Kashfa ya ngono yamtatiza mgombea urais

Kashfa ya ngono yamtatiza mgombea urais

Shine

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2011
Posts
11,481
Reaction score
1,371
Mwanasiasa mashuhuri anayegombea tiketi ya urais ya chama cha Republicans nchini Marekani, amekanusha madai mapya kuwa alijaribu kumlazimisha mwanamke mmoja kufanya mapenzi naye.

Herman Cain anaongoza wanaogombea tiketi hiyo ilikukabiliana na Rais Barack Obama kwenye uchaguzi mwakani.
Akizungumza kwenye runinga ya ABC, Bw Cain amesema madai hayo ni ya uongo na atayajibu ipasavyo katika mkutano na waandishi wa habari leo jumanne.

Bi Sharon Bialek, ndiye mwanamke wa kwanza kujitokeza hadharani kudai kuwa Bw Cain, alijaribu kufanya mapenzi naye kwa lazima miaka kumi na minne iliyopita wakati akitafuta kazi.

Huyo ni mwanamke wa nne kutoa madai hayo na maswali kuhusu tabia ya mwanasiasa huyo huenda yakaathiri mikakati yake ya kugombea urais

Sourse BBC
 
zilipendwa! sasa kama bibie aliombwa kimya kimya ndo nini kuja kumtangazia mwenzake? sifa tu!
 
yaani asiseme siku zote hizo,aje kusema sasa wakati gari lishawaka! Nalog off
 
Siasa na kuchafuana ni njenje
 
yaani asiseme siku zote hizo,aje kusema sasa wakati gari lishawaka!

umeona eh? aoneshe ushahidi kuwa alishawahi kupeleka hayo madai kokote, hata kwa rafiki yake potelea mbali!
 
Back
Top Bottom