Kasi iliyotumika kwa Kabwe, ingetumika pia kwenye masuala ya ufisadi kama Lugumi, Escrow, NSSF

Franco Zetta

JF-Expert Member
Nov 3, 2014
1,661
843
Hakika nime furahishwa na kasi iliyo onyeshwa na kiongozi wetu mpendwa Mhesimiwa JPM kuonyesha chuki ya dhati dhidi ya ubadhilifu na ufisadi katika tuhuma zilizopo juu ya Mkurugenzi wa Jiji ndugu Wilson Kabwe na kutolewa maamuzi ya kusimamishwa utumishi ndani ya wiki moja baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar-es Salaam Ndg. P.Makonda kuibua tuhuma hizo

Ningetarajia kasi iliyo tumika ingefaa pia kuonekana kwenye masuala ya ufisadi mkubwa zaidi kama Lugumi,Escrow,Nssf na kadhalika ambayo ndani yake mna ubadhilifu wa kiwango cha juu zaidi na Fedha ya wananchi kupotea,Kwa kasi kama hiyo natumaini kesi pia zita kwisha haraka kwani kuchelewa zaidi ni hali ya makusudi ya kubuy time na pia kutoa nafasi kwa ushahidi kuchezewa na hatiamaye kesi hizo kukosa nguvu,bahati mbaya ikiwa miongoni mwa wanao husishwa na kutajwa tajwa katika tuhuma hizo bado wangali katika utumishi wa Serikali,

Ni usawa na haki kwa wote ndio kitakacho imarisha nchi hii njema vinginevyo migawanyiko ya Udini,Ukanda na Ukabila vita tumaliza.
 
UMEANDIKA VEMA, NASEMA KUNA UONEVU KATIKA SERIKALI HII. JUSTICE FOR ALL, SITETEI UFISADI , ILA INAONEKANA WANATUMBULIWA WADOGO, WAKUBWA WANAACHWA, THIS IS NOT FAIR!
 
JMP anatumbua majipu kwa kutumia report kwa watu aliowachanguwa na anafukuza watu ambao sheria inamruhusu kuwaajiri na kuwafukuza. Kwa hiyo unaponzungumzia suala la Escrow, Lugumu na NSSF hawezi kufanya chochote mpaka aletewe evidence kuna uwezi. Mfano Rais alichukuwa uwamuzi alipopata report ya wafanyakazi hewa shinyanga.
 
ccm walishakiri ukiwagusa mafisadi nchi itatikisika, hawa wanaotumbuliwa ni wezi tu si MAFISADI.
 
Hivi mkuu hukumsikia mtoto wa MKULIMA aliposema mafisadi wana nguvu sana ukiwagusa nchi itatikisika! Sisi tunawatumbua kina Anne, kabwe, na wengine wa daraja hilo ambao hawana mtandao wa maana wa kuweza kututingisha! Kuna watu ukiwagusa unagusa watu wengi na wenye makucha ya kutishia hata kiti ulichokalia cha ufalme! Ukiona mtu katokea kama Sokoine ujue tumepata mkombozi
 
JMP anatumbua majipu kwa kutumia report kwa watu aliowachanguwa na anafukuza watu ambao sheria inamruhusu kuwaajiri na kuwafukuza. Kwa hiyo unaponzungumzia suala la Escrow, Lugumu na NSSF hawezi kufanya chochote mpaka aletewe evidence kuna uwezi. Mfano Rais alichukuwa uwamuzi alipopata report ya wafanyakazi hewa shinyanga.
Aliyeripoti suala la LuGUMI ni CAG, je ripoti hiyo siyo ushahidi??
 
Hivi kwann watu wamekomaa na NSSF wakati mifuko mingine kama PSPF iko ICU haijiwezi kabisa...
 
Back
Top Bottom