Kati ya Mkuu wa Majeshi(CDF) na Mkuu wa Jeshi la Polisi(IGP) nani ana cheo kikubwa?

Na kukiwa na vurugi ndani ya nchi, nani mwenye mamlala ya kutoa order??
Atatoa order IGP, mambo yanapomzidi ama ataomba msaada akapewa askari ambao watakua chini yake kama ilivyotokea mapango ya Amboni au bila kuombwa msaada CDF anaweza kuingiza vikosi vyake kutuliza ghasia na hii ikitokea IGP atapokea amri toka kwa CDF
 
jeshi LA polisi lipo ndani ya wizara ya mambo ya ndani pamoja na magereza,zimamoto na uhamiaji,jeshi LA wana nchi lipo wizara ya ulinzi ivyo wote ni wakubwa kwa nafasi zao acha kudanganya polisi aipo ndani ya Jwtz

kweli wewe Askari Muoga!!
 
Kama umesoma andiko langu vizuri utanielewa nimesema
kuhusu CDF
" CDF huyu ni kiongozi wa majeshi ya Ulinzi tu ambapo ndani yake kuna kamandi 4 ambapo kila kamandi kuna mkuu wake ambapo wote wanareport kwa CDF"

Kuhusu IGP nimesema
" IGP ni kiongozi wa vikosi vya usalama ambapo vipo 4 lakini ndani ya vikosi hvyo kuna wakuu wake
1 Police
2 Uhamiaji
3 Magereza
4 Fire"

Ukiangalia kwenye CDF kamandi zote wakuu wake (WANAREPORT) kwake pia na wakuu wa kamandi hzo wanateuliwa na Rais

kwenye IGP hakuna neno (KUREPORT) kwa IGP kwa wakuu wa vikosi hvyo vya Usalama nadhani tofauti umeiona hapo vikosi vyote hyo vya Police, Uhamiaji, Fire na Magereza vyote vipo ndani ya wizara moja ya mambo ya ndani na wote kazi zao zinategemeana ukiangalia Uhamiaji hawana Sero za kuwaweka wahamiaji haramu lazima watawekwa kwenye Sero za Police na kutoka Police ni mahakamani from there utakutana na Magereza kuhusu Fire hawa ni kama Police tu ndio maana unaweza kuona mkuu wa Fire alikuwa ni Police tena kutoka vikosi vya polisi kabisa na unaposema Seniority hapo wote seniority wao ni IGP
Sio Kweli kwamba IGP ni Mkuu wa vikosi vya usalama hapo ndo unapokosea. Kama ni hivyo kwa nini CDF asiwe Mkuu wa Polisi kwa sababu Anaitwa anaitwa Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama.

IGP ni kiongozi wa Polisi tu, kila jeshi hapo Linajitegemea. Ila IGP ni senior Kwa hao wengine kwa mujibu Wa seniority ya kijeshi. Kama ilivyo kwa CDF alivyo senior kwa IGP. Kuingiliana kwa majukumu ya Magereza na Polisi na Uhamiaji hakufanyi kuwa Mkuu wa hayo majeshi.

Kila Jeshi likisha pewa Mamlaka Linajitegemea. Wakati wa KAR jeshi lilikuwa moja na Polisi walikuwa ndani yake pamoja na magereza. Polisi ilipoanzishwa Magereza ilikuwa ndani ya Polisi. Magereza ilipoanzishwa ikatoka ikawa idara then Jeshi kamili. Hivyo wanajitegemea hakuna uhusiano wa madaraka zaidi ya kazi na seniority ya kijeshi tu.

Unapozungumzia usalama kumbuka hata TISS wapo humo, je IGP ni kiongozi wa TISS??
 
Sio Kweli kwamba IGP ni Mkuu wa vikosi vya usalama hapo ndo unapokosea. Kama ni hivyo kwa nini CDF asiwe Mkuu wa Polisi kwa sababu Anaitwa anaitwa Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama.

IGP ni kiongozi wa Polisi tu, kila jeshi hapo Linajitegemea. Ila IGP ni senior Kwa hao wengine kwa mujibu Wa seniority ya kijeshi. Kama ilivyo kwa CDF alivyo senior kwa IGP. Kuingiliana kwa majukumu ya Magereza na Polisi na Uhamiaji hakufanyi kuwa Mkuu wa hayo majeshi.

Kila Jeshi likisha pewa Mamlaka Linajitegemea. Wakati wa KAR jeshi lilikuwa moja na Polisi walikuwa ndani yake pamoja na magereza. Polisi ilipoanzishwa Magereza ilikuwa ndani ya Polisi. Magereza ilipoanzishwa ikatoka ikawa idara then Jeshi kamili. Hivyo wanajitegemea hakuna uhusiano wa madaraka zaidi ya kazi na seniority ya kijeshi tu.

Unapozungumzia usalama kumbuka hata TISS wapo humo, je IGP ni kiongozi wa TISS??
Mkuu mbona mnampatia CDF cheo ambacho si chake? Hakuna cheo kinachoitwa mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama bali kuna cheo cha amiri jeshi mkuu wa vikosi vya ulinzi na usalama ambae ni Rais bhasi

CDF ni mkuu wa majeshi ya Ulinzi tu yani Defense force kama jina la cheo chake hilo la usalama linapatikana wapi?
Tafuta barua ya ikulu ya uteuzi wa Mabeyo ambae ni CDF then angalia ameandikwa ni mkuu wa majeshi gani tatizo kuna kusikia kitu na kukifanya ndicho au ndio ilivyo kumbe sivyo yule ni mkuu wa majeshi ya Ulinzi tu nasema kitu ninachokifahamu

Kuhusu Tiss kuwa nayo ni moja ya usalama nayo si kweli hata kidogo Tiss ni intelligence agency kwa maana ya taasisi au idara ya kijasusi watu wanaodeal na usalama ni Police forces
DG ndie kiongozi wa ujasusi (intelligence) hii sio jeshi wala Vikosi hii ni idara au taasisi ndio maana Duniani hakuna intelligence yeyote inayoitwa Jeshi au Vikosi Intelligence zote zinaitwa Agency kwa sababu vinaweza kuingia sehemu yeyote ikiwamo Kwenye Ulinzi na Usalama na Ku operate kama civilian ndio maana leo jeshini kuna kitengo cha intelligence na pia Police kuna kitengo cha intelligence na hata sehemu yeyote mtu kutoka taasisi ya intelligence anaweza kufanya kazi lakini leo huwezi kukuta Mwanajeshi anafanya kazi Police au Police yuko jeshini rabda pawepo na missions ndo inaweza tokea mix ya namna hii
Kazi ya Intelligence ni kudeal na ku operate na vitu vyote lakini in silence way
ndio maana kiongozi wa intelligence jina lake ni Director sasa wote tunajua neno Director linasound civilian sana tofauti na IGP ,CDF

Na kama itathibitika CDF ni mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama nipo tayari kupumzika wiki mbili nipigwe ban Mod lakini CDF ni mkuu wa majeshi ya Ulinzi tu hausiki na Usalama hata kidogo
 
Huelewi kitu na ndio maana mnatusumbua humu kuwaelimisha.

Unaelewa kuna Jeshi la Nchi kavu(infantry),Jeshi la Anga(airforce),Jeshi la Majini(navy),Jeshi la kujenga Taifa nk?.

Hivi unaelewa Jeshi la Nchi kavu halina Ndege vita hata moja?

Hivi unaelewa Jeshi la Anga halina Kifaru hata Kimoja ?.

Kwa taarifa yako Jeshi sio lazima liwe na Kifaru,Ndege au Submarine(Nyambizi).

Marekani wapo wenye akili kama zako wanaamini Jeshi lazima liwe na Ndege zisizo na Rubani(drones) pamoja na Makombora ya Nyuklia.Wanaamini Afrika hakuna nchi yenye Jeshi.

Safi kabisa = hapo umejijibu mwenyewe rafiki. ndio maana kiingereza wakaita CDF Maana yake chief of defence forces nimepigia msitari neno forces. linawakilisha hayo majeshi ya anga, nchi kavu, majini n.k. kwa ujumla ndio huitwa defence forces, ila sio police wala magereza wala uhamiaji au zima moto. they are not defence forces!! ki ukweli umenirahishia kujibu. barikiwa.
 
Jiongeze tena kidogo kwamba kama JWTZ wakienda kufanya kazi za Polisi kama kushambulia majambazi au kusimamia uchaguzi wanakuwa na vyeo gani na nani anakuwa link ili waelewane kwenye mbinuna nani anatoa order?
Jwtz wakienda kushambulia majambazi watatumia mbinu za kijeshi walizofundishwa depo .so hawatapokea order kutoka kwa polisi na pia polisi hawatahusika maeneo hayo
 
Karibu duniani. Marekani wanapoenda Syria wanapiga viwanja vyao vya ndege bila ruhusa ya mtu yeyote, unadhani hilo halionyeshi US ni wakubwa kuliko Syria? - Mkubwa ni Mkubwa tu hata kwenye vifaa vizito. CDF ni mkubwa kwa IGP - na tofauti ni zana nzito - angalia maandamano yakitokea alafu polisi waite Jeshi, Polisi lazima waondoke maana wanaweza kuchanganywa.

level yoyote ya US kulinganisha na Tanzania, ya US ni kubwa; this is common sense. Generali wa US ni mkubwa kwa Generali wa Tanzania, ANYDAY!

Kuwa na Vifaa ni swala la aina ya kazi.Haimaanishi kwa sababu ana vifaa ndio awe mkubwa kwa idara zisizomhusu.

Hata General wa Jeshi la Marekani anaongoza Jeshi lenye vifaa hatari sana duniani na vifaa vyao vinalizidi Jeshi letu kwa mbali sana lakini haina maana kwamba Jenerali wa Marekani ni Mkubwa kwa Jenerali wa Tanzania au Brigedia wa Jeshi la Marekani ni mkubwa kwa Brigedia wa Jeshi la Tanzania.Heshima inabaki palepale bila kujali idadi za Zana za Kivita unazomiliki.
 
F******##### James delicious mkubwa wewe
Unajisikiaje unaponitolea matusi wakati sijakutukana?

Ukitaka matusi nayafahamu ila haina maana kwa sababu hatujuani kunitusi ni sawa kumuongelesha msukuma kizaramo
 
CDF ni Chief of defence force(Military force),
Polisi sio defence force!
Sio kweli kama police sio defence force au twende kwa kiswahili tutaelewana CDF ni kamanda wa vyombo vya ulinzi na usalama ambayo inajumuisha JW, JKT, Mgambo, TAKUKURU, USALAMA, POLICE, PRISON, FIRE na UHAMIAJI
 
Mkuu wa majeshi ndo mkubwa ipo hivi CDF ni mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wakati huo IGP NI mkuu wa jeshi la polisi .......CDF vyombo vyote vya ulinz ns usalama yy ndo mkuu
 
Back
Top Bottom