Kasie Mtoto

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,805
Reaction score
43,230
Kasie Mtoto.......

Nilipokuwa binti mdogo nilikuwa mdadisi sana, nakumbuka nilikuwa nikimuuliza mama Kasie kila mara nikiwa mkubwa ntakuwa nani? Yaani maisha yangu yatakuwaje?


Mama Kasie alinijibu mwanangu Kasie maisha ni kuyapa muda na wakati.... vyovyote utavyokuwa muda haugandi masaa yataenda siku zitapita na hakika utakuwa mkubwa na kuona kuwa utakuwa nani.



Kasie Kigoriii

Muda ukapita nikawa kigori hapo nikapata mpenzi aliye nitoa utando wa mahaba, siku moja kati ya siku zetu tulizo kuwa kwenye mahaba nikimuuliza. ... mpenzi maisha yetu yatakuwaje... tutazeeka pamoja? Tutastaafu pamoja? Tutakuwa na mafanikio gani au penzi letu litazorota? Mpenz akanijibu.....


Kasie Mahaba

Kasie mpenz, vyovyote itavokuwa maisha ni kuyapa wakati, muda na kuvuta subira. Muda haugandi na wakati ukuta.... wakati ukifika utaona tuu jinsi itavokuwa.


Nyakati zote mbili hizo nilikuwa na shauku ya kutaka kujua nini kitatokea mbele.... leo hii naandika hapa nina kurasa na kurasa za Kasie kwa yaliyomtukia.

Basi kwa robo tatu hii iliyobakia kutokana na makadirio ya (analysts) Kasie's future will be........

Kasie Motoo Matata 2018.
 
Kasie mama naona umeamua kuja na shairi tuwape muda wadau wata comment
 
Nimeipenda neno ulilotumia MAISHA NIKUYAPA WAKATI
 
Huwa nampenda sana mtu anayejisifu nafsi yake. Kwa maana hapo hawezi kumsimanga mtu wala kumtusi mtu. Hata kama anadanganya haleti madhara kwa mtu mwingine.
 
mi nakwambia ningekuwepo enzi yako walahi ningefanya tendo la kikubwa nawe!.

tuone hizo berenge berenge za mwaka 2018.. lkn kwani huwa unapenda kuzungumzia mapenzi..?
 
mi nakwambia ningekuwepo enzi yako walahi ningefanya tendo la kikubwa nawe!.

tuone hizo berenge berenge za mwaka 2018.. lkn kwani huwa unapenda kuzungumzia mapenzi..?

Hahahahahahahaa na Mungu alijua hilo, ndo maana hakuruhusu uwepo kipindi cha enzi zangu, alijua vurugu zako kabla hujaumbwa.

Jibu la swali lako ni kuwa.....

Kasie ni Mapenzi na Mapenzi ni Kasie, kuna semi huwa zinasema Born to Win.... Born to Be Rich.... Born to Suffer and the like.
For Kasie. ... Born to Love...... mahaba mwanzo mwisho.

Kuna kipindi nilijaribu kubadilika niwe kama binadamu wengine nijichanganye huku na kule, nikaingia jukwaa la siasa nikaanzisha uzi wa marehemu aliyekuwa mbunge wa maeneo ya Iringa sijui (jina lake limenitoka) ila alikufa kwa kupata ajali ya helikopta kipindi cha harakati za kujiandaa na kampeni za uchaguzi. Sijui kwa nini jina lake limenitoka kabisaaa daah labda ndo uzee huo.
Basi huo uzi ukafutwa aaah nikaandika uzi mwingine kuuliza je siruhusiwi siasani? Maana sikuambiwa kwanini ule uzi ulifutwa. Aaah nikaachana na siasa nikabaki na mahabat yangu na ntaendelea nayo till the day I kick the bucket.

Pole kwa maelezo marefu.
That's Kasie, Kasie Mahaba.
 
Huwa nampenda sana mtu anayejisifu nafsi yake. Kwa maana hapo hawezi kumsimanga mtu wala kumtusi mtu. Hata kama anadanganya haleti madhara kwa mtu mwingine.

Hahahahhahaa sijui ni ubinafsi nilionao au ni hulka tuu, kiukweli mara nyingi huwa najizungumzia mwenyewe mimi kama mimi na mambo ambayo yamenitukia. Najikuta tuu niko hivo. .... si kuwa sijui habari za watu humu JF.... laah hasha na wa fahamu watu wengi tuu na nshakuona na watu kibao kadha wa kadha. Hao baadhi yao ndo huwa wananizungumzia kwenye vikings vyao, wengine hunifata kwenye nyuzi zangu kwa ID mchepuko zao na kunikebehi au kuninanga mie waalaah nawatizama halafu nawaona hivii na vilee tuu (low profile).

Ila hata siku moja hutosikia Kasie anazungumzia flani na flani humu JF nawaambiaga muwe na amani tuu, what happens in Vegas remains in Vegas. Ila......... tukio kama tukio huwa nalileta hapa kama lilivo Kasie akiwa main character na mhusika wa pili namuacha kwenye mabano.

Asante kugundua hilo.
Cool Kasie.
 
Kasie umesahau, mtu mwingine anayejiongelea yeye kama yeye ni mtemi Deo Kisandu
 
Pole umebakiza robo tu na wala si robotatu
 
Kweli hapo lazima utamani kuwa malaika..uzee una karaha zake

Kwa Kasie uzee una raha zake pia na naufurahia maana najua kukabiliana nao.
Kasie ni shiiiddeeer heheheheheheee.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…