Kataa kabisa urafiki au mahusiano ya kawaida na Askari Polisi

20231229_092608.jpg
 
Kabla ya kuwakwepa polisi jitahidi kukwepa aina yoyote ya uhalifu. Jitahidi sana kufuata sheria... Vyombo vingine vya usalama vikikumata lazima vikukabidhi kwa polisi kwahiyo hawakwepeki. Pia polisi ni ndugu zetu hawajashushwa kutoka mbinguni. Binafsi ninaunga mkono mambo ya kutoleta mazoea na mwanausalama yeyote kuanzia polisi, Takukuru, TRA, na TISS. Tena hao Takukuru wakikubana ni bora ukamatwe na polisi. Balaa lao ni zito
unajaribu kutuaminisha kwamba ukifuata Sheria polisi hawana shida na wewe? polisi wanakufuata wanakubambikia tu kesi hata km huna kosa na umefuata Sheria.. wanaanza kukusumbua na kukulazimisha uwape pesa hii si tunasikia kila siku? ww utakuwa pia polisi tumewachoka badilikeni
 
Ahsante kwa kunipa UPOLISI , ni taasisi muhimu kuwepo katka jamii yoyote ndo maana nasisitiza upolisi unaanzia nyumbani .

Kama katika miji yetu hakuna UPOLISI ndipo PANYA ROAD wanapoanzia na hawa Panyaroad ndio wanakuwa Mapolisi na idara Nyingine.

Jiulize unaisimamiaje familia yako, jirani zake wanazisimamiaje familia zao je? Mnazalisha nnn? POLISI HAIKATALIWI
kwenda kuleee..!
 
aliyekuwa Raisi wa Tanzania awamu ya nne aliwahi kusema
"usirithi adui wa mwenzako"

mtoa mada usifundishe watu kuwa na chuki dhidi ya watu flan katika jamii.

leo umesema polisi yule mngine anasema walimu.
yule mwingine anasema Waislam yule mwingine wakristo
yule mwingine anasema wanawake.
Mwisho tutakuwa jamii ya hovyo sana.
..hujamuelewa tu mtoa mada wala hajapandikiza chuki. Ila ninyi polisi mmezidi
 
Askari polisi wa Tanzania wamekuwa chanzo cha maumivu ya watu na familia nyingi sana hapo bongo , ni ajabu iliyoje kuona chombo cha dola ambacho ndio kilipaswa kuwa mstari wa mbele kulinda raia na Mali zao kinageuka na kuwa upanga mkali, tena usio na huruma kwa raia

Polisi wengi wa Tanzania ni binadamu wakatili sana, wananjaa kali, wivu wa kimaendeleo kwa raia, bila kusahau wengi wao ni mbumbumbu na bongo lala, walioshindwa shule na biashara hivyo wakaamua kuukimbilia upolisi ambako huko wamejitwika ubabe kutokana na nguvu kubwa waliyopewa na serikali ovu ya ccm ambayo imekuwa ikiwatumia kutekeleza unyama juu ya raia wenye itikadi tofauti na zile za chama chao.

Hatuwezi kukwepa kukutana na polisi katika maisha yetu ya kila siku na kuna wakati nilazima tushirikiane nao ili jamii iwe katika mstari mnyoofu, lakini kamwe usimfanye askari polisi wa Tz kuwa rafiki yako, wala usitengeneze ushkaji na polisi, kataa kabisa kuwa na mahusiano ya aina yoyote yasiyo ya kikazi baina yako na polisi, hao ni Viumbe wenye tamaa na udumavu wa akili, kwao bundiki ndio suluhisho la mizozo yao na bahati mbaya hawawajibishwi ipasavyo, NARUDIA jiwekeni mbali na polisi, na hata akija kama mpangaji katika nyumba uliyopanga wewe hama, na mshkaji wako akiwa polisi mkatae mazima, dada yako au mwanao akitaka kuolewa na polisi vunja uchumba .

#POLISI SIO RAFIKI, POLISI SIO NDUGU, MKATAE POLISI

polisi hawatoki mars,jupiter au nibiru.ni kaka zenu,wadogo zenu,majirani zenu,wajomba au wapwa zenu.unapopiga ngonjera kwamba watengwe ni kazi bure,sababu jamii hii hii,yenye ndugu na jamaa waalimu na chadema,ndio hiyo hiyo yenye ndugu na jamaa polisi.

wakati mnatumia akili duni na ndogo kabisa kuliko za nzi kwamba muwatenge,mnasahau kwamba mnawaweka katika angle ya kujiona wao sio sehemu yenu zaidi,ingawa haliwezekani hili 100%.

jambo la msingi weka juhudi katika kutambua haki zako unapokuwa mikononi mwa polisi,epuka ujuaji kelele na harakati unapokuwa mikononi mwao,endoa upuuzi huu ulio nao kichwani kwako kwamba wao hawanaga ubinaadam kabisa utakuwa unapunguza kiwewe ukiwa nao.

mwisho kabisa,ili uondokane na haya majungu jiweke mbali na uhalifu,magendo na ukanjanja,utapunguza ukaribu na mazoea kwa polisi kama ambayo unatamani.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
UMEANDIKA KWA HISIA KALI, LAZIMA KUNA TUKIO LILIKUPATA WEWE AU MTU WAKO WA KARIBU. Mimi niliwahi kuangukia mikononi mw polisi saa 2 usiku mtaani kwetu kwa kosa la uzululaji, jamani nyie acheni tu
 
Kuna polisi mmoja tulikuwa tunakutana kwenye bar fulani kuangalia hii mipira yetu ya bongo(Simba na Yanga).Jamaa yeye ni mnazi wa kutupwa wa Yanga.Huwa wakishinda hanipi nafasi ya kupumua ni utani mwanzo mwisho nami nakuwa mpole kama ilivyo desturi ya utani wa jadi.Basi bwana Mungu sio mzee mkumba wamanga ya Algeria wakanipigia Yanga kamba 3-0, kama ilivyoada ya utani mimi nikawa namkera sio yeye tu ni mashabiki wote wa yanga mahali hapo(kwa maneno ya tambo na kejeli bila kumgusa mtu).Kwa furaha yule askari nikamnunulia pombe nikimuona kama mwana tu na tukaendelea kunywa baada ya game na tambo za hapa na pale.Aiseee jamaa(huyo polisi) akamwambia mwenzake yani huyu jamaa nammaindi sana,ananikera sana na simba yake nataka nimbambikie hata kesi ya bangi,ananikera balaa.Mimi yale maneno yote niliyasikia japo alihisi mimi nimelewa sana maana nilikuwa na vibe sana.Tangu pale nikaondoka kwenye meza yake na nikaanza kumkwepa.Baada yeye kugundua hivyo akamtuma jamaa mwingine kuja kuniuliza kulikoni mbona siku hizi huji kwenye meza yetu?Nikamwabia mimi ni mtoto wa kimasikini sina mtu wa kuniwekea dhamana nikiwekwa rumande 😂Hapo ndio ikawa mwisho wa ushikaji wa kinafiki.Tangia siku hiyo ndio nikaamini ujinga,upumbavu wa hawa polisi wetu.
 
OCD ni mkubwa kwenye jeshi ila mwenye madaraka ni OCS kwenye kituo.
sas me nilete chai kwa faida gan?. Na nikujuze tu OCD baada ya kutokea ilo vurugu alitaka ampeleke mahakaman mwana ila OCS alipinga alimuliza tunampeleka mahakaman kwa kosa gan? Na alimwambia OCD hakupaswa kujichukulia sheria mkononi na mda huu mwana yupo uraian na bajaj yake
We huelewi maana ya OCD,officer who commands District kama cjakosea sana.Wilaya ina vituo vingi vya police na kila kituo kina OCS.ila OCD ni mmoja tu kwa wilaya nzima kama unavyoona RPC ni mmoja tu kwa mkoa mzima.OCD akitokea mbele ya ocs hakuna majibizano zaidi ya salute na kufuata maelekezo.Ndo maana watu wanakugomea ni ngum kumpiga OCD mbele ya OCS na askari wake ukatoka na afya yako baada ya hapo.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Sisi sote ni jamii moja HAKUNA matengano UOZO unaouona kwa askari Polisi ndo huo huo uko, sokoni, mahakamani, bank, Zahanati , TRA, TAKUKURU nk .

Basi ni kwakuwa hujakutwa kwenye KONA inayowahusu au jamii inadhani ni HAKI yao kutendwq hivyo na IDARA zingine

Jamii yote DUNIANI inaasili ya kutaka KUONEWA HURUMA , KUDEKEZWA ,KUSAMEHEWA hivyo inapobanwa kilio namba moja ni kupeleka UBAYA.

NCHI ya AMERICA wao kwa utani wanaambiwa wanajifanya POLISI wa Dunia jiulize KWANINI?

UKIANDIKA POLICE wana IQ ndogo itazame jamii yako ikoje ina IQ kubwa ? Utulivu uliopo vp, tusidharau chombo ,peleka lawama kwa aliyekutenda.

Lkn IDARA YA MAJI , ZAHANATI, VYUO , SOKONI kila eneo POLISI yupo hata ndani ya nyumba katka familia POLISI yupo. Kusimamia sheria na taratibu .
Police Tanzania in general wanafanya kazi sana na ndo maana watu wanaweza kuishi kwa amani na kufanya starehe,Ila haiondoi ukweli watu wanailalamikia sana Police.Ni ngum sana kwenda police yetu kusaka huduma ukahudumiwa smoothly bila mikwaruzo.Management ya police bado ina kazi kubwa kulileta jeshi karibu na wananchi.Huwezi kuhubiri police jamii wakati mtu kupata dhamana mpaka ahonge.Huwezi hubiri police jamii kama bado kuna askari wanawafanyia ujambazi raia wasio na hatia.Hizi lugha chafu watu wanazotoa ni njia ya kutoa hasira zao tu.Watu wengi wanaumizwa na police linapokuja swala la mtu mmoja mmoja.
 
We huelewi maana ya OCD,officer who commands District kama cjakosea sana.Wilaya ina vituo vingi vya police na kila kituo kina OCS.ila OCD ni mmoja tu kwa wilaya nzima kama unavyoona RPC ni mmoja tu kwa mkoa mzima.OCD akitokea mbele ya ocs hakuna majibizano zaidi ya salute na kufuata maelekezo.Ndo maana watu wanakugomea ni ngum kumpiga OCD mbele ya OCS na askari wake ukatoka na afya yako baada ya hapo.

watu wanalalamika kupigwa na kutendewa madhira na polisi kwa sababu za kawaida kabisa,mwamba anatupanga kwamba alimpiga OCD na bado akafanikiwa kuwa salama.

late mwangosi alijaribu tu,kumsukuma RPC,kilichofuata ikawa lawama.
 
Kuna polisi mmoja tulikuwa tunakutana kwenye bar fulani kuangalia hii mipira yetu ya bongo(Simba na Yanga).Jamaa yeye ni mnazi wa kutupwa wa Yanga.Huwa wakishinda hanipi nafasi ya kupumua ni utani mwanzo mwisho nami nakuwa mpole kama ilivyo desturi ya utani wa jadi.Basi bwana Mungu sio mzee mkumba wamanga ya Algeria wakanipigia Yanga kamba 3-0, kama ilivyoada ya utani mimi nikawa namkera sio yeye tu ni mashabiki wote wa yanga mahali hapo(kwa maneno ya tambo na kejeli bila kumgusa mtu).Kwa furaha yule askari nikamnunulia pombe nikimuona kama mwana tu na tukaendelea kunywa baada ya game na tambo za hapa na pale.Aiseee jamaa(huyo polisi) akamwambia mwenzake yani huyu jamaa nammaindi sana,ananikera sana na simba yake nataka nimbambikie hata kesi ya bangi,ananikera balaa.Mimi yale maneno yote niliyasikia japo alihisi mimi nimelewa sana maana nilikuwa na vibe sana.Tangu pale nikaondoka kwenye meza yake na nikaanza kumkwepa.Baada yeye kugundua hivyo akamtuma jamaa mwingine kuja kuniuliza kulikoni mbona siku hizi huji kwenye meza yetu?Nikamwabia mimi ni mtoto wa kimasikini sina mtu wa kuniwekea dhamana nikiwekwa rumande 😂Hapo ndio ikawa mwisho wa ushikaji wa kinafiki.Tangia siku hiyo ndio nikaamini ujinga,upumbavu wa hawa
Ndo binadamu tulivyo, wengine uvumilivu hawana , umakini uliouchukua ndiyo Akili.

Yupo mwingine kamuuzi FUNDI wake wa ujenzi kwa ushabiki kamuacha kwenye kazi, yupo mwingine kamuuzi mwenye duka kanyima huduma, nk
 
Kuna demu mmoja mjeda (police) kanizimikia balaa, unataka kuniambiaje weye.!! alinikamata kosa la barabarani kutoka hapo yaani nataka kuoa kabisa kabisa maana si kwa mambo yale aisee !!
Subiri utakiona cha mtema kuni!
Hao waoanage wenyewe kwa wenyewe.
Wife akiitaka pesa yako huna ujanja hapo lazima ataipata.
Kwa jinsi walivyonifanya mimi ni sehemu ya kuwalipa mshahara kipindi kile, sitaki hata kuwasikia.
Tena bila aibu walikuwa wananipigia simu, eti "siunajua tarehe hizi mshahara bado haujaingia!"
 
watu wanalalamika kupigwa na kutendewa madhira na polisi kwa sababu za kawaida kabisa,mwamba anatupanga kwamba alimpiga OCD na bado akafanikiwa kuwa salama.

late mwangosi alijaribu tu,kumsukuma RPC,kilichofuata ikawa lawama.
😂😂 labda kapiga mgambo,kumla vichwa OCD ukafanikiwa kutoka salama,kwa police yetu hii labda uhame nchi haraka.
 
Askari polisi wa Tanzania wamekuwa chanzo cha maumivu ya watu na familia nyingi sana hapo bongo , ni ajabu iliyoje kuona chombo cha dola ambacho ndio kilipaswa kuwa mstari wa mbele kulinda raia na Mali zao kinageuka na kuwa upanga mkali, tena usio na huruma kwa raia

Polisi wengi wa Tanzania ni binadamu wakatili sana, wananjaa kali, wivu wa kimaendeleo kwa raia, bila kusahau wengi wao ni mbumbumbu na bongo lala, walioshindwa shule na biashara hivyo wakaamua kuukimbilia upolisi ambako huko wamejitwika ubabe kutokana na nguvu kubwa waliyopewa na serikali ovu ya ccm ambayo imekuwa ikiwatumia kutekeleza unyama juu ya raia wenye itikadi tofauti na zile za chama chao.

Hatuwezi kukwepa kukutana na polisi katika maisha yetu ya kila siku na kuna wakati nilazima tushirikiane nao ili jamii iwe katika mstari mnyoofu, lakini kamwe usimfanye askari polisi wa Tz kuwa rafiki yako, wala usitengeneze ushkaji na polisi, kataa kabisa kuwa na mahusiano ya aina yoyote yasiyo ya kikazi baina yako na polisi, hao ni Viumbe wenye tamaa na udumavu wa akili, kwao bundiki ndio suluhisho la mizozo yao na bahati mbaya hawawajibishwi ipasavyo, NARUDIA jiwekeni mbali na polisi, na hata akija kama mpangaji katika nyumba uliyopanga wewe hama, na mshkaji wako akiwa polisi mkatae mazima, dada yako au mwanao akitaka kuolewa na polisi vunja uchumba .

#POLISI SIO RAFIKI, POLISI SIO NDUGU, MKATAE POLISI
vipi mzee!!!!,,,,una undugu na wale jamaa wa vingunguti nini?
 
Raia wema ndiyo wanaongoza kubambikia watu kesi. Tena raia mwema anaweza kuwa ndugu yako, rafiki au jamii inayokizunguka ..

Epuka sana kumwamini binadamu.
 
Sawa mkuu,
#POLISI SIO RAFIKI, MKATAE
Mimi nasimama pale pele mkuu ya kuwa ndani ya polisi Kuna polisi wabaya na wazuri. Na kuna polisi wametunusuru na ubaya wa polisi wenzao. Kwa hiyo kuwajumlisha wote binafsi sikubaliani na wewe.
 
Back
Top Bottom