Wanasaikolojia wanasema usikubali au usilazimishe uione jana ni nzuri kuliko leo, hakikisha leo inakua nzuri kuliko jana, ukipata mpenzi hakikisha hamkumbuki x wake kwa mazuri aliyomfanyia kwani hatokua na furaha na wewe, msisababishe wana ccm na watanzania wamkumbuke kikwete ambae alikua kiongozi mbovu kuliko ninyi
Ombwe la uongozi la sasa, na woga wa viongozi kuogopa vivuli vyao, vinawafanya Watanzania wamkumbuke Kikwete na kumuona Kikwete, rais aliyekuwa na mapungufu mengi, kuwa ni kiongozi ambaye kwenye nyanya fulani, hususan uhuru wa watu kujieleza, siasa na vyombo vya habari, kuwa ni rais bora maradufu kuliko huyu wa sasa.
Magufuli angeweza kuwa rais bora zaidi kama angeachia siasa na vyombo vya habari vifanye kazi kwa uhuru.
Kushindwa katika hili kunamfanya awe kiongozi anayepwaya kwenye haya mambo.
Kitu kibaya kabisa ni kwamba, uongozi wa rais Magufuli ulivyoanza ulikuwa na mtaji mkubwa sana wa kisiasa wa kuaminiwa na wananchi. Na kwa kweli mpaka sasa wapo watu wengi wanaomuamini na kumtetea. Na kuna mambo amefanya vizuri -ingawa hata mazuri anayafanya vibaya- lakini tatizo linakuja, rais Magufuli ameutumia mtaji huo vibaya, ameufuja. Amelazimisha vita kubwa dhidi ya upinzani dhaifu ambao haukuwa na hoja ya msingi ya kumpinga. Sasa rais Magufuli ameifanya vita yake mwenyewe aliyoianzisha dhidi ya upinzani kuwa ni hoja ya wapinzani dhidi ya utawala wake. Kimsingi ameupa upinzani ambao ulikuwa unaelekea kuishiwa na hoja hoja mpya, kwamba unaonewa na utawala wa Magufuli.
Yani ni kama unakuwa na nzi mmoja anayekufa kwa kukosa hewa ndani ya nyumba yako, halafu kwa insecurity yako tu unatumia bomu la nyuklia kumuua nzi yule mpaka unahatarisha maisha ya familia yako mwenyewe na kusababisha mgogoro kwamba umetumia nguvu za nyuklia kuua nzi mmoja kinyume na mikataba ya kimataifa.
Ndicho anachofanya Magufuli sasa hivi.