Katiba Mpya: Mambo yote yawe ya Muungano

Mag3,
Mkuu hakuna maneno mengi ila tuzungumzie facts, Kwani hiyo katiba ya Zanzibar inatukwaza nini haswa? Toka wameandika ni shughuli gani za serikali ya Muungano imeshindwa kuzitekeleza kama zamani?
 
MAMBO YOTE YAWE YA MUUNGANO

Baada ya kuyasoma mapungufu na malalamiko ya pande zote mbili nimekuta swala mojaoja ambalo pande zote mbili wamelalamikia. Nalo ni - Kuwepo kwa mkanfanyiko jinsi ya kuchangia shughuli za Muungano baina ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na ugawanaji wa mapato. Hapa inaonekana tunakwenda kiholela tu hakuna uwazi wala mfumo kamili unaoeleweka na wazi kwa kila mshirika ama mwananchi kufahamu kinachoendelea maana orodha ya mambo ya muungano imeainishwa wazi kabisa katika katiba ya Muungano lakini kwa yale yasokuwa ya Muungano hatuna mahala popote yameorodheshwa - HAKUNA.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano imesema hivi katika sehemu ya kwanza, jamhuri ya Muungano wa watu, sehemu ya nne (4) ibara ya 3 ya kwamba - Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za umma katika Jamhuri ya Muungano, na kwa ajili ya mgawanyo wa
madaraka juu ya shughuli hizo baina ya vyombo vilivyotajwa katika ibara hii, kutakuwa na Mambo ya Muungano kama yalivyoorodheshwa katika Nyongeza ya Kwanza iliyoko mwishoni mwa Katiba hii, na pia kutakuwa na Mambo yasiyo ya Muungano ambayo ni mambo mengine yote yasiyo Mambo ya Muungano

Hivyo hakuna mtu anayejua kwa ufasaha ni mambo gani yasokuwa ya Muungano isipokuwa yale ambayo hayakuorodheshwa na ndipo utata ulipoanzia maana mwaka 1964 yalikuwa 11 kabla ya kuvunjika jumuiya ya EAC, yalipoongezwa na kufikia 22 ndio madai yakaanza kutokea japo umuhimu wake ulikuwa kwa Taifa zima, Hivyo tuanze na hili kwanza maana tunapoacha wazi ufa kama huu wa haya yasokuwa ya muungano pasipo kuwa na uhakika nayo, ndipo malalamishi hutokea.

Katiba iliyopo imeainisha wazi mambo ya Muungano kuwa ni:-
1. Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
2. Mambo ya Nchi za Nje.
3. Ulinzi na Usalama.
4. Polisi.
5. Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.
6. Uraia.
7. Uhamiaji.
8. Mikopo na baiashara ya Nchi za Nje.
9. Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
10. Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa
nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.
11.Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.
12.Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya malipo yote halali (pamoja na noti); mabenki (pamoja
mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki;fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika
na fedha za kigeni.
13.Leseni ya viwanda na takwimu.
14.Elimu ya juu.
15.Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya motokaa na mafuata ya aina ya petroli na aina nyinginezo za
mafuta au bidhaa, na gesi asilia.
16.Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yote yanayohusika na kazi za Baraza hilo.
17.Usafiri na usafirishaji wa anga.
18.Utafiti.
19.Utafiti wa hali ya hewa.
20.Takwimu.
21.Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.
22.Uandikishaji wa Vyama vya siasa na Mambo mengine yanayohusiana navyo.

Hivyo jambo lolote ambalo halikuainishwa hapa ina maana sii la Muungano, iwe kwa makosa ya uandishi, kutokuwepo wakati wa uandishi wa katiba hii, kutotazamwa ama halikupendekezwa kuwa la muungano bila sababu maalum. Kufuatia pendekezo langu kuhusu mambo yote yawe ya muungano, ni kutokana na ukweli kwamba msingi mkuu wa muuungano ni mambo gani mloungana hivyo yanapokuwa machache ndivyo muungano unavyokuwa dhaifu na jinsi mnavyoungana kwa mambo mengi zaidi ndivyo uimara wa muungano wenyewe sio swala la aina gani ya muungano ama muundo gani wa muungano.

Kila aina ya muungano inakuwa na malengo yake na uimara wake hutegemea mambo yanayowaunganisha, na pia swala la serikali ngapi ni muundo wa utawala ktk utekelezaji wa shughuli za muungano huo hivyo haya yote haihusiani kabisa na mpango mzima wa uchagiaji wa gharama za uendeshaji ama ugawaaji wa mapato. Hivyo msingi mkuu wa ushirika unatanguliwa na mambo gani mloshikamana na ndio sababu yangu kubwa ya kutanguliza mambo yote yawe ya muungano ili kuuimarisha zaidi muungano huu badala ya kupunguza mambo kutoka 22 ya sasa na kuwa 7 yalopendekezwa na tume ya katiba kuudhoofisha zaidi hata muungano tulokuwa nao.

Swala la mkanganyiko wa uchagiaji na mapato

Mambo yote ya muungano yamejumuisha mambo yote ya umma yaliyopo na mapya yatakayojitokeza katika ngazi zote za Utawala pamoja na serikali zake kulingana na mahitaji yetu kwa ajili ya huduma ya wananchi na maendeleo ya nchi yetu. Kwa maana hiyo kila pato la kodi litokanalo na ukusanyaji kodi zake kama zilivyoainishwa kwa upande wowote wa Jamhuri ya muungano, kodi hizo zitachangia moja kwa moja mfuko wa Taifa kwa asilima maalum itakayo afikiwa kwa mfano itasomeka kodi mapato ya JMT ni asilimi 20. Hivyo nchi washirika yaani Tanzania bara na Tanzania visiwani watawajibika kukusanya mapato hayo kwa niaba ya serikali kuu na hivyo kuwasilisha mapato hayo kwa kipindi ama vipindi maalum vitakacho wekwa kwa kila mwaka. Mapato haya yatatokana na aina zote za kodi na ruzuku kufuatia mamlaka ya sharia ya kodi ya mapato itakayo pitishwa na bunge isipokuwa ushuru wa bidhaa zisizokuwa za kodi.

Na ili kuondokana na mkanganyiko ama uwazi ktk makusanyo ya kodi hizo kila nchi itakuwaa na kiwango kamili cha ongezeko la kodi yake juu ya kodi ya Muungano ambayo kiongozi wa nchi hiyo ama bunge lao watapitisha na kuwa sheria. Mathlan Zanzibar wao watasema kodi ya mapato kwa serikali yao itakuwa asilimia 5 ya pato hivyo kuifanya jumla ya kodi yao kuwa asilimia 25 (20 ya JMT na 5 ya SMZ), makusanyo ya asilimia 5 yanakwenda moja kwa moja mfuko wa serikali ya Zanzibar na bara nao kwa kutazama hali ya maisha na mfumko wa bei watasema kodi yao itakuwa asilimia 10 hivyo kuifanya jumla ya mlipa kodi zake kwa mlipa kodi kufikia asilimia 30. Hivyo tunaweza kutofautiana ktk kodi za ndani lakini sote tunawajibika kwa pamoja kuchangia asilimia 20 ya mapato ya kodi zetu ktk mfuko wa Taifa tokana na ukusanyaji wa kodi ktk mambo yote ya Jamhuri ya muungano.

Kwa kufanya hivi tutaondoa mkanganyiko wa uchangiaji japokuwa watu watapenda kuelewa hiyo Tanzania bara wao wataweza vipi kutenganisha mapato haya ikiwa hakuna serikali ya Tanganyika? Mimi sintopenda kujadili muundo gani wa serikali zetu na kupendekeza upi unatufaa zaidi bali najikita ktk mapungufu ya katiba kwa sababu miaka yote 50 Tanzania bara imekuwa ikiendesha mambo yake yasokuwa ya Muungano pasipo bunge wala serikali maalum la kujadili na kuendesha mambo hayo.

Inatosha kwa leo!.
 
Mag3,
Mkuu hakuna maneno mengi ila tuzungumzie facts, Kwani hiyo katiba ya Zanzibar inatukwaza nini haswa? Toka wameandika ni shughuli gani za serikali ya Muungano imeshindwa kuzitekeleza kama zamani?

Wewe Mkandara ni bogus kabisa
Kwa hiyo akitokea mtu akavunja katiba so long as shughuli za serikali haziathiriwi kwako wewe sawa.
Huu ni Upunguani wa hali ya juu.
Ni sawa na wale wanaotuaminisha kuwa hatuna haja ya katiba mpya,haja yetu ni maji,matibabu na umeme.
Wewe si uliponda madai ya UKAWA na kusema hukuona hoja ya wao kutoka nje.
Mkuu wewe ni mmoja kati ya Vijana wa hovyo kwa kiwango ambacho hakiwezi kuelezeka.
 
Last edited by a moderator:
Wewe Mkandara ni bogus kabisa
Kwa hiyo akitokea mtu akavunja katiba so long as shughuli za serikali haziathiriwi kwako wewe sawa.
Huu ni Upunguani wa hali ya juu.
Ni sawa na wale wanaotuaminisha kuwa hatuna haja ya katiba mpya,haja yetu ni maji,matibabu na umeme.
Wewe si uliponda madai ya UKAWA na kusema hukuona hoja ya wao kutoka nje.
Mkuu wewe ni mmoja kati ya Vijana wa hovyo kwa kiwango ambacho hakiwezi kuelezeka.
Mkuu wangu hakuna sababu ya kutukana, hoja yako itafika pasipo matusi maana nikianza hatutafika popote ila kuvuana nguo. Hapa tunajadili mambo ya Muungano na sio katiba ya Zanzibar, ukitaka anzisha ukumbi wake na tukutane huko.

Labda wewe nambie nani alovunja katiba maana nijuavyo mimi rais wa Zanzibar ndiye alitakiwa kuwa makamu wa rais. haya mageuzi aliyafanya nani na kwa ridhaa gani. Zanzibar wamelazimika kuwa na rais kwa sababu makamu wa rais sio tena kiongozi wa Zanzibar. Kuondolewa kwa Azimio la Arusha wananchi walihusishwa? Viongozi kuvaa kofia mbili wananchi walihusishwa? Takrima kuwa sio rushwa wananchi walihusishwa. Conflict of Interest wananchi walihusishwa?..Iweje swala hili la Zanzibar tu ndio lipewe uzito mkubwa wakati nchi za wenzetu nchi yoyote katika muungano ina bendera yake, ina serikali yake ina kiongozi wake na kadhalika. Mbona Mscotish akijiita hivyo Waingereza hawapigi kelele ili hali sisi tunawaita wote Waingereza!.

Na hata Ufafanuzi wa mambo mengi yaloongezwa ktk Muungano tumekuja yajua majuzi JK alipolihutubia bunge la katiba, hivyo inaonyesha wazi kwamba CCM walikuwa wakifanya mabadiliko ya katiba wenyewe na hivyo Zanzibar kujikuta hawana mamlaka hayo tena. katiba ya muungano ni Katiba ya Tanganyika ilotumika miaka yote na kufanyiwa marekebisho haikuwa sumu kwenu isipokuwa pale zanzibar walipobadilisha yao tena kwa ridhaa ya viongozi wenu?.. Hovyo nani?

Nakuomba sana jadili mada iliyopo hapa (idea), na huna mchango wowote isipokuwa kunisema mimi (simple minded) bora katafute jimbo! UKAWA ni wawakilishi wenu hawaniwakilishi mimi hata kidogo kwa saabu wao wanatazama maslahi ya vyama vyao na kina nyie na Uchadema wenu bakieni nao.
 
Mag3,
Mkuu hakuna maneno mengi ila tuzungumzie facts, Kwani hiyo katiba ya Zanzibar inatukwaza nini haswa? Toka wameandika ni shughuli gani za serikali ya Muungano imeshindwa kuzitekeleza kama zamani?
Mkandara, naomba tu unipe jibu halafu tuendelee na huu mnakasha kuhusu mfumo huu unaoupendekeza wa mambo yooote kuwa ya Muungano. Nauliza tena, je mfumo huo unawezekana bila kuathiri Katiba ya sasa ya Zanzibar? Hilo tu.
 
Last edited by a moderator:
Mkandara, naomba tu unipe jibu halafu tuendelee na huu mnakasha kuhusu mfumo huu unaoupendekeza wa mambo yooote kuwa ya Muungano. Nauliza tena, je mfumo huo unawezekana bila kuathiri Katiba ya sasa ya Zanzibar? Hilo tu.
Mkuu wangu unaniuliza swali ambalo jibu lake liko wazi kabisa. Chochote kinachokubaliwa katika uandishi wa katiba hii mpya na kikapitishwa na wananchi kitabadilisha katiba zote mbili. Tukikubali ushirika wa SHIRIKISHO utabadilisha katiba ya Muungano na ya Zanzibar. Tukipitisha serikali 3 itakuwa hivyo hivyo, tukisema rais atakuwa mmoja na kadhalika, haya ni maamuzi yetu sote na sio swala la kuathiri katiba fulani ama tuna chuki bali ni katika kuboresha mahusiano yetu.

Kwa hiyo sijui hasa ulikuwa unamaanisha nini ya kwamba kuna uwezekano mkubwa lolote litakalo pitishwa halitaweza kubadilishwa visiwani? Kama ndivyo basi sioni sababu ya kuandika katiba mpya maana rais wao alihusika, mabaraza yote mawili yamehusika sijui nani atakayeweka kikwazo.
 
Mkandara, naomba tu unipe jibu halafu tuendelee na huu mnakasha kuhusu mfumo huu unaoupendekeza wa mambo yooote kuwa ya Muungano. Nauliza tena, je mfumo huo unawezekana bila kuathiri Katiba ya sasa ya Zanzibar? Hilo tu.
Mkuu yote hiyo ni kutaka kufunika hoja ya muundo wa S3 na hasa kuzinduka kwa Tanganyika. Ni jitihada za kutaka kuona Tanganyika haitajwi na wala haisikiki. Haiingii akilini kuwa tunaweza kuwa na mambo yote wakati kuna waliyo nayo.

Swali lako nimemuuliza sana katika nyuzi nyingine. Nimemueleza kuwa kwasasa tulikuwa na mambo 22 ambayo ni 47.
Wazanzibar wamekataa na kutaka yapunguzwe wakitaka kuwa na Polisi na Uhamiaji yao.

Hawataki hata kuheshimu katiba ya 1977 leo uwaambie mambo yote ya muungano!
Wameondoa mambo ya muungano bila heshima na hawakufanywa lolote. Leo useme yote ya muungano!

Mkuu hii ni kutaka kutuondoa katika hoja ya msingi. Huu mfumo unaopendekezwa ni ndoto. Ni kitu kisichowezekana
Huwezi kuwa na mambo yote ukiwa tayari una ubinafsi na uhuni na element za ignorance.y

Ukisema yote yawe ya muungano, ina maanisha S1. Hapo hapo anasesma znz wawe na yao, Insanity

Kama haiwezekani,kwani lazima tuwe na muungano.

Na hao wanaotaka mambo yote yawe ya muungano hata siku moja hawawezi ku justify kwa faida ipi.


This is to derail people from the core issue.
 
MAONI KUHUSU KATIBA MPYA

Kwanini mambo yote yawe ya Muungano

Kufuatia mgogoro uliopo baina ya pande mbili za kisiasa kushindwa kufikia muafaka juu ya muundo wa serikali ningependa kusema tatizo la nchi yetu lipo ndani zaidi ya swala la idadi ya serikali zetu iwe 1, 2 au 3 kwa sababu serikali huundwa kwa minajiri ya kugawana mamlaka ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Na ifahamike tu kwamba hakuna muundo maalum wa serikali ziwe ngapi ktk mfumo wa washirika ktk utawala wowote iwe ule wa Muungano (union), Shirikisho (federation), Jumuiya (Confederation/Community) kwa sababu ushirika haujengwi kwa idadi ya serikali bali hali halisi ya matakwa ya wananchi ktk ushirika wao kwa masharti na malengo walotaka kuyafikia ndio hujengwa serikali zake ili kuwafikia wananchi haraka na wepesi zaidi.

Mgogoro wa kisiasa
Sintojikita ktk mgogoro wa kisiasa ulofuatia bunge maalum la katiba kuvunjika kwa sababu huo ni mjadala mrefu sana pengine tutaugusia pale inapopaswa isipokuwa nitakwenda moja kwa moja katika kutoa maoni yangu kuhusiana na mapungufu ya kiutawala ndani ya katiba iliyopo ambayo wananchi walikusudia kufanywa na sio mgogoro juu ya Muungano wetu ama serikali ngapi zinafaa kwa sababu kati ya wananchi walochangia sana mjadala huu wa katiba na kuufuatilia kwa ukaribu sana toka mwaka 2002 hapa JF mimi nilikuwa mmoja wapo.

Kwa mtazamo wangu, baada ya kutazama kwa kina malalamiko ya pande zote mbili ambazo zingependa sana kuishi pamoja kwa amini na utulivu lakini wameshindwa kufikia muafaka wowote juu ya Mustakabali wa taifa hili ndani ya UTAIFA huu imetokana na wote kushindwa kuingia ndani zaidi kutazama kiini cha matakwa ya wananchi bali wametumia siasa zaidi kupanua wigo la hoja za Muungano wenyewe jambo ambalo wangeweza kuwakilisha hoja hiyo katika vikao vya bunge na kadhalika pasipo kuathiri uandishi wa katiba tuitakayo. Hivyo nimekuja na mapendekezo ambayo nina hakika yatagusa hisia za wananchi wa sehemu zote za JMT ikiwa ni kuanza na muundo wa UTAWALA na mamlaka yake.

Ni imani yangu kwamba kutokana na hoja za pande mbili zote ambazo zimejikita zaidi ktk Muungano na serikali ukiwasoma kwa undani utagundua kwamba wanahitilafiana zaidi ktk kugawana MAMLAKA ya utekelezaji wa shughuli za serikali hivyo matatizo hayapo ktk aidha kwenye Muungano wenyewe ama idadi ya serikali. Lakini hata utawala huu umejaribu sana kuongeza hesabu za mikoa, wilaya na hata majimbo lakini kwa vile mabadiliko hayo hayatoi mamlaka kamili kwa vyombo vya serikali hizo ili kutekeleza majukumu yao na kuwajibishwa na wananchi, mabadiliko hayo hayakuleta mafanikio zaidi ama kupunguza kero za wananchi.

Hivyo katiba yetu bado inapwaya sana ktk kutoa mamlaka kwa wananchi na serikali, serikali na halmashauri zake kwa sababu bado mfumo mzima wa utawala wa nchi hii upo bado ktk mageuzi (transition) ya Kisiasa na kiuchumi na ilitakiwa hatua kwa hatua kuweza kufikia mageuzi kamili ikiwa KATIBA ya nchi yetu hii itabadilishwa na kutoa mamlaka hayo kwa vyombo vinavyostahili kuleta mabadiliko yanayokusudiwa. Sheria mama ndiyo dira na mwongozo wa mabadiliko yote na sii kutegemea muundo wa washirika ama idadi ya serikali ndizo hupelekea kupata maendeleo.

Hivyo kwa kuwa naamini kwamba mgogoro mkubwa wananchi wa pande zote mbili unahusiana na maslahi ya nchi hizo inaonyesha wazi kwamba katiba iliyopo ina mapungufu ambayo hayakomei ktk washirika wa muungano wa nchi hizi mbili bali mgogoro huo unashuka hadi ktk tawala za mikoa, wilaya na miji yake kwa madai ya kutopewa huduma bora kulingana na mahitaji yao. Mapungufu haya ya muda mrefu yamezua kero nyingi sana toka Halmashauri za mitaa, miji, wilaya, mikoa, serikali 2 hadi imefikia watu kutokuwa na imani na viongozi ama serikali zao kwa sababu ya muundo mzima wa Utawala wa nchi yetu ulijengwa ktk misingi ya Kijamaa.

Chama tawala kilikuwa na mamlaka yote ya kiutawala toka uchaguzi wa wajumbe wa nyumba kumi, viongozi wa halmashauri, wabunge, mawaziri, baraza kuu la Mawaziri (executive council), mahakimu, uteuzi wa viongozi wote wa taasisi serikali, mashirika ya umma, vyoombo vya serikali, vyama vya ushirika, uteuzi wa watendaji wakuu wa ngazi zote za serikali, nafasi za kazi kwa waajiriwa na kadhalika. Chama tawala pia kilikuwa ndicho chombo pekee kilichomiliki njia kuu za uchumi ambazo ni pamoja na Ardhi, maji, madini, misitu, mafuta, nguvu za umeme, usafiri, njia za habari, bishara za nje, mabenki, bima, viwanda vya chuma, silaha, simenti, mbolea, viwanda, ugawaji na mambo mengi makubwa ambayo kwa wakati ule ndio ilikuwa msingi mkubwa wa ujenzi wa UTAIFA wetu.

Haya yote ni mambo yalokuwa ktk siasa ya Ujamaa na Kujitegemea chini nya chama kimoja na haya hayawezi kuondoka kwa kubadilisha ushirika wetu iwe kwa kuvunja muungano ama kujadili idadi ya serikali zetu, ititiri wa vyama vya siasa na mahitaji yao bali yanahitaji mabadiliko makubwa ya katiba yetu ili Mamlaka hayo yote yapelekwe katika sehemu zinazohusika ili kurahisisha utekelezaji wa shughuli zote za serikali, taasisi na na vyombo vya kijamii ambavyo ndivyo pekee leo hii vinavyotakiwa kuwajibika ktk kushiriki katika kutoa huduma, haki na usawa wa jamii hii. Hatuwezi kuendelea na mfumo ule ule tukitegema kubadilika kwa serikali ndio muarobaini wa mapungufu makubwa ya kikatiba uwajibikaji na mamlaka ya vyombo vya utekelezaji.

Ni Imani yangu kwamba Watanzania wengi wameitaka katiba mpya ambayo italenga kuondoa mapungufu ya katiba yetu ya mwaka 1977. Wananchi wanaitaka katiba ambayo inayojitosheleza ktk maswala yote UTAWALA, KISIASA, KIJAMII na KIUCHUMI kulingana na mazingira ya dunia tuishiyo, hivyo basi

Napendekeza MUUNGANO na sio SHIRIKISHO uendelee kuwepo isipokuwa ktk sehemu ya kwanza ibara ya 4 (3) ya katiba ya JMT ya mwaka 1977 pamoja na rasimu ya katiba ya tume ya Warioba ziyaweke MAMBO YOTE YAWE YA MUUNGANO isipokuwa Ushuru wa bidhaa na mapato yasokuwa ya kodi kama liseni na sheria. Kwa kufanya hivo Serikali zetu, Manispaa, Mashirika ya Umma, na vyombo vya serikali kama TISS, NEC, na kadhalika yote yapewe mamlaka kamili ya kupanga Utekelezaji wa shughuli zao kama itakavyo ainishwa pasipo kuvunja masharti ya katiba na hivyo kuwajibika moja kwa moja na sheria mama ilotungwa kwa manufaa ya wananchi ili kukuza amani na utulivu.

Mambo yote yakiwa ya Muungano yataweza vipi kuondoa mapungufu na kufuta kero za wananchi? Hili nitalizungumzia baada ya kujibu hoja za wanabodi ambao watakuwa na haja ya kulizungumzia hili.

Nawasilisha


Invisible, Mzee Mwanakijiji, Kibunango, Pasco, Mdondoaji, lynxeffect22, JokaKuu Mag3 Mchambuzi Nguruvi3 Barubaru, Waberoya, AshaDii, Zakumi, Mama Mdogo, Ngongo, Nyamizi, Mimibaba, Katavi, bona, Janjaweed, zumbemkuu, TUJITEGEMEE, Mwelewa, MTAZAMO, amkawewe, gfsonwin, Englishlady, Sikonge, Mgaya D.W

ulafi wa madaraka utakuja watokea watu puani na kusababisha machafuko .... vile vichwa vya hekima vilivyoleta rasimu vilifanya utafiti sana kulingana na hali yetu ya sasa .... bado naona umehimu wa kufuata muundo uliopendekezwa na rasimu ya tume na kujikita katika kuimarisha madaraka ya serikali ya jamhuri wa muungano (hivi ndivyo serikali ya marekani na states zinazounda marekani zinazidi kushamiri kulinganisha na nchi nyingine duniani)
 
ulafi wa madaraka utakuja watokea watu puani na kusababisha machafuko .... vile vichwa vya hekima vilivyoleta rasimu vilifanya utafiti sana kulingana na hali yetu ya sasa .... bado naona umehimu wa kufuata muundo uliopendekezwa na rasimu ya tume na kujikita katika kuimarisha madaraka ya serikali ya jamhuri wa muungano (hivi ndivyo serikali ya marekani na states zinazounda marekani zinazidi kushamiri kulinganisha na nchi nyingine duniani)
Mkuu wangu hatushindani ila tunabadilishana mawazo. Hakuna kati yetu anayetaka madaraka kwa sababu hatupo ktk uongozi ngazi yoyote pengine wewe mwenzetu. Ila ningependa sana unieleze Utafiti upi waliufanya maana nijuavyo walikusanya maoni ya wananchi na wao wakatunga rasimu kutokana na maoni hayo au ilikuwa tofauti?

Hiyo Marekani uloitolea mfano ina mahusiano gani na mada hii pengine nifahamishe wapi nafanya makosa maana sikuelewi. Pili, unaweza kunambia hili swala la kuvunja Muungano (Union) na kuunda Shirikisho (federation) wamelipata wapi?

Nguruvi3,
Unaposema kuna jumla ya mambo 47 Je, unaweza kutuambia mambo hayo ni yapi maana sikuelewi kabisa? Mkuu maelezo ya kutoka mambo 11 hadi kufikia 22 yalielezwa wazi na JK ktk ufunguzi wa bunge la katiba hata mimi nilikuwa sijui ukweli ni upi kama hao walivyokuwa wakidai. Baada ya hapo kuna mambo yamewekwa wazi ikiwa ni pamoja na uhalali wa hati ya muungano haitakiwi kurudishana nyuma kuanza kubishana mambo yalokwisha pita. Hii luorodhesha mambo ya muungano ni makosa ikiwa hii ni nchi moja ambayo siku za baadaye likipatikana jambo jingine jipya tutaanza kupigizana makelele upya. Leo tuna fedha za sarafu na noti ikija kuwa smartchip card badala yake tutatoana macho upya!

Kisha nilikwisha kwambia toka zamani ya kwamba mimi sipingani na swala la serikali 3 za shirikisho bila kuvunja Muungano maana Muungano wetu ni Union kwa kidhungu na Shirikisho ni Federation hivyo swala la kuvunja muungano sio swala la uandikaji wa katiba bali ni swala tofauti kabisa na nje ya uandishi ni mkataba mpya ambao unahitaji Kura za wananchi (refendum) hii itakuwa kazi mpya na nyingine kabisa wakati tunaweza kuandika katiba mpya pasipo kuvunja mkataba wa kwanza.

Swala la Tanganyika, mkuu wangu labda niwaulize tena hivi.. je mnakumbuka miaka ya 60 early 80s tulikuwa tukibeba passport zetu kwenda Zanzibar? sasa kama Zanzibar haikuwa nchi kwa nini tuligongewa mihuri ya Entry na kutoka? Kama tulikuwa nchi moja kwa nini tulibeba passport? na Je, Uhamiaji ilikuwa ktk mambo ya Muungano ama? Nilikuuliza pia kule ukumbi wa GT ilikuwaje makamu wa rais hakuwa tena rais wa Zanzibar? yaani maswali yapo mengi sana ila mimi nafahamu tu ya kwamba baada ya kuwa na vyama vingi, mfumo ule wa Kijamaa na chama kimoja usingewezekana tena kwa sababu Mshindi wa Zanzibar anaweza kutoka chama kingine na sio chama tawala, unless Zanzibar iwe mkoa. Mimi sitaki kwenda huko lakini wewe kila siku wataka kunivuta kuhusu Tanganyika na Identity yake, mkuu wapo watu wengi hawaishi kwa majina yao halisi lakini hawajapungukiwa UTU wao hata kidogo.

Pili, Zanzibar walilazimika kutumia neno la rais wa Zanzibar kwa sababu wasingeweza kumwita Waziri mkuu kwa cheo sawa na Pinda maana kwao yule ni zaidi ya waziri mkuu hivyo Katiba yetu ya mwaka 1977 yenyewe ilikuwa na mapungufu mengi tu ambayo yalitakiwa kufanyiwa marekebisho toka tulipoingia Utandawazi na soko huria pamoja na demokrasia ya vyama vingi bila kuathiri katiba yao. Katiba ile ilikuwa na ilitengenezwa kwa manufaa ya CCM chama tawala na sio ya wananchi na ndio maana hatukuulizwa maoni yetu kuhusiana hata mabadiliko ya Mh. Mwinyi.
 
Mkuu Mag3 hili nanlo neno,unajua kuna makada wa CCM walikuwa wakimimina dhihaka tume ya Jaji Warioba wasijie tume ile ilifikia udhaifu mkubwa wa serekali ya Kikwete ambayo ilishindwa kuidhibiti Zanzibar ilipokuwa ikivunja katiba wazi wazi tena pasipo kificho.Ni ukweli usio na shaka kwamba baadhi ya mapendekezo ya tume ya Jaji Warioba yaliangalia ugumu wa kuipokonya Zanzibar mamlaka waliojinyakulia.

Kuna wakati najiuliza maswali mengi nakosa majibu hasa wale wanaolazimisha serekali mbili ikiwa wanajua wanachokipigania kinapingana na hali halisi.

Mkandara, hii ya kwako ni usanii at its best! Wazanzibari walikaa pamoja wakajadiliana kuhusu hatma yao na wakaamua kwa pamoja kujenga msingi imara utakaostahimili changamoto na mikiki mikiki iliyokuwa ikisababishwa na kero za Muungano wa serikali mbili katika nchi moja. Msingi huo imara, Katiba, ulipitishwa na Wazanzibari wote bila kujali itikadi, dini, rangi, jinsia wala kabila iliunda nchi ya Zanzibar ndani ya Muungano yenye mipaka na mamlaka ya juu yasiyoweza kuhojiwa na mamlaka yoyote nyingine ndani na nje ya Muungano. Katiba hiyo pia ilisisitiza kuwa haiwezi kufanyiwa marekebisho isipokuwa na Wazanzibari wenyewe kupitia vyombo vyao walivyojiwekea kulingana na maelekezo ya Katiba hiyo.

Mkandara, unaweza kutudokeza japo kidogo ni njia ipi itatumika kuhakikisha mambo yote yanakuwa ya Muungano bila kuathiri Katiba ya Zanzibar kama ilivyo sasa? Kumbuka kuwa pamoja na kuwa na Katiba ya Muungano bado Zanzibar peke yao waliweza kukaa, wakajadili na kupitisha Katiba inayopingana na ya Muungano na hakuna aliyewajibishwa. Kumbukumbu ziko kwamba hii ni hoja mojawapo iliyowapa wakati mgumu sana Tume ya Mabadiliko ya Katiba; sasa kama si mawazo ya kilaghai na kujaribu kuondoa watu kwenye hoja ya maana na ya msingi, naomba uwe mkweli utuambie mbinu gani ya kisheria itatumika kuwapokonya Wazanzibari haki yao ya Kikatiba ya kujiamulia mambo yao wenyewe...jeshi?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mag3 hili nanlo neno,unajua kuna makada wa CCM walikuwa wakimimina dhihaka tume ya Jaji Warioba wasijie tume ile ilifikia udhaifu mkubwa wa serekali ya Kikwete ambayo ilishindwa kuidhibiti Zanzibar ilipokuwa ikivunja katiba wazi wazi tena pasipo kificho.Ni ukweli usio na shaka kwamba baadhi ya mapendekezo ya tume ya Jaji Warioba yaliangalia ugumu wa kuipokonya Zanzibar mamlaka waliojinyakulia.

Kuna wakati najiuliza maswali mengi nakosa majibu hasa wale wanaolazimisha serekali mbili ikiwa wanajua wanachokipigania kinapingana na hali halisi.
Mkuu wangu nadhani nyote humu mumewahi kuishi nje, nawaomba sana nambieni moja tu. Ni nchi gani ya kidemokrasia ndani ya Muungano ambayo haina mamlaka walojichukulia Zanzibar.

Pili, hili swala la nchi mbili zilizoungana kuunda nchi moja halafu nchi hiyo ikawa na mambo yasokuwa ya Muungano, wakawa wawili tena! Kusema kweli mimi hunipa taabu zaidi kuelewa kuliko nyie, Ebu nifahamisheni na mjadala utakuwa mzuri zaidi ikiwa mtakuwa mnanipa majibu ya hoja zangu maana mimi pia napenda kujifunza kile mnachokijua nyie pengine sikuelewa msingi wa kufanya hivyo. Tujifunze kutafuta solution ya changamoto hizi badala ya kuongeza maswali.
 
Kwanini mambo yote yawe ya Muungano

Kufuatia mgogoro uliopo baina ya pande mbili za kisiasa kushindwa kufikia muafaka juu ya muundo wa serikali ningependa kusema tatizo la nchi yetu lipo ndani zaidi ya swala la idadi ya serikali zetu iwe 1, 2 au 3 kwa sababu serikali huundwa kwa minajiri ya kugawana mamlaka ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Na ifahamike tu kwamba hakuna muundo maalum wa serikali ziwe ngapi ktk mfumo wa washirika ktk utawala wowote iwe ule wa Muungano (union), Shirikisho (federation), Jumuiya (Confederation/Community) kwa sababu ushirika haujengwi kwa idadi ya serikali bali hali halisi ya matakwa ya wananchi ktk ushirika wao kwa masharti na malengo walotaka kuyafikia ndio hujengwa serikali zake ili kuwafikia wananchi haraka na wepesi zaidi.

RED: Kulingana na hoja za wanaJF na za kwako pia , ninadhani umeona mwenyewe kuwa ni vigumu kujadili suala la Katiba Mpya na masuala ya muungano bila kujadili muundo wa muungano na idadi ya serikali kwenye huo muungano.

Ni kweli mambo yote yakiwa ya muungano (muungano ulioridhiwa na pande zote mbili Tanzania Bara na Tanzania Visiwani) kikweli kweli, suluhu itapatikana. Lakini ilikufikia suluhu hii lazima kasoro zote zilizoanzia kwenye 'article of Union', katiba ya JMT toka 1964, 1977, marekebisho ya katiba ya Zanzibar 1982, na yale ya 2010 zipatiwe ufumbuzi kupitia mjadala wa sasa Bunge maalumu la Katiba (BMLK). Na wale, ambao wapo hai, waliohusika (ama kwa makusudi ama bila kukusudia) kusababisha kasoro hizo wakiri kuwa walikosea na waruhusu mjadala wa rasimu ya katiba iliyowasilishwa kweye BMLK uendelea bila vikwazo.

Kama ni vigumu kuendelea na mjadala huo kwenye BMLK (kuvunja mchakato mzima wa sasa wa kupata katiba mpya), basi rasimu ya Tume ya Warioba na maelezo aliyotoa wakati akiwasilisha rasimu hiyo Bungeni vitumike kama rejeo (reference) muhimu kufikia muafaka wakupata katiba mpya kwa utaratibu mwingine utakaopendekezwa. Utaratibu huo lazima uhusishe kuhoji wananchi kama wanataka muungano, na muungano wa muundo gani, wenye serikali ngapi kabla ya kuamua kutunga katiba mpya.
 
Usiwe na upeo wa leo tu, angalia mbali katika haya mambo ya katiba. Je siku za usoni kutakapotokea matatizi kati ya Tanganyika na Zanzibar ambayo katiba inabidi itumike ili kufikia makubaliano unadhani Wazanzibar watakubali katiba yao isitumike na badala yake itumike katiba ya Muungano!? Wazanzibar hawakuwa wajinga pale walipombwa kubadili katika yao ya 2010 na kukataa kata kata kufanya hivyo maana wanajua fika ipo siku katiba yao wataitumia katika kufikia muafaka wa matatizo ya kikatiba kati ya Tanganyika na Zanzibar bilaujali kama watakaokuwa Viongozi wakati huo wataafiki au la. Na hapa ndio utaona umuhimu wa kuwa na katiba yenye kuruhusu Serikali tatu.


Mag3,
Mkuu hakuna maneno mengi ila tuzungumzie facts, Kwani hiyo katiba ya Zanzibar inatukwaza nini haswa? Toka wameandika ni shughuli gani za serikali ya Muungano imeshindwa kuzitekeleza kama zamani?
 
Kwangu mimi naamini serikali moja ndiyo jibu la matatizo yote ikiwa tu wananchi wataridhia. Ila wasiwasi na pia jinsi maoni ya waZnZ wengi alivyo hawatakubali kuwa na nchi moja maana yake Zanzibar inakuwa mkoa au jimbo. Mwisho issue ya aina ya Muungano ndio inaamua mifumo yote ya utawala na matumizi ya rasilimali kwa hiyo ni vizuri referundum kwanza bila kuleta uchakachuzi.
 
Mkandara asante sana kwa bandiko zuri lililojaa uchambuzi yakinifu.............

mie nina swali moja tu kwako, ivi kama Zanzibar mambo haya 22 yaliyoko kwenye Muungano kwa sasa, hawayataki na mpaka apo wameyaongeza kuwa 47 yanaleta utata je tukifanya yote yawe ya muungano unafkiri kitakubalika??

ivi je kuna shida gani basi kukawa kuna S3 labda na rais mmoja ila mawaziri wakuu wa 3 nikiwa na maana kwamba kila serikali iwe na waziri mkuu wake??

na je hatuon ili kukata mzizi wa fitina basi ni afadhal kuirudisha Tanganyika yetu, na Zanzibar ikawepo kisha tukawa na serikal ya Muungano?? at least ikawepo fareness kwenye distribution ya resources?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wangu hatushindani ila tunabadilishana mawazo. Hakuna kati yetu anayetaka madaraka kwa sababu hatupo ktk uongozi ngazi yoyote pengine wewe mwenzetu. Ila ningependa sana unieleze Utafiti upi waliufanya maana nijuavyo walikusanya maoni ya wananchi na wao wakatunga rasimu kutokana na maoni hayo au ilikuwa tofauti?

Hiyo Marekani uloitolea mfano ina mahusiano gani na mada hii pengine nifahamishe wapi nafanya makosa maana sikuelewi. Pili, unaweza kunambia hili swala la kuvunja Muungano (Union) na kuunda Shirikisho (federation) wamelipata wapi?

mkuu kama ulimsikiliza warioba vizuri...hawakufanya kazi ya kukusanya tu maoni na takwimu ... walifanya utafiti pia, waliangalia zile takwimu, waliangalia nchi nyingine duniani, waliangalia hoja zote kinzani, etc. .... ndio wakajaribu kutafuta compromise kutuepusha na hatari iliyoko mbele yetu .... kwa kifupi zanzibar muungano hawautaki!! ... serikali ya zanzibar ina survive kwa sababu ya nguvu kubwa inayoilinda kutoka bara

narudia tena maneno ya warioba kama tunataka kudumisha muungano wa nchi hizi mbili hatuna budi kwenda serikali tatu na kuimarisha madaraka na nguvu ya serikali ya muungano .... mimi sio mwanasheria ila ukiangalia muundo unaopendekezwa na rasimu ni kama muundo wa serikali ya marekani (constitutional republic) ... pia utambue sherikisho pia ni aina ya muungano!

na nasikitika sana na upotoshaji unaofanyika na CCM na vyombo vya habari vilivyopewa vibahasha .... hakuna sehemu rasimu imependekeza kuvunja muungano! .... rasimu imependekeza kuimarisha muungano kwa kubadilisha tu form ya governement kutoka muundo wa united republic (ambao unafanana sana na uingereza sema wao wako chini ya queen [united kingdom]) kwenda kwenye federation ambao unafanana na marekani, ujerumani, uswisi kwa ukaribu zaidi .... katika muundo huu nchi washirika hupewa nguvu za kujiamulia mambo yake ya ndani huku serikali kuu ya muungano ikibakia kusimamia mambo ya kidola kama ulinzi na usalama, mambo ya nje, etc ....

mimi ningekushauri soma zaidi kuhsu american government kisha ulinganishe na kinachopendekezwa na rasimu! ..... marekani kuna magavana 50 wanaosimamia states ila sijawahi kusikia hata mtu mmoja akilalamika sijui marais wengi ... ni kwa sababu wamejiwekea utaratibu mzuri tu wa uwajibikaji ... serikali za states ni ndogo na hata federal government ni ndogo sana (na idadi iko kikatiba) ila departments mbali mbali ndio nyingi kulingana na mahitaji ... hawa wawakilishi wangekua makini wangejikita kwenye maboresho hayo kama kulimit idadi ya wizara, kuhakikisha viongozi wa nchi washirika wanaitwa tu magavana na wana serikali ndogo kadri wanavyojiamulia, kuimarisha makusanyo ya kodi, etc ..... na mimi kwa kuperuzi tu sijaona tatizo lolote kwenye american government kama hayo tunayotishwa na CCm yatatokea tukihamia serikali tatu .... ni kuwa na uwazi, uwajibikaji na utawala wa sheria tu!

naungana na wale wote walioona serikali ya CCM ilikua na nia mbaya na huu mchakato ... haya maswali mengi yanayoibuka yanakosa ufafanuzi ni kwa sababu serikali ilivunja tume na kufunga hadi website ya tume ili wananchi na wadau wengine wasipate access ya taarifa mbali mbali ambazo tume ilizichapisha na kuzitumia kuandaa rasimu .... matokeo yake ni kuwa na wawakilishi wengi hasa wa CCm waliokakarishwa tu cha kusema bila kuhoji wala kujua chimbuko la walichoambiwa kutetea .... hata machapisho walifanya makusudi hawakugawa taarifa zote kwa kila mjumbe wa bunge la katiba ..... MISINFORMATION ni tatizo kubwa sana kwa Tanzania kwa sasa

kama walivyoshauri wengine hapo juu .... hatua sahihi ni kwa bunge la katiba kuvunjwa ... wananchi waulizwe kama wanautaka muungano na kama jibu ni ndio waulizwe wanataka muungano wa serikali ngapi! ... baada ya hapa ndio katiba itungwe kutokana na matakwa ya wananchi .... inasikitisha sana CCM wanaposema takwimu za tume zilizopendekeza serikali tatu ni ndogo ila hawaelezi wao wanangangania serikali mbili kwa takwimu zipi?
 
Mkandara asante sana kwa bandiko zuri lililojaa uchambuzi yakinifu.............

mie nina swali moja tu kwako, ivi kama Zanzibar mambo haya 22 yaliyoko kwenye Muungano kwa sasa, hawayataki na mpaka apo wameyaongeza kuwa 47 yanaleta utata je tukifanya yote yawe ya muungano unafkiri kitakubalika??

ivi je kuna shida gani basi kukawa kuna S3 labda na rais mmoja ila mawaziri wakuu wa 3 nikiwa na maana kwamba kila serikali iwe na waziri mkuu wake??

na je hatuon ili kukata mzizi wa fitina basi ni afadhal kuirudisha Tanganyika yetu, na Zanzibar ikawepo kisha tukawa na serikal ya Muungano?? at least ikawepo fareness kwenye distribution ya resources?
Shuukran sana kwa maswali haya maana naona watu wote hapa wanaishambulia Zanzibar kama vile wao ndio wakosa. lakini ukweli ni upi? Nakuombeni sikilizeni hotuba ya makamu wa rais wa Zanzibar mwaka 2011 wakati wa maandimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tangayika ambayo wengi tunajiuliza iko wapi, lakini hawa hawa wanataka Muungano. Jamani mwee, tumetumia katiba ya Tanganyika kwa miaka 50 ya muungano na hata wimbo wetu wa Taifa ni wa Tanganyika lakini tunachokiona ni Wazanzibar ndio tu wakosa kutaka mabadiliko kwa upande wao, bado tunataka kuipa Tanganyika mkono wa juu ilihali sasa hivi tupo ktk mfumo wa demokrasia ambao lazima kwanza tuepuke mgawanyiko.

Mimi sielewi kuhusu hayo mambo ya Muungano yamefikia 47 kusema kweli ndio kwanza nasikia hapa. Ningeomba msaada wenu kuyafahamu na kama haya ndio msingi wa malalamiko na kero za Muungano maana kero hizo nimezi orodhesha hapo nyuma na kati ya kero hizo Wazanzibar wameuliza mabadiliko ya katiba ya Jamhuri toka mambo ya Muungano 11 hadi kufikia 22 sijaona mahala yakisemwa ni 47. Wazanzibar na sisi sote hatujawahi kuambiwa sababu gani mambo yaliongezeka kufikia 22. Ku question hilo ni wajibu wetu sote japo ilifikia kuwa kero kwa Wazanzibar tusiwalaumu ni haki yao na yetu sote kujua. It is understandable kwa sababu walojua mabadiliko haya ni viongozi tu walokuwa madarakani katika Utawala wa CCM jambo ambalo nasema bado tunaendelea na mfumo wa chama kimoja na hivi sasa zanzibar CUF ina nguvu kubwa ya ushawishi hivyo swala hili likawa blown up kufikia kutafsiri ya kuwa bara na CCM lao moja.

Ni majuzi tu JK katika hotuba yake ya ufunguzi wa bunge maalum la Katiba ametueleza sote sababu zake na kwamba viongozi wa wetu (CCM na baraza la Mapinduzi) walifikia maamuzi hayo kutokana na kuvunjika kwa Jumuiya ya EAC, hatukuyajua sote. Hivyo hata katiba ya Zanzibar ya mwaka 1982 na mwaka 2010 zilifanyiwa marekebisho na kuandikwa upya kichama na ndio maana sisi tunalalamika maana hatukuhusishwa. Hivyo maadam baadhi ya majibu yametolewa na hakuna tena malalamiko ya mambo ya Muungano kufikia 22 sidhani ila kuitafuta njia bora zaidi. Na Warioba na Salim wanamlalamikia JK ya kwamba aliyafahamu yote haya lakini hakuwapa ushauri wake wakati wakiandaa rasimu hii ya katiba mpya.

JK pia hakuwapa mchango wake juu ya serikali ya Muungano kuwa na mambo 7 itakuwa dhoofu na haiwezi kusimamia shughuli zake kwa kutokuwa na vyanzo vya kutosha. To me they should have known that kutokana na experience zao maana hili hata miye hapa nililiona. Hii ina maana JK ana stripe the all idea ya kuwa na mambo ya Muungano machache, na kwamba yale mambo 22 ya Muungano yaliingizwa sio kinyelmela bali kwa sababu ya Usimamizi wake maana Zanzibar (CCM) haikuwa tayari wala haikuwa nje ya Muungano wetu wa nchi moja (chama kimoja). Katiba ya JMT ni katiba ya Tanu (Tanganyika) na ndio tunayoitumia muda wote lakini sisi hatuyaoni ya humo kuwa ni kinyume ila ni yetu sote wakati nayo ilibadilishwa.

Hivyo sio kwamba hawataki MAMBO YOTE YAWE YA MUUNGANO ama hawataki yale mambo 22 yawe ya Muungano isipokuwa baada ya kutokuwa na majibu kwa muda mrefu yalikuwa kero kwao maana tulivunja kanuni za makubaliano ya awali kuingiza mambo ambayo hayakuwepo. Hili sisi hatukubali japo ukweli ni kwamba Usiri wa chama na serikali ya Muungano bado wanatumikia sera za muungano wa vyama kuunda CCM, hivyo kuna mengi ambayo yalitakiwa kuwa wazi kwa waanchi wote leo hii lakini bado ni siri ya chama wakitumia neno Taifa. Ndio kusema siri zote za Taifa ni siri za CCM hivyo ili kuondoa usiri huo na kupata serikali ya Jumuiya ya watu na sio chama tunatakiwa mambo yote yawe na Muungano na hakuna usiri tena.

Ndio maana nasema hivi sioni sababu ya Zanzibar kupinga isipokuwa kuna uwezekano mkubwa pingamizi kutoka Bara na hasa CCM kutokana na usiri wa mambo yake maana hata Hati ya Muungano ilikuwa ni siri ya chama cha TANU na ASP hakuna sababu nyingine, hivyo yawezekana JK na serikali yake walilazimika kuvunja code of conduct ya muungano baina ya TANU na ASP kuonyesha hati hiyo kwani haikuwa swala la wananchi bali utawala ktk fikra za kuunda umoja wa nchi za Afrika. Na bila shaka huu ni mwanzo mzuri wa kuweka vitu vyote wazi ili kuondosha nguvu ya usiri wa chama CCM kuwa ndiye mdhamini wa Utaifa wetu.

Hakuna shida yoyote ya kuwa na serikali 3 isipokuwa kuna utaratibu wake kisheria. nao ni wananchi wenyewe kwanza wakubali kwa kupiga kura wanataka serikali 3. hatuwezi kuandika Katiba yenye serikali 3 pasipo ridhaa ya wananchi kwa sababu katiba Mpya ikisha andikwa ya serikali 3 kisha wananchi wakaikataa mwishoni ina maana katiba nzima itakuwa haifai. Swala la Shirikisho pia kama wananchi watalikataa basi katiba nzima itakuwa haifai maana ikumbukwe tu tunaweza kufanya mabadiliko ya mambo ya muungano, mamlaka yake, shughuli zake na sheria pasipo kuathiri katiba yote, lakini hatuwezi kubadilisha serikali wala aina ya Muungano pasipo kuathiri katiba yote pindi ikikataliwa na wananchi. Na kama sikosei moja ya masharti walopewa tume ya Warioba toka mwanzo ni kutozungumzia Muungano.

Pili, serikali 3 ina maana kuzaliwa kwa Tanganyika hivyo ni lazima kwanza Tanganyika izaliwe, iunde katiba yake, bunge lake, na wawakilishi wake ili mjadala wa katiba mpya uwe na wawakilishi toka pande mbili za Muungano. Hawa wajumbe waliopo hapo ni wajumbe wa Muungano huu tulokuwa nayo leo, hivyo katiba inayoandikwa ni katiba ya Muungano tulonao leo sio Shirikisho ama serikali 3. Hakuna mjumbe yoyote katika baraza hilo anawakilisha Tanganyika na wala hatuna msimamo wa pamoja kisheria isipokuwa vyama vya siasa hivyo kuitaka serikali 3 ni kinyume cha uandishi wa katiba mpya.

Kwa hiyo kama tutakubaliana kuunda serikali 3 ina maana tulivunje bunge hili kwanza, izaliwe Tanganyika ambayo itachagua wajumbe wake kuiwakilisha ktk uandishi wa katiba mpya kwa sababu huwezi kuandika katiba ya nchi ama shirikisho ambalo halipo. Tunaandika katiba mpya ya ushirika tulokuwa nao leo na serikali tulizokuwa nazo leo na sii vinginevyo. otherwise itatulazimu tuuvunje muungano huu kwanza Tangayika uzaliwe na waulizwe wanataka ushirika gani na Zanzibar maana hili la Shirikisho ni makubaliano ya Wazanzibar wote kulingana na katiba yao lakini bara hatukufikia muafaka huo.

Kurudishwa kwa tanganyika kutaondoa tu dhana ya contribution na distribution ya resoures kwa wale wasiotaka kuumiza vichwa maana tumezoea kuona 1+8 = 9. yaani Zanzibar wakiweka 1 nasi tukaweka 9 lazima jibu litakuwa 9 lakini hatuwezi devision theory ya kwamba 9-1=?. Ikiwa mfuko wa Muungano unazo 9 na Zanzibar wamechangia 1 basi bila shaka 8 ni za bara. Tatizo jingine la michango yetu inatukanganya ni kuwepo kwa tofauti kubwa ya Population zanzibar wakiwa na 1.3 mil wakati bara ina watu mil 45. Mchango wa nchi hizi unatakiwa uwe vipi ili iwe fair kwa pande mbili za muungano? Sasa Kwa Wazanzibar wanapoona wanapewa only 4.5 ya pato la taifa wanauliza kulikoni bara ibakie na 95.5, nasi bara tunauliza iweje tuwe na Trillion 100, Zanzibar wachangie only bil. 300 halafu waseme tugawane sawa! Usawa huu ni upi?

Kwangu binafsi nachoelewa ni Wazanzibar kutotaka kufananishwa na Mikoa wa bara ama kuwa chini ya mkoa yaani wao kama nchi ya Muungano kupewa kidogo kuliko mkoa wa Tanzania bara. Hii inatokana na ukweli kwamba serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano imejikita zaidi ktk recurrent expenditures na ndiko kila kiongozi macho yake yanamtoka kuona amepewa ngapi za kutumia na ukubwa wa serikali yake.

Ugonvi mkubwa ni matumizi makubwa ya serikali hizi kiasi kwamba mambo ya Maendeleo yamewekwa pembeni kabisa. lakini ikiwa tutaweka mfumo mzuri wa michango ya maendeleo na mgao wake hatuhitaji kuwa na 1+8=9 bado tunaweza pata jibu tuliwa na 9-1 bila kupewe jibu as long as tutaepuka matumizi makubwa na mabaya ya serikali zetu kwa kuweka mambo yote kuwa ya Muungano. Ila ili kupata uwakilishi mzuri liundwe baraza la wawakilishi wa bara na visiwani lenye idadi ya wajumbe sawa kutoka bara na visiwani (say 25 kila upande) ktk kupitsha sheria na bajeti ya zilizopitishwa ba Bunge kabla ya kupelekwa kwa rais kusainiwa na kuwa act.
 
TUJITEGEMEE BAK lynxeffect22.. Nitawarudia baadaye kujibu ama kuchagia hoja zenu ila nawaomba tu msome kwa makini kazi na majukumu ya ofisi ya makamu wa rais kisha mjiulize mamlaka ya uratibu wa ofisi hiyo (bofya) yamezingatiwa kwa kiasi gani ktk ukusanyaji wa maoni na wananchi na utafiti wa tume ya Warioba. Na je rais aliyoyasema yametoka mdomoni mwake ama ni mkusanyiko wa mawazo ya watawala. Nawaomba tu mfahamu ya kwamba sio kila jambo walofanya CCM (Tanu na ASP) lilikuwa baya kwetu, bali tutazame malengo yake yalikuwa kwa faida ya chama au wananchi wa JMT na tupiganie kuondosha yale yalohofiwa kuhatarisha uhai wa chama hicho ambayo leo hayapo tena na sio Utaifa wetu kama jamii moja.
 
Mkandara,

Nitapita hapa baadayn kwani nimeguswa sana na mada hii adhimu kabisa ila kwa sasa nimebanwa kidogo na shughuli za kikazi LAKIN NIKINAFASIKA NITAPITA TENA KWANI NINA MENGI SANA YA KUCHANGIA HAPA.

Ahsantum kwa mada maridhawa na adhiim sana
 
Kwangu mimi naamini serikali moja ndiyo jibu la matatizo yote ikiwa tu wananchi wataridhia. Ila was iwasi na pia jinsi maoni ya waZnZ wengi alivyo hawatakubali kuwa na nchi moja maana yake Zanzibar inakuwa mkoa au jimbo. Mwisho issue ya aina ya Muungano ndio inaamua mifumo yote ya utawala na matumizi ya rasilimali kwa hiyo ni vizuri referundum kwanza bila kuleta uchakachuzi.

Wazanzibar waliowengi wangependa serikali moja ila wanashurutishwa (kwa ghiliba za kuwa tukiwa na nchi moja Zanzibar itamezwa ) na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa na pia baadhi ya viongozi walioko kwenye serikali ya SUK. Hakuna mahali ambapo nimesikia viongozi hao niliowasema juu waliposimama kwenye mikutano ya hadhara wakawaambia wazanzibar kuwa kuna umuhimu wa kuwa na serikali moja ya jamuhuri ya watu wa Tanzania(Tanganyika na Zanzibar) wakapigwa mawe, zomewa nakadhali, hakuna...!!!

Ukiwahoji tu wanasema ... tu ...wazanzibar hawatakubali....! Najua mwaweza kuuliza kuwa hiki ninachokisema mbona hakikujionyesha kwenye takwimu za tume ya Jaji Warioba. Hakikujitokeza kwa sababu ...hakukuwa na dodoso elekezi la kutafuta maoni hayo.
 
Back
Top Bottom