Katiba mpya ina ugomvi na wastaafu

Andrew Nyerere

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
3,007
2,445
Ibara ya 238;ibara ndogo ya pili,d. Inasema kama mtu amestaafu serikali,jeshi au polisi,asihesabiwe kwamba bado ana madaraka,kws vile tu analipwa pensheni. Hii naona kama vile inawabagua wastaafu kutoa maoni yoyote kuhusu jambo lolote linalitokea. Inawaita wastaafu""kero "".
 
Sasa kama mtu amestaafu nafasi yake na bado anatambuliwa kama ana madaraka huoni kama inapotosha maana ya kustaafu? Kuhusu wastaafu kutoa maoni mimi naona wanaweza wakaendelea kutoa maoni yao kwenye platform tunazozitumia wote na maoni yao yakapewa uzito unaostahili kama walivyofanya Membe na Wasira
 
KATIBA MPYA
Jitihada za Magufuli kukabiliana na ufisadi zitaishia ukingoni kama atakumbatia katiba ya Kikwete na Chenge. Akikubali na kutekeleza ya Warioba ndipo nitajua uimara wa dhamira take na yeye pia atapata nguvu za kukabiliana na vizingiti vya chama chake. Akitusaliti kama alivyofanya matangulizi wake hatafanikiwa na CCM itaendelea kukumbatia mafisadi. Halafu nguvu yake itakuwa majeshi na silaha zao badala ya Mwenyezi Mungu anaemuomba amsaidie na watu wake. Tizama anavyoachia vurugu za uchaguzi wa mega wa Dar! Anataka watu wamwage damu? Haiwezikani kwamba JPM hana habari za vurugu zinazoendelea mlangoni kwake kama sio mnafiki.
 
Samahani hapo juu neno 'take' liwe 'take' na 'mega' ilitakiwa liwe 'meya'. Ni ugeni wangu mimi hapa uwanjani.
 
Ibara ya 238;ibara ndogo ya pili,d. Inasema kama mtu amestaafu serikali,jeshi au polisi,asihesabiwe kwamba bado ana madaraka,kws vile tu analipwa pensheni. Hii naona kama vile inawabagua wastaafu kutoa maoni yoyote kuhusu jambo lolote linalitokea. Inawaita wastaafu""kero "".
Neno "kustaafu" kisheria linapaswa kuwa na tafsiri moja, lakini sivyo ilivyo katika she ria za nchi hii zinazohusu ajira na mafao ya mstaafu serikalini. We we unachangia mfuko wako, kw mfn PPF, PSPF, NSSF nk. Lakini wanasiasa hawachangii wakiwa kazini na wanapotoka kwenye ajira wanachotewa tu huko hazina kwa kisingizio cha "kustaafu" mwanasiasa anastaafu kweli? Wewe umri ukifika unastaafu. Wanasiasa wanastaafu vipi kama kisheria wanaruhusiwa kupewa au kugombea nafasi walizokuwanazo mara kadha wa kadha? [Sheria na 2 ya 1999, na She ria na 3 ya 1999].
 
Nilitegemea uandike kwa ufafanuzi zaidi pia nyie waandishi mmesahau kuandika Makala mbalimbali kuhusu katiba pendekezwa udhaifu wake mmekomaa na majipu wakati huo mnajua majipu hayawezi kuisha bila kuwa na sheria bora kutoka katiba bora.
 
Ibara ya 238;ibara ndogo ya pili,d. Inasema kama mtu amestaafu serikali,jeshi au polisi,asihesabiwe kwamba bado ana madaraka,kws vile tu analipwa pensheni. Hii naona kama vile inawabagua wastaafu kutoa maoni yoyote kuhusu jambo lolote linalitokea. Inawaita wastaafu""kero "".
Sasa ndiyo ninampango wa kuisoma ya zamani
 
Back
Top Bottom