KASI YA UJENZI WA VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI MADINI YAONGEZEKA NCHINI TANZANIA

KASI YA UJENZI WA VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI MADINI YAONGEZEKA NCHINI TANZANIA

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,428

KASI YA UJENZI WA VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI MADINI YAONGEZEKA NCHINI TANZANIA

☑️ Waziri Mavunde aweka Jiwe la Msingi Kiwanda cha Kusindika na Kuyeyusha Nikeli na Shaba - Dodoma

☑️ Ni maelekezo ya Mhe. Rais Samia kuyaongezea thamani madini ndani ya nchi.

☑️ Mradi kuchakata takribani tani 200,00 za nikeli na Shaba kwa mwaka

📍Dodoma, Tanzania

Serikali imeendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuhakikisha rasilimali za madini zinawanufaisha Watanzania kupitia uongezaji thamani ndani ya nchi ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha uchumi wa kijani (green economy) hususan katika utengenezaji wa magari ya umeme, betri za magari, nishati safi na vifaa vya kielektroniki.

Hayo yamewekwa wazi Agosti 26, 2025 na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, wakati akiweka jiwe la msingi la Kiwanda cha kusafisha na kusindika Madini ya Nikeli na Shaba kinachojengwa na Kampuni ya Zhongzhou Mining Co. Ltd, eneo la Zamahero, Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma.

Amesema kuwa, Mradi huo utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba madini yanayochimbwa hapa nchini yaongezewe thamani ndani ya nchi na kuuza bidhaa ya mwishyabadala ya madini ghafi.

“Ujenzi wa kiwanda hiki ni uthibitisho kuwa dhamira ya kuongeza thamani madini nchini, tunataka kuona Tanzania ikibadilika na kuwa taifa linalozalisha bidhaa zenye thamani kubwa kwenye soko la dunia la bidhaa teknolojia.” amesema Mavunde

Waziri Mavunde ameeleza kuwa mradi huo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 15 utakapokamilika utazalisha takribani tani 200,000 za nikeli na shaba kwa mwaka, kuajiri zaidi ya Watanzania 200 hadi 230, na kuchangia kodi na mapato mengine ya Serikali.

“Uwekezaji huu ni kielelezo cha mafanikio ya Serikali katika kufanikisha dira ya uchumi wa viwanda na uongezaji thamani madini kama ilivyoelekezwa na Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020–2025," amesisitiza Mavunde.

Amebainisha kuwa, pia Sera ya Madini ya mwaka 2009 inaelekeza kuyaongezea thamani madini yetu ndani ya nchi na kuongeza kuwa “hivi sasa Tanzania tuna viwanda vinane vya kusafisha madini ya dhahabu (gold refinery) lakini viwanda vya kuonge
 

Attachments

  • Screenshot 2025-08-28 at 09-48-56 Instagram.png
    Screenshot 2025-08-28 at 09-48-56 Instagram.png
    715.8 KB · Views: 18
  • Screenshot 2025-08-28 at 09-49-02 Instagram.png
    Screenshot 2025-08-28 at 09-49-02 Instagram.png
    601.3 KB · Views: 21
  • Screenshot 2025-08-28 at 09-49-16 Instagram.png
    Screenshot 2025-08-28 at 09-49-16 Instagram.png
    661.4 KB · Views: 14
  • Screenshot 2025-08-28 at 09-49-48 Instagram.png
    Screenshot 2025-08-28 at 09-49-48 Instagram.png
    776.8 KB · Views: 16
Back
Top Bottom