Katiba imekaa vizuri sana


Wewe pimbi unatakiwa kujua haki bila uwajibikiji ni 0 katibaa hii imetoa uwajibikiji kama tunu na viongozi hawaajibiki kabisa so sahau haya mambo ya kisiasa
 
Amir jeshi wa Tanzania ni nani? Je Rais wa Zanzibar anapigiwa mizinga kama nani? Sherehe za Mapinduzi nani anatangulia uwanjani?
Sasa mambo ya kupigiwa mizinga yako kwenye sheria sio kwenye katiba. Kumbuka hapa tunaongelea Katiba please tofautisha. Halafu mambo mengine ni ya itifaki tu sawa kaka. Jaribuni basi kupinga kwa hoja. Unaona sasa.
 
Wewe pimbi unatakiwa kujua haki bila uwajibikiji ni 0 katibaa hii imetoa uwajibikiji kama tunu na viongozi hawaajibiki kabisa so sahau haya mambo ya kisiasa
Mimi sijakuelewa. Hivi neno TUNU kwako lina maana gani?
Kwangu mimi najua Tunu ni zawadi spesho ambayo umebahatika kuwa nayo.
Hebu ngoja tuzitaje TUNU zilizo kwenye RASIMU ya Bunge:-
(a) lugha ya Kiswahili;
(b) Muungano;
(c) utu na udugu; na
(d) amani na utulivu.


Hebu niambie Uadilifu ni Zawadi?
 


Kwa nini ulinganishe na Nchi hizo?
Hujui kuwa UNITED Countris in Africa ni moja tu.
Duniani hazizidi Tano?
Nimejaribu kuweka vipengere vingi tu, vilivyo sahihishwa na kutoa vitu ambavyo vinabadilika.
Huwezi ukaweka maelezo marefu ya miiko ya watumishi wa umma kwenye katiba. sasa sheria zitafanya nini?
Huwezi ukaelezea kila kitu kwenye katiba ila katiba itatoa mwelekeo, kama hii ya sasa.
 
misingi ya utawala bora
 
Akishika dola CHADEMA au CUF au UKAWA wanavyojiita huoni kama kutakuwa na crisis? Lazima wataifanyia hiyo katiba fundamental changes na hiyo itakuwa katiba gani inayobadilishwa ovyo? Angalia nchi kama marekani akishika huyu au yule huwezi kubadilisha muundo wa serikali lakini hapa kila mtu ana lake kwa vile hakuna maridhiano kwa sababu CCM hakikusikiliza sauti za vyama vya upinzani
Pili, hamjajifundisha chochote kutokana na kura ya maoni ya scotland? Sasa hivi England wanalalamika wabunge wa scotland iweje wanajadili mambo yasiyowahusu. Huo ni muungano wa zaidi ya miaka 300. lakini it was inevitable. na hapa pia mpende msipende lazima Tanganyika itadai haki yake at some point, iwe sa hivi au baadaye tukiwa hatupo, iwe kwa amani au fujo. Lakini CCM hamjali vizazi vijavyo mnachokiona ni hapa na sasa hivi na vitambi vyenu.
 
Tatizo lako ndugu yangu unacomment tuuuuuuu. Hutoi ni vipengere vipi vitakavyo badilishwa? Sijui hata kama umeisoma hii Rasimu.Hebu nakuomba tujadili pointi kwa point. Niambie kifungu kipi kinacho weza kubadilishwa kwenye katiba wakiingia hao unaowasema?
 
Uhuru wa taaluma, ubunifu, ugunduzi na usanii

 

Kwahiyo hapa hoja ya UKAWA ni serikali 3, mambo mengine ya wananchi wao hayawahusu.
 

Unataka nikuwekee sura nzima ya saba hapa? Inaanza hivi;
SURA YA SABA
MUUNDO WA JAMHURI YA MUUNGANO
Muundo wa Muungano
70. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa na muundo wa Serikali
mbili ambazo ni:
(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano; na
(b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Ukibadilisha hapo umeshaibadilisha katiba nzima maanake msingi wa katiba ni muundo wa muungano. Hii katiba tunayo wote na nakuhakikishia kwamba nimeisoma mara mbili juu chini!
 

OK. Sasa wewe ulikuwa unataka Serikali tatu au moja au ya mkataba?
Ukotayari kujifunza mantiki ya serikali mbili?
Hebu soma vipengere vyote.
Halafu hebu niambie nitatizo gani kuwa na serikali mbili?
Kwasababu katika mantiki yako ya serikali tatu inatekelezwa kwa kuwa na makamu watatu wa rais
1. Makamu wa kwanza ndiye aliye na mamlaka kote
2. Makamu wa pili wa raisi ndiye Raisi wa zanzibar.
3 Makamu wa tatu wa rais ndiye mtendaji mkuu wa serikali kwa mantiki hiyo ndiye msimamizi wa mambo ya Muungano na mambo yote ya Tanzania bara.


Halafu ikumbukwe Makamu wa kwanza wa rais na makamu wa tatu wa rais wanasifa ya kuwa marais wa JMT ikitokea rais hayupo.

Serikali, Mahakama na Bunge vimetenganishwa.
Katika Rasimu ya pili Jaji na Spika walikuwa na uwezo wa kuwa Rais.

Huoni ingeleta mgongano wa maslahi. Maana Spika anaweza akashirikiana na wabinge au vyoyote kumuondoa rais.
Na ikubukwe kwenye Rasimu hii ya mwisho wabunge wanao uwezo wa kumuondoa rais madarakani.

Sijui umeelewa!!!!
 
Angalia hapa tena.


Mbona mkalia kutuambia masuala ya haki za wavuvi ,wakulima,wafugaji kwa nini hamsemi kama mbuge anaruhusiwa kugombea mpaka atakapochoka yeye! Mtu anayejua kusoma na kuandika anaweza kuwa mbuge determination ya mtu anayejua kusoma na kuandika unaijuaje? Manake hata STD VII wanamaliza hawajui kusoma na kuandika?kwa nini mumewaondolea wananchi mamlaka ya kumwajibisha Rais? Mmesema idadi ya wabunge ktk bunge iwe 50 kwa 50 bila hata kuonesha hyo inapatikanaje nakwambia hvi hii katiba endapo itapita mungu nijalie uzima ktk kipindi cha miaka 10 tu itafanyiwa amendment kwanza hatutakuwa na wazee kama wewe Bungeni
 

Sorry kumwajibisha mbuge
 
Kwahiyo hapa hoja ya UKAWA ni serikali 3, mambo mengine ya wananchi wao hayawahusu.
Hayo mambo yote ya wananchi bado yangepatikana iwe kwa serikali moja, mbili au tatu. Hiyo tu ni danganya toto ambayo CCM wanaitumia kuwahadaa wananchi kama wewe. Hivi unadhani kwa serikali tatu 50/50 ya wanawake isingepatikana? Au mambo ya wakulima, wavuvi, wachimba madini na kadhalika yasingezingatiwa? Mambo hayo yanatekelezeka kwa muundo wowote wa serikali kwa hiyo hoja yako haina mashiko!
 

Kwajinsi ulivyo comment unaonekana hujaisoma hii rasimu. Nakuomba nivyema ukaisoma badala ya kuleta bra bra hapa. hebu nipe kifungu kinachosema mbunge asiwe na kikomo.
 

Katiba ya warioba haikusema hayo.
Nakuomba ndugu unijibu maswali yangu mengi tu nimekuuliza unayakwepa kwepa tu.
 
Kwajinsi ulivyo comment unaonekana hujaisoma hii rasimu. Nakuomba nivyema ukaisoma badala ya kuleta bra bra hapa. hebu nipe kifungu kinachosema mbunge asiwe na kikomo.

Sio kifungu ni ibara vifungu vinaaply ktk acts eg Public service act no 8 of 2002 dk 2 nakuletea
 
Katiba ya warioba haikusema hayo.
Nakuomba ndugu unijibu maswali yangu mengi tu nimekuuliza unayakwepa kwepa tu.
Katiba ya warioba haingeongelea mambo hayo kwa sababu kwenye mfumo wa serikali tatu, hayo siyo mambo ya muungano! Hayo mambo yote yangetajwa kwenye katiba ya Tanganyika na katiba ya Zanzibar. CCM wamewatupia changa la macho tena wananchi kama wewe kwa kuwaambia eti mzisome rasimu zote mbili mzilinganishe wakati siyo sahihi kufanya hivyo! Ya warioba ilijikita kwenye yale mambo ya muungano tu! Mambo ya ardhi, vijana, wakulima, wavuvi na kadhalika yote yangetajwa kwenye katiba za nchi washirika. Sijui umeelewa?!
Umeniuliza swali moja tu nalo ni 'Kwahiyo hapa hoja ya UKAWA ni serikali 3, mambo mengine ya wananchi wao hayawahusu.' Naamini nimekujibu vilivyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…