Mimi ni mmja wa waathirika wa tigo hawajarudisha hela yangu yangu tarehe 17-8-2016Wakuu Naomba hili tuliangalie kwa jicho la tatu .
Kuna malalamiko mengi sana kuhusiana na ucheleweshaji wa kurudisha fedha za wateja zinazotumwa kwa makosa kwa watu wasiohusika .
Ukiongea na customer care unaambiwa fedha zako ziko salama na utarudishiwa ndani ya masaa 24 lakini hawarudishi hata baada ya wiki , ukiwauliza unaambiwa utaratibu ni lazima wawasiliane na yule uliyemtumia hela , na kwamba kutokupatikana kwake ndio sababu ya kuchelewesha kurudisha hela , uongo mtupu ! Maana ni kwamba wateja wote hata kama wako hewani , hakuna ofisa yeyote wa Tigo anayejishughulisha kuwapigia simu kama wanavyodai , Tatizo liko wapi ? Ni kweli kwamba baadhi ya watu wa kitengo cha fedha si waaminifu kama nilivyodokezwa na mtu wa jikoni ? Na kwamba wanasubiri baadhi ya wateja wakate tamaa ili wazipige hela zao ?
Viongozi wa TIGOPESA tupeni majibu .
NB - UZI HUU NI WA UCHUNGUZI NA UTAENDELEA KUONGEZWA NYAMA KWA KADRI TAARIFA ZINAVYOTUFIKIA .
Wakuu Naomba hili tuliangalie kwa jicho la tatu .
Kuna malalamiko mengi sana kuhusiana na ucheleweshaji wa kurudisha fedha za wateja zinazotumwa kwa makosa kwa watu wasiohusika .
Ukiongea na customer care unaambiwa fedha zako ziko salama na utarudishiwa ndani ya masaa 24 lakini hawarudishi hata baada ya wiki , ukiwauliza unaambiwa utaratibu ni lazima wawasiliane na yule uliyemtumia hela , na kwamba kutokupatikana kwake ndio sababu ya kuchelewesha kurudisha hela , uongo mtupu ! Maana ni kwamba wateja wote hata kama wako hewani , hakuna ofisa yeyote wa Tigo anayejishughulisha kuwapigia simu kama wanavyodai , Tatizo liko wapi ? Ni kweli kwamba baadhi ya watu wa kitengo cha fedha si waaminifu kama nilivyodokezwa na mtu wa jikoni ? Na kwamba wanasubiri baadhi ya wateja wakate tamaa ili wazipige hela zao ?
Viongozi wa TIGOPESA tupeni majibu .
NB - UZI HUU NI WA UCHUNGUZI NA UTAENDELEA KUONGEZWA NYAMA KWA KADRI TAARIFA ZINAVYOTUFIKIA .
TCRA wanahusika zaidi na maandishi ya wafuasi wa chadema tu , hawahusiki na mambo kama haya .Wasiliana na TCRA
Pole sana mkuu .Mimi ni mmja wa waathirika wa tigo hawajarudisha hela yangu yangu tarehe 17-8-2016
Acha siasa,fata taratibu za kisheria.TCRA wanahusika zaidi na maandishi ya wafuasi wa chadema tu , hawahusiki na mambo kama haya .
TCRA waache siasa kwanza wao halafu mimi nitafuata .Acha siasa,fata taratibu za kisheria.
Mimi nilituma hela kutoka tigo kwendaa airtell elfu 50 kwa bahati mbaya nikawa nimekoasea namba nilituma kwa mtindo wa hela kuingia kwenye account moja moja baadae nikawasiliana na tigo wakanizungusha baadae wakanambia hela imeshatolewa na wakati mimi nikiipiga ile namba haipatikan nikaenda airtell wakasema hiyo line ilikuwa inadaiwa so sytem ime deduct hiyo hela had huyo mtu aje aweke hela ndio wao wataiota kuiruhisha tigo huyo mtu mwenyewe alikiwa anadaiwa 110,000 alikopa kwenye timiza sasa hapo nilishindwa kuelewa nani alitakiwa kusimamia haki yangu na nani kaniibia maan kama nime comfirm hela ni zangu na nimekosea kutuma why niwajibike kulipa hela mtu mwingine policy zao sizijui ndio maana sikujua pakuamzia nilirud tigo nikawaelezea ishu kamili wakasema hwana cha kufanya sababu hela ipo mikononi mwa airtll..nipo dar na nilienda tigo mliman city na airtell miliman city na morroco had niakaachana hiyo hela...jiulize aliepo mkoani..!
Kwanza kabisa pole kwa usumbufu kama mteja wa tigo/pesa.
Kama unatuma pesa kwa mteja wa tigopesa alie sajiliwa JINA LINATOKEA kukosea kupo lakini kukurejeshea pesa baada ya kukosea kuna njia zake n utaratibu wake.Mfano: A kamtumia B lakini A kumbe kamlipa deni B lakini yy A anasema kakosea ndio ugumu unapo kuja ni mpk B apigiwe simu kisha akubali kua kweli kapokea kima kosa hyo pesa.
Kutuma pesa kwenda MTANDAO MWINGINE hii kweli changamoto kiasi kwakua ukituma pesa AIRTEL/VODA/ZANTEL kimakosa.Cha kwanza kabisa piga kule waifungie ile line iliyopokea pesa kimakosa.Baadae ndio upige tigo kwa msaada zaidi.
Na kwa mteja ambaye HAJASAJILIWA wa tigopesa jitaidini kutuma kwa FUMBO LA SIRI ambayo hawezi toa mpk apate namba yako ya simu.na kwa hii uwa inarejea kwako mara baada ya kumaliza kuongea na namba 100.Au baada ya siku 7 hata kama hujaongea na namba 100.
Hili ndio linaongoza zaidi kwa wateja wasio wa aminifu kupata huduma za kimwili {ngono} na kumlipa mtu wake pesa.Baada ya kumaliza haja zao wanazuia pesa wakisema wamekosea kutuma.
Ndio zinazo chelewa sana.
Au mdeni n mdeni /VIKOBA/UPATU//WAPENZI.
Nashea nanyi kama WAKALA/MTEJA WA TIGOPESA.
Vodacom mtambo sana. Mm nikitaka kutuma pesa ni voda halafu mawakala wao wapo wengi sana.Wezi tu hao mbona Vodacom ukikosea ndani ya saa 24 unakuwa umerudishiwa fedha yako
Hili ni pigo kubwa sana kwa watumiaji wengi wa tigo. Huwa siachi hata sh 1. Nikiweka salio najiunga basi. Hio ndio pona ya hela yangu.Tigo ni jipu. Ukiweka salio na kama hujajiunga na kifurushi chochote lazima huwa wanakukata tu
Voda huwa hawaibi salio la vocha. Ukiwa unaona salio lako linapungua baada ya kiweka vocha jaribu kuhakiki mambo haya;Voda wanaiba tu salio la vocha...
Kwenye M-pesa wamefaulu uaminifu.
Tigo hovyo kabisa, ndio maana walipewa cheo cha ule mchezo mchafu...
Ulishawahi kutuma pesa kwa kutumia vodacoma wewe?Voda ndiyo wanaboa zaidi ukituma pesa transaction yao inaonyesha jina mwishoni kabisa baada ya kubonyeza 1
Hii inafanya watu wengi kutuma pesa kusikokusudiwa kimakosa,,
Tigo inakupa option ya kuhakiki jina la mtu unaye mtumia kabla ya kubonyeza 1.
Ila Naunga hoja hawa Customer service wanaboa kupita maelezo.
Ni pm namba uliyoitumia hiyo pesa mkuukiukweli hawa jamaa mi siwaelewi kabisa..tarehe 17/11 nilituma pesa kimakosa kwenda kwa mtu wa voda 50,000/=, baada ya kugundua nimekosea hapo hapo nikampigia sim yule niliyemtumia akawa hapatikani niawema afadhali hapatikani atakua hajaitoa,nikapiga sim tigo hapo hapo wakasema wewasiliana na watu wa voda hela wameizuia huyo mtu hawez kutoa nisubiri masaa 72 pesa itarudi,nikasubiri zaidi ya masaa 72 nikawapigia wakasema nisubir tena masaa 72 kama huyo mtu atakua hajatoa pesa watarudisha,nnachoshangaa kivip huyo mtu awe katoa pesa wakati nili toa taarifa mda mchache baada ya kukosea na vip iwezekane atoe pesa wakati hapatikani mda wote(maana nilikua nampigia almost kila siku,na nilimtumia text incase akipatikana ntapata delivery report),nikasubir tena masaa 72 nilipowapigia wakaanza kuongwa kwa ukali,nikawapigia voda nao sikuwaelewa...hadi leo pesa yangu haijarudi na tule mtu haptikani mpaka leo..hivi TCRA hawahusiki na hizi kesi?
Aliyeibiwa ni mimi au wewe?Voda huwa hawaibi salio la vocha. Ukiwa unaona salio lako linapungua baada ya kiweka vocha jaribu kuhakiki mambo haya;
1. Angalia kama kuna huduma za kulipia ulizojiunga nazo. Mfano: Caller tune, huduma za kupata habari kama nipashe, kabumbu, mwananchi, sokoni, etc..
2. Angalia kama simu yako ni Tecno au Aitel. Hizi simu huwa zinakuwa na uwezo wa data hata zikiwa zile simu ndogo za burtton. Hakikisha umezima data.
Aidha, kama unatumia smartphone hakikksha umezima data kabla ya kuweka vocha.
3. Hakikisha hudaiwi nipige tafu.
Nasisitiza tena, VODACOM HAIWEZI KUKUIBIA VOCHA