Kati ya ndugu zako wa damu wote ni yupi unaempenda zaidi?

Nampenda mtoto wa mama yangu mdogo
i just love her yani na tumefanana mno huwa namuwasilisha kama mwanangu na 100% wanajua ni mwanangu
nampenda kuliko hata first born wangu..
Inashangaza kidogo ina nakubali....kuna vitu vinakuja automatically
 
Fohadi Mie ndugu yangu nayempenda zaidi ni sister yangu ambaye tumefuatana we share a lot in common!

My bro first borne tumeenda astray kwa itikadi na mambo mengi tho we still brothers. We have social connection ila sio kama na sisteri wangu!
nakujua wewe huwezi enda proportional na bro...lazima tu muachane njia panda....maana matunda ya kimasihara unayachuma sana hahahahhah.

ila kweli, hata mimi kuna ndugu zangu wawili kati ya hao kupiga nao story daaaah ni nadra....huwaga hatuwasiliani kama hatuna inshu zakuambiana..na kama tukiwasiliana kwa simu basi ni salamu tu na kutakiana maisha mema..zile mood za kujadili mipango ya kila mmoja wetu ni 25%...Hatuna ugomvi na tunapendana sana ila tu hatufatiliani
 
nakujua wewe huwezi enda proportional na bro...lazima tu muachane njia panda....maana matunda ya kimasihara unayachuma sana hahahahhah.

ila kweli, hata mimi kuna ndugu zangu wawili kati ya hao kupiga nao story daaaah ni nadra....huwaga hatuwasiliani kama hatuna inshu zakuambiana..na kama tukiwasiliana kwa simu basi ni salamu tu na kutakiana maisha mema..zile mood za kujadili mipango ya kila mmoja wetu ni 25%...Hatuna ugomvi na tunapendana sana ila tu hatufatiliani
Hahahah tuna gap sana hapo katikati! Almost 10 years!
 
Dah....inatokea, hata vidole havifanani urefu.

Mimi kwa kweli sina ndugu ambaye naweza sema ni "rafiki" yangu/tumeshibana hasa.

Wote tunapendana, lakini kikawaida tu.

BTW, mleta mada(Fohadi ) kwa nini hutaki dogo wako ajue unampenda? Unaogopa nini? Vizuri ajue, ili iwe rahisi ku reciprocate, ama?
 
Alizaliwa miaka 8 baada yangu. Nikiwa mtoto wa 3 kuzaliwa kati ya watoto 5, huyu yeye ndie kitinda mimba cha Mama Fohadi na ndiye kaka wa mwisho wa familia. Japokuwa nina upendo wa dhati kwa ndugu zangu wa damu wote ila upendo kwa huyu jamaa naona kabisa umepitiliza. Hajui na hakuna anejua ila mimi binafsi ndiye ninaejua.

Nikiwa na miaka 11, yeye alikuwa na miaka 3. Kipindi hicho nilikuwa kila nikitoka shule lazima niende uwanjani kucheza chandimu na watoto wenzangu. Mara nyingi kati ya hizo, nilikuwa nambeba mgongoni naenda nae hadi uwanjani, namkalisha sehemu mimi nacheza mpira nikimaliza tunarudi wote home. Nilikuwa napenda sana kutembea nae popote pale na siku zote nilitamani kumfanya awe proud na sisi wakubwa zake.

Nikiwa kama Kaka mkubwa katika familia nilitamani kumuonesha upendo na raha ya kuwa na kaka mkubwa kwani sikubahatika kuwa na kaka mkubwa. Mimi ndiye mtoto wa kiume wa kwanza katika familia yetu. Kwetu sisi, mtoto wa kwanza na wapili wote ni wakike na sisi tuliobaki (3,4,5) wote ni wakiume huku mimi nikiwa ndiye 'brother kaka'.

Wakati fulani nimemaliza NECTA ya form two, nilikuwa siendi shule hivyo kila siku nilikuwa namsindikiza asubuhi hadi shule kule alikokuwa anasoma chekechea. Sio kwamba asingeweza kufika peke yake hapana, ila nilitamani nimuoneshe kuwa mimi ni mmoja wa kaka zake na anapaswa kujivunia mimi/sisi.

Sikumbuki kama kwenye maisha yangu ya kujitambua nimewahi kumpiga yule dogo. Sikuwahi kumdekeza ila sikuwahi kuwa katili kwake. Pengine kutokana na gap kubwa la umri kati yetu, kadri miaka ilivyokuwa inasonga ndivyo tulivyozidi kuwa sio watu wa story nyingi.

Miaka imekatika, leo dogo amemaliza kidato cha nne na anajitambua. Pamoja na kukua kiumri, ila bado namchukulia kama yule yule niliyekuwa nambeba mgongoni. Kwa wakati huu ndipo nimegundua nampenda sana huyu jamaa kuliko ndugu zangu wengine japo wote nawathamini na kuwapenda. Juzi dogo kanipigia simu akanambia anatamani sana nimpeleke kwa mkapa tukaangalie Derby ya kariakoo. Sikuweza kukataa ila pia kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu (mimi na yeye) hatukuweza kwenda uwanjani na pengine Mungu alitaka hela zetu za viingilio zipone. Hakuna ombi ambalo amewahi kuniomba nikakataa. Ila ile request yake ilinifanya nifikilie zaidi jinsi gani mkubwa anabeba tumaini la wadogo zake when they face imposibilities.

Mara nyingi kila nikimuangalia huwa najiona nipo responsible kwa ajili ya kesho yake. Hajui kina cha upendo wangu kwake kilivyo na sitataka hata siku moja ajue. Ila kiukweli harakati zangu zote za kimaisha ambazo huwa nazifanya kwa kutokata tamaa yeye huwa ni mmoja wa watu wanaonipush kuzidi kupambana zaidi ili siku moja niwe funguo ya dunia yake awe anachotaka.

Hata mimi sijui kwanini nampenda sana, sifahamu labda kwakuwa ni last born nampa upendo ulio jaa huruma ndani yake.. Kitu pekee ninachojua ni kuwa huyu nampenda sana kuliko ndugu zangu wengine. Wale ndugu zangu 3 upendo wangu kwao ni 100% ila huyu ni zaidi ya 100%.

Ninamshukuru Mungu sina ndugu ninaemchukia kati ya ndugu zangu. Wewe unampenda nani zaidi kati ya ndugu zako wa damu? Kwanini huyo?

big up sana bro...
 
Sisi tupo wa4....mimi ni wa3...!!tumegawana yaan namba 2 na 4 ndo wanapatana vbaya mno...wanasaidiana kwenye kila sehem...na hua hata wakinileteaga malalamiko yao hua sishughulikii

Mimi namba 3 nnapatana na namba 1....almost kila kitu tunaambiana...!!matatizo tunasaidiana...!!na wao hawatunigilii...!!

Mda pekee tunaokua pamoja ni kwenye masuala ya mzazi...!!maendeleo ya familia
 
Huwaga napenda threads za family kama hivi

Bwana weee... ninao ndugu weengi kwa baba na kwa mama wawili. Hakuna kitu napenda kama familia. Koote naclick. Ila nimekua zaidi na hawa wawili. Ikatokea siku nimeshindwa kuprovide kitu toka nasoma roho inaniumaaaaaaa mpk najisikia kulia. Si kwamba nalipa ada hapana. Ila napenda kuwaspoil. Wote wawili ni boys. Nawapenda sana. Ila last born mkorofi sana pumbav zake anadekezwa sana na mamake. Nakapenda ila nayefatana naye ndo tunapatana sana. Tumekua wote. Tumesoma wote boarding toka primary. Yaani siku ya wali shuleni ama kila kitu matron ama masister wakiangalia pembeni tu nammiminia mdogo wangu chakula sijui nyama sijui nn kwahiyo kwenye suala la kula haataaaa hakua na shaka juu ya kushiba. Pia kulikua na duka lanaitwa kijiweni. Kipocket money changu nampa mfanyakazi ama dayscholar aniletee madonati nilikua prefect kwahiyo akija tu nakua getini napokea nampa na mdogo wangu.

Kuna siku dogo alikua agha khan anafanyiwa operation sasa nikawa hospitalu mimi na mama. Wallet yake anataka aiache kabla aingie theatre mama akadakia inipe nikutunzie dogo akamjibu si labda uniue. Akainipa mimi. Mama akasema kwahiyo munanisaliti.

Kuna siku nikawa na helaaaa weee.. mama akanigandaaaa balaaaa nimuazime.. huwezi amini nilimnyima niliapa sigawi hata sumni hata kukopesha kwa riba. Basi bwana, tumekaa kidogo dogo akanitwangia ananambia aisee sister nimekwamaaa nahitaji hela mambo mengi sana. Nikamwuliza amekuambia mamako eh? akaliruka hilo swali. Akanitajia amount anayotaka. Nikamjibu sasa hivi unapokea mzigo... nikafika kwa wakala chaap 1m ikasoma kwake. Nikaja mdai anipe 300k ingine nikamwambia basi bwana we ni ndugu yangu na mm nitapata shida ila mama ndo nilimkunjia bana. Nampenda sana dogo. Tumebondana sana enzi za utoto hadi kuombeana vifo
 
Dah....inatokea, hata vidole havifanani urefu.

Mimi kwa kweli sina ndugu ambaye naweza sema ni "rafiki" yangu/tumeshibana hasa.

Wote tunapendana, lakini kikawaida tu.

BTW, mleta mada(Fohadi ) kwa nini hutaki dogo wako ajue unampenda? Unaogopa nini? Vizuri ajue, ili iwe rahisi ku reciprocate, ama?
akijua haitakuwa siri tena...anaweza akavimba au akaanza kutumia hiyo weakness 'kuniumiza' vibaya...na kikubwa zaidi ndugu zangu wengine wakijua itakuwa vibaya sana kwao..ninaweza leta disunity fulani..na ndio maana hata wazazi wana mtoto wao wanaempenda kuliko wote ila hawawezi kuweka hadharani....nimeamua nibaki na siri yangu.
 
Back
Top Bottom