Kashfa ya kigogo Ikulu yaibuka upya

Kashfa ya kigogo Ikulu yaibuka upya

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
KITAIFA
Na Patricia Kimelemeta, Mwananchi

Posted Jumanne,Marchi19 2013 saa 21:35 PM

KWA UFUPI

Mpango huo unadaiwa kusukwa Juni mwaka jana kwa maofisa haokuitaka Wizara ya Fedha kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya safari hewa ya Rais.

Dar es Salaam. Sakata la Mkuu wa Itifaki wa Ikulu, Anthony Itatiro, ambaye anahusishwa na njama za kutaka kuchota kiasi cha Sh3 bilioni kwa ajili ya safari hewa ya Rais, limechukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje kutaka kujua hatima ya kigogo huyo jana.

Itatiro na maofisa wanne wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walituhumiwa mwaka jana kuidhinisha kuchota kiasi hicho cha fedha bila ya kuwapo kwa ziara ya Rais kwenda nchi yoyote ya kigeni.

Mpango huo unadaiwa kusukwa Juni mwaka jana kwa maofisa haokuitaka Wizara ya Fedha kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya safari hewa ya Rais.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Juma Mahadhi alitoa maelezo hayo baada ya kuulizwa swali na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge, Edward Lowassa.

Lowassa, ambaye pia ni Mbunge wa Monduli aliuliza swali hilo ghafla kwa Mahadhi wakati akitoka nje, baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati yake kilichofanyika kwenye ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.

Mahadhi, ambaye alilazimika kutoa ufafanuzi wa swali hilo baada ya kubanwa zaidi na waandishi wa habari, alisema Rais Kikwete ndiyo mwenye mamlaka ya kuchukua hatua dhidi ya Itatiro kutokana na ripoti ya uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkaguzi wa Ndani wa Wizara hiyo.

Alisema pia kuwa walishauriwa kuwa maofisa walioshirikiana na Itatiro nao wachukuliwe hatua za kinidhamu kufuatia njama hizo.

Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Katibu Mkuu Ombeni Sefue hakupokea simu. Pia hakujibu pindi alipotumiwa ujumbe mfupi kwa njia ya simu. Naye Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utumishi, George Yambesi alisema hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwani alikuwa likizo.

Mahadhi alisema wakati tukio hilo linatokea viongozi wakuu wa wizara hiyo walikuwa kwenye majukumu mengine ya Serikali, jambo ambalo lilisababisha nafasi zao kukaimiwa na watendaji hao.

"Wale maofisa walitumia mwanya wao wa kukaimu nafasi ile ndiyo wakasuka mpango huo," aliongeza Mahadhi.

Alisema kutokana na hali hiyo baadhi ya maofisa hao wamechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo ya kuwashusha vyeo na kuwabadilisha vitengo.

Mahadhi alisema kwamba huwa ni utaratibu wa kawaida kwa Rais anaposafiri maofisa wa Itifaki na wale wa Wizara ya Mambo ya Nje kupewa fedha na hazina kwa ajili ya kufanikisha ziara zake.

"Ila maofisa hawa walitumia mwanya huo kuihadaa Wizara ya Fedha kwa kuandaa hoja ya safari feki ili kupata fedha hizo," aliongeza Mahadhi.

Maofisa wengine ni pamoja na ofisa katika Idara ya Itifaki, Shamim Khalfa, Kaimu Mhasibu Mkuu, Kasim Laizer, Mhasibu, Deltha Mafie na karani wa fedha) aitwaye, Shabani Kesi.

Tunaiba Pesa za WALIPA KODI... TUNAKOPA PESA HATUNA
 
Tumezoea...CCM hakuna wa kumfunga paka kengele...dawa yao ni kuwang'oa 2015...
 
Tumezoea...CCM hakuna wa kumfunga paka kengele...dawa yao ni kuwang'oa 2015...
Lowassa alipouliza swali hilo ghafla hivyo, je hakujua matokeo yake> Au naye ameanza kuwa mwana harakati dhidi ya ufisadi? Aangaliye asiwe feki kama Anne Kilango katika eneo hilo.
 
kwa hiyo wanataka kutuambia Mh rahisi amekalia ripoti ya TAKUKURU?

au ndo kama kawaida ulikuwa upepo tu umeshapita
 
Lowassa alipouliza swali hilo ghafla hivyo, je hakujua matokeo yake> Au naye ameanza kuwa mwana harakati dhidi ya ufisadi? Aangaliye asiwe feki kama Anne Kilango katika eneo hilo.

Lowassa ni Jembe, alijua fika anachokifanya maana deal hiyo ilikuwa inamhusisha pia mkuu wa kaya! Jamaa ni Strategist mzuri, siku zote huwa anatembea na little dirt briefcase, Lyatonga huwa anasema ukimwaga ugali yeye anamwaga mboga...CCM wanalindana kwa ufisadi wao! hakuna msafi bali wanazidiana kwa kunuka...
 
Hakika kabisa, hakuna aliyemsafi ila tofauti yao ni "Kuzidiana Kunuka". Mwl.Nyerere (1995) katika sherehe za May Day huko Mbeya alisema".. CCM kinanuka reushwa"
 
Watu wameshaanza kusifia vitu bila hata kuelewa habari yenyewe.

Someni habari vizuri muelewe, halafu ndio muanze kuchangia.

Msisifie watu wanaowachezea akili.
 
Huyu FastJet kazidi mno kupaa mpaka anawapa mwanya maofisa waandamizi wa Ikulu wanapata tamaa ya kukwarua kijanja! Wameshaona hakuna faida kwa safari za mara kwa mara nao wakaona wachukue chao mapema ila ilibuma!

Ni mojawapo ya kashfa mbaya sana!
 
Duuh! sikujua kama ziara moja ya rais inaweza kujenga kilometa kadhaa za barabaara, au shule kadhaa zikawa na madawati na vifaa vya kutosha vya wanafunzi wetu kujifunzia na tukaepukana na mazero. Bil 3 si mchezo ati, yaani milioni elfu 3, pesa mingi.

Kwa kuwa tunaongozwa na maziro acha watoto waendelee kupata mazero. Halafu pesa zenyewe wanakopa, wanazitumia kwa starehe zao wakiondoka madarakani wanatuachia madeni na hakuna walichofanya, aaarrrgggggg!! inatia hasira sana.
 
Shilingi bilioni 3 kwa safari za nje ya nchi,sasa tumultiply hiyo na safari zake,halafu tukipata jibu,tulinganishe ni kiasi alichopewa kwenye bakuli wakati wa hizo safari tuone kama zinalipa na si hasara kwa taifa.

Na pia safari nyingi huwa ni kupiga saini za kimangungo tu huku akipandishwa farasi.
 
Watu wameshaanza kusifia vitu bila hata kuelewa habari yenyewe.

Someni habari vizuri muelewe, halafu ndio muanze kuchangia.

Msisifie watu wanaowachezea akili.
Hata hili halieleweki, wewe naona akili zako kuna mtu anazo kakushikia, mwambie akurudishie unadhalilika huku.
 
Kwa RAHISI kama jk ni bayana kuwa watu huwa wanadandia kwenye safari zake za mara kwa mara na kufaidi marupurupu yote ya safari. Mimi wala sioni ajabu.
 
Kwa RAHISI kama jk ni bayana kuwa watu huwa wanadandia kwenye safari zake za mara kwa mara na kufaidi marupurupu yote ya safari. Mimi wala sioni ajabu.
Hii ni dili ambayo imebumbulukiwa,hili ni dili hewa la safari za nje,nadhani madili hewa ya safari za ndani feki ya milioni mia kadhaa ni kitu ya kawaida hapa na pale kwenye michongo yao,kila mahali ni michongo tu.Nchi yetu hovyo kweli.
 
Hivi kale ka gauge ketu ka safari zimefika ngapi tuzidishe mara Bil 3 du kumbe Tanzania tunahela za mchezo
 
Hii ni dili ambayo imebumbulukiwa,hili ni dili hewa la safari za nje,nadhani madili hewa ya safari za ndani feki ya milioni mia kadhaa ni kitu ya kawaida hapa na pale kwenye michongo yao,kila mahali ni michongo tu.Nchi yetu hovyo kweli.
Kwa style hii maghorofa ya mil 800 yatajengwa sana Mbezi Beach
 
Hiki si kioja cha kwanza, na kuna uhakika kwa asilimia mia kwamba hawa watu watakuwa free wana enjoy maisha bila kugushwa na mtu yoyote!
Je tunakumbuka wale jamaa wa EPA waliishia wapi? Rudisheni pesa kazi iendelee, hakuna kugushwa mtu!
Bado tunasafari ndefu
 
Back
Top Bottom