Kwa mjibu wa msemaji wa jeshi la Polisi kupitia Clouds Fm leo asubuhi mtu mmoja aliyemtaja kwa jina moja kama Komba ameshakamatwa kuhusiana na kuwepo mtandao mkubwa ndani na nje ya jeshi hilo unajiusisha na kuwalaghai vijana wanaotaka kujiunga na jeshi la polisi.
Inasemekana vijana zaidi ya 200 walitapeliwa kiasi cha shillingi 800,000/= kila mmoja kwa minajiri ya kuwawezesha kujiunga na Chuo cha Polisi Moshi baada ya kuhonga kitita hicho walitakiwa kulipa tena 25,000/= kama nauli ya kuwafikisha Moshi na kweli mabasi matatu yalikodishwa nakuwafikisha Moshi chuoni.
Baada yakufika chuoni taratibu zote za kuwasajili pamoja na kutakiwa kulipia gharama nyingine za kiasi cha shillingi 50,000/=,walinyolewa vipara na kuanza kupiga kwata kama makuruta wengine.
Kwa mshangao wa vijana hao siku ya pili waliitwa nakuambiwa kuwa wanatakiwa kuondoka hapo chuoni kwa vile sio makuruta halali na hawako kwenye kompyuta za chuo.
Kilichowashangaza zaidi ni pale walipokuwa wanatoka kweye lango la chuo kurudi makwao waliyaona mabasi yale yale yaliyowaleta yakiingia na vijana wengine ambao bila shaka nao wlikuwa wameingizwa mkenge!.