Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Kwa sasa, mtu anayeongoza kwa kutajwa sana hapa nchini, iwe kwenye social media ama Radio, TV na Magazeti bila shaka ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Iwe kwa uzuri au kwa ubaya ila ukweli utabaki pale pale kuwa Makonda ndiye mtu mashuhuri zaidi hapa nchini kwa Mwezi Machi 2017.
Katazo la kumuandika Makonda limekuwa zigo zito kwa media zote. Iwe za Serikali ama binafsi. Iwe mitandao ya kijamii ama vijiweni. Hata hapa JF lilifanyika jaribio la kufuta neno Makonda hata hivyo ikaonekana kuwa ni zoezi gumu.
Uchunguzi unabaini kuwa magazeti yanahomuandika sana Makonda hasa Tanzania Daima, Mtanzania, Jambo Leo, Mwanahalisi au hata Mawio mauzo yameongezeka mara dufu. Juzi nilikuwa naongea na Mhariri wa gazeti moja akamshukuru sana Makonda kwa kuwaongezea kipato. Tena wakaahidi kuwa wataendelea kumuandika bila kujali katazo hilo. Tena alienda mbali kwa kusema kuwa kuacha kumuandika Makonda ni kukaribisha ukata kwenye Media.
Niwasihi sana Watanzania. Tusichukue maamuzi ya pupa na jazba. Mdogo wangu Nape juzi alikuwa na jazba ila leo anajuta kwa alichofanya pale Protea Hotel