Katiba mpya- Mwarubaini wa mawaziri Mizigo kina

Janja PORI

JF-Expert Member
Jul 31, 2011
825
246
KATIBA MPYA MWARUBAINI –MAWAZIRI MIZIGO
MFUMO WA KUCHAGUA MAWAZIRI KWA KUANGALIA MAENEO/MIKOA/UZALENDO WA KICHAMA UTAENDELEA KUTULETEA MAWAZIRI MIZIGO SIKU ZOTE
Nchi yetu kamwe haitakaa ipige hatua kimaendeleo kama tutaendelea kuchagua viongozi wa kusimamia wizara zetu kwa kuangalia anakotoka, anatukana na kupambana kwa kiwango gani dhidi ya wapinzani , uwezo wa kupambana na wanaharakati/wanahabari. Wizara ni taasisi nyeti katika Taifa lolote lile, wizara ndiyo inaibua, kupanga na kutekeleza sera mbali za taifa. Wizara kama ilivyo katika wizara mbalimbali , ni taasisi ambayo inapaswa kutoa majibu ya matatizo ya watanzania.
Wizara ndio (Think Tank ya Setikali katika secta husika). Ukiteuwa waziri aliyebobea kwenye majungu, fitina, matusi dhidi ya wale wanaojaribu kukosoa serikali inapokosea usitegemee wizara husika itawasaidia watanzania zaidi ya kutumia rasimali za umma kuendeleza kile kilichomfanya apewe uwaziri huo. Ali kadhalika ukiteuwa waziri kwa kuwa tu aliamua kufunga ndoa na serikali na kuwaancha wapiga kura wake ili kuwezesha mpango haramu wa kupora ardhi ya wananchi badala ya kuwatetea au ukamteuwa kwa kuwa katika mkoa husika ilikuwa ni lazima apatikane waziri baada ya kuwaengua wengine, pia katika hili usitegemee mawaziri hao kuwa badiliko lolote zaidi ya kuongeza idadi ya mawaziri mizigo.
Moja kati ya kazi kubwa ya mawaziri ni kumshauri Rais katika mambo makubwa ya kitaifa. Ikiwa kama hili ndilo jukumu kubwa la Mawaziri , unategemea watamshauri nini Mhe Raisi ilhali vichwani mwao wanawaza kupoteza democrasia ya vyama vingi nchini, watamshauri nini Rais wakati wengine hata elimu zao zinawatosha wenyewe.
Ukiona mawaziri wanateuliwa bila hata kujali uwezo wao kielimu katika kushika nyazifa nyeti kama hizi za kitaifa, tambua kuwa hizi ni fadhila na tusishangae kusikia tena naibu waziri kataja Bunjumbura kuwa ni moja wa mikoa ya Tanzania katika mikutano mbalimbali. Iweje wizara, ituhumiwe kusimamia ukatili dhidi ya watanzania, na Rais kutangaza kuunda tume ya kijaji alafu Naibu Waziri aliyekuwa madarakani katika kusimamia oparasheni hiyo apandishwe cheo katika wizara hiyo hiyo. kwanini waziri huyu asingeungana na mkubwa wake kupisha uchunguzi.
Najua kuna mengi ya kusema kuhusu uteuzi wa Rais Kikwete likiwepo la kufanya uteuzi kwa kuangalia kambi za 2015, lakini haya machache yanatosha kutoa taswira ya namna gani Taifa linaangamia kwa kukosa maarifa. Ni jambo la kujiuliza , ni kwanini mbunge aliyeonekana wazi wazi akishambulia vyombo vya habari na taasisi zake ndiye anapewa dhamana ya kusimamia Wenye jukumu la kusimamia tasnia ya habari nchini. Je, waziri huyo anaweza leo kukaa meza moja na Baraza la habari au Jukwaa la Wahariri wakati alishawatangazia watanzania kuwa vyombo hivyo havina mamlaka ya kusimamia Tasnia ya Habari nchini.
Tujiulize kama , Mbunge alishaomba katika moja ya mikutano yake na Waziri mkuu huko Loliondo apunguziwe jimbo kuwa ni mzigo kwake, inakuwaje leo Tanzania nzima iwe ndogo kuliko jimbo lake? Niulize? watanzania ni kwamba ikulu yetu haina macho au ni kwamba walifanya mchezo wa bahati nasibu kuwapata mawaziri hawa. Tulitegemea kwa kuwa tayari kilio cha kuwaondoa mawaziri mizigo kimemfikia Mh Rais tena kupitia chama ambacho yeye ni Mwenyekiti, kingemrahishia na kumpa jeuri ya kuteuwa mawaziri majembe wenye vigezo vyote kusimamia taasisi hizi nyeti za kitaifa.
Haya yote ndugu watanzania yanatendeka kwa kuwa Rais wetu ameshindwa kutumia busara binafsi katika kutumia madaraka yake ya uteuzi kwa mujibu wa Katiba inayompa hayo madaraka. Mwalimu Nyerere alipata kusema kuwa, katiba yetu hii ikipata Rais asiyemakini anawezafanya vitendo visivyotegemewa. Nasema hivyo kwa kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano tunayokaribia kuizika mapema mwaka huu hasa Ibara ya 55, inampa Rais mamlaka kuteuwa mawaziri kwa idadi yoyote na pia lazima watokane na wabunge.
Ni kweli kuwa Rais, ametumia Katiba kufanya uteuzi ila alipaswa kutumia uhuru binafsi kuteuwa mawazii wenye vigezo vya kuwatoa watanzania wote katika lindi la umaskini. Kigezo cha kuwa mbunge ni kujua kusoma na kuandika, na kwa kuwa Katiba ya sasa inamtaka Raisi kuwapata mawaziri ndani ya Bunge, Raisi alipaswa kuangalia umuhimu wa nafasi za uwaziri katika kuteua mawaziri. Rais alipaswa kutumia hekima na kujiwekea viwango vyake mawaziri anaowata ambavyo vitakuwa na maslahi kwa Taifa. Suala la kuteua mawaziri kwa kuangalia uwakilishi wa kila mkoa au kigezo cha kuwa mbunge au nani anasimamia hoja za chama zaidi kitaendelea kutupa mawaziri mizigo hadi tutakapopat Katiba mapema mwaka huu. Na katiba mpya isipopatikana mapema huenda pia baraza hili likafumuliwa tena kabla ya uchaguzi wa 2015.
Mwarobaini wa tatizo hili ni katiba mpya. Katiba mpya imeweka hadi na vigezo vya kielimu vya mtu anaefaa kuteuliwa kusimamia wizara. Kifungu cha 101 cha Rasimu ya Pili ya Katiba mpya kinazungumzia vigezo ama sifa za mtu kuteuliwa kuwa waziri au naibu waziri. Vigezo hivyo ni pamoja na kuwa lazima awe :
a) Raia wa Muungano wa kuzaliwa,
b) Awe na uzoefu na Weledi,
c) Awe na shahada ya elimu juu inayotambulika na sheria za nchi na,
d) Pia waziri hatatokana na wabunge.
Tujipongeze sana Watanzaia kwa kuamua kujikomba wenyewe kwa kuona kuwa nafasi za uwaziri kumbe hazikuwa kwa maslahi ya Watanzania bali vikundi vya watu na vyama vyao. Kwa katiba mpya hii tutapata mawaziri kwa kuangalia taaluma zao na uzoefu katika kusimamia mambo ya wananchi na sio kuangalia uwezo wa kuimba tarabu bungeni , ama sio kwa kuangalia mkoa wa fulani upate uwakilisha. Mfumo huu wa sasa wa uteuzi umemfanya raisi arudie rudie makosa yale yale kwa kuwa katiba inamtaka ateue kiongozi ndani ya bunge au kama atataka kupata nje ya Bunge anapaswa kuteuwa kwanza awe mbunge kama ilivyo kwa Asha Rose Migiro. Rais anaweza kumchagua waziri au naibu waziri asiyekuwa hata na vigezo vya kuendelea na ubunge wake huo kwa kuwa mfumo huu wa uteuzi unavigezo hafifu kikatiba. Jambo la msingi kuwa nalo macho sana, kipindi cha Bunge la katiba ni vipengele hivyo hapo juu visije vikabadilishwa kwa nguvu ya wengi Bungeni. Namalizia kwa kusema Rais wetu tupe viongozi wenye uwezo wa kuangoza watanzania na kuwatoa katika dimbwi la umaskini kwa kuangalia uwezo wao kitaalum na pia uzoefu katika kutetea hoja zenye maslahi kwa Watanzania na si vinginevyo.
Mwananchi wa kawaida - Onesmo Olengurumwa
 

Attachments

  • MFUMO WA KUCHAGUA MAWAZIRI KWA KUANGALIA MAENEO.doc
    44 KB · Views: 103
Back
Top Bottom