Kassim Majaliwa anatoa wapi mamlaka ya kubadili sheria za TRA?

Kassim Majaliwa anatoa wapi mamlaka ya kubadili sheria za TRA?

Unaweza kuwa sahihi mkuu lakini bila kumtaja mtoto hata mmoja wa kigogo serikalini anayeuza hayo mataili mtaa wa Livingston kariakoo halafu hataki kulipa kodi uzi huu unakuwa hauna maana kabisa.
huyu lengo lake halikuwa kikao na matamshi ya waziri mkuu! Kwani sijawah ona kikao hapa duniani watu wanakuja na maamuzi au barua bila kujadili kwanza chanzo cha mgogoro! Kama vile hoja yake ilikuwa kulipua hao watoto yeye angelipua tu kwa kuwataja sio kuleta mijorojongo(mizunguko ) humu! Mbona wakina riziwan kikwete wanatajwa tu hovyo hovyo hata na tuhuma ambazo hazijathibitika miaka sasa
 
Utakuwa muhusika siyo bure, kwanini umeongelea upande mmoja tu, je kuweka makadirio makubwa ili mshawishi rushwa, hapo vipi?
 
Tuache siasa kwenye mambo yaliyotungiwa sheria na bunge na ambayo mtu binafsi kama waziri mkuu hawezi kuyatengua kwa maneno ya jukwaani bila barua au muongozo

Matamko ya waziri mkuu kassim Majaliwa kariakoo kuwa TRA wafanye kazi kwa kauli zao za majukwaani bila barua au marekebisho ya sheria bungeni ni kuwahadaa wafanyabiashara

Kuna tuhuma kuwa watoto wa viongozi kariakoo wanauza matairi na hawalipi kodi kwa kigezo cha matamko ya Baba na Mama zao viongozi wakuu wa kitaifa mtaa wa livingstone street

Vijana wa TRA wanatishwa na watoto hawa wa vigogo kwa matamko ya simu na memo

Kwanini Kassim Majaliwa anaogopa kuwapa barua TRA ya kupindisha sheria za kodi bali analazimisha watekeleze matamko ya maneno yake mdomoni

Waziri mkuu majaliwa ameshangaza uma wa watanzania kuitaka mamlaka ya mapato Tanzania kufanya kazi kwa matamko ya wanasiasa na sio kwa kufuata sheria na utaratibu za fedha

Kassim Majaliwa analazimisha TRA wafanye kazi kwa maneno yao ya majukwaani na sio kwa maandishi au taratibu za fedha zilizotungwa na bunge

TRA ni taasisi ya uma sio mali ya wanasiasa,Ipo kisheria na inafanya kazi kwa kufuata sheria za kodi zilizotungwa na bunge

Kassim Majaliwa aache kuwadanganya wafanyabiashara awaambie ukweli kuwa hizo kodi zimetungwa na bunge lao na yeye hana uwezo wa kurekebisha sheria za kodi kwa matamko ya jukwaani

Kassim Majaliwa anapaswa kutambua walioanzisha TRA walianzisha kwa kufuata sheria na akitaka kurekebisha afuate sheria au yeye anataka kuturudisha kwenye kodi ya kichwa ya kufukuzana mitaani
Ohhhhh! Kumbe bunge letu ndio limeweka sera ambayo kontena la vitenge kutoka China ushuru wake ni 300M wakati contena kama hilo Kenya linalipiwa ushuru wa 45M

Kwahiyo inawezekana Bunge letu limejaa vilaza na Bunge la Kenya limejaa watu wenye akili
 
Back
Top Bottom