Katiba Mpya na Muundo wa Serikali

ThisisDenis

Senior Member
Apr 14, 2013
149
129
Kuna haja ya kuweka serikali zaidi yamoja? Huu si uharibifu wa mali za uma na tamaa za madaraka? Haja ipi ambayo inasababisha hasa kuwepo kwa serikali zaidi ya moja ndani yanchi moja?

Amini nawaambia kukosekana kwa uaminifu na kutojiamini kwa viongozi wetu kutapelekea uvunjifu wa amani tulionayo. Na Tanzania ni next target after Rwanda, hatujawahi shuhudia machafuko lakini tuendako hakuna usalama hata kidogo.

Sipendi kudanganya umma na kutoa hotuba za kwenye makaratasi, bora tuambiane ukweli. Hali sio nzuri, wajuaji wamekua wengi na majina machafu yanazidi kuongezeka na hakuna anaesema. Wamekaa kimyaa .
 
Kuna haja ya kuweka serikali zaidi yamoja ? Huu si uhalibifu wa mali za uma na tamaa za madaraka, Haja ipi ambayo inasababisha hasa kuwepo kwa serikali zaidi ya moja ndani yanchi moja. Amini nawaambia kukosekana kwa uaminifu na kutojiamini kwa viongozi wetu kutapelekea uvunjifu wa amani tulionayo. Na Tanzania ni next target after Rwanda, hatujawahi shuhudia machafuko lakini tuendako hakuna usalama hata kidogo, sipendi kudanganya uma na kutoa hotuba za kwenye makaratasi bora tuambiane ukweli. Hali sio nzuri wajuaji wamekua wengi n majina machafu yanazidi kuongezeka na hakuna anaesema. Wamekaa kimyaa
As we

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Hatupendi ukweli/ sijui ni uoga wa maisha au nikuogopa ajira hewa tulizo nazo. Najua wengi wenu mnashindwa kuthubutu kwa kuogopa kuanguka. Dhambi hiyo itakutafuna hadi kufa.
 
wito wangu kwa Mh. dr. samia Rais wa Tanzania na Mh. prof. Juma Jaji Mkuu wa Tanzania - kuelekea siku ya kilele cha wiki ya sheria

Tanzania ni muungano wa nchi mbili Tangayika na Zanzibar. kila nchi ina sheria zake mbali na zile zianazotumika kwa pande zote. Ningeomba tuongeze juhudi ya kuimarisha Muungano. Tunahitaji kuwa na sheria zinatuunganisha watanzania huku tujaribu kuondoa sheria zinazotutenga na kuleta ubaguzi. mfano sioni mantiki mimi kama wakili Tanganyika siwezi kufanya kazi zanzibar mpaka nipate kibali kwa jaji mkuu, hali kadhalika wakili wa zanzibr haruhusiwi kufanya kazi Tanganyika. Chama cha mawakili Zanzibar kimeweka wazi kwamba hakiruhusu nafasi yake ya juu yaani rais wa ZLS kuongozwa na Mtanganyika.
Pia Leseni yangu ya udereva haifanyi kazi zanzibar. lakini dereva wa gari la serikali akifika zanzibar anaendesha tu. Hii ni baadhi ya mfano wa sheria chache za kibaguzi. Hivyo natoa rai sherii hizi zifutwe. Tuige sheria za kenya zinaruhusu Mawakili wa nchi za Afrika mashariki kupractice katika nchi yao bila vikwazo vyovyote.
 
Back
Top Bottom