Mpangawangu
JF-Expert Member
- Mar 5, 2014
- 887
- 965
Wakuu nimeona leo ni vema tudadavue juu ya dhana ya uongo anayo jipambanua nayo ZITTO kwa siku za hivi karibuni eti ya kuwa kwamba yeye ana unyerere na ujamaaa!!!
Tujiulize kupitia mfano wa kijana mdogo sana kwenye siasa za nchini,achilia mbali baba wa Taifa Nyerere anayeta kufanana naye
1.wakati ZITTO anaendesha Hammer kama gari ghali na la kifahari ya million zaidi ya 300 Mnyika kwa ubunge wake wote ana Toyota Vitz tuh ya isiyo zidi hata million 10.
2.wakati Zitto ni mtu wa kunufaika na feva za mashirika ya umma kama NSSF walimuonga Appartment aliyokuwa anaishi mama yake Tabata segerea,na akawa anaishi UDSM alikopewa makazi mchumba wake.mwenzie Mnyika
mpaka leo anaishi ghetto paepale sinza.
3.wakati Zitto mavazi yake ni suti za guchi na gharama kama bepari la kisasa ukiondoa yale magwanda aliyo lazimika kuyachoma motto,ajawahi kuvaa hata kaunda inayo fanana na zile za nyerere ili aonekane ni mnyerere,wakati huohuo Mnyika ajawahi kuvaa suti siyo tuh ya gharama bali hata ya kushonesha kwa fundi,vivazi vyake ni kaunda,gwanda na mashati ya batiki au vitenge
4.wakati Zitto anaamua kung'atuka na bunge kukubali kumpa posho zake zote baada ya kuombewa na mkuu wa nchi tofauti na ilivyo kuwa kwa Mansoori wa zanzibar ama Mpendazoe wa ccm 2010,tulitegemea kuona uzalendo wake kwa kukataa fedha ambazo so halali yake.Kama mnyika alivyo kataa posho zote anazopaswa kulipwa na Halamashauri ya Jiji la Dar es salaam,kwa miaka yake yote ya ubunge na kuwaambia wazipeleke kwenye taasisi za elimu na watoto yatima
5.ZITTO anajiita mjamaa wakati palipokuwa jimboni kwake huko kigoma kaskazini hajawahi hata sikumoja kukusanyika na wananchi wake na kufanya jambo lolote la kijamaa kama matengenezo ya barabara na uchimbaji wa mitaro,wakati myika tunaona ujamaa wake kwa kushinda nae kwenye vichochoro vya makurumla na mburahati mpaka manzese midizini na sisi kwa sisi.
6.Wakati Zitto ana akaunti za fedha ujerumani na kweingineko nje ya nchi,na huku waleti yake siku zote anatumia dollar wala siyo shillingi,Mnyika mwenzie anakaunti NMB tuh.benki ya makabwela.
MWISHO NAMALIZIA HIVI HAYO MAISHA YA KUIGIZA YA KIONGOZI MKUU WA ACT,hayana chembe wala vinasaba vya unyerere,Ndiyo maana hapa PRESS na waandishi wa habari huitishia SERENA na siyo kilabuni kwa ndumbiko au chini ya mti
Over.
Andiko lako limejaa chuki na mwendelezo wa mahangaiko dhidi ya anguko la chama.
Kwanza nakubaliana na wewe kuwa Mnyika ni mtu makini aliejaa weledi.
lkn unapomlinfanisha na Zitto unamdhalilisha zitto.
Kuhusu dhana ya Ujamaa,unamisconception,ujamaa sio umaskini,ujamaa hasa wa kisayansi (Scientific socialism)unaruhusu umiliki wa mali,muhimu ziwe hazikutokana na unyonyaji.
Msingi mkuu wa ujamaa ni usawa,hapa haimanishi wote tuishi nyumba za Nyasi au wotr tutembelee magari yanayofanana.
Usawa unaozungumziwa ni ile wa kuwa na fursa sawa kutumia rasilimali za taifa.
Kuwa na fursa sawa katika huduma.
Mfano ,Kuwepo na shule bora ambazo sifa za kujiunga zitakuwa bayana na hivyo yeyote mwenye sifa hizo apatiwe nafasi bila kujali ni mtoto wa nani.
Hapo nyuma tulikuwa na shule za vipaji kama vile Tabora boys,Msalato,Mzumbe,Kibaha,Mazengo n.k shule hizo walisoma watoto ea viongozi na wale wa makapuku katika darasa moja bila ubaguzi.
Watoto walipata fursa sawa katika elimu tofauti na sasa ambapo wenye Fedha wanapata elimu bora kuliko watoto wa makapuku.
Kuhusu Unyerere kati ya Zitto na Mnyika hakuna aliefikia kile kiwango cha uzalendo lkn ukiwalinganisha Zitto na nyika Zitto ni mzalendo zaidi ya mnyika.
Wotr wakati ni wabunge wa chadema walikubaliana kupinga posho bungeni.
Lkn ni zitto pekee ambae umma ulimshuhudia akizikataa posho kwa vitendo
Ni zitto aliegomea posho tangu 2011,
Tangu 2011 Mnyika anachukua posho kinyume na Ilani ya chadema ya 2010.
Zitto alikataa kulipwa posho wakati wa Bunge la katiba,hakuchukua hata kumi lkn Mnyika na wenzake walizichukua.
Zitto unaweza kumpinga kwa chuki zako lkn anania ya dhati na taifa hili.
tumia muda Wako kuusoma. ujamaa ili usiendelee kupotosha watu kwa vivu usivyovijua