Kasi ya utendaji ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa inatufuta machozi wazalendo

Labda aanzishe mapambano akiwa nje ya ccm! Ukishakuwa ndani ya ccm, kamwe huwezi kuwa Mzalendo.
MSIWAKATISHE TAMAA WAKUSANYAJI MAPATO:

Mhe.Kassim Majaliwa PM:

Aliagiza kusimamishwa kazi kwa mkaguzi mkuu,mkaguzi msaidizi na baadhi ya watumishi wa wizara ya fedha na mipango kupisha uchunguzi juu ya tuhuma ya ufujaji wa pesa unaowakabili.

"Mmetenga mil 279 mkasema zimetumika kwenye kazi maalumu bila kutujuza hiyo kazi maalumu ni ipi na alieifanya kazi hiyo ni nani ilifanyika lini na wapi" Majaliwa.

"Msiwakatishe tamaa wakusanyaji mapato,wapo kule TRA wanakusanya mapato,wapo halmashauri,wapo watendaji wa serikali za mitaa huko wanafanya kazi kubwa sana ya ukusanyaji mapato,msiwakatishe tamaa wafanyeni kuwa na imani na wizara ili wawe na uhakika na imani na kazi zao" Majaliwa.

Ni waziri mkuu Mhe.Kassim Majaliwa kwenye mkutano na wakuu wa wizara ya fedha pale ukumbi wa hazina jijini Dodoma.

Nini fikra zako.
 
Huyu anafanya kazi kwa ajili ya kujionesha, Hana uchapakazi wowote, Ni one man show, kwanini wasiweke mfumo? Ni one man show ya kutafuta sofa, Majaliwa hafai
Cha kushangaza unaweza kuwa unasema majaliwa hafai kisha ukasema mama ndo anafaa. Nani kwako unaona anafaa?
 
MSIWAKATISHE TAMAA WAKUSANYAJI MAPATO:

Mhe.Kassim Majaliwa PM:

Aliagiza kusimamishwa kazi kwa mkaguzi mkuu,mkaguzi msaidizi na baadhi ya watumishi wa wizara ya fedha na mipango kupisha uchunguzi juu ya tuhuma ya ufujaji wa pesa unaowakabili.

"Mmetenga mil 279 mkasema zimetumika kwenye kazi maalumu bila kutujuza hiyo kazi maalumu ni ipi na alieifanya kazi hiyo ni nani ilifanyika lini na wapi" Majaliwa.

"Msiwakatishe tamaa wakusanyaji mapato,wapo kule TRA wanakusanya mapato,wapo halmashauri,wapo watendaji wa serikali za mitaa huko wanafanya kazi kubwa sana ya ukusanyaji mapato,msiwakatishe tamaa wafanyeni kuwa na imani na wizara ili wawe na uhakika na imani na kazi zao" Majaliwa.

Ni waziri mkuu Mhe.Kassim Majaliwa kwenye mkutano na wakuu wa wizara ya fedha pale ukumbi wa hazina jijini Dodoma.

Nini fikra zako.
Ishu ni kwamba, Nchi yetu imeoza! Kila sekta watu wanapiga tu. Na sababu kubwa ni uwepo wa ccm, chama kinachpenda kuwalinda na kuwakumbatia wahalifu.

Anachokifanya huyo Waziri Mkuu kwa sasa, ni kutwanga tu maji kwenye kinu. Atawasimamisha hao jamaa wa BOT, wakati huo huo watumishi wa sekta nyingine za umma wanaendelea kutafuna hela za umma.

Ili kukomesha wizi na ufisadi uliokithiri nchini, Rais akubali kujenga mfumo imara kupitia Katiba Mpya na pia sheria kali dhidi ya wabadhirifu wa mali za umma na wezi! Kinyume na hapo, kwangu hizo hatua naona kama maigizo tu. Maana mwisho wa siku, hakuna kinacho badilika! Watu wanaendelea tu kuiba.
 
Huyu anafanya kazi kwa ajili ya kujionesha, Hana uchapakazi wowote, Ni one man show, kwanini wasiweke mfumo? Ni one man show ya kutafuta sofa, Majaliwa hafai
Kwako wewe ni one man show!! Lkn kwetu sisi tunaamini ni mtu aliyepikwa na akapikika vya kutosha! na mwamba JPM. Ndo maana aliumia sana kwa kifo cha JPM. Majaliwa ndiye rais ajaye Tanzania hii, kama huamini! kamuulize ndugu yako mayala.
 
UTENDAJI KAZI: MAJALIWA KASSIM MAJALIWA

Tarehe 10/4/2021 anafanya ziara kukagua ujenzi wa bwawa la umeme la Julius Nyerere lililopo Rufiji na kuwaahidi Watanzania kuwa ujenzi utaendelea kama kawaida na kumalizika kwa muda uliopangwa.

Tarehe 19/4/2021 anakwenda kuukagua mradi wa mabasi ya mwendokasi baada ya malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya Ufanisi wa mradi huo, anakuta utendaji ni mbovu anamsimamisha kazi mkurugenzi wa fedha wa mradi huo Susana Steven Chaula.

Tarehe 19/4 /2021 anakwenda kukagua bandari ya nchi kavu Ubungo Baada ya magari ya mizigo kukwama kwa zaidi ya siku tatu..anafanya mazungumzo na madereva pamoja na watendaji wa bandari

Tarehe 19/4/2021 anafanya ziara kiwanda cha kuunganisha magari cha GFA kilichopo Kibaha, Pwani. Anawahakikishia wawekezaji hao kuwa Vijana wa kitanZania ni waaminifu. Siku kadhaa baada ya Spika wa bunge kunukuliwa akisema vijana wa Kitanzania SIO waaminifu.

Tarehe 21/4/2021 anaenda kukagua ujenzi wa stesheni ya Treni ya umeme iliyopo Pugu Dar, anasema "Mradi utaenda kama JPM alivyoahidi.."

Tarehe 20/5/2021 anafanya ziara Tanesco. Anazungumza na uongozi wa Tanesco kuhusu tatizo lililojitokeza katika ununuaji wa LUKU lililopelekea wananchi washindwe kununua LUKU siku tatu mfululizo, anaamuru meneja Tehama na wenzake waendelee kukaa pembeni kupisha uchunguzi.

Tarehe 28/5/2021 anafanya ziara ya kushtukiza wizara ya fedha, anakuta watendaji wa wizara hiyo wakijilipa posho ya zaidi ya billioni 1.6 kwa kazi zisizochukua hata nusu saa, anawasimamisha kazi watendaji wakuu saba.
Old wine in old bottles!
Msaidizi mkuu wa JPM pamoja na madudu yao.
 
Huyu anafanya kazi kwa ajili ya kujionesha, Hana uchapakazi wowote, Ni one man show, kwanini wasiweke mfumo? Ni one man show ya kutafuta sofa, Majaliwa hafai
Ukiulizwa ulichopinga siajabu ukasema haujui, one man show ndio nini au unakariri tu, kwahiyo kazi zake ulitaka afanye nani, binadamu tuna matatizo mengi ila yako ya mezidi, yaan unaonekana umelewa hata kama sikuoni
 
UTENDAJI KAZI: MAJALIWA KASSIM MAJALIWA

Tarehe 10/4/2021 anafanya ziara kukagua ujenzi wa bwawa la umeme la Julius Nyerere lililopo Rufiji na kuwaahidi Watanzania kuwa ujenzi utaendelea kama kawaida na kumalizika kwa muda uliopangwa.

Tarehe 19/4/2021 anakwenda kuukagua mradi wa mabasi ya mwendokasi baada ya malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya Ufanisi wa mradi huo, anakuta utendaji ni mbovu anamsimamisha kazi mkurugenzi wa fedha wa mradi huo Susana Steven Chaula.

Tarehe 19/4 /2021 anakwenda kukagua bandari ya nchi kavu Ubungo Baada ya magari ya mizigo kukwama kwa zaidi ya siku tatu..anafanya mazungumzo na madereva pamoja na watendaji wa bandari

Tarehe 19/4/2021 anafanya ziara kiwanda cha kuunganisha magari cha GFA kilichopo Kibaha, Pwani. Anawahakikishia wawekezaji hao kuwa Vijana wa kitanZania ni waaminifu. Siku kadhaa baada ya Spika wa bunge kunukuliwa akisema vijana wa Kitanzania SIO waaminifu.

Tarehe 21/4/2021 anaenda kukagua ujenzi wa stesheni ya Treni ya umeme iliyopo Pugu Dar, anasema "Mradi utaenda kama JPM alivyoahidi.."

Tarehe 20/5/2021 anafanya ziara Tanesco. Anazungumza na uongozi wa Tanesco kuhusu tatizo lililojitokeza katika ununuaji wa LUKU lililopelekea wananchi washindwe kununua LUKU siku tatu mfululizo, anaamuru meneja Tehama na wenzake waendelee kukaa pembeni kupisha uchunguzi.

Tarehe 28/5/2021 anafanya ziara ya kushtukiza wizara ya fedha, anakuta watendaji wa wizara hiyo wakijilipa posho ya zaidi ya billioni 1.6 kwa kazi zisizochukua hata nusu saa, anawasimamisha kazi watendaji wakuu saba.
Huyu ndiye YULE ajaye!!!
 
Nyinyi watu wengine sijui huwa mnafikiri kwa kutumia brain za namna gani?

Kwani waziri Mkuu Majaliwa anamtumikia nani? Ni waziri Mkuu wa serikali gani?

Unapotaka kuwaaminisha watu kwamba Majaliwa anachapa kazi kuliko raisi huo ni upuuzi mtupu. Majaliwa kama mtendaji mkuu wa serikali anatekeleza majukumu yake kama anavyopangiwa na bosi wake mama Samia Suluhu Hassan. Hebu acheni ushamba wenu nyinyi mataga!
 
Wiki jana nimeingia benki moja Mikoa Fulani nikakuta watumishi wamejikusanya kwa majonzi. Baadhi yao niliwafahamu Na nilipowadodosa wakadai mikopo yao kukwamishwa na maafisa utumishi.

Walidai kupewa majibu hayo na maafisa wa benki. Kuwa maafisa utumishi wamegoma kuingiza makato kwenye mfumo wa mishahara ambapo ndiyo taratibu ili mikopo itolewe kwa walengwa.

Wengi walionekana kuhuzunishwa na Jambo hilo .\

Nikajiuliza, ni nini kimesababisha maafisa utumishi hao kutotoa majibu ya uhakika au wahusika kurekebisha mfumo ili wahitaji wa mikopo waweze kupata stahiki zao.

Ni majuzi tuu tuishuhudia mfumo wa Lulu au ulipaji umeme ukihujumiwa na kuzua keep kwa watumiaji umeme nchi nzima. Ambapo Baada ya Waziri Mkuu kuingilia kati, na massa machache baadae tatizo likaisha.

Je, hapa Nako kuna umuhimu wa Wa Waziri Mkuu kuingilia kati ili Watumishi hawa wapate stahiki zao?
 
Kwako wewe ni one man show!! Lkn kwetu sisi tunaamini ni mtu aliyepikwa na akapikika vya kutosha! na mwamba JPM. Ndo maana aliumia sana kwa kifo cha JPM. Majaliwa ndiye rais ajaye Tanzania hii, kama huamini! kamuulize ndugu yako mayala.
Naona musiba aka veronica mmepata tenda ya kumfanyia promo Majaliwa.

Majaliwa ni waziri Mkuu wa serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan,anatekeleza majukumu kama anavyopangiwa na bosi wake. Mbona mnajitoa ufahamu?
 
Mwendazake alishamlaani.. hawezi kuwa Raisi, naona kuna kikundi cha kampeni kimeshaanza.
Na matamasha yake ya kiki coordinators kama kimeumana vile yanabuma.
Hauziki ataishia kuwa PM.

Everyday is Saturday.............................. :cool:
 
Huyu anafanya kazi kwa ajili ya kujionesha, Hana uchapakazi wowote, Ni one man show, kwanini wasiweke mfumo? Ni one man show ya kutafuta sofa, Majaliwa hafai

Una wivu weweeee..... hadi na wewe unaishia kutafuta sofa😂😂😂
Ungekua mke mwenzangu ningekufunza kwa vitendo na ungeishia kungejinyonga tuu🙄🙄
 
watanzania wanasubiria na bakora zao tayari kuwapa wapinzani kura zote kwa asilimia zote.

Ila hiyo itatokea endapo tu wapinzani watacheza uzuri karata zao.
Huko upinzani kuna nani ya kunifanya niharibu kura yangu kumpa? Yule chizi wa ubeleji? Are you serious?
Umesema vyema, hiyo itatokea endapo watacheza karata zao vizuri, ikiwa ni pamoja na kupata mtu credible na mwenye kuweza kuaminika kupewa uongozi wa nchi.
 
Back
Top Bottom