Mkunde Original
JF-Expert Member
- Jul 20, 2013
- 807
- 647
Habari za jioni mabibi na mabwana,
Baada ya kitambo kirefu cha kupotea humu, leo nimekuja na habari ambayo nimekutana nayo mwisho wa wiki iliyopita.
Ilikuwa hivi, kulikuwa na mtoko flani hivi ambao ilinibidi kwenda peke yangu kwasababu ubavu wangu ulikuwa umesafiri. Kama kawaida ya kina mama/dada kwenye mitoko kama hiyo ni kawaida kujikoki na kujiremba vilivyo. Basi nashukuru Mola kioo hakikunidanganya nikajopoa podoo kisha huyoo nikaingia kwenye bajaji yangu hadi ukumbini kwenye eneo la tukio. Kwa uzoefu wa jiji letu hili wengi huwa hawazingatii muda hivo nilijikuta nimefika ukumbini mapema na shughuli hata haijaanza ila kwakuwa mualiko ulisema shughuli inaanza kuanzia saa 12 kamili jioni, mie nilifika palesaa moja kasoro usiku. Meza bado zilikuwa tupu na watu waliokuwa ukumbini hawakufika hata 20. Basi nikachagua meza moja ya pembeni nikakaa ambayo ilikuwa katikati ya ukumbi kana kwamba siko mbali na dancing floor (maana napenda kucheza mziki), siko mbali na mlango wa kutokea iwapo nimeboreka hata katikati ya shughuli naweza ondoka bila hadhira kubwa kunitazama au kugundua. Pia sikuwa mbali na upande wowote ambao wangeanza ku save chakula kwa maana nsio wa kwanza wala wa mwisho (yees, napenda msosi looh).
Basi baada ya kukaa kwenye hiyo meza nilikaa kiti ambacho naangalia mbele, huwa sipendi kuwa eneo la tukio halafu unakaa kiti ambacho inabidi uangalie matukio kupitia screen au projector tu kwasababu kiti kimegeuka upande tofauti na stage, huwa napenda kuangalia vitu mubashara. Basi nikaja kuhudumiwa kinywaji ninachotumia (hii sherehe ilikuwa ya watu wazito flani hivi wa hapa Dar). Nikimaanisha kuwa ilikuwa na vitu vingi alivyo hitaji mgeni ambavyo si rahisi kuvikuta kwenye sherehe nyingine za kawaida za kuombana michango kwa kukabana mashati na vitisho.
Baada kama ya nusu saa hivi wakaja wakaka 3 ambao si watu wazima ila wanaonekana ni wanaume wenye familia zao. Kwa mtizamo wako vizuri kwa maana ya kuwa wako presentable na wanaonekana ni wacheshi. Basi sijui wao walipiga mahesabu gani, ila walikuja moja kwa moja kwenye meza niliyokaa, wakanisalimia na kuniambia, ''samahani dada tunaweza kukaa hapa?'' nikawaambia sawa haina shida mnaweza kukaa, basi mmoja akakaa upande wangu wa kulia mwingine akakaa upande wangu wa kushoto na wa tatu akakaa kiti ambacho kwenye ile meza ya duara tunakuwa tunatizamana au anatutizama sisi wote watatu na sie tunakuwa tunamuona uso kwa uso. Huku wao wakiwa wanafahamiana na kujuana, wakawa wanaongea maongezi yao ya hapa na pale, mie kwakuwa nilikuwa mwenyewe na ile shughuli haikuwa ya ndugu zangu basi nikawa niko tuu kimya na saa ingine naji keep busy na simu yangu. Vinywaji vilivyokolea wakaanza kuniongelesha na kunijumuisha kwenyemaongezi yao, wakati huo watu wengine watano wakaja kukaa kwenye meza yetu na kufanya meza yetu iwe na watu nane.
Nikajikuta nachangamka na story zao ila si kwa kuchangia kuongea laah, bali kwa kusikiliza na kucheka maana walikuwa wacheshi na habari walizokuwa wakiongelea ni za kuchekesha kiasi kwamba hata nikawa simsikilizi MC au muendesha shughuli. Ulipofika wakati wa chakula kule kwenye menu kulikuwa na kila aina ya chakula unayoijua, meza maalum ya desert pia ilikuwepo na meza maalum ya matunda. Mie nikajihudumia nnavoweza kula niarudi mezani kula, sasa waliporudi wale jamaa watatu looh, kwani hata niliweza kula hahahahahahhahaaaaaaa, nilianza kucheka maana nilishindwa kuvumilia. Wamepakua chakula sawa halafu kwenye matunda wakachukua maembe ya kunyonya.... vile viembe vidogo vya kunyonya, wote watatu kila mmoja alichukua viembe vitatu. Nikawa najisemea kimoyo moyo hawa wakaka jamani mbona watanashati hivi kiasi cha kutaka kula embe la kunyonya mbele za watu tena wakiwa watanashati hivi? sikuwaelewa. Simaanishi kuwa unatakiwa kula embe la kunyonya ukiwa mchafu hapana, ila kuna vyakula mie kwa mtazamo wangu vinafaa kuliwa mtu ukiwa nyumbani na si eneo la umma au public kwa maana jinsi ya ulaji wake inataka ili ufurahie ulaji shurti ujiachie.
Wale bwana watatu wakati wa kula walikuwa na table manners zote, hawakuongea neno hata moja vivo hivyo mie ila tuu nilikuwa nashikwa na kicheko na kujikuta nacheka chinichini. Kumbe walikuwa wananiona nnavocheka. Walipomaliza kula hapo ndo shughuli ikaanza.....
Wakaanza kula yale maembe hehehehehehehehhehehee natamaninigewachukua video ili muone maana nikiwasimulia hapa sijui kama mtapata taswira hasa nnayotaka muipate....
Halafu walivkuwa wakila hayo maembe utasema walikuwa wanaigana, kila moja akashika embe lake mkononi anaanza kula huku kwenye mkia ambako hakuna kitovu, basi anaanza kulinyonya weeeh hadi linatoboka. Sasa huyo mmoja akawa anayonya embe hadi anafumba macho kuonesha kuwa anapata utamu ile mbaya hahahahahahaa hapo nilishindwa kuvumilia na sikuendelea kula tena, nilicheka kwanguvu hadi nikapaliwa hahahahahahaaa. Wengine wawili nao wakala wananyonya kila mmoja embe lake huku wakigumia kama vile mtu anakula denda na hisia zimeanza kupanda..... nikaanza kusikia miguno pale mezani ya mmmmhh mmmhhh mmmh huku mtu kashikilia embe nyonyo lake mkononi anali mumunya na kugumia huku macho kayafumba hehehehehehheee. Basi hilo zoezi likaisha wakaenda kunawa wakarudi mezani kuendelea kugonga vyombo, waliporudi wakaanza kuongea, unajua bwana raha ya kufanya kitu shurti ukifurahie... hapa tumekula embe yaani kwa raha zetu na nafasi, wakaendelea na maelezo meengi pale mezani mie nikawa nacheka tuu. Ulipowadia muda wa kutoa mkono wa pongezi basi nikaenda wapongeza wenye shughuli huyo nikaondoka kurudi nyumbani.
Njia nzima nikawa nawawaza wale wakaka, kiukweli waliniburudisha maana sikujiona mpweke jpo sikuwa nafahamiana na mtu yeyote. Ila nikajisemea labda tuu kwakuwa mie na aibu zangu, kuna vyakula siwezi kula mbele za watu, kama hilo embe la kunyonya maana kwanza hata sura na mdomo vinavokaa wakati wa kulila hutaki hata kujiangalia kwenye kioo sembuse watu wengine kunitazama nikila embe nyonyo hahahahhaaaa.
Basi ni hayo tuu sina jingine, aliuporudi ubani nilimsimulia akasema hao watakuwa walikutamani mke wangu walitaka ujichanganye wakurubuni bora ulipoondoka. Sijui ni kweli au wivu tuu wa ubavu wangu maana kama ni hivyo siku nyingine hatoniruhusu niende shsereheni akiwa hayupo.
Niwatakie jioni njema yenye utulivu na amani na week end njema kuonana tena ni majaaliwa. (poleni kwa maelezo marefu)
Alamsiki.