denyol
Member
- Mar 19, 2012
- 51
- 6
mfumo wa ccm uliotengenezwa kwa miaka mingi, unawafanya wanachama na viongozi wa ngazi za chini kufanya lolote watakaloambiwa na viongozi wao wa juu ili waweze kuingia ktk uongozi wa ngazi za juu, utawawezesha viongozi wa chama hiki kuendelea kuwanyonya wananchi wa kawaida ambao hawana fedha kwa kipindi kirefu zaidi, huku viongozi hawa wa chini wakiwa na ndoto ya siku moja nao kutapata nafasi ya kushika madaraka ya juu ktk chama na serikali. Wanachama wa kawaida wanahangaika na shilingi elfu tatu tatu wanazopewa wakihudhuria mikutano au vikao vya chama. Kwa muda mrefu wanaotetea chama hiki wana uvivu wa kufikiri, wanadhani wakipata ugali wa siku moja unatosha, kumbe wanaacha deni kubwa kwa watoto wao ambao hawana shule za kueleweka, huduma mbovu za hospitali, usafiri, na vingi tu nk.
Kwa wapenda mabadiliko hawana budi kuangalia mbinu mpya, hasa ya kutafuta volunteers wa kutosha kutoa elimu maeneo ya vijijini kwa wanawake na wanaume maskini wa nchi hii, na baadhi ya vijana ambao bado wanashabikia ccm, nadhani ni kwa ajili ya njaa au bongo lala. Kijiji kwa kijiji, mtaa kwa mtaa, kijiwe kwa kijiwe mpaka elimu ya ukombozi itambae kwa wote, waondoe chama hiki dhalimu. Wanamabadiliko wasipopata ushindi mkubwa ktk uchaguzi wa mwaka 2015, ccm watafanya ujanja wao na kuendelea kubaki madarakani kimabavu! Kila la kheri wapenda mabadiliko!