Mwakaboko King
JF-Expert Member
- Apr 22, 2015
- 1,099
- 207
Kuna baadhi ya watu fulani wamekuwa na hasira kuhusu mamlaka ya Rais yaliyoanishwa kwenye Katiba Inayopendekezwa ile Sura ya nane,Kuanzia Ibara ya 80 mpaka 98. Watu hao wamefikia hatua ya kutaka apunguziwe mamlaka huku wengine hasira zao zikipitiliza wakitaka hata yale aliyonayo yaondolewe yote kabisa abaki kama mtumishi wa kawaida!
Jambo la kunishangaza ni pale watu hao wanaposhindwa kuelewa kuwa mamlaka au heshima ya mfalme ni wingi wa watu wake!wanashindwa kuelewa kuwa Mamlaka ya Rais ni wingi wa kura zake,hawezi kulinganishwa na mtu yeyote katika nchi na Katiba Inayopendekezwa ambayo wananchi wataipigia kura imelizingatia hili.
Kwa mujibu wa Katiba ya 1977 Tanzania tunao utaratibu wa kumpata Rais kupitia sanduku la kura (nguvu ya umma) ambazo humpa Mamlaka ya kuongoza na kutawala.Rais ni Mkuu wa Nchi,kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.
Kwa Tanzania Rais ni alama na taswira ya Jamhuri ya Muungano na watu wake na pia ni alama ya umoja ,uhuru wa nchi na mamlaka yake!
Sasa inawezekanaje Kiongozi Mkuu wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama vya nchi ukataka alinganishwe na mjumbe au mbunge au waziri? Hilo haliwezekani fuatilia nchi zote ambazo wamekubali upuuzi huu utaona marais wao ni kama mapambo tu na wana jina lao eti wanabaki kuwa Ceremonial hawana mamlaka ya maamuZi ya nchi wapo wapo tu, hili halikubaliki Tanzania Rais ni MAMLAKA hata UKAWA wanalijua hili ndo maana wanajaribu jaribu kuungana wakiamini kuwa watashinda nafasi ya Urais nao wawe na kiongozi mwenye mamlaka katika nchi.
Mungu Ibariki Tanzania!
Nawasilisha!