Katiba Mpya: Mawaziri & Bunge! + Madaraka Mikoani!

Miaka ya nyuma kidogo tuliwahi kuwa na mjadala kuhusu mambo haya ya kikatiba na kugundua kuwa raisi wa Tanzania ana madaraka makubwa sana.

Jambo la kwanza katika katiba mpya ni lazima liwe la kupunguza madaraka ya rais.


  1. Asiwe mtu wa kwanza na wa mwisho katika kuteua watu wanaofanya kazi za umma.
  2. Asiruhusiwe kuteua watu wanaofanya kazi za kila siku na wanachi huko mikoani kama vile wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya.
  3. Asiwe madaraka ya mwisho katika kuteua na kufukuza kazi watu wanaofanya kazi za serikali zinazohitaji utaalamu maalumu kama wakuu wa polisi, wakuu wa majeshi, makatibu wakuu wa wizara, makamishana na wakurugenzi wa idara mbalimbali, mahakimu na wakuu wa idara zote zinazosimamia sheria kama TAKUKURU, DCI, DPP, na kadhalika.

Vile vile madaraka ya viongozi wote wa kisiasa walioteuliwa na rais kama vile mawaziri yapunguzwe:

  1. Wasiwe na uamuzi wa mwisho katika wizara, majukumu yao yawe ya kisiasa tu; uamuzi wa mwisho wa kitaalamu uwe unasimamiwa na katibu mkuu.
  2. Wakuu wa mikoa/wilaya wawe wanagombea nafasi hizo kwa njia ya uchaguzi, Nafasi nyingine zote za serikali za kiwango cha kati zinazohitaji utaalamu maalumu kama zile za mahakimu, makamishna, wakurugenzi na nafasi za namna hiyo ziwe za mkataba unaotathminiwa kila baada ya muda fulani; ziwe zinatangazwa kusudi raia wote wawe na nafasi ya kuzimba. Raia wawe na na nafasi ya kukata rufaa iwapo wanadhani aliyepewa nafasi hana sifa sahihi.
  3. Nafasi za uongozi za ngazi ya juu serikalini ziwe zinatolewa na bunge, rais anaweza kupendekeza lakini uamuzi wa miwisho uwe unafanywa na bunge.

Kuna mambo mengi ya kutatua kwenye katiba ili kupunguza uzito wa madaraka yanayowekwa chini ya mtu mmoja. Ila tukishapunguza madaraka ya raisi na wateule wake tutakuwa tumetatua tatizo kubwa sana.

Ipo powa.
 
Back
Top Bottom