Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Ni kosa kutoa siri za vikao vya baraza la mawaziri,lowassa haaminiki, kama anaweza kutoa siri za vikao, tutawezaje kumwamini kwa kumpa nchi yetu aisimamie, akamatwe na kushtakiwa kwa kuyaleta mambo ya vikao katika public;

Government Negotiation team ni Baraza la Mawaziri? Mtanyooka mwaka huu
 
lile punyeto lao la goli la mkono mwisho wake ni bafuni...tushamjua mbaya wetu nae ni JAKAYA kikwete.....
 
Watu wengi waliowahi kukubali kufanya jambo kwa kumlinda mkulu wamejuta kwani ni mwrpesi kukuachia mzigo kikinuka. Full uswahili
 
Jamani mwaka h uu patamu! Tuombe uzima tu, kuna msemo usemao za mwizi arobaini na hakuna siri chini ya jua; wote tujiandae kuyajua yale tuliyokuwa tumefichwa muda mrefu ndani ya inji hii, hakuna wa kuogopwa tena kwa uovu huo, wizi, mauaji, dhuluma na utumwa wa watumishi wa umma, let the opposition spit it all out!
 
Kwanini ripoti nyingi za ripoti za bunge zinazohusu maswala ya ufisadi kuna kipengele kinasema kuna vitu vikiwekwa hadharani nchi itatikisika? Ripoti ya Richmond na Escrow zinasema hivyo. Nani huyo akiguswa nchi itatikisika?
Sasa hivi watu wakimuona JK watakuwa wanaona SI Unit ya Ufisadi nchini.

Haha Si Unit ya ufisadi ni Prof
 
Majibu ya El ni mepesi mno watanzania kama waziri alilazimishwa kwa simu toka ngazi za juu kwa nini El hakukataa kuupitisha na kuomba kujiuzulu wakati huo kwa manufaa ya taifa? nini kinatushawishi tusimwamini kama mpenda madaraka kwa kushindwa kuachia ngazi wakati huo? mbona Sokoine alitofautiana na baba wa taifa akaacha ofisi akarudi Monduli kuchunga ng'ombe mpaka Nyerere akamfuata ndio akarudi ofisini?majibu mepesi mno haya kwa nini yy asingewasiliana na hiyo ngazi ya juu kupata mantiki ya kumtaka kupitisha mkataba huo wenye utata na kubainisha utata anaouona kwenye huo mkataba kwa hiyo mamlaka ya juu? tufikiri kabla hatujaandika kajibu kashfa ya richmond.
 
haha..., kweli watanzania wanafki haswaa.., sasa Lowassa mnamnafkisha kwa lipi huko CDM?pesa zake au?maana siwezi amini mtu kajitetea miaka 8 yeye sio fisadi, halafu ghafla kahamia CDM utetezi wa muda mfupi tu umekubaliwa!

Samahani mkuu, mi sio mwanachama wa cdm, ila ni mpelelezi huru, na wala sijamtetea ,huo ni upelelezi binafsi tu.
 
Unaongea kwasababu haupo ndani ya system hasingeweza kufanya hivyo wangemfuhata huko huko kwani huoni pale bungeni magamba nyeupe yanahambiwa nyeusi na yanasema ndiyo ooo !!!!!!!
 
...Hakika ujio wa Lowassa UKAWA unatakiwa uchukuliwe kama blessing...as opposed to curse...kama ambavyo baadhi wanaonekana kufikiri....

.....Kuna mengi maovu yamejificha nyuma ya utawala uliopo madarakani toka 2005...na hamna mwenye kuyajua katika TZ hii kuliko Lowassa....

....Bado ninaamini kuwa mengi yatajitokeza wakati wa kampeni na pia baada ya utawala huu wa JK kuondoka madarakani...na ndipo wabongo watashangaa yaliyotendwa na utawala huu..

...tusisahau pia kuwa kuna mauzauza tele ya escrow ambayo hayajasemwa wala kupatiwa majibu...yakiwepo yale ya wizi wa mabilioni (cash money)kupitia stanbic...na pia ile kampuni hewa ya simba trust....

....Pia lazima tuje kujua sababu za kuwasamehe wezi wa EPA waliorudisha pesa kwa magunia kwenye mabenki....Haya na mengine meeengi lazima yatafunguliwa tu....sasa ni wakati wa watanzania kuyajua maovu tele ya utawala huu...hata ale mauzauza ya meremeta na mengine tele...yatajulikana tu..maana sasa UKAWA kuna mtu (Lowassa) aliye defect toka genge la ccm....

...Ofu yangu kubwa ni juu ya usalama wa mzee huyu mzee Lowassa...maana hawakawii hawa hata kumtumia vibaka wamshughulikie...kama ambavyo tumeona imetokea kwa wengine walioonyesha kutaka kuyasema yale yasiyofaa kusemwa dhidi ya status quo....
 
Samahani sana ndugu zangu kwa haya nitakayoyanene.
Humu ndani kumejaa ndorobo kwa sababu kwa muda kama miaka 2 nimekuwa nikielezea sakata la richmond na uhusiano wake na EL [kwamba hahusiki]lakini mlikuwa mnanibeza hivi sasa mtaamini kwa vile yuko chadema?????
Ndorrobbo Nyie"""""""" Ukweli ukidhihiri uongo hujitenga. Kampeni chafu zinazohusiana na EL zilikuwa zinaendeshwa na viongozi ndani ya chama chake [kwani walimuona ni tishio kwao kisiasa] Itakuwa dhambi sana kumwita EL kuwa ni msaliti kwani CCM pamoja na mwenyekiti wake wamemfukuza kiaina.
 
Swali la kwanini mnamuogopa Lowasa limeshajibiwa jana na hatuhitaji majibu zaidi.

Tunaomba kabla hujaondoka madarakani urudishe pesa zetu zote mlizotuibia na kutuongezea umasikini, ugumu wa maisha, ujinga, vifo vya watanzania wengi na uporaji wa mali za taifa hili kwa maslahi yenu wenyewe na familia zenu.

Mmetudanganya, mmetufanya wajinga, mmeturubuni, mmewaua ndugu zetu, mmeua elimu yetu alafu leo tena msimame majukwaani kusema tuichague tena CCM? Hapana, ONDOKENI TUMEWACHOKA.

Kwa hili lililotokea jana, Rais yeyote mwenye utu, haiba na utashi mwema kwa uongozi na wananchi wake, mwajibikaji na mpenda haki, Mcha Mungu lazima angechukua hatua ya kujiuzuru. ONDOKENI TUMEWACHOKA.

Pesa uchukue wewe na familia yako, mjinufaishe wenyewe, kila mali za taifa mmiliki wenyewe alafu na pesa za madawati ya shule pamoja na Maabara tuchangie sie..... shame on you corrupt government. ONDOKENI TUMEWACHOKA.

Mliuficha ukweli mkidhani hautakuja kutoka, mkawakandamiza wengi na wengine hata kuwaua, kuwatoa meno, kuwapiga na kuwatesa ili tu wasiongelee uovu wenu uliokithiri ndani ya Taifa hili.. ONDOKENI TUMEWACHOKA

Mmeiharibu CCM na kukifanta kuwa chama cha kidugu kupitisha maslahi yenu ili kulinda maslahi yenu. MUDA WENU UMEKWISHA. Mali mlizoiba na mambi mliyotufanyia yanatosha sana na hamna jipya la kutufanyia wanachi.... ONDOKENI TUMEWACHOKA


Mmevigeuza vyombo vya Usalama wa Taifa kuwa vyombi vya kutekeleza maamuzi yenu na kufanya mambo mnayoyataka mkihisi mtakaa milele katika dola, hapana... Udhalimu wenu, uonevu wenu na mambo yote mliyotufanyia watanzania mkihisi muda huu hautafika sasa halitasalia jiwe ambalo halitageuzwa mpaka wote muwe mmeondoka katika mfumo wa kinyonyaji, wizi na uonevu mlioujenga ndani ya nchi hii. ONDOKENI TUMEWACHOKA

Ni muda sasa umefika wa kuwa na Tanzania Mpya, sio Tanzania ile mliotudanganya ni ya KASI MPYA YA WIZI, NGUVU MPYA YA UKANDAMIZAJI WA DEMOKRASIA NA MAONI YA WENGI ila Tanzania yenye uwezo wa kuwanufaisha watanzania wote kulingana na rasilimali ilizojaaliwa.

JEI KEI na Familia yako, Chama Cha Mapinduzi..... ONDOKENI TUMEWACHOKA

Tumechoka!! Tunahitaji Joshua mpya wa kutuvusha kuelekea nchi ya Ahadi.

Tunahitaji kiongozi mpya wa kutufanya tufurahie utajiri wetu.

Ni mimi Fandre baba Cheupe
#SAFARI YA MATUMAINI INAENDELEA
#UKAWA TUMAINI LETU
 
Muda huu katika kukakiribishwa na kukabidhiwa kadi MH.LOWASSA ndani ya CHADEMA ,ameulizwa swali moja kuwa

Swali: Mh. Edward Lowassa unazungumiaje kuhusu kashfa ya Richmond?

Majibu Lowassa:
Nipende tu kusema mimi kama waziri mkuu kwa kawaida ya sheria huwa ninaletewa mkataba muda wa mwisho kuupitia na kuupitisha huwa sihusiki na kuandaa mikataba,mwenye mamlaka ni waziri husika.

Hivyo baada ya kuletewa mkataba husika wa Richmond niliupitia na kiukweli niliuwekea shaka kwa sababu nilishawahi kuwa waziri wizara ya maji nina uzoefu na kuandaa mikataba, nilishauri mkataba huo uvunjwe lakini waziri wa nishati akawasiliana na "NGAZI YA JUU" na kulazimishwa kuupitisha mkataba huo.

Baada ya kugundulika kuwa mkataba huo ulikuwa na mapungufu mengi, "NILICHUKUA MAAMUZI MAGUMU KWA AJILI YA SERIKALI, na kubeba mzigo wote ndio maana hadi leo wanasema mimi ni FISADI WA RICHMOND, nipende kumaliza kwa kusema kwamba MWENYE USHAHIDI WA RICHMOND AENDE MAHAKAMANI AKANISHTAKI.

mwisho.

Kupata majibu sahihi ya Hilo suala. Aliye Na ripoti ya tume ya mwakyembe atuwekee hapa,hili tusome yale ambayo hayakusomwa siku Ile dodoma. Hii itasaidia kila moja kujiridhisha Na ukweli wa mambo ulivyokuwa.
 
Kwa kauli hii ya ndugu EL: "Nipende tu kusema mimi kama waziri mkuu kwa kawaida ya sheria huwa ninaletewa mkataba muda wa mwisho kuupitia na kuupitisha huwa sihusiki na kuandaa mikataba, mwenye mamlaka ni waziri husika". Kwa namna nyingine anataka kutueleza anaye stahili kuwa wakwanza kutupiwa lawama awe aliye kuwa waziri wa nishati na madini (ndugu NK)? ambaye majuzi alimtaja kuwa ni mmoja wa matajiri watanzania anao wakubali.
 
vyovyote ilivyo uamuzi huzingatia siasa na hali halisi lowasa alijua richmond ni matapeli alikuwa na haki na mamlaka ya kukataa ushauri

Kama hukubaliani nao Jiuzulu...Ndio maana Lowasa alijiuzulu kuchukua responsibility
 
EL ni dhaifu , ameshindwa kutekeleza wajib wake akiwa kama mtendaji wa serikali [w/mkuu] kwa kumuogopa mkuu wake,
ilipaswa auvunje mkataba wa richmond au angejiuzulu ,
 
Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowassa ni mchapakazi,mvumilivu,mwenye ujasiri na hufanya maamuzi magumu pale inapobidi.
Ukweli huu unaweza kuchagizwa na kisa hiki; Wakati huo Mh.Lowassa akiwa Waziri wa Ardhi, Ndugu yangu mmoja aliwahi kuwa Afisa ardhi mkoa mmoja , alitumia madaraka yake vibaya kwa kujimilikisha viwanja na kugawa ardhi kinyume na taratibu katika mkoa huo, Mh.Lowassa alipata taarifa hizo na kumfukuza maramoja.Ndugu yangu huyu anamchukia Lowassa mpaka leo, lakini ukimuuliza ni kweli alitumia madaraka yake vibaya anakiri ni kweli lakini analaumu uamuzi uliokuwa umechukuliwa dhidi yake.

SWALI;
1.Je, ana usahihi wa kumlaumu na kumchukia Mh.Lowassa?
2.Je, ni wangapi wanaomchukia Lowassa sababu tu ya uzembe, uvivu na kulewa madaraka vilivyomo ndani yao?

My take;
Tuache chuki binafsi, tuwe wazalendo na tutangulize maslahi ya taifa mbele.
 
Back
Top Bottom