Katiba izuie wazee kugombe u-Rais

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
4,009
2,173
Katiba yetu inasema mtu anayetaka kugombea u-Rais ni lazima awe ametimiza umri wa miaka 40. Umri wa juu wa kugombea kuwa Rais haukutajwa!!

Baada ya kuangalia yanayotokea
Senegal nimekuwa na tamaa ya katiba yetu kuweka kikomo cha umri wa juu kwa mtu kugombea u-Rais. Naona si rahisi kuwa na mzee wa kiafrika anayeweza kutuendeleza. Wengi wanatafuta kufa vizuri badala ya kuishi vizuri.

Napendekeza miaka 65 uwe ni umri wa juu kwa m-TZ kugombea kuwa Rais. Hii itampa fursa ya kutimiza vipindi viwili kabla ya kustaafu (miaka 75) angalau akiwa na ubongo salama kwa maisha yetu. Hiyo 65 tayari ni nje ya wastani wa maisha ya m-Tz. Akistaafu akiwa 75 pia itatupunguzia wastaafu wanaotaka kulishwa bure bila faida kwa nchi.

Naomba jopo la katiba litakapowatembelea popote Tz, tuwe pamoja kusisitiza hili.
Naomba samahani kwa wale ambao munamuunga mkono yule jamaa yetu aliyejaa ‘kihelehele' cha kutafuta u-Rais wa 2015.
 
hili ni la msingi sana kuwe na lower na upper age limit ya kugombea!!
 
Tatizo lenu mnamgwaya Dr. Slaa, kichwa cha ukweli. Binafsi napendekeza upper limit age iwe miaka 85. Hapo akili itakuwa inacharge kama ya mtoto mchanga kwa mbaliiii, halafu tukitaka kumwondoa ikulu tunambeba kilaini kama yule wa Tunisia
 
hili ni jambo la maana sana-hatuhitaji kuendeshwa na wazee tena-maana wazee wameshatufikisha pabaya sana
hawa wazee wote wawili walioanza mbio za 2015 hii 2012 wanatakiwa kukatwazwa hata kuchukua fomu za kugombea
 
Tatizo lenu mnamgwaya Dr. Slaa, kichwa cha ukweli. Binafsi napendekeza upper limit age iwe miaka 85. Hapo akili itakuwa inacharge kama ya mtoto mchanga kwa mbaliiii, halafu tukitaka kumwondoa ikulu tunambeba kilaini kama yule wa Tunisia
Wazee wana kawaida ya kung'ang'ania pindi wakionja Ikulu wengi hutamani kufia madarakani. Waone akina Kibaki, Wade na Mugabe.
 
Naomba samahani kwa wale ambao munamuunga mkono yule jamaa yetu aliyejaa ‘kihelehele' cha kutafuta u-Rais wa 2015.
[/QUOTE]

Kwa hiyo mabadiliko hayo yanamlenga huyo mtu, Tanzania huwa tunafanya kwa kumkomoa mtu mmoja badala ya kufanya mambo kwa maslahi ya nchi. Tulishuhudia miaka ile ya nyuma CCM walipoweka shahada kama kigezo cha kugombea urais, kumbe kuna mtu walimlenga. Mpaka leo Marais wetu wana hizo shahada lakini maumivu matupu, Sasa mpaka wanajiita madokta.
MIMI NAAMNI UZEE SIO SABABU YA MTU KUTOKUWA RAISI AU UJANA NI NI KETE YA KUWA RAIS, RAIS WA ZAMBIA WA SASA ANAFANYA MAMBO AMBAYO WANASHINDWA KUFANYA MARAISI WENGINE AMBAO NI WADOGO KULIKO YEYE.
SISI WATANZANIA HATUNA TATIZO NA UZEE WALA UJANA WA MTU, TUNACHOANGALIA NI UWEZO BINAFSI. MWAKA 2005 TULIAMBIWA VIJANA WANATAKA RAISI KIJANA, TUKALETEWA RAISI KIJANA MWENYE MIAKA ZAIDI YA HAMSINI MPAKA LEO TUNAPATA MAUMIVU MAZITO.
 
Tatizo lenu mnamgwaya Dr. Slaa, kichwa cha ukweli. Binafsi napendekeza upper limit age iwe miaka 85. Hapo akili itakuwa inacharge kama ya mtoto mchanga kwa mbaliiii, halafu tukitaka kumwondoa ikulu tunambeba kilaini kama yule wa Tunisia

Unamaanisha tuweke upper age limit ya kugombea iwe 85 years,ili kum-favour Slaa?
Kazi ipo watanzania!
 
Mkuu nakuunga mkono kwa asilimia mia moja kamili

Mkuu Kimbunga,
Mbona kuna Marais wazee lakini ni makini mfano Rais wa China Hu Jintao ana umri wa miaka 70, Castro wa Cuba mpaka anaondoka madarakani alikuwa na umri wa 85, Mahamoud Abbas Rais wa Palestina ana umri wa miaka 77.
 
Unasemaje huyu wa Senegal Mzee Wade ni akili gani zile...tuache kuwatetea uzee ni janga...wewe si unajua kuwa CCM imekaukiwa vijana wenye hekima,wamejaa waropokaji tu pole UVCCM...
 
Back
Top Bottom