Kasi ya utendaji ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa inatufuta machozi wazalendo

Una wivu weweeee..... hadi na wewe unaishia kutafuta sofa๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Ungekua mke mwenzangu ningekufunza kwa vitendo na ungeishia kungejinyonga tuu๐Ÿ™„๐Ÿ™„

๐Ÿ˜‚ ๐Ÿ˜‚ ๐Ÿ˜‚
 
Kimsingi, kwa mtazamo wangu, pm ndiye anatakiwa awe hivi. Raisi asiwe mtu Wa kusikika hovyo....

ni km second master shuleni. Ukiona Shule imesimama barabara kitaaluma na maendeleo kwa ujumla, basi jua hapo kuna second master mmoja hatari sana......anasimamia nidhamu vema (yake mwenyewe na ya wengine), anaunganisha walimu vema, anawaunganisha walimu na mkuu wa shule vizuri, anamshauri vema mkuu wa shule n.k. mkuu wa shule anakuwa busy kufuatilia mambo mengine ya kimaendeleo kwa shule au walimu kutoka kwa wadau mbalimbali au wakubwa wao.

rais inabidi awe busy kusoma tu mchezo unavyoenda na kurekebisha hapa na pale huku akiwa busy kuangalia maelfu ya fursa yaliyopo nchini na duniani kwa ujumla katika kuleta maendeleo.

nafurahishwa na utaratibu huu wa mama Samia wa kumpa nguvu pm.....watendaji wa serikali lazima watetemeke pale pm, sio anapotokea tu, bali hata anaposikika redioni tu. huu ndiyo utaratibu mzuri, sio raisi unaongea ongea tu kila leo na kuingilia kila jambo mara tatu kwa siku kama dozi ya aspirin!
 
Ww mbna taahira,nan anakujua nchi hii????
Huko upinzani kuna nani ya kunifanya niharibu kura yangu kumpa? Yule chizi wa ubeleji? Are you serious?
Umesema vyema, hiyo itatokea endapo watacheza karata zao vizuri, ikiwa ni pamoja na kupata mtu credible na mwenye kuweza kuaminika kupewa uongozi wa nchi.
 
UTENDAJI KAZI: MAJALIWA KASSIM MAJALIWA

โ€ขTarehe 10/4/2021 anafanya ziara kukagua ujenzi wa bwawa la umeme la Julius Nyerere lililopo Rufiji na kuwaahidi Watanzania kuwa ujenzi utaendelea kama kawaida na kumalizika kwa muda uliopangwa.

โ€ขTarehe 19/4/2021 anakwenda kuukagua mradi wa mabasi ya mwendokasi baada ya malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya Ufanisi wa mradi huo, anakuta utendaji ni mbovu anamsimamisha kazi mkurugenzi wa fedha wa mradi huo Susana Steven Chaula.

โ€ขTarehe 19/4 /2021 anakwenda kukagua bandari ya nchi kavu Ubungo Baada ya magari ya mizigo kukwama kwa zaidi ya siku tatu..anafanya mazungumzo na madereva pamoja na watendaji wa bandari

โ€ขTarehe 19/4/2021 anafanya ziara kiwanda cha kuunganisha magari cha GFA kilichopo Kibaha, Pwani. Anawahakikishia wawekezaji hao kuwa Vijana wa kitanZania ni waaminifu. Siku kadhaa baada ya Spika wa bunge kunukuliwa akisema vijana wa Kitanzania SIO waaminifu.

โ€ขTarehe 21/4/2021 anaenda kukagua ujenzi wa stesheni ya Treni ya umeme iliyopo Pugu Dar, anasema "Mradi utaenda kama JPM alivyoahidi.."

โ€ขTarehe 20/5/2021 anafanya ziara Tanesco. Anazungumza na uongozi wa Tanesco kuhusu tatizo lililojitokeza katika ununuaji wa LUKU lililopelekea wananchi washindwe kununua LUKU siku tatu mfululizo, anaamuru meneja Tehama na wenzake waendelee kukaa pembeni kupisha uchunguzi.

โ€ขTarehe 28/5/2021 anafanya ziara ya kushtukiza wizara ya fedha, anakuta watendaji wa wizara hiyo wakijilipa posho ya zaidi ya billioni 1.6 kwa kazi zisizochukua hata nusu saa, anawasimamisha kazi watendaji wakuu saba.
Hapo unyonge wenu Ni upi?
 
Huyu anafanya kazi kwa ajili ya kujionesha, Hana uchapakazi wowote, Ni one man show, kwanini wasiweke mfumo? Ni one man show ya kutafuta sofa, Majaliwa hafai
Mkuu umenena....kutakuwa Kuna tatizo kubwa la mfumo wa kudhibiti fedha wizarani....hivi kweli watendaji watafanyaje malipo hewa wizarani....uongozi upo... na taratibu zipo....pesa inatokaje Waziri mkuu.....waziri na Katibu wake wasijue.
 
Wiki jana nimeingia benki moja Mikoa Fulani nikakuta watumishi wamejikusanya kwa majonzi. Baadhi yao niliwafahamu Na nilipowadodosa wakadai mikopo yao kukwamishwa na maafisa utumishi.

Walidai kupewa majibu hayo na maafisa wa benki. Kuwa maafisa utumishi wamegoma kuingiza makato kwenye mfumo wa mishahara ambapo ndiyo taratibu ili mikopo itolewe kwa walengwa.

Wengi walionekana kuhuzunishwa na Jambo hilo .\

Nikajiuliza, ni nini kimesababisha maafisa utumishi hao kutotoa majibu ya uhakika au wahusika kurekebisha mfumo ili wahitaji wa mikopo waweze kupata stahiki zao.

Ni majuzi tuu tuishuhudia mfumo wa Lulu au ulipaji umeme ukihujumiwa na kuzua keep kwa watumiaji umeme nchi nzima. Ambapo Baada ya Waziri Mkuu kuingilia kati, na massa machache baadae tatizo likaisha.

Je, hapa Nako kuna umuhimu wa Wa Waziri Mkuu kuingilia kati ili Watumishi hawa wapate stahiki zao?
 
Watu wanapiga pesa bhanaa... Duh,!! Wizara ya Fedha kibokoo...
 
Sasa namuona Mhe. Waziri Mkuu ktk viwango vyake, .
kamwe usirudi nyuma wala usikubali kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa....wee chapa kazi......kanyaga twendee.....usimuonee aibu mbadhirifu au wezi wa mali za umaa.
 
UTENDAJI KAZI: MAJALIWA KASSIM MAJALIWA

โ€ขTarehe 10/4/2021 anafanya ziara kukagua ujenzi wa bwawa la umeme la Julius Nyerere lililopo Rufiji na kuwaahidi Watanzania kuwa ujenzi utaendelea kama kawaida na kumalizika kwa muda uliopangwa.

โ€ขTarehe 19/4/2021 anakwenda kuukagua mradi wa mabasi ya mwendokasi baada ya malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya Ufanisi wa mradi huo, anakuta utendaji ni mbovu anamsimamisha kazi mkurugenzi wa fedha wa mradi huo Susana Steven Chaula.

โ€ขTarehe 19/4 /2021 anakwenda kukagua bandari ya nchi kavu Ubungo Baada ya magari ya mizigo kukwama kwa zaidi ya siku tatu..anafanya mazungumzo na madereva pamoja na watendaji wa bandari

โ€ขTarehe 19/4/2021 anafanya ziara kiwanda cha kuunganisha magari cha GFA kilichopo Kibaha, Pwani. Anawahakikishia wawekezaji hao kuwa Vijana wa kitanZania ni waaminifu. Siku kadhaa baada ya Spika wa bunge kunukuliwa akisema vijana wa Kitanzania SIO waaminifu.

โ€ขTarehe 21/4/2021 anaenda kukagua ujenzi wa stesheni ya Treni ya umeme iliyopo Pugu Dar, anasema "Mradi utaenda kama JPM alivyoahidi.."

โ€ขTarehe 20/5/2021 anafanya ziara Tanesco. Anazungumza na uongozi wa Tanesco kuhusu tatizo lililojitokeza katika ununuaji wa LUKU lililopelekea wananchi washindwe kununua LUKU siku tatu mfululizo, anaamuru meneja Tehama na wenzake waendelee kukaa pembeni kupisha uchunguzi.

โ€ขTarehe 28/5/2021 anafanya ziara ya kushtukiza wizara ya fedha, anakuta watendaji wa wizara hiyo wakijilipa posho ya zaidi ya billioni 1.6 kwa kazi zisizochukua hata nusu saa, anawasimamisha kazi watendaji wakuu saba.
Majaliwa for presidency 2025
 
Back
Top Bottom