Kataa daladala: Ni usafiri wa ovyo na unadhalilisha sana

DA HUSTLA

JF-Expert Member
Mar 5, 2012
3,664
3,882
Imagine uko na mtoto wako mmeshika bomba konda anakufokea ujipange vizuri abiria wengine waingie

This is embarrassment of the lifetime!

Imagine dunga dunga ana mdunga mkeo au dadako au mama ako mbele yako, huna cha kufanya utia tia huruma kama kubwa jinga.

Imagine umeoga zako safi asubuhi, umepiga pasi na ka pafyumu kako..ukifika unakoenda shati limejikunja kama limeliwa na mbuzi unanuka shombo ambazo hata harufu haileweki ni ya nini.

Imagine uko na mkeo/mkwe/mzazi mnaanza kugombania daladala.. halafu ukifika home na wewe unaitwa mume/baba unakoroma kabisa...


Aisee, ukweli usemwe daladala ni usafiri wa hovyo kuwahi kutokea na unadhalilisha sana.

Kwanza kupanda daladala/mwendokasi ni risk ya magonjwa ya hewa, ngozi n.k. Pia kujaza watu namna hiyo ikitokea ajali magnitude ya tatizo ni kubwa sana.

Tutafuteni hata corolla wakuu tuepuke na huu udhalishaji tuongeze hata wigo wa walipa kodi kwa kununua mafuta na vipuri.




#kataadaladala

#Daladala ni kero


#Daladala ni mateso

#Daladala ni unyanyasaji

#Daladala ni laana

#Daladala ni umaskini


#Daladala ni usafiri wa makapuku na watu wa hovyo

#Vunja roho ya kupanda daladala.


Screenshot_20230817-182414.jpg
 
Unaruhusuje wewe uko na mama yako, mkeo au mwanao na wote mnasimama kwenye daladala??

Mfaitie apate siti wewe usimame.

Halafu option sio kununua gari tu kuna uber,bolt , bajaji , boda na vikampuni kibao vya usafirishaji sio lazima ununue gari.
 
Back
Top Bottom