozwe na majizi ya richmond,escrow,epa,meremeta,deepgreen eti??? tembo malaki wameuawa ndio TISS wanaona ni bora kuliko ukawa??? duuh nchi maskini mwaka wa 50 huu bado umeme maji makazi kilimo elimu afya ni shida ndio unadai TISS wanawataka hao??

shida ni katiba mkuu siku TISS wakitibitishwa na independent body ili wawe free from political influence ndio mwisho wa ccm

ila msitudanganye eti polisi hawashawishiki wakati hujiulizi kura milion 6 (NEC) hakuna hata familia ya mwanajeshi hta mmoja iliowapa kura ukawa???
muhim wekeni tume huru na badilini katiba CCM inatoka mapema sana
 
Kazi za TISS ni kutengeneza tension za hovyo ktk jamii zinazoibeba CCM?
Kazi za TISS ni kuilinda CCM isiondoke madarakani?
Kazi za TISS ni kuwakandamiza upinzani kwa maelekezo ya CCM?
Sawa mkuu!...
 
Sasa kama huko ukawa kuna watu kama wema ambao ndio candidates wa uwaziri nani anataka nchi iingie shimoni! Mkae mkijua kuwa post za Instagram sio sawa na kuendesha nchi.
duuh kwahyo sepetu wa chadema ndio TISS hawamsupport ila alipokuwa anaendesha kampeni za mama samia 2015 TISS walimsupport???? duuuh ndio maana watz wanawadharau ccm mmezidi undumilakuwili
 
Ccm ni chama kikongwe kinamuda mrefu katika utawala. Kipo kila kata kitongoji vijijini na mijini. Vyama vya upinzani venyewe viongozi wao wametokana na Ccm. Muundo wa serikali ya nchi umetokana na Ccm.

Upinzani wanahitaji rasmali ya watu na uchumi kuifikia Ccm ndio maana Nccr ilivuma sasa almost hakipo wakaja Cuf nao ndio hivyo tena. Sasa Chadema na wao bado wana tatizo kubwa la uchumi na ubunifu. Ndio maana upinzani upo zaidi baadhi miji mikuu hapa nchini ndipo kidogo wana mafanikio. Ccm ina mizizi ndani ya nchi hii viongozi wengi wamepitia Ccm iwe wa kijeshi au kiserikali n.k. tutambue hilo.

Ccm kuondoka madarakani sio upinzani ushinde hapana kabisa tena hadi pale Ccm yenyewe ipate migogoro tena mikubwa ndipo viongozi wa ndani ya Ccm tena wawe wengi wajitenge na kuanzisha siasa zenye nguvu za watu kiuchumi n.k. na wajijenge kabla kuanzia kwenye mashina ndipo Ccm inaweza ikashindwa.

Illa kwa hali ya sasa Ccm ni chama tawala na kinafaa kuongoza japo kinamapungufu mengi lakini kwa upinzani ulivyo bora ya Ccm. Mwenye kufahamu siasa na historia ya nchi hii atatambua na kuujua ukweli.
 
Mwisho mtasema Tanzania ikigawanywa UKAWA mtaingia Ikulu. Mmekosa busara na hoja za mashiko awamu hii....Inasikitisha. Dah!
 
Tiss kazi yake ni kuhakikisha nchi inakuwa salama katika kipindi chote

Unaweza ukaona tiss inaikumbatia ccm lakini huwezi jua kilichopo ndani yake......Vyama vya upinzani vinakosa support kutoka tiss kutokana na kutoeleweka vimekuwa havina agenda maalum....vimekuwa vyama vinavyoongozwa na matukio havina vision yoyote....

Chama cha upinzani kinamchukua mtu huyo huyo aliyekatwa na tiss kutokana na kutokuwa na maadili katika ustawi wa taifa kumsimisha kugombea urais

Kwa kweli upinzani tanzania mkae chini kama mnafaa kupewe nchi hii na sio kuja na vihoja
 
Kukaa kwako , kulala kwako, kustarehe kwako, kujikuna kwako, kubarizi kwako, kusoma kwako, kuuza kwako genge, kuingia kwako JF muda wowote , kuangalia kwako taarifa ya habari saa 2 usiku, kwenda kwako msibani, harusini, n.k koooteeeee huko kunafanikishwa na kazi iliyotukuka ya hao mabwana either direct or indirect , either in a visible or invisible manner. Siku ukiwakosa wazalendo kama hawa hakika utalia na kusaga meno.

Ni kweli kuwa TISS ni taasisi muhimu sana hapa nchini. Hata hivyo haya uliyoandika hapo umeteleza sana, hiyo sio kazi yao, hizo kwenye red umetumia sana 'hisia za kujipendekeza'. TISS sio Mungu.

Ungekuwa ni afisa usalama wa taifa, ungejua kuwa hizo kwenye red ni kazi za mwenyezi Mungu na hakuna hata moja inayofanywa na TISS. Na kama huwa unasoma misahafu basi kasome Zaburi 127:1-2 pia itakusaidia. Hata hivyo nakielewa sana ninachokuandikia hapa kwa vitendo kabisa. ('practically'.)
 
Ungejua unyeti na umuhimu wa hao mabwana wa mstari , hakika usingekuja kubwabwaja maneno mbofu mbofu hapa jamvini namna hiyo.

Kukaa kwako , kulala kwako, kusatehe kwako, kujikuna kwako, kubarizi kwako, kusoma kwako, kuuza kwako genge, kuingia kwako JF muda wowote , kuangalia kwako taarifa ya habari saa 2 usiku, kwenda kwako msibani, harusini, n.k koooteeeee huko kunafanikishwa na kazi iliyotukuka ya hao mabwana either direct or indirect , either in a visible or invisible manner. Siku ukiwakosa wazalendo kama hawa hakika utalia na kusaga meno.

Ila kwasababu Watanzania ni watu wa style ya kinyonga , leo hii tutawaona kama hawafahi ila siku wakiingia hao wengine mnao dhani watakuja kuwaletea maziwa , asali na siagi. ndipo mtajuuuuta kukutwa na bwana pepsi na kubaki kusema " Tungejua......" .

Asiye sikia la mkuu .
Mkuu umeandika points zenye uzito wa kipekee.
Watanzania wanaona vyombo vya ulinzi na usalama ni kama adui yao ila kumbukeni tuko Salama kwa sababu ya hivyo vyombo vilivyoko active.

Kuna watu husema wanajeshi wa Tanzania wanakula mishahara ya bure aisee wananchi kuweni makini na midomo jamani, utaona Kenya au nchi nyingine inacheka nawewe kwa sababu una ulinzi siku ukikosa ulinzi hao hao waliocheka nawewe wanakuja kubeba vitu kama wanatoa kwenye nyumba za bibi zao.

FB_IMG_1489394038334.jpg
 
Mkuu umeandika points zenye uzito wa kipekee.
Watanzania wanaona vyombo vya ulinzi na usalama ni kama adui yao ila kumbukeni tuko Salama kwa sababu ya hivyo vyombo vilivyoko active, kuna watu husema wanajeshi wa Tanzania wanakula mishahara ya bure aisee wananchi kuweni makini na midomo jamani, utaona Kenya au nchi nyingine inacheka nawewe kwa sababu una ulinzi siku ukikosa ulinzi hao hao waliocheka nawewe wanakuja kubeba vitu kama wanatoa kwenye nyumba za bibi zao.View attachment 480417
Mkuu umemaliza kila kitu kabisa. Hongera sana , kumbe bado JF ina GT wa kutosha.
 
Back
Top Bottom