Katavi University of Agriculture (KUA)

andreakalima

JF-Expert Member
Jun 2, 2012
4,071
2,000
Duniani kote vyuo vikuu ni chanzo cha kuzalisha wataalamu wa sekta mbali mbali na kufanya tafiti za kutatua matatizo yanayoikumba jamii husika. Hapa nchini kumekuwa na wimbi la uanzishwaji wa vyuo vikuu kwa wingi sana, ni jambo zuri la kupigiwa mfano, mojawapo ni chuo kikuu cha umma cha kilimo cha KATAVI. Mwenye kujua chuo hiki kinatoa kozi gani na kwa ngazi gani atufahamishe tafadhali.
 
mpolomoko

Member
Jun 11, 2016
7
45
Hakuna chuo kama hiki duniani, niko katavi kwa sasa, hakuna chuo kama hiko.. Umekisikia wapi mkuu??? Nachojua ndio kipo kwenye mpango wa kuanzishwa ila hata hawajaanza kufyeka eneo husika ili ujenzi uanze.
 
Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,189
2,000
Duniani kote vyuo vikuu ni chanzo cha kuzalisha wataalamu wa sekta mbali mbali na kufanya tafiti za kutatua matatizo yanayoikumba jamii husika. Hapa nchini kumekuwa na wimbi la uanzishwaji wa vyuo vikuu kwa wingi sana, ni jambo zuri la kupigiwa mfano, mojawapo ni chuo kikuu cha umma cha kilimo cha KATAVI. Mwenye kujua chuo hiki kinatoa kozi gani na kwa ngazi gani atufahamishe tafadhali.
SIKU ZA KARIBUNI NILIWEKA POST INAYOFANANA NA HII KWA MAJADILIANO. AIDHA ILIONDOLEWA AU ILIKOSA WACHANGIAJI. NASHUKURU UMEIFUFUA!
 
bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,337
2,000
Mh mwenye nchi jana anasema bora vyuo viwe vichache hata kama vina wanafunzi milioni moja. Magufuli inabidi awe anapewa ushauri wa kitaalam. Tunaweza kujikuta na hospital moja pia. Vyuo vikuu huleta ushindani, hufungua maendeleo kama Dodoma, huruhusu mawazo tofauti na specialization mbali mbali.
Aviboreshe vilivyopo na kuhakikisha ni bora si kuwaza kuvipunguza.
 
Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,400
2,000
Kila mkoa kijengwe chuo kikuu halafu wasome wa mkoa huo huo ...vyuo vya kata hovyo kabisa, kisa mkoa fulani ilimradi tu. Hii nayo ilikuwa ni siasa kweli kweli, si Butihama, si katavi, si, si, ....
 
Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,189
2,000
Kila mkoa kijengwe chuo kikuu halafu wasome wa mkoa huo huo ...vyuo vya kata hovyo kabisa, kisa mkoa fulani ilimradi tu. Hii nayo ilikuwa ni siasa kweli kweli, si Butihama, si katavi, si, si, ....
Hoja yenye sababu ya uanzishwaji chuo ndio msingi na wala sio wingi. Baba wa Taifa aliona mbali kuanzisha SUA mahali kama Morogoro. Sababu hizohizo au mfano wake ungetumika kwa Katavi University of Agriculture. Maeneo haya yanafanana kwa karibu kiuzalishaji,maliasili na hali ya hewa. Uwepo wa Chuo kikuu cha aina hiyo kwa vyovyote kingechochea maendeleo ukanda huo
 
Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,189
2,000
Hoja yenye sababu ya uanzishwaji chuo ndio msingi na wala sio wingi. Baba wa Taifa aliona mbali kuanzisha SUA mahali kama Morogoro. Sababu hizohizo au mfano wake ungetumika kwa Katavi University of Agriculture. Maeneo haya yanafanana kwa karibu kiuzalishaji,maliasili na hali ya hewa. Uwepo wa Chuo kikuu cha aina hiyo kwa vyovyote kingechochea maendeleo ukanda huo
Sina uhakika kama Mkuu amepewa hii habari kwa undani. Nimeona dhamira yake ni kuimarisha zaidi Universities za serikali.
 
Leo Asubuhi

Member
Apr 5, 2017
64
125
Kwa taarifa, Chuo cha Katavi ulikuwa mradi wa wakubwa ,wananchi walinyanganywa ardhi wakadanganywa kwa tathmini ya uwongo, lile eneo likachukuliwa hati ile hati ilipochukuliwa wakubwa wakaenda benki ya uwekezaji TIB wakachukua mkopo wa mamilioni, hela ikatoka wakagawana .mpaka leo hakuna chuo,wananchi walilizwa na eneo likaenda,kwanii huu wizi haufuatiliwi ? Meya aliyepita wa manispaa ya mpanda anazo taarifa sahihi
 
double R

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,279

Wezi wako serious kuliko walinzi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom