Game Theory
Platinum Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 835
Baada ya kulalmikiwa tangu enzi za Mkapa, Bandari ya DAR walijidai watarekebisha na watarahisisha utaratibu wa kutoa mizigo
Sasa hivi unaambiwa kuwa hali imezidi kuwa mbaya. Yaani Meli ikishashusha makontena Dar inaelekea Mombasa basi wewe unaweza kutoa Contena au LORI lako kule Mombasa kwa masaa 12 tuu wakati DAR kuna UHAKIKA wa mizigo kukwama kwa WIKI TATU MPAKA NNE
Na suala lingine ni la NUMBER PLATE registration
Hivi kama Tanzania ni nchi moja kwa nini Gari ziwe na numberplate za ZANZIBAR? kwa faida ya nani? na kwa nini mtu ulipie kuwa na number plate za Zanzibar wakati nayo ni Tanzania? jE UNAPATA MATATIZO KUTOA MAGARI YAKO DAR?
Solution: SHUSHA GARI ZAKO ZANZIBAR achana na DAR kule kuna wazimu mtupu
Hii mada ilikuwa wapi hii.!!!!!! thanks DrWHO
Nafikri ni wakati muafaka hapa JF wa kuwawashia moto hawa TPA na pale Airport.
Wakati fulani nimeingia DIA mwenzangu aliyekuwa mbele ktk mstari akaambiwa ......"wewe kwa nini huna passport mpya........utakuwa huondoki hapa wewe.......ikabidi aitwe et Afisa wa juu kuhusiana na ile hali!!!!!,....yaani Mtanzania anarudi nyumbani kasimamishwa approximately 10 minutes eti kwa nini hana passport mpya....." zamu yangu ilipofika..............." wewe hii paasport mpya umeitoa wapi?.................." yaani pale Airport kuna vichekesho pale, wakati huo joto kweli kweli, siji zile AC wameshatengeneza!!!!!...............
Katika hili mwanangu umenena....
Hapa mmh hapana... huko Zenji ndio kumeoza hata mpaka.....
KATIBU Mkuu Wizara ya Miundombinu, Omar Chambo, ameunda kamati maalum itakayoshughulikia tatizo la msongamano wa meli na mlundikano wa makontena katika Bandari ya Dar es Salaam.
Kamati hiyo itakuwa chini ya Uenyekiti wa Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Jason Rugaihuruza.
Akizungumza ofisini kwake jana, Rugaihuruza alisema kamati hiyo ina jukumu la kuhakikisha kila mdau anatekeleza mpango huo wa dharura kama ilivyokubaliwa na wadau wote.
Rugaihuruza alisema, hiyo inatokana na kasi ya uondoshaji wa makontena bandarini kuendelea kuzorota na kuwa 300 kwa siku.
"Idadi hii bado ni ndogo kulinganisha na idadi ya makontena yaliyopo kwenye yadi na yanayopakuliwa kutoka kwenye meli," alisema Rugaihuruza na kuongeza:
"Hali hii inaendelea kusababisha mlundikano wa makontena kwenye yadi za Tics kuwa mkubwa wakati uwezo wa yadi hiyo ni kuhifadhi makontena 7,500 kwa wakati mmoja, lakini Februari 29, mwaka huu kulikuwa na makontena 10,144 ambayo ni asilimia 34 zaidi ya uwezo wake."
Aliwataja wajumbe wa kamati hiyo kuwa ni Kitengo cha Kontena(Tics), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wakala wa uondoshaji mizigo(Taffa), Wakala wa Meli(Tasaa), Wakala wa Barabara (Tanroads), Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi kavu (Sumatra) na Wakala wa vituo vya kuhudumia makontena nje ya bandari(ICDs).Habari hii na Boniface Meena
How in the world the private security company conduct check up in the airport. Tanzanian is dead, and trust me i'm not responsible for the funeral.
Sambamba na mipango ya muda mfupi kuondoa msongamano pale Dar Port, serikali ingeharakisha ujenzi wa daraja la Kigamboni ili upanuzi wa Bandari ufanyike kwa upande wa Kigamboni ambapo kuna ardhi ya kutosha na by extension ni sehemu ya Bandari.
Huu utaraibu wa kuhamisha makontena na kuyapeleka Ubungo na kwingineko sio tu ni gharama bali pia ki-usalama ni hatari sana kwani kontena always zina attract waharifu.
Mipango ya kujenga Bandarini nyingine Bagamoyo na kwingineko iwe ni ni super longterm strategy something like 20-30 years plan.
Mimi hili suala la bandari na swiss cargo (Air port)...uzalendo ulishanishindaga siku nyingi.
Mkuu Masatu,
Hili suala kila nikilikumbuka kichwani, kichwa huwa kinauma. Kwanini tumeshindwa kutengeneza daraja la Kigamboni mpaka leo?
Kwenye serikali yangu ya kusadikika kichwani, Kigamboni ndio center kuu ya utalii Tanzania. Daraja la kisasa linajengwa, hoteli za kitalii, uwanja wa golf, barabara za maana, sehemu kwa ajili ya michezo mbalimbali kuanzia kuendesha magari mpaka baiskeli, matokeo yake kazi kama laki moja zinaweza kuwa created. Kila nikiwa likizo Spain na kuangalia jinsi wanavyotengeneza pesa kwenye visiwa vyao, wakati kikubwa walicho nacho ni bahari tu. Sisi tuna bahari, tuna culture, tuna wanyama kaskazini, tuna mlima Kilimanjaro, pia tuna vijana wenye nguvu wanaosubiri mama wa Kizungu kama kule Mombasa. Ukiweka pamoja, matokeo yake ni boom kwenye utalii.
Jambo lingine ni bandari ya Tanga pamoja na ile ya Mtwara. Tanga kwa nchi za Uganda, Rwanda, Burundi nk wakati Mtwara kwa ajili ya nchi za kusini.
Lakini kwa akili zetu, tunaongelea vyandarua vya dola 5M. Tukiwa wabunifu na
kutokuwa mafisadi, hatuhitahi Bush atupe vyandarua.