Katiba Mpya: Mambo yote yawe ya Muungano

Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
MAONI KUHUSU KATIBA MPYA

Kwanini mambo yote yawe ya Muungano

Kufuatia mgogoro uliopo baina ya pande mbili za kisiasa kushindwa kufikia muafaka juu ya muundo wa serikali ningependa kusema tatizo la nchi yetu lipo ndani zaidi ya swala la idadi ya serikali zetu iwe 1, 2 au 3 kwa sababu serikali huundwa kwa minajiri ya kugawana mamlaka ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Na ifahamike tu kwamba hakuna muundo maalum wa serikali ziwe ngapi ktk mfumo wa washirika ktk utawala wowote iwe ule wa Muungano (union), Shirikisho (federation), Jumuiya (Confederation/Community) kwa sababu ushirika haujengwi kwa idadi ya serikali bali hali halisi ya matakwa ya wananchi ktk ushirika wao kwa masharti na malengo walotaka kuyafikia ndio hujengwa serikali zake ili kuwafikia wananchi haraka na wepesi zaidi.

Mgogoro wa kisiasa
Sintojikita ktk mgogoro wa kisiasa ulofuatia bunge maalum la katiba kuvunjika kwa sababu huo ni mjadala mrefu sana pengine tutaugusia pale inapopaswa isipokuwa nitakwenda moja kwa moja katika kutoa maoni yangu kuhusiana na mapungufu ya kiutawala ndani ya katiba iliyopo ambayo wananchi walikusudia kufanywa na sio mgogoro juu ya Muungano wetu ama serikali ngapi zinafaa kwa sababu kati ya wananchi walochangia sana mjadala huu wa katiba na kuufuatilia kwa ukaribu sana toka mwaka 2002 hapa JF mimi nilikuwa mmoja wapo.

Kwa mtazamo wangu, baada ya kutazama kwa kina malalamiko ya pande zote mbili ambazo zingependa sana kuishi pamoja kwa amini na utulivu lakini wameshindwa kufikia muafaka wowote juu ya Mustakabali wa taifa hili ndani ya UTAIFA huu imetokana na wote kushindwa kuingia ndani zaidi kutazama kiini cha matakwa ya wananchi bali wametumia siasa zaidi kupanua wigo la hoja za Muungano wenyewe jambo ambalo wangeweza kuwakilisha hoja hiyo katika vikao vya bunge na kadhalika pasipo kuathiri uandishi wa katiba tuitakayo. Hivyo nimekuja na mapendekezo ambayo nina hakika yatagusa hisia za wananchi wa sehemu zote za JMT ikiwa ni kuanza na muundo wa UTAWALA na mamlaka yake.

Ni imani yangu kwamba kutokana na hoja za pande mbili zote ambazo zimejikita zaidi ktk Muungano na serikali ukiwasoma kwa undani utagundua kwamba wanahitilafiana zaidi ktk kugawana MAMLAKA ya utekelezaji wa shughuli za serikali hivyo matatizo hayapo ktk aidha kwenye Muungano wenyewe ama idadi ya serikali. Lakini hata utawala huu umejaribu sana kuongeza hesabu za mikoa, wilaya na hata majimbo lakini kwa vile mabadiliko hayo hayatoi mamlaka kamili kwa vyombo vya serikali hizo ili kutekeleza majukumu yao na kuwajibishwa na wananchi, mabadiliko hayo hayakuleta mafanikio zaidi ama kupunguza kero za wananchi.

Hivyo katiba yetu bado inapwaya sana ktk kutoa mamlaka kwa wananchi na serikali, serikali na halmashauri zake kwa sababu bado mfumo mzima wa utawala wa nchi hii upo bado ktk mageuzi (transition) ya Kisiasa na kiuchumi na ilitakiwa hatua kwa hatua kuweza kufikia mageuzi kamili ikiwa KATIBA ya nchi yetu hii itabadilishwa na kutoa mamlaka hayo kwa vyombo vinavyostahili kuleta mabadiliko yanayokusudiwa. Sheria mama ndiyo dira na mwongozo wa mabadiliko yote na sii kutegemea muundo wa washirika ama idadi ya serikali ndizo hupelekea kupata maendeleo.

Hivyo kwa kuwa naamini kwamba mgogoro mkubwa wananchi wa pande zote mbili unahusiana na maslahi ya nchi hizo inaonyesha wazi kwamba katiba iliyopo ina mapungufu ambayo hayakomei ktk washirika wa muungano wa nchi hizi mbili bali mgogoro huo unashuka hadi ktk tawala za mikoa, wilaya na miji yake kwa madai ya kutopewa huduma bora kulingana na mahitaji yao. Mapungufu haya ya muda mrefu yamezua kero nyingi sana toka Halmashauri za mitaa, miji, wilaya, mikoa, serikali 2 hadi imefikia watu kutokuwa na imani na viongozi ama serikali zao kwa sababu ya muundo mzima wa Utawala wa nchi yetu ulijengwa ktk misingi ya Kijamaa.

Chama tawala kilikuwa na mamlaka yote ya kiutawala toka uchaguzi wa wajumbe wa nyumba kumi, viongozi wa halmashauri, wabunge, mawaziri, baraza kuu la Mawaziri (executive council), mahakimu, uteuzi wa viongozi wote wa taasisi serikali, mashirika ya umma, vyoombo vya serikali, vyama vya ushirika, uteuzi wa watendaji wakuu wa ngazi zote za serikali, nafasi za kazi kwa waajiriwa na kadhalika. Chama tawala pia kilikuwa ndicho chombo pekee kilichomiliki njia kuu za uchumi ambazo ni pamoja na Ardhi, maji, madini, misitu, mafuta, nguvu za umeme, usafiri, njia za habari, bishara za nje, mabenki, bima, viwanda vya chuma, silaha, simenti, mbolea, viwanda, ugawaji na mambo mengi makubwa ambayo kwa wakati ule ndio ilikuwa msingi mkubwa wa ujenzi wa UTAIFA wetu.

Haya yote ni mambo yalokuwa ktk siasa ya Ujamaa na Kujitegemea chini nya chama kimoja na haya hayawezi kuondoka kwa kubadilisha ushirika wetu iwe kwa kuvunja muungano ama kujadili idadi ya serikali zetu, ititiri wa vyama vya siasa na mahitaji yao bali yanahitaji mabadiliko makubwa ya katiba yetu ili Mamlaka hayo yote yapelekwe katika sehemu zinazohusika ili kurahisisha utekelezaji wa shughuli zote za serikali, taasisi na na vyombo vya kijamii ambavyo ndivyo pekee leo hii vinavyotakiwa kuwajibika ktk kushiriki katika kutoa huduma, haki na usawa wa jamii hii. Hatuwezi kuendelea na mfumo ule ule tukitegema kubadilika kwa serikali ndio muarobaini wa mapungufu makubwa ya kikatiba uwajibikaji na mamlaka ya vyombo vya utekelezaji.

Ni Imani yangu kwamba Watanzania wengi wameitaka katiba mpya ambayo italenga kuondoa mapungufu ya katiba yetu ya mwaka 1977. Wananchi wanaitaka katiba ambayo inayojitosheleza ktk maswala yote UTAWALA, KISIASA, KIJAMII na KIUCHUMI kulingana na mazingira ya dunia tuishiyo, hivyo basi

Napendekeza MUUNGANO na sio SHIRIKISHO uendelee kuwepo isipokuwa ktk sehemu ya kwanza ibara ya 4 (3) ya katiba ya JMT ya mwaka 1977 pamoja na rasimu ya katiba ya tume ya Warioba ziyaweke MAMBO YOTE YAWE YA MUUNGANO isipokuwa Ushuru wa bidhaa na mapato yasokuwa ya kodi kama liseni na sheria. Kwa kufanya hivo Serikali zetu, Manispaa, Mashirika ya Umma, na vyombo vya serikali kama TISS, NEC, na kadhalika yote yapewe mamlaka kamili ya kupanga Utekelezaji wa shughuli zao kama itakavyo ainishwa pasipo kuvunja masharti ya katiba na hivyo kuwajibika moja kwa moja na sheria mama ilotungwa kwa manufaa ya wananchi ili kukuza amani na utulivu.

Mambo yote yakiwa ya Muungano yataweza vipi kuondoa mapungufu na kufuta kero za wananchi? Hili nitalizungumzia baada ya kujibu hoja za wanabodi ambao watakuwa na haja ya kulizungumzia hili.

Nawasilisha

Invisible, Mzee Mwanakijiji, Kibunango, Pasco, Mdondoaji, lynxeffect22, JokaKuu Mag3 Mchambuzi Nguruvi3 Barubaru, Waberoya, AshaDii, Zakumi, Mama Mdogo, Ngongo, Nyamizi, Mimibaba, Katavi, bona, Janjaweed, zumbemkuu, TUJITEGEMEE, Mwelewa, MTAZAMO, amkawewe, gfsonwin, Englishlady, Sikonge, Mgaya D.W
 
Last edited by a moderator:

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
38,974
2,000

Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Mkuu Mkandara, nakushukuru kwa maoni haya, mimi nilishauri Katiba: Nashauri Bunge Lililopo Livunjwe!

Ila kwa upande wa muundo wa serikali, nilishauri https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...uungano-then-twende-kwenye-serikali-moja.html

Pasco
Shukran lakini kabla sijaendelea nilitaka kukujibu tu ya kwamba swala la serikali ngapi sio hoja kabisa kwa sababu haliondoi mapungufu ya utendaji na kero zake bali litazidisha kero hizo. Kwa mfano tukikubali serikali moja Hoja ya Tanganyika kuimeza Zanzibar litakamilika, kwani Zanzibar hako ka nchi kadogo huru wanavyodai wenyewe, haitakuwa na serikali yake, haitakuwa na bunge lake wala mahakama yao, haitakuwa na viongozi wake isipokuwa uongozi kama wa mkoa jambo ambalo linavunja mkataba wa kwanza wa Muungano. Kero zake zitafika hadi mbinguni!

Pili, swala la serikali ngapi ni swala la wananchi kupigia kura (referendum) kuchagua NDIO ama HAPANA na sio kupitia kukusanya maoni ya wananchi. kama ingekuwa rahisi hivyo basi kwa nini hata rais na wabunge tusiwachague kwa maoni ya wananchi? haiwezekani sio na ndivyo ilivyo ktk swala zito kama Muundo wa serikali japo muundo huo ulitungwa enzi hizo. Hoja kama hii ilitakiwa kupelekwa kama muswada Bungeni na kama ungepita basi kura zingepigwa aidha Zanzibar tu ama JMT kwa sababu kuna mapendekezo matatu makubwa.
 
MrFroasty

JF-Expert Member
Jun 23, 2009
1,060
1,500

Hapo kwenye bold panashangaza kwamba umegundua kama utavunja mkataba wa kwanza muungano.Sasa kuingiza mambo yote kwenye muungano itakuwa unafanya nini?

Nadhani unajidanganya kusema wananchi wote wanataka kuendelea na muungano, na kwa ushahidi gani ? Mie mmoja naamini kwa ushahidi wa kisanyansi kuwa muungano uliopo hauna nia ya dhati ya kuwaletea wananchi maendeleo ya aina yoyote hususan yale ya kiuchumi.

Motivation ya kuundwa kwake ilijikita zaidi na hoja kama za akina Lukuvi, zina chembe za udikteta wa kikristo chungu tele!
 
Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
14,428
2,000
Mkandara na Pasco mnaweza kuwa na mawazo mazuri sana kuhusiana na Katiba Mpya na hali ilivyo kwa sasa.

Ijulikane kuwa suluhisho la ama kuendelea na majadiliano ya Tija Bunge la Katiba linatokana na msimamo wa CCM.

Ninakumbuka mh. Rais akiwa Mbeya kama sikosei aliomba UKAWA warudi bungeni mchakato uanze upya!!!! Kwa hiyo kuna makosa kwa bunge lilopita?!!! Kwa nini waanze upya kama walikuwa sahihi?

Kinachotakiwa ni Rasimu ya tume ya Warioba kuboreshwa na si kubadilishwa au kukataliwa. Yale ni maoni ya wananchi wawakilishi. Wasituletee vurugu.

:mad:
 
Last edited by a moderator:

Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Hapo kwenye bold panashangaza kwamba umegundua kama utavunja mkataba wa kwanza muungano.Sasa kuingiza mambo yote kwenye muungano itakuwa unafanya nini?

Nadhani unajidanganya kusema wananchi wote wanataka kuendelea na muungano, na kwa ushahidi gani ? Mie mmoja naamini kwa ushahidi wa kisanyansi kuwa muungano uliopo hauna nia ya dhati ya kuwaletea wananchi maendeleo ya aina yoyote hususan yale ya kiuchumi.

Motivation ya kuundwa kwake ilijikita zaidi na hoja kama za akina Lukuvi, zina chembe za udikteta wa kikristo chungu tele!
Mkuu nitakujibu kwa wepesi zaidi pasipo maelezo mengi.
1. Wananchi wa pande zote mbili waliomba mwongozo wao yaani Katiba ya JMT na sii kwamba hawautaki Muungano.
2. Maoni ya wananchi yalotolewa katika rasimu ya katiba toka pande zote ni kutaka mwongozo mpya (katiba) tofauti na dhana ya kwamba hawautaki Muungano.
3. Mchakato wa Katiba mpya umeanza na marais wa pande zote, ikafuatia uteuzi wa tume ambayo imekwenda sehemu zote kukusanya maoni, na wajumbe wa baraza la Muungano kutoka pande zote wote wana chagamoto la uandishi wa katiba mpya, hivyo kama tusingeutaka Muungano huu, hoja ingekuwa tofauti kabisa na wala hakuna ambaye angeomba katiba mpya ya JMT maana Jamhuri hiyo ya MUUNGANO haitakiwi.

Swala la serikali moja

Toka awali ya majadiliano ya Muungano huu swala la serikali moja lilijadiliwa na kufikia makubaliano kabla hata ya hati kusainiwa na viongozi wote wa pande mbili walitoa sababu za makubaliano yao na swala hili walilitolea sababu ya kwamba Tanganyika itaimeza Zanzibar. Hivyo, kufikiria kuunda serikali moja pasipo kutatua hoja ile ya msingi ni kupuuza tahadhali ile ikiwa hatuna vigezo vya kuridhia ama kuondoa shaka hilo. Hivyo, Tanganyika kuimeza Zanzibar bado ni changamoto ambayo hatuna majibu yake na ni mjadala mzito zaidi ya kuunda katiba mpya. Serikali moja itaondoa mamlaka ya Zanzibar kuendesha serikali yake, bunge lake na mahakama zake jambo ambalo linataka maridhiano na sidhani kama Zanzibar wako tayari kwa hilo japo najua Bara hatuna tatizo kabisa.

Swala la mambo yote kuwa ya Muungano

Hili haliwezi kuwa kundi moja na swala la serikali gani tunazihitaji kwa sababu ni makubaliano ambayo yanaweza kuwekwa ama kuondolewa wakati wowote wa ushirika wetu na pasipo kuvunja ushirika huu. Kwa mfano hadi sasa hivi ktk ushirika wetu wa Jumuiya ya EAC bado tunajadiliana Mambo gani yawe ktk ushirika wetu pasipo kuathiri ushirika iwe ni swala la sarafu moja, uhamiaji, ajira na kadhalika. Tunaweza kukubali ama kutokubaliana na tukaendelea na ushirika uliopo. Hivyo Mambo ya Muungano hayawezi kuvunja ushirika isipokuwa muundo wa ushirika unaweza. Ni rahisi kuondoa/kuongeza jambo moja ktk ushirika kama walivyofanya CCM na serikali ya mapinduzi toka mwaka 1977 mambo 11 mengine yaliongezwa kwa sababu maalum kutokana na hali halisi lakini hatuwezi kugeuza muundo wa serikali kila tunapojisikia.

nadhani umenielewa!
 
Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Hapo kwenye bold panashangaza kwamba umegundua kama utavunja mkataba wa kwanza muungano.Sasa kuingiza mambo yote kwenye muungano itakuwa unafanya nini?

Nadhani unajidanganya kusema wananchi wote wanataka kuendelea na muungano, na kwa ushahidi gani ? Mie mmoja naamini kwa ushahidi wa kisanyansi kuwa muungano uliopo hauna nia ya dhati ya kuwaletea wananchi maendeleo ya aina yoyote hususan yale ya kiuchumi.

Motivation ya kuundwa kwake ilijikita zaidi na hoja kama za akina Lukuvi, zina chembe za udikteta wa kikristo chungu tele!
Mkuu nitakujibu kwa wepesi zaidi pasipo maelezo mengi.
1. Wananchi wa pande zote mbili waliomba mwongozo wao yaani Katiba ya JMT na sii kwamba hawautaki Muungano.
2. Maoni ya wananchi yalotolewa katika rasimu ya katiba toka pande zote ni kutaka mwongozo mpya (katiba) tofauti na dhana ya kwamba hawautaki Muungano.
3. Mchakato wa Katiba mpya umeanza na marais wa pande zote, ikafuatia uteuzi wa tume ambayo imekwenda sehemu zote kukusanya maoni, na wajumbe wa baraza la Muungano kutoka pande zote wote wana chagamoto la uandishi wa katiba mpya, hivyo kama tusingeutaka Muungano huu, hoja ingekuwa tofauti kabisa na wala hakuna ambaye angeomba katiba mpya ya JMT maana Jamhuri hiyo ya MUUNGANO haitakiwi.

Swala la serikali moja na Mambo ya muungano.

Toka awali ya majadiliano ya Muungano huu swala la serikali moja lilijadiliwa na kufikia makubaliano kabla hata ya hati kusainiwa na viongozi wote wa pande mbili walitoa sababu za makubaliano yao na swala hili walilitolea sababu ya kwamba Tanganyika itaimeza Zanzibar. Hivyo, kufikiria kuunda serikali moja pasipo kutatua hoja ile ya msingi ni kupuuza tahadhali ile ikiwa hatuna vigezo vya kuridhia ama kuondoa shaka hilo. Hivyo, Tanganyika kuimeza Zanzibar bado ni changamoto ambayo hatuna majibu yake na ni mjadala mzito zaidi ya kuunda katiba mpya. Serikali moja itaondoa mamlaka ya Zanzibar kuendesha serikali yake, bunge lake na mahakama zake jambo ambalo linataka maridhiano na sidhani kama Zanzibar wako tayari kwa hilo japo najua Bara hatuna tatizo kabisa.

Swala la mambo yote kuwa yaMuungano

Hili haliwezi kuwa kundi moja na swala mla serikali gani tunazihitaji kwa sababu ni makubaliano ambayo yanaweza kuwekwa ama kuondolewa wakati wowote wa ushirika wetu na pasipo kuvunja ushirika. Kwa mfano hadi sasa hivi ktk ushirika wetu wa Jumuiya ya EAC bado tunajadiliana Mambo gani yawe ktk ushirika wetu pasipo kuathiri ushirika iwe ni swala la sarafu moja, uhamiaji, ajira na kadhalika. Haya tunaweza kukubali ama kutokubaliana na tukaendelea na ushirika. Hivyo Mambo ya Muungano hayawezi kuvunja ushirika isipokuwa muundo wa ushirika unaweza kama hauzingatii tofauti zetu. Ni rahisi kuondoa/kuongeza jambo moja ktk ushirika kama walivyofanya CCM na serikali ya mapinduzi toka mwaka 1964 mambo 11 mengine yaliongezwa kwa sababu maalum kutokana na hali halisi pasipo kuvunja muungano lakini hatuwezi kugeuza muundo wa serikali kila tunapoona inatakiwa.

nadhani umenielewa!

NB: kyalankota Nitakujibu baadaye kidogo kuhusu tofauti baina ya mambo na ushirika na serikali moja!
 
Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
simply haiwezekani mkuu
Simply haiwezekani kwa nini? nipe hata sababu chache nitazitolea maelezo zaidi. Je, ugonvi wetu mkubwa sio ktk mambo haya ya Muungano ambapo yamekuwa maswala ya CHAKO CHANGU, CHANGU CHANGU?. Mimi nimetoa ushauri wa CHANGU CHAKO, CHAKO CHANGU kuondoa mzizi wa fitna, kila mtu aweke chake mezani halafu tugawame kutokana na ulichoweka.
 
Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
12,029
2,000
Simply haiwezekani kwa nini? nipe hata sababu chache nitazitolea maelezo zaidi. Je, ugonvi wetu sio ktk mambo haya ya Muungano ambapo yamekuwa maswala ya CHAKO CHANGU, CHANGU CHANGU. Mimi nimetoa ushauri wa CHANGU CHAKO, CHAKO CHANGU kuondoa mzizi wa fitna, kila mtu aweke chake mezani halafu tugawame kutokana na ulichoweka.
Mkandara, hii ya kwako ni usanii at its best! Wazanzibari walikaa pamoja wakajadiliana kuhusu hatma yao na wakaamua kwa pamoja kujenga msingi imara utakaostahimili changamoto na mikiki mikiki iliyokuwa ikisababishwa na kero za Muungano wa serikali mbili katika nchi moja. Msingi huo imara, Katiba, ulipitishwa na Wazanzibari wote bila kujali itikadi, dini, rangi, jinsia wala kabila iliunda nchi ya Zanzibar ndani ya Muungano yenye mipaka na mamlaka ya juu yasiyoweza kuhojiwa na mamlaka yoyote nyingine ndani na nje ya Muungano. Katiba hiyo pia ilisisitiza kuwa haiwezi kufanyiwa marekebisho isipokuwa na Wazanzibari wenyewe kupitia vyombo vyao walivyojiwekea kulingana na maelekezo ya Katiba hiyo.

Mkandara, unaweza kutudokeza japo kidogo ni njia ipi itatumika kuhakikisha mambo yote yanakuwa ya Muungano bila kuathiri Katiba ya Zanzibar kama ilivyo sasa? Kumbuka kuwa pamoja na kuwa na Katiba ya Muungano bado Zanzibar peke yao waliweza kukaa, wakajadili na kupitisha Katiba inayopingana na ya Muungano na hakuna aliyewajibishwa. Kumbukumbu ziko kwamba hii ni hoja mojawapo iliyowapa wakati mgumu sana Tume ya Mabadiliko ya Katiba; sasa kama si mawazo ya kilaghai na kujaribu kuondoa watu kwenye hoja ya maana na ya msingi, naomba uwe mkweli utuambie mbinu gani ya kisheria itatumika kuwapokonya Wazanzibari haki yao ya Kikatiba ya kujiamulia mambo yao wenyewe...jeshi?
 
Mdondoaji

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
5,108
1,225
Mkandara,

Naunga mkono hoja kwamba swala la serikali ngapi ni irrelevant sana sana lishadidiwa na wanasiasa kulinda status quo zao hapa kwanza wananchi waulizwe wanautaka muungano au la. Likiwa jibu ndio then waulizwe mambo gani yawemo katika muungano? na mapendekezo waweke mambo yote ndani ya muungano wananchi waamue. Zipigwe kura za maoni.

Hili nalizungumza hasa nikilenga kuweka uhuru wa kuchambua kwa wananchi wajue wanataka nini na nini hawakitaki ili itakapowekwa wazi muungano tuliouchagua ni huu then kila mtu aufyate kimya na kuendelea na maisha.

Nitachangia zaidi baadae lakini hili ndio wazo ninaloliunga mie

Ikibidi tuwe na Serikali moja so be kwani kuna kipi cha ajabu? Ili mradi cha muhimu dola iwe moja na yenye nguvu kushinda dola za nchi washirika.
 
Kilala Makusaro

JF-Expert Member
Oct 31, 2013
688
500
Simply haiwezekani kwa nini? nipe hata sababu chache nitazitolea maelezo zaidi. Je, ugonvi wetu mkubwa sio ktk mambo haya ya Muungano ambapo yamekuwa maswala ya CHAKO CHANGU, CHANGU CHANGU?. Mimi nimetoa ushauri wa CHANGU CHAKO, CHAKO CHANGU kuondoa mzizi wa fitna, kila mtu aweke chake mezani halafu tugawame kutokana na ulichoweka.

Nimesoma hoja ya vizuri ila hujajibu hoja ya wazanzibari. Wanataka nchi yao na wamesema haya miaka mingi kuwa wanataka mamlaka kamili. Sasa wewe ukitoa ushauri wa kuua hatua moja waliyoipiga kuelekea mamlaka kamili, ni uchokozi usiovumilika. HAPA HAKUNA KUPINDA PINDA " WAZANZIBAR WANATAKA MAMLAKA KAMILI"

We unapiga tu porojo!!!!
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,203
2,000
Mambo yote yakiwa ya Muungano yataweza vipi kuondoa mapungufu na kufuta kero za wananchi? Hili nitalizungumzia baada ya kujibu hoja za wanabodi ambao watakuwa na haja ya kulizungumzia hili.

Nawasilisha

Mkuu wangu Mkandara; unaposema mambo yote yawe ya Muungano unamaanisha kuwa iwepo Serikali Moja kuu na siyo Serikali Mbili za sasa au Tatu zinazopendekezwa na Rasimu ya Tume ya Warioba? Sioni namna ya kuwa na "mambo yote" yawe ya Muungano halafu uwe na mfumo wa zaidi ya Serikali moja kuu.
 
Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Mag3,

Mkuu wangu kwanza nitakuomba subira, kumbuka kwamba hii katiba ya mwaka 1977 ni katiba ya Tanganyika sio yao lakini walikubali itumike bila kuandika katiba mpya. Be realistic kidogo, hivi kweli sisi tungekubali kutumia katiba yao pasipo kukangamaa? Halafu haiwezekani nchi yoyote ndani ya muungano yenye Bunge lake, serikali yake na mahakama yake (mihimili mitatu) wasiwe na mwongozo wao - haiwezekani ndio kumezwa kwenyewe huko.

Na ikiwa swala ni kuchanganya katiba yao na ile ya muungano, mimi nadhani ni kutokana na serikali ya muungano kushindwa kutoa majibu ya malalamiko yao kwa miaka zaidi ya 30. Maana ni lazima kwanza tujiulize hao Wazanzibar walifikiaje kufanya maamuzi hayo? Je wao walikuwa na malalamiko gani ambayo kwa fikra zao waliona lazima wawe na katiba hiyo halafu ndio tuchambuane maana tusipende sana kusoma upande mmoja tu wa habari tukashindwa kutoa majibu kwa swali tuloulizwa miaka 30 ya Muungano. je, upande wa pili wa shilingi unatupa taaswila gani?

Mkuu majibu yako nitaliweka kesho Inshaallah tukijaliwa kuamka salama.
 
Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Nimesoma hoja ya vizuri ila hujajibu hoja ya wazanzibari. Wanataka nchi yao na wamesema haya miaka mingi kuwa wanataka mamlaka kamili. Sasa wewe ukitoa ushauri wa kuua hatua moja waliyoipiga kuelekea mamlaka kamili, ni uchokozi usiovumilika. HAPA HAKUNA KUPINDA PINDA " WAZANZIBAR WANATAKA MAMLAKA KAMILI"

We unapiga tu porojo!!!!
Mkuu hili neno mamlaka kamili wala lisikutishe hivo hata mkeo nyumbani anatakiwa kulinda UTU wake uheshimiwe na pia awe na mamlaka kamili ndani ya ndoa wao wanasema - Independent! isikutishe sana hii. Kwa kufanya hivyo hana maana anataka naye awe mume ama baba mwenye nyumba. Haya ni mamlaka ya kufanya shughuli za nyumbani sio kila kitu lazima amuulize mume hata kununua sidiria yake mwenyewe lazima mume apitishe! haiondoi jambo lolote bali inaimarisha mahusiano na unyumba mkuu wangu.
 
Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Mkuu wangu Mkandara; unaposema mambo yote yawe ya Muungano unamaanisha kuwa iwepo Serikali Moja kuu na siyo Serikali Mbili za sasa au Tatu zinazopendekezwa na Rasimu ya Tume ya Warioba? Sioni namna ya kuwa na "mambo yote" yawe ya Muungano halafu uwe na mfumo wa zaidi ya Serikali moja kuu.
Hapana mkuu wangu kuwa na mambo yote ya Muungano inaondoa kile tunachoita - Chako changu, changu changu na tunaweza kuwa na muundo wa serikali moja 2 au 3 na bado mambo yote yakawa ya muungano.

Hii ina reflect tu kwamba kila mtu atachangia asilimia sawa ya pato lake mezani kisha tunapanga matumizi kwa wote na kisha mapato yake tutayagawa kwa asilimia sawa ya mchango yetu, isipokuwa tu katika miradi ya maendeleo ambayo tutatumia mikopo na misaada ya kimataifa kuwekeza pale itakapo stahili na kuzinufaisha nchi zote kupitia mfuko wa taifa - Changu chako, chako changu!

Kwa hiyo tuseme kama tutaona umuhimu wa kujenga bandari Zanzibar kuongeza pato la Taifa, tutajenga bandari hiyo na bila shaka pato la Zanzibar litaongezeka, na mwisho wa mwaka Zanzibar itachagia zaidi mfuko wa taifa kuliko mwaka jana kutokana na ongezeko la pato kutoka bandari hiyo, hivyo pande zote mbili zimefaidika na uwekezaji huo Zanzibar. Hii ya kugawana Umaskini haiwezi kutusaidia kitu zaidi ya kuongeza mfarakano zaidi.

Kesho nitawawekea sehemu ya pili Inshaallah tuijadili zaidi na nitawapa ufafanuzi juu ya mitazamo ya pande zote mbili kuhusiana na malalamiko ya Muungano. I think I can link and pin every single arguement we do have with haya MAMBO YA MUUNGANO.
- Mungu nisaidie
 
Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Inaendelea...

Wanabodi, hatua ilotakiwa kufuata katika sehemu hii ya pili, ilikuwa kuelezea mambo yote yawe ni ya muungano itakuwa na malengo gani muhimu na msingi ktk mwelekeo wa utekelezaji mzuri wa shughuli za serikali. Lakini kutokana na kutoelewa kwa nini nimependekeza hivyo, kwa sababu hizi itanibidi nirudi nyuma kidogo kuzungumzia kwanza sababu za mfarakano huu uliopo na ulodumu kwa miaka 30 pasipo kupatiwa ufumbuzi, halafu ndipo nitarudi kuelezea zaidi Mambo yote yakiwa ya Muungano yatawezaje kuondosha mapungufu ya katiba iliyopo na pia kufuta kero za wananchi wa pande zote mbili.

Awali ya yote, nawaomba wasomaji wenzangu tujikumbushe na turudi nyuma kujiuliza ni mapungufu gani yalosababisha wananchi kudai katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Nadhani hili ndilo swala la msingi pamoja na kwamba yapo mengi sana isipokuwa tutazame kiini cha kuitaka katiba mpya maana kama pasingekuwa na Mapungufu basi hapakuwa na sababu wala haja ya kuandika katiba Mpya bali tungeomba katiba iliyopo ifanyiwe marekebisho ama kuandika au kufuta baadhi ya vipengele vya sheria.

Na kama wananchi wa pande zote mbili walikuwa hawautaki Muungano basi pia wasingeomba katiba mpya bali wangeomba taratibu za upigaji kura ili kuvunja muungano huu. Hizi ndizo taratibu zinazokubalika kisheria na sii vinginevyo. Hivyo ni basi tujiulize ni malalamiko gani haswa yaliyosababisha wananchi kutoridhika na katiba ya mwaka 1977.

Wananchi wa Tanzania visiwani (Zanzibar)

Wananchi wa Zanzibar wamedai kwa muda mrefu sana juu ya Muungano huu kutokana na Tanzania bara kutumia mamlaka ya serikali ya Muungano kujinufaisha haswa katika mambo yote ya muungano na yasokuwa na Muungano wakati fursa kama hiyo Zanzibar hawana. Hili ni swala ambalo halikuanza jana bali toka wakati wa hayati marehemu Sheikh Abeid Karume aliwahi kuulizwa na akasema hivi "Muungano ni sawa na koti, unalivaa unapolihitaji na unalivua likikubana" haya ni maneno mazito sana na yanavuta uradi mkubwa (Meditation) na ukiyatafakari kwa kina utayaona ambayo hayakuonekana wakati ule. Hivyo kuna watu walitia shaka muungano huu na kutaka kujua kama unaweza kuvunjwa ikiwa hatutafikia maridhiano.

Haya leo hii yasemekana Tanzania bara tumelivaa koti la Muungano na limetupendeza hivyo kulivua imekuwa kazi kubwa kwa sababu ya fursa tulizopata kutokana na mamlaka tulonayo. Na ukweli ni kwamba nani atakayekubali kulivua koti linalompa fursa kubwa japo linambana? Waasisi wetu hawakuyaona haya na hivyo mapungufu yalojitokeza ni FURSA SAWA kwa nchi washirika. Na hili limetokana na ukweli kwamba toka nchi yetu itoke ktk mfumo wa Ujamaa kuingia Utandawazi na soko huria, hii katiba iliyopo haija ainisha wazi ikaeleweka mipaka na mamlaka ya Serikali ya Muungano katika mambo ya Muungano,

Wazanzibar wanadai pia kuwepo kwa uchakachuaji kuhusiana na uchangiaji wa gharama za uendeshaji shughuli za mambo ya Muungano baina ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ikifuatiwa na ugawanaji wa mapato. Hapa inaonekana tunakwenda kiholela tu hakuna mfumo kamili unaoeleweka na wazi kwa kila mshirika kufahamu kinachoendelea.
Wananchi wa Zanzibar wameendelea kuweka madai mengine ya kwamba Rais wao aliondolewa katika nafasi ya utawala kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Pia swala la ongezeko la mambo ya Muungano iliyoongezwa kutoka mambo 11 mwaka 1964 mpaka kufikia 22 mwaka 1992 haya yote yamepunguza uhuru wa Zanzibar kwa mambo yake yasiyokuwa ya muungano.

Wananchi wa Tanzania Bara (Tanganyika)
Wananchi wa Tanzania Bara, wao wanasema kuwepo kwa Muungano wa Serikali mbili ndio umepoteza utambulisho wa kihistoria wa Tanganyika (Identity) na fursa ya watu wa upande wa Tanzania Bara kutetea maslahi yao ndani ya Muungano kiasi kwamba wakitazama upande wa pili, Zanzibar sasa imekuwa nchi huru, ina serikali yake, ina bunge lake ina mahakama zake ina bendera yake, wimbo wake wa taifa ili mradi wao hawakumezwa na muundo huu basi matokeo yake ilomezwa ni Tanganyika.

Watanzania bara wanadai tena ya kwamba Zanzibar imebadilisha Katiba yake mwaka 2010 pasipo ridhaa ya serikali ya Muungano na kujitambulisha kama nchi na kuchukua madaraka kinyume cha katiba ya JMT. Aidha Sheria zinazotungwa na Bunge la Muungano lazima zipelekwe kama muswada kwenye Baraza lao la Wawakilishi kuidhinishwa ili zipate kutumika Zanzibar.

Kuna swala la Ardhi ambalo wananchi wa Tanzania Bara wanalalamika kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi Zanzibar wakati wenzao wanayo haki hiyo huku Bara. Vile vile kuna sitoelewa kuhusu jinsi ya uchangiaji gharama za uendeshaji wa shughuli za mambo ya Muungano pamoja na ugawajiwa mapato ndani ya muundo wa serikali mbili.

Haya ndiyo maswala muhimu sana yalochangia kuleta mgogoro mkubwa baina ya wananchi wa Tanzania bara na visiwani kiasi kwamba uandikaji wa katiba mpya umekwama kutokana na kutoelewana juu ya muundo gani wa ushirika unaweza kuyaondoa mapungufu hayo, ndipo maoni yakaanza kukusanywa kupitia tume ya Warioba ambao wameleta rasimu yenye mapendekezo ya kubadilisha muundo wa serikali mbili kwanza ili kuzipa utambulisho nchi zote mbili washirika na kisha kugawana tena mambo ya Muungano ili serikali ya JMT isiwe na mamlaka nayo.

Navyoamini mimi ni kwamba bado tunazunguka mbuyu kutafuta muundo wa serikali kwa sababu Tanzania inaweza kuwa na muundo wowote ule ili mradi tu kunakuwa na Mamlaka ya kutosha, uwazi na katika masuala ya Muungano ili kuiweka nchi pamoja na kuwa na Taifa imara mbele ya mataifa. Na ni muundo gani wa Utawala unaotufaa sisi leo hii ni uamuzi wetu wenyewe. Hata hivyo uamuzi huo ni lazima ujibu maswali ya wananchi katika malalamiko yao ili vigezo vitakavyo tumika vimelenga kuondosha mapungufu yaloainishwa hapo juu.

Je, Muundo wa serikali ulopendekezwa kweli utajibu hofu ya baadhi ya watu Muungano kuvunjika? maana swala la serikali tatu limetazama malalamiko na mahitaji ya kwanza ya Watanzania bara na hapo ndipo tulipokwama hadi sasa wakati hoja na malalamiko ni mengi. Mimi naamini pia ya kwamba idadi ya Serikali haina uhusiano wowote na kiini cha malalamiko ya wananchi kwa sababu ukisoma kwa makini malalamiko hayo mengi yamehusiana na MAMBO YA MUUNGANO. Na ndipo nilipokuja na mapendekezo haya nikiacha yale ambayo yanaweza kupatiwa ufumbuzi kwa kuzingatia kwamba sasa hivi hatupo tena katika Ujamaa ambao rais wa jamhuri alikuwa na mamlaka yote juu ya utekelezaji wa shughuli za serikali chini ya itikadi moja.

Ikumbukwe ilivunja hata Jumuiya ya EAC baada ya mkutano wa Uganda ambao nchi husika zilikubaliana zote kuhusu kugawa fursa sawa lakini Kenya walokuwa wamevaa koti la Jumuiya walikataa na ikafikia kikomo cha EAC. Tusirudie makosa hayo tena katika Muungano huu wala huo wa Jumuiya ya EAC ambao hadi sasa haujafikia hatua tulokuwa kabla ya kuvunjika kwake. Ningetegemea sana sisi Watanzania kujifunza kutokana na makosa yalofanywa wakati ule japo washirika wa Jumuiya hizo walikuwa na serikali zao zenye mamlaka kamili lakini utengano ukatokea ktk mapungufu ya uchangiaji na ugawanaji wa MAMBO YA JUMUIYA.

Mambo yote yakiwa ya Muungano yataweza vipi kuondoa mapungufu na kufuta kero za wananchi? Hili nitalizungumzia baada ya kujibu hoja za wanabodi ambao watakuwa na haja ya kulizungumzia hili.
 
Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
12,029
2,000
Mkandara tuache maneno mengi yanayozidi tu kuchanganya watu; let us come down to earth. Nimetaka ufafanuzi katika eneo moja tu...je huo mfumo wa Mambo yote kuwa ya Muungano unawezekana bila kuathiri Katiba ya Zanzibar kama ilivyo?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom