Katavi: Watu wanne wadaiwa kumchinja baba wakitaka urithi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Jeshi la Polisi mkoani Katavi linawashikilia watu wanne, watatu wa familia moja kwa tuhuma za kumuua kwa kumkata na kitu chenye ncha kali shingoni baba yao mzazi Lumba Nhalima (57), kisha kumkata sehemu zake za siri.

jeshi.jpg

Kamanda wa Polisi mkoani Katavi, Benjamin Kuzaga, picha mtandao

Tukio hilo limetokea Mei 10, majira ya saa tatu usiku katika Kijiji cha Kasekese wilayani Tanganyika mkoani Katavi, wakati marehemu akitoka kunywa pombe na kuelekea nyumbani.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo jana, Kamanda wa Polisi mkoani Katavi, Benjamin Kuzaga, alisema siku ya tukio watuhumiwa walimnywesha pombe nyingi baba yao ili ashindwe kujitambua.

Alisema akiwa njiani kurudi nyumbani, alikutana na watuhumiwa hao ambao ni Sali Lumba (32), Jonas Lumba (28), Paulo Lumba (19) na mtu mwingine ambaye alikuwa anakunywa naye pombe Thomas Malongo (54).

Kuzaga alisema baada ya uchunguzi walibaini kabla ya kifo chake marehemu alikuwa akilalamika kuwa watoto wake wakubwa wanne ambao ni wa mke mkubwa wanataka kumuua ili warithi mali zake.

Hata hivyo, Kuzaga alisema chanzo cha kifo chake kinahusishwa na imani za kishirikina pamoja na tamaa za kurithi mali, hivyo jeshi hilo linaendelea kufanya msako kuwatafuta watuhumiwa wengine waliohusika na tukio hilo.

Alisema watuhumiwa wanne wanao washikilia wamekiri kuhusika kupanga njama na kufanikisha mauaji hayo na jeshi hilo limetoa rai kwa wananchi wa mkoa huo kuachana na dhana potofu za kujipatia kipato kwa njia ambazo si halali, ikiwamo imani za kishirikina.

NIPASHE
 
Yaani kijana badala ya kutafuta kwa jasho ili upate mali zako halali, unakaa kusubiria mali za urithi. Wacha tu wavune wlichopanda
 
Inaonesha huyu dingi alioa bi mdogo akakabidhi mali zote huko..
 
Uo urithi utakuta ata nika nyumba ka ajabu ajabu tu..watu bhana

sijui itakuaje
 
Wakatwe na wao nyeti zao wakiwa huko gerezani sababu hawana kazi nazo hapo ni kifungo cha maisha.

Boost your Immune System to fight a Covid-19.
 
Back
Top Bottom