Kasi ya utendaji wa Rais Magufuli yasababisha idadi ndogo ya wananchi kujitokeza kujiandikisha uchaguzi Serikali za Mitaa

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Maendeleo na yanayoletwa kutonana na utendaji na usimamizi mzuri wa mapato na mali ya umma katika awamu hii ya Tano chini ya rais John P Magufuli imekuwa sababu ya wananchi kuona kuwa haina haja ya kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Wananchi wengi wanaona kuwa wapige kura wasipige kura serikali ya awamu ya tano itatekeleza maendeleo wanayoyataka.Picha iliyopo kwa wananchi wengi ni kuwa haina haja ya kupoteza muda wakati maendeleo na usimamizi wa mapato ya serikali utakuwepo hata kama wapige kura au wasipige.

Kwa ufupi rais JPM amewapa imani kubwa sana wananchi juu ya namna alivyoleta maendeleo kwa muda mfupi na kudhibiti wapiga deals.Leo hii maeneo kama Yombo Vituka na Buza kuna vituo vya afya vikubwa vimekamilika kujengwa.Hivyo hawa wataogombea nafasi serikali za mitaa ni kama kukamilisha matakwa ya sheria tu.

Ila imani kubwa kwa wananchi ni kwa JPM ambae analeta maendeleo bila ya kubagua chama au mtu.
 
Mna spin habari.

Watu wanasusia uchaguzi kwa sababu wanaona hauna maana, wanaochaguliwa hata wakiwa wa upinzani, CCM inawarubuni na kuwanunua na kuwafanya wawe ndani ya CCM.

Hivyo wananchi wamepiga kura ya kutokuwa na imani na chaguzi hizi, kwa kutojiandikisha.

Wangekuwa wana support CCM wangejiandikisha kwa wingi kuipigia kura CCM.

Moja ya jinsi uchaguzi unavyotathiminiwa ni kuangalia watu walioshiriki uchaguzi.

Low voter participartion, means low credibility.

Watu wamesusia uchaguzi. Kwa sababu wanaona ni mazingaombwe ya kijinga tu.
 
Udikteta, kukandamiza wananchi hasa wa vyama vingine, kuviingilia vyama kwa lengo la kuvivuruga, kuwanunua au kuwalazimisha viongozi wa vyama vingine kuunga mkono juhudi, kuendesha serikali kwa misingi ya upendeleo wa kivyama, ukabila na undugu, nk, ndiyo sababu hasa ya watu kugomea zoezi la kupiga kura.
 
Maendeleo na yanayoletwa kutonana na utendaji na usimamizi mzuri wa mapato na mali ya umma katika awamu hii ya Tano chini ya rais John P Magufuli imekuwa sababu ya wananchi kuona kuwa haina haja ya kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.Wananchi wengi wanaona kuwa wapige kura wasipige kura serikali ya awamu ya tano itatekeleza maendeleo wanayoyataka.Picha iliyopo kwa wananchi wengi ni kuwa haina haja ya kupoteza muda wakati maendeleo na usimamizi wa mapato ya serikali utakuwepo hata kama wapige kura au wasipige.Kwa ufupi rais JPM amewapa imani kubwa sana wananchi juu ya namna alivyoleta maendeleo kwa muda mfupi na kudhibiti wapiga deals.Leo hii maeneo kama Yombo Vituka na Buza kuna vituo vya afya vikubwa vimekamilika kujengwa.Hivyo hawa wataogombea nafasi serikali za mitaa ni kama kukamilisha matakwa ya sheria tu.Ila imani kubwa kwa wananchi ni kwa JPM ambae analeta maendeleo bila ya kubagua chama au mtu.
Hivi akili za Lumumba huwa zikoje??? Yaani watu wakuunge mkono kisha wasusie kuja kujiandikisha!!! Aisee!! Hapo wangekuwa wanafurika vituon na sio kususia!!
Mkuu matokeo tayari yanajulikana kuwa ni lazima sisiem ishinde kwa kila hali ndo maana watu hawaon umuhimu wa kupoteza mda wao bure!!
Yaani umfunge mikono na miguu mpinzani wako afu uwanja ni wako, refa pia ni wako, maandalizi yote ya pambano umefanya wewe kisha uwambie watazamaji waje ukumbini kuangalia pambano ambalo tayari inajulikana ni lazima ushinde!!!!
 
Watanzania sio wajinga kama mnavojidanganya, wanawajibu kwa vitendo mkienda kulia wao wanapita kushoto ili mjue hawana muda tena na ninyi wababaishaji, siasa ni hoja za kiushindani, na hoja hujibiwa kwa hoja namshangaa mwana ccm anayefurahi wanachofanyiwa upinzani, ujue iko siku ccm itakua chama pinzani pia mtalipwa kulingana na matendo ya leo
 
Wanasaikolojia wanasema usikubali au usilazimishe uione jana ni nzuri kuliko leo, hakikisha leo inakua nzuri kuliko jana, ukipata mpenzi hakikisha hamkumbuki x wake kwa mazuri aliyomfanyia kwani hatokua na furaha na wewe, msisababishe wana ccm na watanzania wamkumbuke kikwete ambae alikua kiongozi mbovu kuliko ninyi
 
Wanasaikolojia wanasema usikubali au usilazimishe uione jana ni nzuri kuliko leo, hakikisha leo inakua nzuri kuliko jana, ukipata mpenzi hakikisha hamkumbuki x wake kwa mazuri aliyomfanyia kwani hatokua na furaha na wewe, msisababishe wana ccm na watanzania wamkumbuke kikwete ambae alikua kiongozi mbovu kuliko ninyi
Ombwe la uongozi la sasa, na woga wa viongozi kuogopa vivuli vyao, vinawafanya Watanzania wamkumbuke Kikwete na kumuona Kikwete, rais aliyekuwa na mapungufu mengi, kuwa ni kiongozi ambaye kwenye nyanya fulani, hususan uhuru wa watu kujieleza, siasa na vyombo vya habari, kuwa ni rais bora maradufu kuliko huyu wa sasa.

Magufuli angeweza kuwa rais bora zaidi kama angeachia siasa na vyombo vya habari vifanye kazi kwa uhuru.

Kushindwa katika hili kunamfanya awe kiongozi anayepwaya kwenye haya mambo.

Kitu kibaya kabisa ni kwamba, uongozi wa rais Magufuli ulivyoanza ulikuwa na mtaji mkubwa sana wa kisiasa wa kuaminiwa na wananchi. Na kwa kweli mpaka sasa wapo watu wengi wanaomuamini na kumtetea. Na kuna mambo amefanya vizuri -ingawa hata mazuri anayafanya vibaya- lakini tatizo linakuja, rais Magufuli ameutumia mtaji huo vibaya, ameufuja. Amelazimisha vita kubwa dhidi ya upinzani dhaifu ambao haukuwa na hoja ya msingi ya kumpinga. Sasa rais Magufuli ameifanya vita yake mwenyewe aliyoianzisha dhidi ya upinzani kuwa ni hoja ya wapinzani dhidi ya utawala wake. Kimsingi ameupa upinzani ambao ulikuwa unaelekea kuishiwa na hoja hoja mpya, kwamba unaonewa na utawala wa Magufuli.

Yani ni kama unakuwa na nzi mmoja anayekufa kwa kukosa hewa ndani ya nyumba yako, halafu kwa insecurity yako tu unatumia bomu la nyuklia kumuua nzi yule mpaka unahatarisha maisha ya familia yako mwenyewe na kusababisha mgogoro kwamba umetumia nguvu za nyuklia kuua nzi mmoja kinyume na mikataba ya kimataifa.

Ndicho anachofanya Magufuli sasa hivi.
 
Hivi akili za Lumumba huwa zikoje??? Yaani watu wakuunge mkono kisha wasusie kuja kujiandikisha!!! Aisee!! Hapo wangekuwa wanafurika vituon na sio kususia!!
Mkuu matokeo tayari yanajulikana kuwa ni lazima sisiem ishinde kwa kila hali ndo maana watu hawaon umuhimu wa kupoteza mda wao bure!!
Yaani umfunge mikono na miguu mpinzani wako afu uwanja ni wako, refa pia ni wako, maandalizi yote ya pambano umefanya wewe kisha uwambie watazamaji waje ukumbini kuangalia pambano ambalo tayari inajulikana ni lazima ushinde!!!!
Wafurike vituoni kufanya nini? Wakati wana uhakika wa barabara kujengwa,vituo vya afya kujengwa ,ubadhirifu umedhibitiwa aslimia 85.Huko miaka ya nyuma mlikuwa mnafanya hizo siasa za maji taka mbona haya maendeleo hayakufanyika! Tunahitaji muda wa kufanya kazi sio kila wakati mikutano ya siasa za maji taka.
 
Kiranga mkuu watu wengi tulimuunga mkono lakini shida ilianzia pale mtu anapoaminiwa na kuanza kujaa kiburi, unafahamu kua kumzuia mtu mwingine asifanye kitu fulani huku wewe ukikifanya ni dhambi kubwa? Na mtu mwenye mtazamo utafahamu kua siasa ya nchi hii itakua ngumu miaka ijayo itatengeneza kitu kibaya sana, huwezi kusema kila sehemu mlikosea kuchagua upinzani mara marndeleo hayana vyama hapo unakua unaichanganya akili yako mwenyewe na sio ya wale unaowaelezea hayo mambo.
 
Uzi huu umenikumbusha thread moja ya Mwana JamiiForums aliyetumia historia ya hadithi ya mfalme mmoja:


 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom