Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,801
- 43,177
Yaani kuna watu wanaboa jamani, nilikuwa na week end yangu murua pande za Lushoto nilikuwa kwenye kiota flani hv. Nilitoka kazini ijumaa muda wa lunch nikakanyaga wese mdogo mdogo nikafika mombo kwenye saa 3. Nikaagizia mbuzi nikawa nakula taratibu kwenye meza nilikaa na watu mara bin vuu nikasikia mbaba mmoja aliyekuwa anapiga debe chai ya maziwa, rangi, kahawa, ya viungo na blah blah akaanza kuita kwanguvu Kasinde Kasinde Kasindee huku akiangalia huku na huku kuona kama ataitika mtu. Nilisikia ila nami nikaangaza kuangalia kama kuna Kasinde mwingine. Alipoona hakuna anayeitikia akanyamaza.
Nikawaza badae nikajua yule mbaba muuza chai alitumwa na mtu, aliniboa kwakweli maana kama mtu umeniona mahali na unataka kunisalimia si unifate tuu na kunisalimia kistaarabu kuliko kuniita kwa kupayuka hivo.
Wakati nakula yaliingia magari mengi mengi hivo pia watu walikuwa wengi. Nsharudi zangu home kesho ofcn another week end kula ujana tena. Ila hii tabia si nzuri looh