Alichokifanya mfalme Leonidas wa Ugiriki ndio anachokifanya Magufuli Tanzania

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,676
106,771
1081645

Ugiriki ya zamani ilikua imeundwa na miji ipatayo mia moja ambapo kila mji ulikua na utawala wake, Mji wa Athens na Sparta ndio ulikua miji mikubwa na yenye nguvu zaidi, japo miji hii mra nyingi ilikua inapigana kwa ajili ya kugombania ardhi lakini vilikua vimejiunga pamoja ili kujilinda na uvamizi wa kutoka nje. .. Technically Sparta and Athens determined as city- state…!!!

Leonidas alizaliwa 530-480 B.C. alikua mfalme wa mji unaoitwa Sparta tangu mwaka 490 B.C mpaka wa kifo chake katika vita ya Thermopylae dhidi ya Persia
Leonidas alikua mtoto wa mfalme wa Anaxandrides, alikua mfalme baada ya kaka yake Cleomenes I kufa kati hali ya utata mwaka 490BC (huyu pia alikua mototo wa Anaxandrides sema hii familia kidogo ilikua inamkanganyiko maana baba yake Leonidas alimuoa mpwa wake na kumfanya mke wa pili ndipo alipozaliwa Leonidas. baada ya kaka yake clemence kufa ilibidi Leonidas ashike ufalme kwakua clemence hakua na mtoto wa kiume wa kurithi kiti chake, kwao ilikua mwiko kuwa na kiongozi mwanamke)
Akiwa mfalme pia Leonidas alikua kiongozi wa jeshi pia mwanasiasa, kama kawaida ya wanaume wote wa Sparta, Leonidas alifunzwa kuwa sawa kimwili (mapigano) na kiakili toka akiwa mdogo ili kuandaliwa kuwa kiongozi.

Wanajeshi wa ugiriki (Sparta) walijulikana kama Hoplites, ambapo hoplites walikua wanajeshi wenye ngao ya duara,mkuki na upanga mfupi wa chuma. Kwenye vita walikua wanatumia mfumo wa vita unaofahamika kama phalanx ambapo hoplites alikua anasima mbele ya mwenzake kisha anatumia ngao yake kujilinda na kumlinda mwenzake kama likitokea shambulio la mbele. Kama phalnx ikivunjika au adui akishambulia kutoka upande wa kushoto au kulia basi inakua hatarii zaidi kwa Hoplites
Mwanzoni mwa karne ya 5 BC nchi ya Persia ilikua inafanya uvamizi nchini ugiriki ,lakini jeshi lile la vile vimiji zaidi ya mia vilivyoungana kijeshi viliirudisha nyuma jeshi la Persian lilipotaka kuvamia katika vita inayojulikana kama Battle of Marathon ilikua mwaka 490 B.C chini ya mfalme Darius I wa Persia . Miaka kumi baadae mtoto wa Darius aitwae Xerxes I (519-465 B.C.), kwa mara ya pili alianzisha uvamizi nchini Ugiriki.

Chini ya mfalme Xerxes I, jeshi la Persian lilivamia ugiriki kupitia pwani ya mashariki akishirikiana na jeshi la maji la Persian lililokua linapita pwani. Ili kufika sehemu walipokua wanaeleka katika eneo linaloitwa Attica ambapo pia attica ilikua ni mji unaoongoozwa na Athens, Jeshi la Persia ilitakiwa lipite sehemu moja ya pwani inayoitwa Thermopylae (au “Hot Gates,” ilijulikana hivo kwakua ilikua karibu na chemichemi ya sulfur). Katika kipindi cha majira ya joto ya mwaka 480 B.C., Leonidas alikua anaongoza jeshi la wat 6,000 mpaka 7,000 kutoka miji mbalimbali iliyopo ugiriki ukijumuisha na wanajeshi 300 kutoka katika mji wake wa Sparta Aliongoza jeshi hilo kuziwia jeshi la Persia kupita ile sehemu inayoitwa Thermopylae.

Wananchi wa Sparta walikua na miungu yao walioiabudu, kulikua kuna mtu ambae alikua kama nabii wao ambae alikua anawapa maagizo wananchi kutoka kwa miungu hiyo. Kabla ya kwenda vitani Leonidas alienda kuonana na huyo nabii ili ampe maono kuhusu vita hiyo anayokwenda kupambana, nabii alimkataza kua asiiende atapoteza maisha ya wengi ni bora ajislimishe kwa jeshi la Persia, leonida alikata kata kata kua hataweza kujisalimiisha lazima akawaziwie pale kwenye hot gate, walimsihi sana na kumshauri lakini alikataa na kuituna miungo yake
Leonidas aliongoza jeshi lake hadi pale hotgate akiamini kua jeshi la Persia lazima lipitie pale alipambana nao na kuwaua wanajeshi wengi wa Persia kisha akajenga ukuta kwa kutumia maiti za wale wanajeshi.

Leonidas akiwa hajui kumbe jeshi lingine lilipita njia inayopita milimani hivyo wakatokezea nyuma ya jeshi la leonida, baada ya kugundua hilo makamanda walimshauri kua ni bora wajisalimishe maana washazungukwa ila Leonidas alikataa kabisa akasema sharia ya nchi ya Sparta hairuhusu kujisalimisha ni bora afe pale. Makamanda kutoka ile miji mbalimbali walichkua majeshi yao na kumuacha Leonidas akiwa na wanajeshi 300 tu!
Akiwa na wanajeshi 300 tu Leonidas alipambana na jeshi la zaidi ya watu 15000, mwisho alizidiiwa na kuuwawa..walimkata kichwa .

Ufanano wa Mfalme Leonidas na Rais Wetu Pombe JM
1081648

Ukiangalia kwa ukaribu tabia za mfalme huyo tuliye muangalia hapo utaona kabisa wanafanana na rais wetu wa Tanzania, na kuna mambo raisi anayfanya ni kama aliyokua anafanya mfalme Leonidas. Mambo hayo ni..
  • kujiamini kulikopitiliza.
By default Mungu katuumba na roho ya uoga na ujasili, vitu hivyo viwili vinatakiwa kuwa katika hali ya msawazo yaani kimoja kisizidi mwenzake. Sasa kwa raisi wetu kujiamini kumepitiliza…anajiona yeye ndio mwanaume wengine sio! Ataongea lolote, ataamua lolote hata kama hilo atakaloongea au kuamua litakua na madhara kwa taifa. Ilimradi anajiona yeye ndio yeye mwenye msimamo na kuyumbishwa. Wenyewe hua tunamsikia mtu akipendekeza hiki basi yeye anamshushua hapo hapo (kumbuka alivyojibiwa waziri mkuu katika sakata la korosho) ili mradi yeye ni raisi, yeye ndio mwenye sauti nchini. Kujiamini kulikopitiliza sio ushujaa muda mwingine ni ujinga. Kujiamini huko ndiko kulipelekea leonida kuteketeza wanajeshi 300.
  • Kutotaka kushauriwa na kukosolewa
Sijui ni nini lakini raisi wetu naona ana allergy ya kushauriwa, kwake yeye kushauriwa ni mwiko kabisa na ukimkosoa utaitwa mchochezi kisha utabambikiziwa kesi ya ukimbizi. Mtu anayejiamini kupitiliza hawezi kushauriwa maana anaona yuko sahaihi na ukimkosoa anaona unamdharirisha uwezo wake. Kama rais unayeaongoza 40mil ya watu inatakiwa uongozwe na ufikiri sio ego zako! Japo ni sahihi muda mwingine inabidi utoe maamuzi magumu bila kufuata ushauri lakini lazima upime matokeo ya uamuzii huo kwa taifa lako. Kumbuka rais alichokifanya kwenye zile meli za samaki za china mwisho zikapelekea kuighalimu taifa.

Rais kukosolewa sio dhambi unakua unaelezwa sehemu penye udhaifu wako ili ukajirekebishe, kama alichofanya kwa miungu yao ndio nawe unafanya kwa viongozi wa dini! Imefika hatua serikali yako inawasingizia viongoozi wa dini ukimbizii kisa wamekukosoa..nyaraka mbalimbali zimeandikwa na makasisi wa dini yako lakiini umeishia kuwasumbua! Muheshimiwa Rais Mungu mwenyewe aliona kua kichwa kimoja hakitoshi ndio maana akaongezea kumuumba mwanamke ilia je kumshauri, na mengine. Mungu mwenyewe upande wake wa kuume yupo Yesu kristo ushawahi kujiuliza anafanya nini pale? Kasome injili ya Yohana1:1-10 utafahamu. Ila wewe mwenzewtu upande wako wa kuume umemuweka Paul makonda badala ya mawaziri na washauri wako! Muheshimiwa ifike hatua uone kua kukosolewa ni jambo la kawaida nan chi hii kuwepo upinzani sio dhambi, hata Mungu mwenyewe ana upinzani na kila kitu hapa duniani kimewekewa mpinzani wake ili kubalnce nature. Anagalia mkono wa kuume kuna wa kushoto, uzuri una ubaya, ukali una upole, Baraka ina laana,Mungu ana shetani,, mbingu ina ardhi, moto una maji ILA CCM haitaki vyama vya upinzani kwanini lakini??

Yaani rais wangu unaniangusha mnoo asee sikukutegemea kabisa, wewe ni nani usishauriwe? Wewe ni nani ujiamini kupitiliza hivo? Wewe ni nani usikosolewe? Kingine rais uaachane na kutafuta public attention kwa vitu vidogovidogo mambo hayo mwachie mbowe na Tundu lissu.
Kama mfalme Leonidas alivyoongoza wanajeshi 300 kwenye kifo ndio rais wetu anavyolipeleka taifa la watu mil 40+ kwenye kifo, yes our president is leading us to our death! kifo cha uchumi, elimu,afya, amani,upendo,uhuru wa kujieleza, nk nk.
Taifa letu kiuchumi ndio tunakufa taratiibu taratibu ukichukulia pato la mwanachi mmoja mmoja wa kawaida, hakuna haki ya kujieleza nchini kwetu..ngoja tu niishie hapa maana mengi yanatia kinyaa kabisa.

Our president proclaiming himself that he might be the leader of Angels in Heaven, hollyshit!! This is blasphemy our God never lie and compromising..Kama kweli unatak siku moja kuwa kiongozi wa malaika basi simama kwenye ukweli, Malaika ni roho wa Mungu na Mungu hafungamani na uongo. Kubali kuambiwa ukweli hata kama mchungu though some truth are too much to bear we had to maintain the lies but for God sake Yatupasa tuambiane ukeli na kukubali kushauriiwa
Kushauriwa sio dhambi, kuwa upinzani sio dhambi,kukosolewa sio dhambi. Aint a guilty to criticize
 
Mada ni nzuri ila wafia chama na misukule itaishia tu kukupinga kwa sababu wao wanaona bahari iko shwari kabisa! Hawa viumbe hawataki kabisa watu wenye mawazo mbadala, na akitokea mtu wa aina hiyo mara zote huambiwa ni mtu wa chama fulani cha upinzani as if watanzania wote ni wafuasi wa vyama vya siasa.
 
Mada ni nzuri ila wafia chama na misukule itaishia tu kukupinga kwa sababu wao wanaona bahari iko shwari kabisa! Hawa viumbe hawataki kabisa watu wenye mawazo mbadala, na akitokea mtu wa aina hiyo mara zote huambiwa ni mtu wa chama fulani cha upinzani as if watanzania wote ni wafuasi wa vyama vya siasa.
Binafsi siipondi ccm wala kuitetea chadema,cuf au act.. naongea tu yale mawazo yangu navyoona kitu fulani hakiko sawa!
 
Gazeti kubwaaaa limejaa majungu ,husuda na wivu tu,ni bora ungehakiki uzi wako ukaleta kusudio,nani wa kusoma nyuzi ndefu hivi ya kifala?,peleka shuleni huko "literature"

Mkata viuno kushangilia kila asemacho jiwe hawezi kuelewa kilichoandikwa hapa.
 
Back
Top Bottom