Kati ya Mkuu wa Majeshi(CDF) na Mkuu wa Jeshi la Polisi(IGP) nani ana cheo kikubwa?

Na hauwez kuthibitisha, mpk pale siku tz itakapoingia mzigon , tutaona km igp ndiye atakaye enda kuongoza frontline, maana iv iv naona hauwez kuelewa mkuu, mm sio MWANASIASA au mwanasheria nianze kutafuta vifungu vya katiba, km iyo biblia kna vfungu vng tu sivijui , ila nachoandika ndiyo nachojua
Ndio tatizo linapokuja,usikubali kitu bila kuonyeshwa kinasimama wapi kwenye katiba au sheria.

Vitu havipo tunavyoambiwa bali tunavyothibitishiwa kwa reference inayojisimamia.

Sasa ukiambiwa tu na huna reference na ukabaki kuimba kama kasuti watu watakushangaa.
 
Katiba haisemi ivo, kwa nchi inayoongozwa kikatiba mambo yote hutokana na katiba huwezi kujisemea kwa utashi wako tu.

Katiba tuliyonayo(1977 inawatambua polisi, magereza na jwtz kama majeshi, ila katiba pendekezwa( rasimu ya waryoba inawatambua magereza kwamba sio jeshi isipokua polisi na jwtz ndio majeshi tu.

Magereza wanaachwa kwa sababu hawapo kwenye Muungano, ndio maana tunaita Magereza Tanzania bara na kuna magereza Zenji(wanajitegemea).
Kwa mantiki hiyo polisi, magereza na jwtz ni majeshi ila utata unakuja kutokana na sisi kutazama mifano ya nchi zingine kama USA polisi huitwa police department sio jeshi, kitu kingine ni ile hulka ya polisi kushuka hadhi kutokana na muingiliano wake na jamii, pia mitazamo, maslahi na majukumu kupishana inachangia kudharauliana otherwise kikinuka wote wanaenda front sio magereza sio polisi wala sio jwtz wote wanasonga, sijui wale jamaa wa moto maana hata armoury hawana
Ukilinganisha na Marekani utachanganya kidogo.

Kimsingi pamoja na Police Department lakin pia majukumu ya FBI(Federal Bureau of Investigation) kwa Tanzania ni majukumu ya jeshi la polisi.

Hivyo zingatia hilo.
 
Mkuu mbona mnampatia CDF cheo ambacho si chake? Hakuna cheo kinachoitwa mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama bali kuna cheo cha amiri jeshi mkuu wa vikosi vya ulinzi na usalama ambae ni Rais bhasi

CDF ni mkuu wa majeshi ya Ulinzi tu yani Defense force kama jina la cheo chake hilo la usalama linapatikana wapi?
Tafuta barua ya ikulu ya uteuzi wa Mabeyo ambae ni CDF then angalia ameandikwa ni mkuu wa majeshi gani tatizo kuna kusikia kitu na kukifanya ndicho au ndio ilivyo kumbe sivyo yule ni mkuu wa majeshi ya Ulinzi tu nasema kitu ninachokifahamu

Kuhusu Tiss kuwa nayo ni moja ya usalama nayo si kweli hata kidogo Tiss ni intelligence agency kwa maana ya taasisi au idara ya kijasusi watu wanaodeal na usalama ni Police forces
DG ndie kiongozi wa ujasusi (intelligence) hii sio jeshi wala Vikosi hii ni idara au taasisi ndio maana Duniani hakuna intelligence yeyote inayoitwa Jeshi au Vikosi Intelligence zote zinaitwa Agency kwa sababu vinaweza kuingia sehemu yeyote ikiwamo Kwenye Ulinzi na Usalama na Ku operate kama civilian ndio maana leo jeshini kuna kitengo cha intelligence na pia Police kuna kitengo cha intelligence na hata sehemu yeyote mtu kutoka taasisi ya intelligence anaweza kufanya kazi lakini leo huwezi kukuta Mwanajeshi anafanya kazi Police au Police yuko jeshini rabda pawepo na missions ndo inaweza tokea mix ya namna hii
Kazi ya Intelligence ni kudeal na ku operate na vitu vyote lakini in silence way
ndio maana kiongozi wa intelligence jina lake ni Director sasa wote tunajua neno Director linasound civilian sana tofauti na IGP ,CDF

Na kama itathibitika CDF ni mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama nipo tayari kupumzika wiki mbili nipigwe ban Mod lakini CDF ni mkuu wa majeshi ya Ulinzi tu hausiki na Usalama hata kidogo
Mengi hapo juu upo sahihi, isipokuwa tu unaposema TISS si Jeshi. Hapo umekosea,au haupo well informed
 
Umesoma katiba ya nchi gani inayosema hivyo?watu Kwa kuongea tusivyovijua hatujambo.
mkuu, si kila kitu utakipata kwenye katiba tuu! mind you, katiba ni frame work ya all laws (mather or fundamental laws). kwa hiyo ukitaka kufahamu protocols ni vema kusoma katiba na vitu vingine ambavyo si katiba lakini bado inaelezea nini ni nini? na kwa mazingira yapi na kwa wakati gani?
 
Sio kweli kama police sio defence force au twende kwa kiswahili tutaelewana CDF ni kamanda wa vyombo vya ulinzi na usalama ambayo inajumuisha JW, JKT, Mgambo, TAKUKURU, USALAMA, POLICE, PRISON, FIRE na UHAMIAJI
Chief of Defence Forces(CDF). Au huelewi defence ni nini?
 
Wanajamvi Mjue kwamba kuna Vyeo na Madaraka.Pia Mlinganyo huu mnatakiwa kutulia ili Mpate Majibu.Naanza na Ranks/Vyeo.Katika Vyeo tujue kwamba JWTZ wanatumia International Ranks lakini kwa Police sivyo na hata uvalishwaji kimfumo sivyo.
 
Katiba imempa mkuu wa majeshi (CDF) kuwa mkuu wa vyombo vyote VYA ulinzi Na Usalama Na imefafanua ifuatavyo. Ataongoza 1.Regular force 2.Reserve force 3. Volunteers Reserve Na Other displinary forces.(magereza,police,uhamiaji,TIS Zimamoto nk) Na Yeye ndio Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi Na Usalama wa Taifa. Na hili limekaa sawa kwa maana Rais ndio Amiri JESHI mkuu Na mkuu wa majeshi ndio MTENDAJI mkuu wa Amri za amiri JESHI mkuu huwezi kuwa Na Command nyingi katika Operation hao waliobakia watapokea Amri za operation kutoka kwa CDF.
Hapa umemaliza kila kitu
 
Jiulize wakati wa vita mfano vita ya Kagera Police walipigana? Jibu ni ndiyo na je walikuwa chini ya command ya nani? Jibu ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama. Je IGP alikuwa anapokea amri kutoka kwa nani? Jibu ni CDF. Je Police kwa nini hawakuwa na command yao? Kwa sababu huwezi kuwa na wa majeshi wawili nchi moja
Huu ni mfano hai, hakuna ubishi katika hili
 
Huu uzi umenifanya niwajue vilaza wa JF....Yaani watu ni wabishi halafu hawajui kitu....Mpaka inabidi nicheke tu

Jitu linakazania eti CDF ni mkuu wa majeshi ya ulinzi na USALAMA....Na mtu anaongea haya kutoka kichwani mwake tu, hana reference yoyote....

Jitu linakazania kuwa jeshi la polisi ni sehemu ya majeshi ya ulinzi,

Sio kila jambo linahitaji kufikiria, mambo mengine yanahitaji kusoma official documents na kujua...Wote wanaosema polisi ni part ya jeshi la ulinzi wanaongea bila ujuzi wowote....

IGP ni mkubwa wa Tanzania Police Force

CDF ni mkubwa wa Tanzania People's Defence Force (JWTZ)

Polisi sio part ya jeshi jamani, muwe mnafanya hata karesearch kidogo

Hebu someni barua ya uteuzi wa CDF mpya baada ya mwamuyange...Haijataja Majeshi ya Ulinzi na USALAMA kama wanavyotuaminisha baadhi ya watu humu

Pitieni website za police na ya jeshi (kwa sasa ipo down i think)
 
"Nataka heshima iliyopo kwenye JWTZ, ihamie kwenye majeshi mengine likiwepo jeshi la polisi"

JPM

Wanaweza kuwa sawa ila CDF anaheshimika zaidi (sijui kwanini)
 
Mengi hapo juu upo sahihi, isipokuwa tu unaposema TISS si Jeshi. Hapo umekosea,au haupo well informed
Tiss ni Jeshi gani? ???
Je unajua maana ya jeshi au kazi za jeshi ww?

Nitajie taasisi ya intelligence Duniani inayoitwa ni Jeshi?

Intelligence zote zinaitwa Agency kwa maana ya idara au taasisi hakuna Jeshi lolote Duniani linaloweza ku operate civilian kama ambavyo taasisi nying za intelligence zinavyofanya

Kazi ya Intelligence Agency ni kukusanya taarifa za intelligence (kijasusi) na kuzifanyia kazi au kuzipeleka kwa wahusika zikafanyiwe kazi sijawai kuona Duniani jeshi la intelligence agency ktk mapambano kama tunavyoona majeshi ya Ulinzi au Vikosi vya usalama

Je umewai kuona gwaride la Tiss kama unavyowaona wengine POLICE, JESHI LA WANANCHI ,MAGEREZA, ZIMAMOTO AU UHAMIAJI?
Hakuna jeshi duniani linalo operate kwa Siri zaid ya intelligence Agency leo hata Baba yako hawezi kukwambia kuwa yeye ni intelligence agency officer unadhani kwa nini? mbona baba yako akiwa hata Mgambo inajua?

Tiss ni kama CIA ,MOSSAD ,BND ,MI6 je CIA ni jeshi? hizi ni idara au taasisi za kijasusi na kazi zao ni kukusanya taarifa za intelligence na kuzifanyia kazi au kupeleka kwenye kitengo kinachohusika zikafanyiwe ndio maana kuna kitengo cha intelligence ndani ya Jeshi au Vikosi vya usalama mpaka Mitaani kuna watu wa taasisi hii na kazi zao ni kukusanya taarifa za intelligence tu
 
Back
Top Bottom