Katiba Itamke Kinagaubaga Uraia wa Tanzania

JamboJema

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
1,143
209
Uraia wa Tanzania utamkwe pasina kuweka mashaka. Sina tatizo na aina zote za 'uraia' tulizonazo...ila ningependa ule wa kuandikishwa kigezo kimoja kiwe mwombaji awe na moja ya sifa kuwa ameoa/ameolewa na Mtanzania wa kuzaliwa. Kama hawezi hili na hata kama anamanufaa vipi na nchi yetu, basi apewe Hadhi ya Ukaazi ya Kudumu ila sio uraia. Mgeni mwenye Hati ya Ukaaji atenganishwe kabisa namna ya kupata huduma mbalimbali...ie. mashuleni, mahospitalini na hata kwenye kupata bidhaa mbalimbali. Hili litasaidia kupunguza na kuzuia uzalishaji wa wahamiaji haramu.
 
2tawezaje kutoa maoni ya katiba mpya wakati katiba ya zamani hatuijui ndugu zangu kweli Tanzania
 
2tawezaje kutoa maoni ya katiba mpya wakati katiba ya zamani hatuijui ndugu zangu kweli Tanzania
Kwa maoni yangu...haja ya kuijua katiba ya zamani ni kama lengo letu ni kurekebisha hiyo katiba. Lakini kama tunataka katiba mpya, tuseme kila tunachofikiri kiwemo kwenye katiba. Hii haitubani kwamba lazima ya zamani tuifahamu.
 
Back
Top Bottom