Katiba Mpya: Mawaziri & Bunge! + Madaraka Mikoani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba Mpya: Mawaziri & Bunge! + Madaraka Mikoani!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by W. J. Malecela, Apr 29, 2012.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  Pendekezo kwenye katiba mpya:-

  1. Wakati umefika sasa Rais awapendekeze anaowataka kushika Uwaziri, halafu wapitiwe na kamati za bunge za wizara zao kwanza kwa kuzingatia ripoti za kutoka Usalama wa Taifa na TAKUKURU, iwapo kamati zitaridhia, basi jina lipelekwe kwenye full bunge, akpitia na huko ndio awe Waziri.

  Suala la hivi karibuni la Bunge na Mawaziri, kwa kweli ni a very big distraction kwa National agenda kwa sababu ninaamini by now sekta muhimu za taifa zitakua zimesimama au zinakwenda very slow kutokana na hofu ya kuvunjwa kwa Cabinet, na markets kwa kawaida huwa hazifanyi vizuri sana kama inavyotakiwa taifa linapokuwa kwenye kipindi kama hichi tulichonacho sasa, lakini tukiweka huo mfumo kwenye katiba yetu mpya, tutapunguza sana this kind of distractions kwa sababu Bunge litakuwa na nguvu kubwa kisheria ya kuwasimamisha kazi mawaziri wazembe badala ya kusubiri Waziri Mkuu au Rais, au Kamati Kuu ya chama, tawala.

  2. Tufike mahali ni muhimu tukawa na kipengele kitakachotoa nguvu za kisheria na kiutawala kwa mikoa, badala ya miko kubaki ikisubiri orders kutoka Serikali kuu Dar kila wakati, the process is too slow na inaacha miko ikiwa powerless as opposed na mataifa yote Duniani yaliyoendelea, ambako mikoa ina guvu kubwa sana kufanya maamuzi yake kisheria na kiuchumi, pamoja na kisiasa huku ikizingatia katiba ya jamhuri.

  - Mikoa ipewe uhuru na mamlaka ya kuamua maamuzi muhimu ya mikoa hiyo, itapunguza sana hata ziara za Viongozi wakuu kwenye mikoa kila siku kama wanavyofanya sasa, wananchi wapewe nafasi kimkoa kuamua wanyoyataka kuyafanya as far as maendeleo is concern.

  3. Kipengele cha kuhamia Dodoma, ifike mahali sasa tuamue kama kweli tunataka kuhamia Dodoma au tubaki Dar, I mean hivi kweli sio ni very expensive kuendesha Serikali Dodoma na Dar kama tunavyofanya sasa hivi jamani!, I mean toka nikiwa mtoto mdogo ninasikia kuhamia Dodoma, na mpaka leo bado ni hadithi tu vipi? Mawaziri wana ofisi Dar na Dodoma, so is nyumba za Serikali, jamani kuwepo na huruma japo kidogo na hela za wananchi.

  MUCH RESPECT!

  William.
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  good one, sera za chadema hizo...
   
 3. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #3
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - What a coincidence!

  William!
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Wewe unacopy sera za CDM unapaste hapa. lakini hapo mwishoni mtu wa kwanza ambaye angetakiwa kutekeleza kuhamia dodoma ni baba yako wakati akiwa waziri mkuu
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Miaka ya nyuma kidogo tuliwahi kuwa na mjadala kuhusu mambo haya ya kikatiba na kugundua kuwa raisi wa Tanzania ana madaraka makubwa sana.

  Jambo la kwanza katika katiba mpya ni lazima liwe la kupunguza madaraka ya rais.


  1. Asiwe mtu wa kwanza na wa mwisho katika kuteua watu wanaofanya kazi za umma.
  2. Asiruhusiwe kuteua watu wanaofanya kazi za kila siku na wanachi huko mikoani kama vile wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya.
  3. Asiwe madaraka ya mwisho katika kuteua na kufukuza kazi watu wanaofanya kazi za serikali zinazohitaji utaalamu maalumu kama wakuu wa polisi, wakuu wa majeshi, makatibu wakuu wa wizara, makamishana na wakurugenzi wa idara mbalimbali, mahakimu na wakuu wa idara zote zinazosimamia sheria kama TAKUKURU, DCI, DPP, na kadhalika.

  Vile vile madaraka ya viongozi wote wa kisiasa walioteuliwa na rais kama vile mawaziri yapunguzwe:

  1. Wasiwe na uamuzi wa mwisho katika wizara, majukumu yao yawe ya kisiasa tu; uamuzi wa mwisho wa kitaalamu uwe unasimamiwa na katibu mkuu.
  2. Wakuu wa mikoa/wilaya wawe wanagombea nafasi hizo kwa njia ya uchaguzi, Nafasi nyingine zote za serikali za kiwango cha kati zinazohitaji utaalamu maalumu kama zile za mahakimu, makamishna, wakurugenzi na nafasi za namna hiyo ziwe za mkataba unaotathminiwa kila baada ya muda fulani; ziwe zinatangazwa kusudi raia wote wawe na nafasi ya kuzimba. Raia wawe na na nafasi ya kukata rufaa iwapo wanadhani aliyepewa nafasi hana sifa sahihi.
  3. Nafasi za uongozi za ngazi ya juu serikalini ziwe zinatolewa na bunge, rais anaweza kupendekeza lakini uamuzi wa miwisho uwe unafanywa na bunge.

  Kuna mambo mengi ya kutatua kwenye katiba ili kupunguza uzito wa madaraka yanayowekwa chini ya mtu mmoja. Ila tukishapunguza madaraka ya raisi na wateule wake tutakuwa tumetatua tatizo kubwa sana.
   
 6. S

  Seacliff Senior Member

  #6
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Willy, everybody seems to want you to move to CDM but I know you can't and I respect that. Pamoja na kwamba mimi ni mwanachama wa CDM sidhani kuwa ni lazima uwe CDM ili uwe na uchu wa kuendeleza nchi yako. In any case, hoja yako ya kuwapa nguvu wakuu wa mikoa ina kasoro kwa sababu hawachaguliwi na wananchi wanaowaongoza kwa hivyo bosi wao yuko Dar. Labda kama tunataka wawe na nguvu kama unavyosema, tupendekeze kwenye katiba mpya wachaguliwe kama wanavyochaguliwa governers huko Marekani. What do you hink about that?
   
 7. c

  collezione JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Mutuz
  Kwenye hiyo sera ya mikoa, ndo ile ile tunaililia kila siku (sera ya majimbo) nakushukuru kwa upeo wako.

  Mutuz wewe umekaa marekani zaidi ya mika 22. Umeona jinsi states gvt inavyofanya kazi. And jinsi implimentation inavyokuwa success.

  Ndo hivyo tunachotaka Tanzania kwenye katiba mpya. Tuachane na mfumo wa westMinisters. Tuingie kwenye states gvt. Ikimaanisha, tuwape wananchi nguvu zaidi, na kupunguza madaraka serikali kuu (decentralisation).

  Mfumo wa sasa hivi, una risk nyingi. Mfano, waziri wa Nishati let's Ngeleja na Malima. Wakiwa watu wa deal na rushwa. Ina maana sector yote ya nishati Tanzania inaangamia. Ndo kile tulichokuwa tunakiona. Nchi nzima iko gizani. Kutokana na uzembe wa mtu mmoja, Taifa zima liko gizani.

  Mutuz tukisema tuweke ki_mkoa. Itakuwa too small. Mi naona tufanye kimajimbo. Ambapo, mikoa 3-4 inaungana, na inapewa power kusolve matatizo ya wananchi. Bila kusubiri maamuzi ya waziri anayeishi Dar-es-Salaam.

  Na hiki ndo wananchofanya Marekani... States gvt ndo siri kubwa ya China kutupita kimaendeleo. wakati tulikuwa sawa hapo nyuma
   
 8. w

  wamwala Senior Member

  #8
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Le Mutuz analysis nzuri sana unasubiri nn huko Magamba? hamia CDM tujenge nchi pamoja. Magamba ni kupoteza muda tu hakuna jipya na 2015 ndio byebye
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Willy hiyo ya kwanza sawa japo itahitaji masahihisho kidogo.

  Hiyo ya pili kwa nini usingesema tu kwamba tuwe na Serikali za Majimbo? Au umeogopa kutamka hivyo kwa kuwa ni sera ya CDM. Nadhani tunakoenda tunahitaji utawala wa majimbo hili suala la ugatuzi wa madaraka naona halitusaidii sana. Utawala wa Majimbo ukiundwa vizuri kuepusha vimelea vya ukabila utatusaidia sana.
   
 10. c

  collezione JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Ndugu, mimi sielewi ubaguzi gani mnauongelea....

  Hii propaganda ya ubaguzi mkitaka kuikuza, itakuzika kweli. Na mwisho wake hatutafanya kitu chochote.

  Unapoongelea sera ya majimbo inaleta ubaguzi, embu tumuulize Mutuz amekaa miaka 23 USA, ameona ubaguzi wowote.
  Waliokaa Canada na wenyewe watuambie. Wale wa China na wenyewe watuambie kama kuna ubaguzi.

  Hizi propaganda za ubaguzi kwenye sera za majimbo. Zinaletwa na watu wachache wasiopenda maendeleo ya nchi yetu. Bado wanafaidika na madaraka makubwa ya central gvt, kwasababu ya deals zao.

  Embu tujikumbushe mfumo wa sasa hivi wa mikoa. Leo ukienda Dodoma utawakuta wahaya. Au ukienda mwanza utawakuta wazaramo. Ina maana basi tukitoa mfumo wa mikoa tukaweka majimbo basi ubaguzi unakuja ghafla???

  Kwenye sera ya majimbo. swala kubwa linalo_ongelewa ni kwamba, Badala ya kusubiri maaumuzi ya Raisi au waziri anayeishi Dar-es-Salaam. states(majimbo) yanakuwa na vipaumbele vyao na uhuru wa kupanga mikakati yao, kutokana na mahitaji ya wananchi. Sasa kwa kufanya hivi, chanzo cha ubaguzi hapo ni nini????

  My Take: tusiendekeze hizi propaganda zisizo na maana. Miaka 50 ijayo wajuukuu zetu watakuta madini yote yamekauka. Na bado Tanzania ni maskini. Kutokana na ukiritimba uliokuwepo (states gvt is a soln for now, kama tuko serious na nchi yetu)

  Na nawaomba waTanzania wote tufikirie sera ya majimbo. Sio kwa Chadema tu, CCM, NCCR, TLP na hata ambao hawaamini siasa. Tukae chini kupanga mikakati ya nchi yetu. Kwa vizazi vijavyo.
   
 11. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,278
  Trophy Points: 280
  Kwa mtu makini kabisa kama atasoma kwa umakini thread hii ya Willy atagunduwa kitu kimoja rahisi sana kuhusu huyu William, nitajaribu kueleza kwa uchache.

  William inaoneka haamini anachokifanya na ni vigumu kuelewa yeye mpaka leo ni mwanachama wa CCM kwa vigenzo vipi? yupo kiitikadi au kimaslahi?

  Maana thread nzima ya Willy ni sera za Chadema, sasa mpaka leo sijaelewa hasa baadhi ya watu wako kwenye vyama kwa sababu ya Itikadi ya chama au itikadi yatumbo?

  Nimefikia tamati ya kugunduwa huyu Willy ni mtu dhaifu sana na kamwe milele hatokuwa mwanasiasa na hata akilazimisha kuwa Mwanasiasa basi atakuwa Political loser maana anategemea kuishi Maisha ya siasa kwa kutegemea kimvuli cha Baba yake ndio maana inashangaza mtu ni Member wa CCM lakini Itikadi zake ni za Chadema!!

  Hapa ndipo Willy anaposumbuwa Ubongo wa watu wengi kama yeye Itikadi yake anaiona iko upande fulani ni kwa nini asitoke CCM na aende akaungane na na wale wanaofanana na yeye kiitikadi?

  Huyu amezoea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi, si mwanasiasa si lolote ni mbabaishaji tu kama walivyo wababaishaji wengine, 23 years in New York, unarudi miezi 3 Bongo unataka kuwawakilisha Watanzania kwenye Bunge usilojuwa hata kazi zake!!
   
 12. c

  collezione JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Matola

  Wakuu mnakosea mnaposema Willy hajielewi. Kwasababu ya hii mada ya "majimbo".

  Mimi binafsi sio muumini wa siasa, na wala sio mshabiki wa chama chochote. Ila pale penye ukweli lazima wote tukubali, regardless ya vyama.

  CHADEMa, sio wa kwanza kuleta sera ya majimbo duniani. Hii sera ya majimbo inatumika na nchi mbalimbali USA, India, Canada, China nk. Na ime_prove to work success.

  Sasa basi tunapoongelea sera ya majimbo sio kwasababu ya kutaka ushindi wa Chadema. Bali tuangalie maslahi ya Taifa letu kwa vizazi vijavyo.

  Miaka 100 ijayo wewe, mimi, Willy inawezekana tusiwepo duniani. Hata CCM, Chadema, mbowe, Kikwete, Nape, Zitto. Wanawezekana wasiwepo Duniani.

  Swali linakuja, mikakakti gani tunaacha ili wajukuu zetu waje kufaidi busara zetu?? Hilo ndo swali la msingi. Nawaomba wana-bodi tuache ushabiki wa vyama, tu_stand in the name of our wisdom.

  Miaka zaidi ya 100 iliyopita Marekani walivyoamua kuweka sera za majimbo. Walifanya hivyo kwa ajili ya wajukuu zao. Ndo maana leo waMarekani wanafaidi hizo busara za mababu zao.

  Na sisi tuamue hili kwa vizazi vyetu. Regardless Chadema wameleta hii mada. Tuamue kama nchi na sio kwasababu Chadema wamesema. Tusimame kwemye ukweli. Kwamba "sera ya majimbo itatusaidia waTanzania".
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #13
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Honestly, sikujua kama hii ndio sera ya CDM isipokuwa hoja ya Wakuu wa Mikoa kuchaguliwa na wananchi ninaamini inatakiwa kujadilika, iwapo sasa hivi tunao Madiwani wanaochaguliwa na wananchi, swali ni kwa nini tusifike mpaka kwenye mikoa?

  - Kwamba nime-paste sera za CDM hapana, ni msimamo wangu na hasa baada ya kusoma na pamoja na kuishi US na kujionea sera kama hizi zikifanya kazi tena perfectly!

  - Mimi Kuingia CDM hilo wala halina mjadala ni halipo kabisaa!

  William.
   
 14. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #14
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Tatizo lako ni huwezi kutofautisha hoja na chuki yako kwangu binafsi, ila elewa hivi hunizuii anything zaidi tu ya kukuonea huruma si unajua wataalamu wa afya wanasema ukiwa na chuki na mtu mwingine bila sababu kama wewe ulivyo unaweza kuishia kuwa na magonjwa yasiyotibika, ha! ha! ha! ha!

  - In the future jifunze kujadili hoja kuliko mtao hoja, maana kujadili mleta hoja kila kukicha ni very unproductive kwa taifa!

  William.
   
 15. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #15
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Mkuu naona hujawahi kupata ujumbe wangu kwamba hoja ikishakuwa na baba yako au wa member yoyote hapa, huwa ninaidharau kwamba sio hoja ila ni viroja na huwa siisomi mpaka mwisho!


  William.
   
 16. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hiyo point hapo juu nimeipenda. Kwa kufanya hivyo itazuia Rais kuweka mawaziri washkaji/wapambe wake au ndugu zake na mpaka wakiweza kupitishwa na bunge that means watakua vetted kiukweli.

  Sema swali ni kwamba iwapo bunge likichagua mawaziri na wakawa ndio hao wanaiba hela na kuchezea mali za nchi bunge litakua vipi accountable for that...Nani atakua na nguvu ya kusema hawana imani na bunge/wabunge na decisions zao za kuchagua mawaziri?? how are you going to be accountable for your actions??!!
   
 17. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #17
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Ukisha kuwa na hiyo System in place, automatically unakuwa na System ya checks and balance, na nchi zote zilizoendelea Duniani, kamati ya bunge ya wizara ndiyo yenye power over wizara na waziri, na ndio maana ni muhimu sana kamati za bunge zikawa na wabunge wa Upinzani kwenye Uongozi wake, ni kuhakikisha kuna checking system!

  William.
   
 18. m

  mkurugenz JF-Expert Member

  #18
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  ni sera ya cdm,so tuitoe ktk tume ya ktb itapokuja
   
 19. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #19
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hapa ninashangaza kila mtu anapokuja na hojawengine hukimbilia kusema "hiyo hoja ya chama fulani". Ikiwa hoja ya majimbo ni ya CDM, jee wakija Wamarekani, Wakanada, Waustralia, Wahispania...wakasema "hiyo ni sera yetu, tuliianzisha sisi karne 5 zilizopita? Ikiwa chama kimeingiza sera mpya, au kimeiga sera kutoka kwengie, lakii sera hiyo ikaonekana na nzuri kwa taifa, na ikwa watu kutoka vyama vyengine wameipenda, kuna haja gani ya kuendelea kung'ang'ania "hiyo ni sera yetu?"
  :focus:
  Iwe ni kuweka mikoa/majimbo au kanda, cha muhimu katika suala hili ni kuimarisha demokrasia na kufanikisha utendaji na uwajibikaji. Kama aliyosema Willy, tunachagua madiwani kuongoza kata, kwa nini tushindwe kuchagua watu wa kuongoza halmashauri, wilaya na mikoa? Ulimwqengu wa leo ni wa kiushindani - kiasiasa, kiuchumi na kijamii - kwa hivyo kuwapo na watu waliochaguliwa na wananchi wenyewe, hawa watalazimika kuwajibika kwa wananchi, na watatenda kazi zao kwa hofu kuwa sio tu wananchi wanaweza kuwaadhibu kwenye visanduku, bali pia watawafikisha mahakamani kama watahalifu sheria.

  Kwa sasa tayari tuna mzigo ndani ya mzigo katika mfumo tulionao. Tumeongeza mikoa na wilaya mpya bila ya sababu. Kutawalika kwa nchi si kila uchao kuicharanga nchi katika mikoa na wilaya mpya, kama ambavyo uwajibikaji hauletwi na kuunda mawizara lukuki. Ilitokezea "coincidence" kuwa wakati ambapo Ufaransa na Italia wanaamua kupuunguza mzigo wa kiutawala kwa kufuta maelfu ya kata na mamia ya wilaya, wakati huo huo Tanzania tukiwa na matatizo kushinda ya Ufaransa na Utalia, sisi wakulu wetu wakawa wanaongeza wilaya mpya. Cha kutoona haya, baadaye tunakwenda kwao kupeleka bakuli la kuongozea wilaya, mikoa, wizara zetu lukuki.

  Watanzania, for the sake of Tanzania, for the sake our forthcoming generations, tuacheni sera za chama kwanza, tuifikirie nchi kwanza, tufkirie vizazi vyetu miaka 100 ijayo kama alivyosema collezione
   
 20. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #20
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Mheshimiwa W.,
  Kwa mara ya kwanza leo nimekupa like, kwani atleast leo umeongea point.
   
Loading...