Kati ya Zitto na Mnyika nani mjamaa?

Kati ya Zitto na Mnyika nani mjamaa?

asanusye

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
216
Reaction score
131
Wakuu nimeona leo ni vema tudadavue juu ya dhana ya uongo anayo jipambanua nayo ZITTO kwa siku za hivi karibuni eti ya kuwa kwamba yeye ana unyerere na ujamaaa!!!

Tujiulize kupitia mfano wa kijana mdogo sana kwenye siasa za nchini,achilia mbali baba wa Taifa Nyerere anayeta kufanana naye
1.wakati ZITTO anaendesha Hammer kama gari ghali na la kifahari ya million zaidi ya 300 Mnyika kwa ubunge wake wote ana Toyota Vitz tuh ya isiyo zidi hata million 10.

2.wakati Zitto ni mtu wa kunufaika na feva za mashirika ya umma kama NSSF walimuonga Appartment aliyokuwa anaishi mama yake Tabata segerea,na akawa anaishi UDSM alikopewa makazi mchumba wake.mwenzie Mnyika
mpaka leo anaishi ghetto paepale sinza.

3.wakati Zitto mavazi yake ni suti za guchi na gharama kama bepari la kisasa ukiondoa yale magwanda aliyo lazimika kuyachoma motto,ajawahi kuvaa hata kaunda inayo fanana na zile za nyerere ili aonekane ni mnyerere,wakati huohuo Mnyika ajawahi kuvaa suti siyo tuh ya gharama bali hata ya kushonesha kwa fundi,vivazi vyake ni kaunda,gwanda na mashati ya batiki au vitenge

4.wakati Zitto anaamua kung'atuka na bunge kukubali kumpa posho zake zote baada ya kuombewa na mkuu wa nchi tofauti na ilivyo kuwa kwa Mansoori wa zanzibar ama Mpendazoe wa ccm 2010,tulitegemea kuona uzalendo wake kwa kukataa fedha ambazo so halali yake.Kama mnyika alivyo kataa posho zote anazopaswa kulipwa na Halamashauri ya Jiji la Dar es salaam,kwa miaka yake yote ya ubunge na kuwaambia wazipeleke kwenye taasisi za elimu na watoto yatima

5.ZITTO anajiita mjamaa wakati palipokuwa jimboni kwake huko kigoma kaskazini hajawahi hata sikumoja kukusanyika na wananchi wake na kufanya jambo lolote la kijamaa kama matengenezo ya barabara na uchimbaji wa mitaro,wakati myika tunaona ujamaa wake kwa kushinda nae kwenye vichochoro vya makurumla na mburahati mpaka manzese midizini na sisi kwa sisi.

6.Wakati Zitto ana akaunti za fedha ujerumani na kweingineko nje ya nchi,na huku waleti yake siku zote anatumia dollar wala siyo shillingi,Mnyika mwenzie anakaunti NMB tuh.benki ya makabwela.

MWISHO NAMALIZIA HIVI HAYO MAISHA YA KUIGIZA YA KIONGOZI MKUU WA ACT,hayana chembe wala vinasaba vya unyerere,Ndiyo maana hapa PRESS na waandishi wa habari huitishia SERENA na siyo kilabuni kwa ndumbiko au chini ya mti
Over.
 
Ujamaa ni imani, moyo kabla ya silaha.
 
yah! nilishangaa kwenye hili bunge la juzi kumuona mnyika kwenye vitz dah nikajiuliza mbona kazi kubwa anayofanya mnyika bungeni haviendani na gari anayotembelea!!!!!!! viongoz wengine igeni mfano wa mh mnyika,mnyika hakika ndiye mjamaa na wala sio zitto
 
ebu leteni picha ya lile ghorofa la zito analojengewa na ma-ccm pale dodoma!
 
Hivi kutembelea Vitz ndio ujamaa? Kuna watu mjini hapa wana maghorofa hata nane lakini wengine wanatumia bajaji kama vyombo vya usafiri. Acheni kudanganyana.
 
Mzalendo na Ujamaa ulikuwa ni kwa Mwalimu tu, wengine hebu tuache usanii!!
 
Nadhani watu hamjui maana ya ujamaa, na kama hiki pia ndicho alichokimaanisha Zitto aliposema ni mjamaa, hata yeye hajui maana ya ujamaa.
 
Zitto mjamaa ila ana mashamba eti yanayopita 300million!!!!

Mjamaa ila ana nyumba mbili huko Kigoma zenye thamani zaidi ya 250 million!!

Mjamaa ila ana kampuni lukuki zinazofanya biashara na mashirika ya umma huku akiwemo pia kwenye vitalu vya gesi!!!

Kwa wataalamu wa body language ukimtazama tu kwa umakini usoni bwana Zitto utamuona kajaa unafiki na hila!!!!
 
Last edited by a moderator:
Dhana ya Ujamaa ni ngumu, watu wanaropoka tu ujamaa - hebu soma hiki kipande kinachoeleea ujamaa then compare na dunia / Tanzania ilivyo sasa.

"Nchi yenye Ujamaa kamili ni nchi ya wafanya kazi; haina ubepari wala ukabaila. Haina tabaka mbili za watu: tabaka la chini la watu wanaoishi kwa kufanya kazi, na tabaka la juu la watu wanaoishi kwa kufanyiwa kazi. Katika nchi ya Ujamaa kamili mtu hamnyonyi mtu, bali kila awezaye kufanya kazi hufanya kazi, na kila mfanya kazi hupata pato la haki kwa kazi aifanyayo na wala mapato ya wafanya kazi mbali mbali hayapitani mno."
 
Hivi kutembelea Vitz ndio ujamaa? Kuna watu mjini hapa wana maghorofa hata nane lakini wengine wanatumia bajaji kama vyombo vya usafiri. Acheni kudanganyana.

Makada wa CCM kama sio wanafiki hembu tuambieni ni kipi kinachowafanya mmtetee Zitto na kumpigia chapuo??!!!

Nini haswa anawakuna kiasi ya kwamba mpo tayari kushinda mitandaoni mkimwandikia mapambio???!!
 
Mimi nashindwa kuelewa kwanza kama Zitto anaelewa maana ya neno ujamaa.
 
kwa kuwa umemtaja zitto kwa sifa hizi sina hakika kama huu uzi utaendelea kukaa
 
Uzalendo zitto anautoa wapi? Kama ameshatangaza nia ya kuwakimbia wananchi wake wa kigoma kaskazini na kukimbilia majimbo mengine. Je uzalendo uko wapi?
 
Hilo nalijua lakini hatukati tamaa,najua wakisemwa wengine sawa na akisemwa Zitto imesemwa JF.ila ipo siku tutakuja hapa na picha za vikao vya siri.hizi sio zama za msaki wa mwananchi,ZITTO alipokuwa anaamua mpaka kicha cha habari kiweje kesho.na kweli kinatokea vilevile kama alivyo panga.na Mjue Dunia haina siri,iwe kikao cha siri au simu ya siri akisha piga huwa anatabia ya kujitamba.
 
mkuu all the best katika mapambano ya ccm kwa kivuri cha ACT
 
Uzalendo zitto anautoa wapi? Kama ameshatangaza nia ya kuwakimbia wananchi wake wa kigoma kaskazini na kukimbilia majimbo mengine. Je uzalendo uko wapi?
sasa kama nyumbani ameshindwa kuonesha uzalendo hadi amewakimbia unategemea atauonesha wap?
 
Kwangu mimi "mzalendo" ndio jina la muhimu zaidi kuliko mjamaa. Kwa watanzania wengi ujamaa imebaki kama imani fulani tu. Ujamaa ulimanisha umiliki wa pamoja wa rasilimali, ushirikiano katika shughuli za kijamii, n.k
Uzalendo ni kujitoa kwa ajili ya jamii kwa kutanguliza zaidi maslahi ya jamii husika zaidi ya yalebya binafsi.
Tutafakari kama taifa wazalendo wapo ? Na kama wapo ni kina nani. Tunaposema tuna wajamaa tunadanganyana mchana kweupe! Mwalimu Nyerere aliondoka na falsafa yake!
 
Wakuu nimeona leo ni vema tudadavue juu ya dhana ya uongo anayo jipambanua nayo ZITTO kwa siku za hivi karibuni eti ya kuwa kwamba yeye ana unyerere na ujamaaa!!!

Tujiulize kupitia mfano wa kijana mdogo sana kwenye siasa za nchini,achilia mbali baba wa Taifa Nyerere anayeta kufanana naye
1.wakati ZITTO anaendesha Hammer kama gari ghali na la kifahari ya million zaidi ya 300 Mnyika kwa ubunge wake wote ana Toyota Vitz tuh ya isiyo zidi hata million 10.

2.wakati Zitto ni mtu wa kunufaika na feva za mashirika ya umma kama NSSF walimuonga Appartment aliyokuwa anaishi mama yake Tabata segerea,na akawa anaishi UDSM alikopewa makazi mchumba wake.mwenzie Mnyika
mpaka leo anaishi ghetto paepale sinza.

3.wakati Zitto mavazi yake ni suti za guchi na gharama kama bepari la kisasa ukiondoa yale magwanda aliyo lazimika kuyachoma motto,ajawahi kuvaa hata kaunda inayo fanana na zile za nyerere ili aonekane ni mnyerere,wakati huohuo Mnyika ajawahi kuvaa suti siyo tuh ya gharama bali hata ya kushonesha kwa fundi,vivazi vyake ni kaunda,gwanda na mashati ya batiki au vitenge

4.wakati Zitto anaamua kung'atuka na bunge kukubali kumpa posho zake zote baada ya kuombewa na mkuu wa nchi tofauti na ilivyo kuwa kwa Mansoori wa zanzibar ama Mpendazoe wa ccm 2010,tulitegemea kuona uzalendo wake kwa kukataa fedha ambazo so halali yake.Kama mnyika alivyo kataa posho zote anazopaswa kulipwa na Halamashauri ya Jiji la Dar es salaam,kwa miaka yake yote ya ubunge na kuwaambia wazipeleke kwenye taasisi za elimu na watoto yatima

5.ZITTO anajiita mjamaa wakati palipokuwa jimboni kwake huko kigoma kaskazini hajawahi hata sikumoja kukusanyika na wananchi wake na kufanya jambo lolote la kijamaa kama matengenezo ya barabara na uchimbaji wa mitaro,wakati myika tunaona ujamaa wake kwa kushinda nae kwenye vichochoro vya makurumla na mburahati mpaka manzese midizini na sisi kwa sisi.

6.Wakati Zitto ana akaunti za fedha ujerumani na kweingineko nje ya nchi,na huku waleti yake siku zote anatumia dollar wala siyo shillingi,Mnyika mwenzie anakaunti NMB tuh.benki ya makabwela.

MWISHO NAMALIZIA HIVI HAYO MAISHA YA KUIGIZA YA KIONGOZI MKUU WA ACT,hayana chembe wala vinasaba vya unyerere,Ndiyo maana hapa PRESS na waandishi wa habari huitishia SERENA na siyo kilabuni kwa ndumbiko au chini ya mti
Over.

Hivi mnyika ndo nani mkuu, embu fafanua kidogo!
 
Kama humjui mnyika NENDA MILEMBE.......this platform is too heavy to be carried by tabularasa like you...............ukishatoka milembe pitia pale kwa mama makinda pia atakusaidia kukufafanulia ni nani huyo..............hapa tuache wenye misuli ya ubongo pekee.samahani kama nimekukwaza lakini.niwie radhi ndivyo nilivyo,majibu yangu yapo straight sana
 
Back
Top Bottom