Makonda, Mnyeti, Gambo na Mwanri mapengo yenu kwenye mikoa mliyoondoka yanaonekana

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
714
1,137
Tangu kuondoka kwa Wakuu wa Mikoa kama Makonda, Mnyeti, Gambo na Mwanri mikoa hiyo kama imesinyaa kwa baadhi ya mambo.

Sisemi kuwa maendeleo ndiyo yamesinyaa ila kuna baadhi ya mambo kama hayako sawa. Ule usafi wa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi mkoani DSM kama imekosa muendelezo wake. DSM imekuwa kama sio Jiji Kuu la biashara tena.

Kule Arusha nako zile heka heka za hapa na pale hazisikiki tena kwenye vyombo vya habari hata kwenye mitandao pia. Tabora ama Toronto chini ya Mwanri imekuwa kimya sana hata attention ya media sio sana. Kadhalika kule Manyara kwa Mnyeti kuko kimya sana.

Mara nyingine unaweza usiwajue hata Wakuu wa Mikoa hiyo kwa majina yao. Wamekuja na style mpya kabisa ya kuongoza mikoa hiyo.
Na hapa ndipo unapoweza kujua uongozi sio tu kuwaletea maendeleo watu bali pia jamii inakukubali kwa kiwango gani.

Kazi za hawa Wakuu wapya wa mikoa zimekuwa hazionekani sana kama za watangulizi wao, zimekuwa kama kazi za wahandishi wa maji, wanafanya kazi kubwa sana lakini hazionekani kwani baada ya kumaliza kazi zao huwa wanafukia mabomba chini ya ardhi na kuzificha udongoni.

Kuna baadhi ya wakuu wa mikoa wanashindwa na Wakuu wa Wilaya katika kuonesha uwezo wao wa kusimamia mambo. Kijana kama Ole wa Hai anaonekana sana kwa kuwa muibuaji wa mambo mengi.

Kusema ukweli kuna mikoa hasa hasa DSM na Arusha inawahitaji wakuu wa mikoa wenye kelele nyingi kwa sababu ya asili ya mikoa yenyewe. Kwa sasa Mkuu wa Mkoa anayeonekana kufaa kwa kelele ni wa kule Mbeya. Amekuwa kama kinara wa kuonekana sana kuwashinda wenzake. Na hapo ndipo tunawapo wakumbuka akina Makonda na wenzake.

Lakini pia kuna watu wanapenda sana uongozi lakini kama uongozi hauwataki wao. Makonda bado ataendelea kuwa kinara wa enzi zake. Inaonekana kama uongozi unampenda sana Makonda. Absence yake bado inaonekana sana mpaka leo mjini DSM.

Sio kila mtu anaweza kuwa Mkuu wa Mkoa wa DSM na Arusha. Makonda kafanya transformation nyingi sana mkoani DSM
 
Makonda ni raia asiye na kazi sawa na mzuzuraji Kama sie. Leo Rashidi Gwajima ndie boss wa Makonda. Leo Gwajima ana hadhi kiserikali na kichama pia kuliko Makonda
 
Makonda aliwaumiza mno chadema baada ya kuthibiti biashara ya dawa za kulevya na kumtaja mwenyekiti wake hadharani bila woga.

Kabla Makonda hajataja nilikuwaga najiuliza kwa nini kuna mateja wengi hivi Kinondoni mtaa wa Ufipa?

Sent from my Infinix X622 using JamiiForums mobile app

Alitumia Vita vya madawa kupigia Pesa in bashite style nani yupo ndani Hadi leo kwenye list yake. Yule wa Hai alitaka kuiga kwa kuwasingizia matajiri wa mabus eti wameharibu reli akakutana na mamangi wanaijua pesa kuliko mtengeneza pesa akabuma
 
Sio usafi tu, hata usalama pia. Juzi kati vijana wa panya road walifunga mitaa ya Pugu, Kigogo fresh na Majohe kisa eti mwenzao kauliwa wakati akiiba pikipiki. Maduka yalifungwa kabisa na watu wakalazimishwa kujifungia ndani. Enzi za Makonda ho ujinga usingeusikia
 
Hasa Makonda jiji limepoa sana, limekuwa ka mkoani vile
Mwanri pengo sikuizi siingii YouTube kabisa kuona vituko vyake
 
Makonda ni raia asiye na kazi sawa na mzuzuraji Kama sie. Leo Rashidi Gwajima ndie boss wa Makonda. Leo Gwajima ana hadhi kiserikali na kichama pia kuliko Makonda
Makonda ana hela anaishi vzri tu
Labda power ndiyo hana kwa sasa
Any way muda bado upo anaweza kurudi

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Naona Makonda mwenyewe umeamua kuanzisha Uzi ili kujipa promo, ili Mzee akuchague tena. Tuliza Mshono Jomba nchi ina Vijana wengi hii hatuna ajira.

Wenzio uliowataja hapo wote mmeshapata mitaji ya kutosha kujiajiri, nendeni Mkajiajiri
Na wewe ni mwanae umetoa coment
 
Ile saga ya Machinga Complex iliishia wapi ??

Kuna haja ya kujua namna ubadhirifu uliofanyika pale suluhisho lake likikuwa vipi??
 
Tangu kuondoka kwa Wakuu wa Mikoa kama Makonda, Mnyeti, Gambo na Mwanri mikoa hiyo kama imesinyaa kwa baadhi ya mambo...
Kwani kelele ndio kielelezo cha uchapaji kazi? Fully nonesense
 
Ile saga ya Machinga Complex iliishia wapi ??

Kuna haja ya kujua namna ubadhirifu uliofanyika pale suluhisho lake likikuwa vipi??

Kuna shida gani hapo machinga complex mkuu?

Ishu ya machinjio na masoko ya kimkakati ndio muhimu zaidi hapo Daslamu.
 
Back
Top Bottom