Katiba isiyompa rais mamlaka haitufai.

kimjaacho mtu ndo kinachotoka hii mboga kawaulize wa kwenu jana na leo asubuhi wamekula ya wapi?ukimaliza uliza mkeo kakupikia ya wapi vile!

Siongea na walevi km wewe wasio na hoja. UMEKALILISHWA kojoa lala tena usingizi wa asbh ni mtamu pia kwa watoto km wewe
 
hapa ndipo huelewi maana ya madaraka ya wananchi.

kupora madaraka ya wananchi inaweza kutokea kwa njia nyingi lakini moja wapo ni pale wananchi wanapokosa udhibiti wa watumishi wao, wanakosa udhibiti wa mali zao na wakabaki kulalamika tu na hawana la kufanya.

wananchi wenye madaraka yao wanaogopwa na viongozi wao kutokufanya kinyume na wananchi wanavyotaka.

wananchi walioporwa madaraka linapotokea tatizo lolote wanaamini viongozi wao watakaloamua ndio mwisho.

ki msingi baadhi ya madaraka ya wananchi yamekasimiwa kwa chombo chao ambacho ni bunge hivyo ukisikia chombo chao kinalalamika kuwa serikali imezoea kukaidi maagizo ya bunge ujue chombo hicho hakina madaraka tena ya kusimamia kama katiba inavyosema.

kimsingi raisi na seriakali zikipewa madaraka makubwa wanao uwezo wa kupora madaraka ya wananchi na kuanza kufanya wao wanavyotaka na wananchi wanakuwa hawana la kufanya.

sijui wewe madaraka ya wananchi unayozungumza ni yapi?

Hao viongozi wanaopora madaraka yako wewe mwananchi umewaona wapi TAnzania?wanayapora kutoka wapi?kwani mamlaka ya viongozi wa Tanzania especially rais wetu yanatoka kwa nani?hivi mpaka sasa hujajua tu Wananchi ndo mamlaka yenyewe!Madaraka na mamlaka ya hao viongozi tunawapa sisi kikatiba kama hujui hiyo ni kazi nyingine ukisema wamekupora sikuelewi?Pia kuna Bunge/ wananchi ambalo linafanya kazi yake kutunga sheria na kupitisha mambo mbalimbali,Rais lazima awe na mamlaka yaliyoainishwa Kikatiba na si vinginevyo na ndiyo maana anaitwa Rais asipokuwa na mamlaka sio Rais huyo!!! Sasa wewe unaposema hatuna mfumo wa kushughulikia uvunjaji wa sheria za nchi kwa kiongozi endapo amethibitika kutenda makosa ya kuvunja Katiba nchi ambayo aliapa kuilinda na kuitetea sikuelewi, Tatizo lako unaendeshwa kwa hisia hapa!
 
hapa ndipo huelewi maana ya madaraka ya wananchi.

kupora madaraka ya wananchi inaweza kutokea kwa njia nyingi lakini moja wapo ni pale wananchi wanapokosa udhibiti wa watumishi wao, wanakosa udhibiti wa mali zao na wakabaki kulalamika tu na hawana la kufanya.

wananchi wenye madaraka yao wanaogopwa na viongozi wao kutokufanya kinyume na wananchi wanavyotaka.

wananchi walioporwa madaraka linapotokea tatizo lolote wanaamini viongozi wao watakaloamua ndio mwisho.

ki msingi baadhi ya madaraka ya wananchi yamekasimiwa kwa chombo chao ambacho ni bunge hivyo ukisikia chombo chao kinalalamika kuwa serikali imezoea kukaidi maagizo ya bunge ujue chombo hicho hakina madaraka tena ya kusimamia kama katiba inavyosema.

kimsingi raisi na seriakali zikipewa madaraka makubwa wanao uwezo wa kupora madaraka ya wananchi na kuanza kufanya wao wanavyotaka na wananchi wanakuwa hawana la kufanya.

sijui wewe madaraka ya wananchi unayozungumza ni yapi?

Unaruka moto afu unakanyaga tena we vipi wananchi ndo mamlaka ya mwisho unaposema wanaporwa hueleweki????
 
....Rais anapokuwa na madaraka makubwa sana na kufanya Institutions kama Bunge,TAKUKURU na Mahakama kufanya kazi with 'handbreaks on" ni tatizo kubwa!Na tatizo kubwa zaidi ni kutoa madaraka"God-like powers' kwenye Taasisi moja(Rais) tu ambapo kama mtendaji wake ni mdhaifu,basi mambo mengi sana yanaharibika na kuliweka taifa katika hali tete.Logic ya kupunguza madaraka ya Rais ni pamoja na kuwapa madaraka zaidi Wananchi(kwa kupitia bunge) katika maamuzi maagumu yanaayohusu mustakabali wa nchi yao.Mnaotaka taasisi ya urais iwe na madaraka makubwa,inaonyesha ni kwa jinsi gani mnavyotaka demokrasia iendelee kudidimizwa!
Kuna sababu gani kwa mfano...
1.Bunge lisipewe dhamani,kikatiba la kuipitia na kuipitisha mikataba yote mikubwa serekiali inayoingia?
2.Wakurugenzi wakubwa wa mashirika yenye maslahi mapana kwa nchi kama TANAPA,BANDARI,TANESCO nk....wasiteuliwe tu na Rais na wakawa-ratified na Bunge?
3Kuna haja ya kuwa na wakuu wa wilaya in the first place?na kama ipo kwa nini wasichaguliwe tu na wananchi?
Lastly....taasisi ya uraisi iwe na meno lakini sii kwa kiasi tunachokiona sasa na kwa awamu zilizopita.
 
Kuna baadhi ya watu fulani wamekuwa na hasira kuhusu mamlaka ya Rais yaliyoanishwa kwenye Katiba Inayopendekezwa ile Sura ya nane,Kuanzia Ibara ya 80 mpaka 98. Watu hao wamefikia hatua ya kutaka apunguziwe mamlaka huku wengine hasira zao zikipitiliza wakitaka hata yale aliyonayo yaondolewe yote kabisa abaki kama mtumishi wa kawaida!

Jambo la kunishangaza ni pale watu hao wanaposhindwa kuelewa kuwa mamlaka au heshima ya mfalme ni wingi wa watu wake!wanashindwa kuelewa kuwa Mamlaka ya Rais ni wingi wa kura zake,hawezi kulinganishwa na mtu yeyote katika nchi na Katiba Inayopendekezwa ambayo wananchi wataipigia kura imelizingatia hili.

Kwa mujibu wa Katiba ya 1977 Tanzania tunao utaratibu wa kumpata Rais kupitia sanduku la kura (nguvu ya umma) ambazo humpa Mamlaka ya kuongoza na kutawala.Rais ni Mkuu wa Nchi,kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.

Kwa Tanzania Rais ni alama na taswira ya Jamhuri ya Muungano na watu wake na pia ni alama ya umoja ,uhuru wa nchi na mamlaka yake!

Sasa inawezekanaje Kiongozi Mkuu wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama vya nchi ukataka alinganishwe na mjumbe au mbunge au waziri? Hilo haliwezekani fuatilia nchi zote ambazo wamekubali upuuzi huu utaona marais wao ni kama mapambo tu na wana jina lao eti wanabaki kuwa Ceremonial hawana mamlaka ya maamuZi ya nchi wapo wapo tu, hili halikubaliki Tanzania Rais ni MAMLAKA hata UKAWA wanalijua hili ndo maana wanajaribu kuungana wakiamini kuwa watashinda nafasi ya Urais nao wawe na kiongozi mwenye mamlaka katika nchi.

Mungu Ibariki Tanzania!

Nawasilisha!
Nani anasema kuwa tunataka katiba isiyompa mamlaka raisi? Au unataka awe na mamlaka ya kuingilia ndoa yako?
 
kimsingi mimi siangalii kitu gani tumeandika bali ninachoangalia nini maana ya taifa, serikali ni nini? ina wajibu gani na kwa nani?

nikitokea hapo naona lipo tatizo letu sisi kuchanganya idea za ufalme na idea za uraisi katika demokrasia.

lakini tukitaka kuangalia ustawi wa wananchi na hapo ndipo tuanzie kutafuta tuandikeje mambo kama hayo.

kwanza mimi naweza kusema jeshi liondolewe kabisa mikononi mwa serikali.

sababu ni kutokana na raisi akikabidhiwa jeshi anakuwa na nguvu za kifalme ambazo zinamfanya kupora madaraka ya wananchi.

uongozi wa nchi kwa mtizamo wangu unatakiwa kugawanywa katika mihimili mitatu. raisi na seriakali yake wao wabaki kusiamamia mali zetu na kuzitumia kutuletea maendeleo.

kama ni maamuzi ya kiamiri jeshi mkuu basi mihimili mitatu inakaa kufanya maamuzi.

hebu jiulize mtu mnamkabidhi uongozi wa nchi anajifanya raisi wa milele na wananchi wakitaka aachie anatumia vyombo vya wananchi kupambana na wananchi.

haya yanatokea kwa sababu tumetengeneza mifumo ya kumkabidhi mtu mmoja kila kitu ili atuongoze na pale mtu huyo anapoamua kuasi hatuna njia bali ama kukubali kuwa wajinga au kuingia katika vurugu. sidhani kama utaratibu huu ni wa kisasa bali tunakopi mawazo ya watu wa zamani wakati sisi tunao uwezo wa kuboresha zaidi ili tuwe salama zaidi.

Rais wa nchi ndo kiongozi mkiu wa nchi na amiri jeshi mkuu na hapo unasemaje?
 
Huna hoja hapa wala huelewi ndo walewale Rais abaki Amiri jeshi mkuu Nonsense!!! Then what nini utendaji wake katika Serikali hujaisoma Katiba ya 1977 na hii Inayopendekezwa hujaisoma nenda kasome tena kwa kuelewa acha kutumika!
Hujajibu swali langu. Nini kitakachotokea rais mteule akitokea chama A halafu chama chenye wabunge wengi bungeni ni chama B? Rais atachagua waziri mkuu na mawaziri wengine kutokea chama kipi? Je bunge litawakubali hao mawaziri? Watashirikiana nao vema?Nyie wanaCCM tatizo lenu mnadhani kwamba mko peke yenu nchi hii na kwamba upinzani haukui. Think again!Tunataka katiba imara inayoangalia all posibilities ili iweze kukaa as long as possible bila kubadilishwa. Katiba ni sacred!
 
sio tu kukaa bila kubadilishwa bali kuna jambo linatutafuna nchi hii sana.

watu wanaunda makundi ya kusaka uraisi na hapa wapo watendaji wazuri katika makundi haya lakini wapo wahuni tu watoto wa mjini wanaokaa vijiweni kusikiliza dili, ziwe za utapeli au nini na wao wanajiingiza katika makundi haya na kupiga kelele kama nini.

wananyemelea nafasi alizopewa raisi za uteuzi na akipata hawa hawana utaalamu wowote wao wanatafuta pa kupigia dili.

wakikaa nyuma mtu ni vigumu kuwageuka hawa fitina na kila kitu kichafu wanakijua na hawa ndio wamekuwa chimbuko kubwa la utendaji mbovu wa serikali nyingi zinazolea mifumo ya kuwaingiza watu wajanjanja tu kwenye uongozi.

tutengeneze mifumo ambayo raisi akichaguliwa kwanza kuna vyombo vya kuangalia anayoyafanya na hawa wahuni waone kuwa hawana nafasi.

hebu angalia mashirika ya serikali yanavyokufa, hivi kweli hapa tanzania kuna mtu binafsi mtanzania wa kuwa na mtaji kuliko serikali yetu? kama hakuna iweje watu binafsi wapate watendaji bora na waendeshe makampuni kwa faida na mashirika ya serikali yanakufa?

jibu la haya yote ni kuweka uongozi wa nchi katika mihimili mitatu na mtendaji yeyote anayeingia katika utendaji wa umma anaona akifanya uzembe au ndivyo sivyo wapo wa kumbana.

tunaposema kuzuia mtu mmoja ua kundi la watu kushikilia vyombo vyote kimsingi haina maana ya kusema huyu akitoka kundi hili basi yule atoke kundi lile.

hapa ni kila chombo kuwa na mambo yake na yanayojitegemea na kundi la watu au mtu fulani lisiwe na ushawishi au maamuzi ya moja kwa moja katika chombo au mhimili mmoja usiwe na peremende au bakora za kuwanyamazisha au kuwashughulikia mihimili mingine. na tutafute jinsi ya kufanya uongozi wa juu kwa kila chombo cha juu kiutawala kuwajibika kwa wananchi hivyo wanachombo wakati wote wanajua wanatakiwa kuwaridhisha wananchi.

hapo inakuwa haijalishi watendaji wanatoka wapi.

Acha mawazo ya Giningi na kutuletea utawala wa kambale wewe tangu lini ukaona Serikali ikashinda kurun eti kisa wabunge wengi wanatoka upinzani afu Rais chama Tawala ha ha ha ha kwani huyo Rais kashindaje huo uchaguzi????? Si ina maana amepata sappti kubwa kutoka majimboni ha ha ha acha kutokwa na povu wewe!
 
sio tu kukaa bila kubadilishwa bali kuna jambo linatutafuna nchi hii sana.

watu wanaunda makundi ya kusaka uraisi na hapa wapo watendaji wazuri katika makundi haya lakini wapo wahuni tu watoto wa mjini wanaokaa vijiweni kusikiliza dili, ziwe za utapeli au nini na wao wanajiingiza katika makundi haya na kupiga kelele kama nini.

wananyemelea nafasi alizopewa raisi za uteuzi na akipata hawa hawana utaalamu wowote wao wanatafuta pa kupigia dili.

wakikaa nyuma mtu ni vigumu kuwageuka hawa fitina na kila kitu kichafu wanakijua na hawa ndio wamekuwa chimbuko kubwa la utendaji mbovu wa serikali nyingi zinazolea mifumo ya kuwaingiza watu wajanjanja tu kwenye uongozi.

tutengeneze mifumo ambayo raisi akichaguliwa kwanza kuna vyombo vya kuangalia anayoyafanya na hawa wahuni waone kuwa hawana nafasi.

hebu angalia mashirika ya serikali yanavyokufa, hivi kweli hapa tanzania kuna mtu binafsi mtanzania wa kuwa na mtaji kuliko serikali yetu? kama hakuna iweje watu binafsi wapate watendaji bora na waendeshe makampuni kwa faida na mashirika ya serikali yanakufa?

jibu la haya yote ni kuweka uongozi wa nchi katika mihimili mitatu na mtendaji yeyote anayeingia katika utendaji wa umma anaona akifanya uzembe au ndivyo sivyo wapo wa kumbana.

tunaposema kuzuia mtu mmoja ua kundi la watu kushikilia vyombo vyote kimsingi haina maana ya kusema huyu akitoka kundi hili basi yule atoke kundi lile.

hapa ni kila chombo kuwa na mambo yake na yanayojitegemea na kundi la watu au mtu fulani lisiwe na ushawishi au maamuzi ya moja kwa moja katika chombo au mhimili mmoja usiwe na peremende au bakora za kuwanyamazisha au kuwashughulikia mihimili mingine. na tutafute jinsi ya kufanya uongozi wa juu kwa kila chombo cha juu kiutawala kuwajibika kwa wananchi hivyo wanachombo wakati wote wanajua wanatakiwa kuwaridhisha wananchi.

hapo inakuwa haijalishi watendaji wanatoka wapi.

Mzee unaongea nini hasa maana una mambo kibao afu mchanganyiko!nikuulize swali hivi Tz hakuna mihimili 3?
 
Lukindo, kweli hayo maneno aliyatoa Mwl. ndiyo maana alisistiza Kiongozi wa nchi ni lazima awe na msimamo unaoongozwa na misingi ya katiba ya nchi katika kutoa maamuzi.

Nakushangaa Lukindo kwa kusema “Nafikiri unachotaka kutwambia ni kuwa rais akiamka asubuhi na kuamua kuahirisha uchaguzi mkuu iwe sawa tu maana ana mamlaka hayo!” Usituambie unafikiri, soma Katiba inasema je?Ndiyo maana Baba wa Taifa alikemea tabia hiyo.Maneno yako uliyoyasema sii ya kikatiba bali ni mawazo yako ambayo hayapo kwenye Katiba ya nchi, hivyo nasisitiza kuwa nchi inaongozwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo kulingana na Katiba ya nchi na sii vinginevyo.
....inayompa rais madaraka ya kuteua mpaka mkuu wa wilaya baada ya kushauriana na 'kamati ya uteuzi' anayoiteua mwenyewe baada ya kushauriana na wasaidizi wake anaowateua mwenyewe pia!?
 
....inayompa rais madaraka ya kuteua mpaka mkuu wa wilaya baada ya kushauriana na 'kamati ya uteuzi' anayoiteua mwenyewe baada ya kushauriana na wasaidizi wake anaowateua mwenyewe pia!?
?????"?????????????????????? image.jpg
 
kinadharia ipo lakini kiurtendaji hakuna.

huwezi kuwa na mihimili mitatu kama wabunge wanateuliwa kushika nyadhifa serikalini, huwezi kuwa na mihimili mitatu kama majaji wanateuliwa na serikali.

huwezi kuwa na mihimili mitatu kama bunge na mahakama wanazidiwa nguvu na serikali na wao kubaki kuongea tu lakibni maamuzi yao serikali ikiamua kutekeleza sawa na ikikaidi hawana la kufanya.

mfumo wa utendaji unaifanya mihimili yote kuungana lakini hakuna wa kumkosoa mwingine pale mmoja anapotoka kwenye mstari.

kuingiza siasa bungeni ni njia moja wapo inayoua bunge. mpinzani akitoa hoja anajaribu kukiinua chama chake kupitia hiyo hoja na matokeo yake ni walioko madarakani kuona huwezi kuwa mjinga kukata tawi ulilolikalia hivyo hata kama hoja ni ya msingi iliyoibuliwa lakini kama inawapaka matope wataitetea serikali.

wabunge wanachangia bungeni kutafuta kuteuliwa na katika hilo lazima wawe wanatetea serikali kwa uonekane ni mwenzao.

hivypo utaona fursa za utendaji ndani ya serikali kwa wabunge na siasa kuingia bungeni vinafanya bunge kuungana na serikali kwa upande mmoja na bunge kugeuka chombo cha vyama vya siasa na kuacha jukumu la msingi la kufanya kazi ya wananchi.

lakini bila ya kuingia kwenye majukumu ya msingi ya kila mhimili tunatakiwa tujiulize kwa nini tuwe na mihimili mitatu na sio kuwa na chombo kimoja kina taasisi ndani yake zinafanya kazi zote?

utagundua kuwa hii mihimili haikulenga mambo ya chini katika mhimili bali inalenga kugawanya uongozi wa nchi ili kuwa katika safe side kuepuka wananchi kuporwa madaraka. mababu zetu kwa uzoefu wao waligundua ukiwa na chombo kimoja ni rahisi sana wananchi kuporwa chombo hicho na kiongozi au viongozi lakini wakabaini ukiwa na vyombo mfano 3 kama havishirikiani na ukavilinganisha nguvu kuwa hakuna chombo cha kulalia kingine basi wananchi wanakuwa salama kwa maana chombo kimoja kikitaka kuasi vipo vyombo vingine kufanya kazi ya wananchi ya kurudisha mambo kwenye mstari.

hoja ya kuwa na mihimili mitatu
Mzee unaongea nini hasa maana una mambo kibao afu mchanganyiko!nikuulize swali hivi Tz hakuna mihimili 3?
 
Hii sio debate.. Utakuwa na tatizo kama utaiita hii ni debate.. Ndo maana ckupata shida kuandika niliyoyaandika.. Ungemsaidia kumjibia kwa kutaja hizo nchi ambazo zimeathirika kwa mfumo huu wa kupunguziwa madaraka..

Vinginevyo huna sababu ya msingi ya kuandika ulichoandika..

Nikicheck avatar yako tu nakuelewa wewe ni mtu wa namna gani!!! Hata sipati shida ya kuargue na wewe maana nafasi ya Urais katika nchi hujaielewa vizuri.
 
Nikicheck avatar yako tu nakuelewa wewe ni mtu wa namna gani!!! Hata sipati shida ya kuargue na wewe maana nafasi ya Urais katika nchi hujaielewa vizuri.

Ndio tatizo unapokosa hoja na kuja na viroja.. Hamna kitu ulichoandika cha ku-argue hapa.. Nimekuuliza swali umeshindwa kujibu kwa kuwa una ajenda yako..
 
Ili mjadala uendelee kuwa mzuri ndani ya JF, ni vema wachangiaji kujenga hoja. Si vema kusema kwa sababu unasema, sema kwa sababu kuna jambo la kusema ili wasomaji wapate kuelimika na kujifunza kitu kipya au kuendelea kupanua mawazo kwa kile alichokuwa nacho mwanzoni na kuongeza kitu kipya utakachoandikia jamii. Nashauri wachangiaji tutumie jamvi hili kujuzana kwa manufaa ya maendeleo yetu wenyewe na taifa kwa ujumla.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom