Kasie's Crush... He Crush on Me....

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,805
Reaction score
43,230
Hello ladies and gentlemen,

Allow me to take this opportunity and give you a brief of what happens to Kasie yesterday evening.

Hili tukio limenifikirisha na kunifanya niwatazame wanaume kwa upya, kwa jinsi ninavowafahamu wanaume ya jana ilinishangaza kidogo. Labda waje watiririke hapa kueleza nini hasa huwajia akilini.

Kasie ni kibibi cha kukaribia kustaafu hivo hata mikunjo kwenye sura imeshajitokeza kwa wingi, ngozi ya mwili haijanyooka kama ya kischana au mtoto bali imeanza kusinyaa na misuli ya nyama za mwili imeanza kulegea. Tangu mwaka huu uanze ni wanja wa chini ya macho tuu ndo ambao bado unakubali, lipstick poa na mashedo yote ya uso yalishakataa.

Sasa jana nilitumwa kikazi ofisi ya Pretoria hivo nikaenda na Gautren sikutaka kuendesha ili nipumzike hivo nilitumia usafiri huo wa umma.
Saa ya kwenda nilienda vizuri saa ya kurudi ndo nikakutana na hii kasumba.

Wakati narudi ilikuwa saa moja na dakika kadhaa usiku nikakata ticket na kuingia kwenye seat yangu ya dirishani. Kabla treni halijaondoka akaja kijana mmoja hivi akakaa siti ye mbele yangu hivo tukawa tunatizamana. Nasema ni kijana kwasababu muonekano wake ni kati ya umri wa miaka 28 - 34 hivi. Mie nilikuwa busy na simu yangu naperuzi JF yule kijana alianza kunitizama kila nikimuangalia ananitizama mmhhh nikasema hapa iko namna. Akaanza kunyoosha miguu yake ikawa inagusana na yangu kama vile ananistua kitu ..... mie nikaona ule mseti wote ulivokuwa nikasema ngoja nijikaushe kama sisikii kitu nione mwisho wake utakuwaje.

Nilipofikia Sandton mie nikateremka huyo kuelekea madaladala yalipo na nilifanya makusudi hivo ili nione atanifata? Hehehehehhee wajua yule kijana alinifata sasa mie niko mbele yeye nyuma wala hakunisemesha kitu, ile nafika kwenye daladala nimeingia kumbe siti yangu ndo ikawa ya mwisho akaja akamuuliza dereva hivo daladala inaenda wapi? Akajibiwa imeshajaa hahahahahhaa daah hadi nikamuonea huruma.

Akabaki pale chini na akaonekana hata haelewi aende wapi... nikajisemea huyu yawezekana alikuwa haendi huku Sandton ila kushuka huku kunifatilia tuu daah.
Basi kituo cha daladala kilichofuata mie nikashuka nikachukua taxi hadi nyumbani. Nikipoingia kwwnye taxi nikaendelea kukukwaza yule kijana na kufikiria......

Hivi wanaume wanapokutana na mwanamke ambaye on the first place au kwa muonekano wa kwanza sio mzuri au havutii kw maana ya sura na shape kama Kasie nilivo na uzee huu... sasa kinachomfanya aanze kutongoza tena kwa kunigusa gusa miguu yangu kwa miguu yake.... ni kuwa anajifunza kutongoza? Ana stress kiasi kwamba mwanamke yeyote ajaye mbele yake atamtongoza? Ni tabia tuu ya mtu husika kutongoza mwanamke yeyote? Au alishakuja na sulika za hali ya juu hivo anavaa mwanamke yeyote a jaribu kutongoza akikubali apige kazi?

Ni kipi haswa... mbona waschana wazuri wapo?

Pole wee kijana kiukweli hata ungeniongelesha nisingekubali.... basi tuu ukorofi wa kas6ie.

Alhamis njema nyote.

Kasinde.
 
Mtihani mkubwa na kosa linalowakabili wengi ni hapo kutofautisha tamaa na upendo...

Kasie nani kakwambia hauvutii au sio mzuri? Umetumia vigezo gani kufikia hilo hitimisho?
Uzuri wa mtu uko machoni kwa mtu. Yeye anaweza akajiona havutii. Lakini hatuwezi jua huyo kijana aliona nini kilichomvutia kwa bibi. Labda ile mikunjo? Au rangi yake?.
 
Uzuri wa mtu uko machoni kwa mtu. Yeye anaweza akajiona havutii. Lakini hatuwezi jua huyo kijana aliona nini kilichomvutia kwa bibi. Labda ile mikunjo? Au rangi yake?.

Ndio maana nasema, ni kazi sana kujua nani anakupenda na yupi anakutamani, wanaume kuna wakati tuna mambo ya ajabu sana...wakati mwingine mtuombee tu itapendeza.
 
Hahaaa. Dada yangu wa Kinyamwezi katika ubora wako mwenyewe.

Siku zote kuna vitu huwa vikitokea vinakuwa ni kama kikohozi yaani mtu anaweza jizuia ila mwisho wa siku inashindikana. Na ndio ilivyokuwa kwa huyo Kaka sasa.
 
Wala usishangae ,sisi wanaume tunaweza safiri safar ya masaa 48 kumfuata mwanamke ,,maajabu nikwamba ukishamla tu unaanza kujilaumu kwann umepoteza muda na pesa !!.

Nahapa ndo wanawake wengi mnapotezwa nakuingizwa chakiume sababu Tafasir yenu yakwanza kwahuyu mwanamme huwa ni "Ananipenda sana ndo maana kapoteza muda na pesa nakutembea umbali mrefu kwaajili yangu"

[emoji23] [emoji23] [emoji23] mama papuchi tunaifatiliaga sana hata km nikutoka Beijing na kwenda Washington DC.
 
Mimi nina swali Kasie huo uzee wako na shepu mbaya unayotaja wengine ndio wanapenda namba hizo kama za kwako usiwapangie wapende wapi kwingine kuzuri, una damu kali sana ya either kupendwa tu ili mtu apate kitu chake aishie au una damu ya kupendwa tu bila ya mtu kuhitaji kitu chochote kutoka kwako au unadamu ya kupendwa ili uolewe moja kwa moja ila wewe unatolea nje, shepu sio tatizo umri sio tatizo tatizo linaweza likaja hapo baadae kwenye tabia ya kwake au yakwako ndio vinaweza vikamfanya asikupende kabisa na si umri wala uzee au ngozi kuwa nzee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…