Kata ya Kishiri wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, tumekosa maji safi na salama kwenye familia zetu kwa muda wa wiki mbili sasa

Junior Lecturer

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
904
526
Waziri mwenye mamlaka popote ulipo.

Kata ya Kishiri wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza ,tumekosa maji safi na salama kwenye familia zetu kwa muda wa week mbili sasa.

Hapo katikati Mheshimiwa ulikuja kama siku tatu, waka achia maji ulivyo ondoka ukaondoka nao.

Tuki piga simu MWAUWASA wanasema tatizo hakujaripotiwa ofisini kwao.
Tuna tumia maji ya majaribani pamoja na wanyama.

Tunaomba tatizo kipokelewe na kushughulikiwa. Pia, tupewe mwongozo ni namna gani MWAUWASA wanataka kero ya maji iripotiwe kwao na waweze kushughulikia kwa wakati!

Nipo tayari kutoa ushirikiano endapo itahitajika. Pengine kuna mtu ana uhujumu MWAUWASA . Ziwa Victoria lipo Mwanza na Kishiri tunakufa kiu kweli?
 
Pale kigoto ya bulale ni zaidi ya miezi miwili hakuna maji, kitongoji jirani cha tarazo sana zaidi ya wiki bila huduma ya maji. Orodha ni ndefu ya maeneo yasiyokuwa na huduma hiyo ndani ya jiji lioiloko pembeni ya ziwa Victoria!
Nilipata nafasi kutembelea kujiji kimoja huko Ukerewe kinaitwa Kagunguli mwaka 2019. Rais alipofanya ziara huko walihakikisha maji yanapatikana. Matangi mawili ya plastiki yaliwekwa ili kutunza maji na baadhi ya wakazi wakapelekewa maji hadi majumbani mwao. Baada ya ujio huo maji yalikatika na zoezi la kuyafuata ziwani umbali wa kilomita kama tatu au nne likaendelea kama kawaida. Kibaya zaidi ule msingi wa yale matangi umeanza kubomoka na haijulikani ni lini matengenezo yatafanyika. Kulikoni!
 
Siku hizi nimejifunza kuwaogopa kina Balile wanaotafuta tafsiri za "tusi" hata kama unaonewa wapaswa kubaki kimya. Njia yao ya oktoba 28 wanazidi kuiwekea vikwazo. Kichinjio kipo
 
Back
Top Bottom