Narudia tena, Usafiri wa daladala hapa Dar es Salaam ni kwa ajili ya watu masikini

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,701
36,119
Habari wanajukwaa!

Natumaini hamjambo,

Hii sio kashfa bali ni ukweli mtupu.

Usafiri wa daladala hapa Dar ni kwaajili ya maskini.

Vijana tutafute pesa huku tukimwomba Mungu atuepushe na Usafiri huu uliojaa karaha na kadhia.

Haiwekani mtu una pesa zako usimame Kariakoo mpaka Mbagala, au usimame Kariakoo mpaka Tegeta.

Jioni ukitoka mjini kwenda pembezoni mwa jiji unavizia basi la kugeuka nalo ili upate siti, nako ukishangaa hupati.

Makonda jioni wanaringa kama wasichana mabikira.

Watu wananuka sigara mnapumuliana.

Mwendokasi nako niliwahi kupanda jioni nako hali ni ngumu. Kuna mfanyakazi mwenzangu alikatwa kidole na mlango wa mwendokasi asubuhi wakati anakuja kazini.
Hii picha chini haina uhusiano na mada bali iko hapo kuchangamsha mada.
Ni mimi mwanadaladala mwenzenu.
FB_IMG_16239970538761465.jpg
 
Siyo kwa maskini, ni kwa ajili ya watu wanaohitaji kutumia usafiri wa daladala kwa wakati husika. Mfano wengine wana magari yao lakini wakati mwingine hutumia daladala kuepuka usumbufu wa kuendesha, maana kuendesha gari siyo rahisi kama mtoa mada unavyofikiria au kama wanapiga bajeti ya mafuta.
 
Mafuta ya elfu 50 yanatosha wiki mzima, sasa ukimwona mtu mpaka anapaki gari nyumbani kwasababu ya mafuta kukata huyo bado maskini
Siyo kwa maskini, ni kwa ajili ya watu wanaohitaji kutumia usafiri wa daladala kwa wakati husika.....mfano wengine wana magari yao lakini wakati mwingine hutumia daladala kuepuka usumbufu wa kuendesha, maana kuendesha gari siyo rahisi kama mtoa mada unavyofikiria au kama wanapiga bajeti ya mafuta....
 
Nyuzi kama hizi nazipenda sana yani zinanitoa stress na vile sina gari wala pikipiki mimi natembea na nauli tu.

Mtu 50 alfu anasema gharama ya mafuta ya wiki kwa gari ya usafiri.

Wakati huo kwa wiki gharama yangu mimi ya usafiri ni 10 alfu.

Wakuu sisi tiobarikiwa kumiliki nauli pia tumshukuru Mola pia.
 
Sio kweli.

Kuna bosi mmoja mkinga ,

Ana magari mengi tu,

Naona anayapaki tu na kwenye mwendokasi anadandia.
 
Back
Top Bottom