Kashfa: Tigopesa wanadhulumu hela za wateja?

Mkuu wanaiba..hizo huduma huwa wanaunganisha juu kwa juu
 
Mkuu wanaiba..hizo huduma huwa wanaunganisha juu kwa juu
Kuunganishwa juu kwa juu kweli inawezekana. Japo watu wengine hujiunga bila kujua.
Mfano kuna namba huwa inapiga nadhan ni 255901761234 na nyingine za namna hiyo. Hizo namba zikikupigia ukajifanya unapokea na kubonyeza wanavyokwambia ndo inakula kwako. Na huduma zingine ukijiunga kuondoa ni ngumu kweli kweli.
 
Asante kwa maelezo yako. Hizo ni assumption tu,mwenye haki ya kubatilisha muamala ni yule aliyefanya. Hayo mengine ni ngumu kama kampuni kuthibitisha eti kwa kuhakiki kwa mpokeaji what if naye akasema uongo? Yaanze kufanya kazi za mahakama. Vodacom wanaweza vipi?
Kama upo huko Tigo,muache ubabaishaji mzingatie Turnaround time sio kuleta milolongo.
 
Mi nilifikiri niko peke yangu. Mwezi wa 11 mwaka jana nlilikosea tuma tigo pesa tsh 25,000/= nilifuatilia kupitia customer care kila mtu akawa akinipa majibu yake kila nilipo piga. Nimezungushwa wiki nikaamua kunyanyua mikoo juuu. Tarehe 31/12/2016 nikajikuta tena natuma tsh 60,000/= kimakosa kwenda namba ya tigo nikaambiwa ndani ya masaa 72. Nimepiga juzi nikaambiwa eti pesa nimesha rudishiwa tayari tangu tarehe 31/12/2016 ilihali saokweli. Nikachukua line ya tigo na kuitupilia chooni. Hawa jamaa tigo ni wezi sana!
 
Nimekuwa mtumiaji wa mtandao wa [HASHTAG]#Tigo[/HASHTAG] toka mwaka 2005, nimeiona ikipitia katika hatua mbalimbali kihuduma hata kubadili brand ya Nina lao. Nawafaham vizuri. Katika jambo ambalo nadhani wanfanya vibaya kabisa ni katika kitengo cha huduma kwa wateja na [HASHTAG]#TigoPessa[/HASHTAG]. Nitatoa mifano michache.

Kama kunamtandao ambao wahudumu wao wanachelewa kupokea simu pale wanapohitaji msaada ni hawa Tigo. Na wengi wa vijana wale wanaopokea simu labda hawajafunzwa vizuri juu ya Yale wanayopaswa kusaidia wateja ama wamekaa mud a mrefu na kuifanya kazi ile kwa mazoea au no wachache kiasi kwamba unaweza kuwekwa online kusubiria hadi dakika 40+ au mpaka simu unakata yenyewe bila kupewa msaada.

Mwezi wa Tisa mwaka Jana nilienda kuwachukulia vijana Wang wawili Vyeti vya kuzaliwa pale RITA nikaambiwa na mtoa huduma nilipie Vyeti vile katika akaunti ya RITA ya tigo ambayo IPO pale ofisini jumla ya tsh 13,000. Baada ya kufanya malipo mhudumu yule akaniambia alikosea Kunipa maelekezo, na kwamba nilipaswa kufanya muamala mmoja mmoja kwa kila cheti (6,500 kwa kila cheti). Hivyo nikaamua kulipa tena 6,500 kwa kila cheti hivyo nikawa nimelipa jumla ya tsh 26,000 badala ya 13,000.

Ikabidi muda ule ule niwapigie [HASHTAG]#Tigo[/HASHTAG] kuwaeleza jambo hilo na wakanuambia nivumilie baada ya masaa 72 watanurudishua hela ile iliyozidi. Siku tatu zukapita nikawapigia, wakasema nisubiri 24hrs tena, lakini hakuna kitu. Nikawapigia tena wakanipa masaa 72 tena lakini PSA haijarudi.

Nikaenda ofisi kwao wakanipa tena 72 hrs lakini hakuna pesa iliyorudi. Mpaka muda huu zaidi ya miezi minne hakuna dalili zozote za kupata pesa hiyo.

Ukienda kuwaeleza TCRA kitengo cha huduma kwa wateja malalamiko ya namna hii utaishia kupewa vipeperushi juu ya huduma zao!...mambo ya MSI GI kama haya watakuambia wanayashughulikia lakini huwezi kuona mambadiliko yeyote. Nimeamua kunyamaza. Labda huto tupesa wanatotupiga tunawasaidia kuongeza mbwembwe mjini.
 
Wanafanya makusudi tu. Mimi niliituma hela from tigo pesa to crdb akaunti ya mtu mwingine. Kwenye salio langu hela ilitoka kwenye akaunti haikuingia.

Nikatoa taarifa nikaambiwa subiri 24hrs hela itaonekana kwa niliemtumia. Baada ya 24hrs bila bila wakasema tena 24hrs itarudi kwangu.

Baada ya 24hrs bila bila nilietakiwa kumtumia hela ananiona namzingua tu, nikampigia simu rafiki mmoja boss pale tigo, akaniambia nitumie msg ya muamala nikamtumia. Ndani ya nusu saa hela imerudi kwangu. Hapo ndio nilipoamini kuna ucheleweshaji wa makusudi.
 
Kwani tigo nao mtandao hameni toa lain Ktk cm tupa weka kampuni nyingine ukiacha kifatilia pesa wanapiga wenyewe hao wezi wakubwa.
 
Kaz ipo mie tigo pesa nishaacha kutumia na wanadeni langu

Ila ofisini kwao nilistopisha shughuli kwa mda kadhaa mpk wakanipa pango la bure serikalini kwa masaa kadhaa
 
Huu uzi umenigusa ni leo tuu imenitokea nilituma hela kimakosa kwa wakala wa Voda ikaenda kwa mwingine ashukuliwe mungu kuna jamaa angu yupo voda makao makuu kanifanyia mchakAto baada ya dk 3 pesa ikarudi la sivyo ningeisoma namba... Kwa Voda kawaida ukikosea muamala kurudishiwa pesa ako ni siku 4 na sio masaa 24
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…