Kashfa: Tigopesa wanadhulumu hela za wateja?

Sasa kama hela wameizuia na hawarudishi ilikotoka maana yake nini ?
 
Sasa kama hela wameizuia na hawarudishi ilikotoka maana yake nini ?
***
Erythrocyte
Kiriport ni lazima kuwe promptly on the sports kabla yule iliyomfikia hajafanya lolote,lakini akiwa sharp akatoa faster,sasa hapo Kampuni itakuwa imezuia nini?/
•BAADA YA KU-MISSEND TURIPOTI WITHIN A MINUTES.
 
Tigo cku hizi wamejirekebisha kidogo,bt linapokuja suala la wizi ktk mitandao ya simu wote ni kitu kimoja ujanja ujanja mwanzo mwisho.Na hii inasababishwa na wahudum wasio waaminifu mi ni wakala hata sisi wanatupiga sana
 
Mimi nasikitika tu pale TIGO walipokuwa wanatuhamasisha na TIGO AFYA Bima na pindi tulipojisajili ndipo Longo Longo zikaanza na fedha zetu walitukata na hadi leo hii hakuna kinachoeleweka - Usanii mtupu
 

Mkuu hoja zako ulizoleta hata hazina mashiko kabisa:

Mtandao wa simu lazima uwe responsible kumtaarifu mpokeaji kwamba kiasi flani cha pesa kilochotwa kwenye account yako kimakosa kimerudisha kwa number ambayo ilikosea ikakutumia wewe.

Hapo mhusika atakua anajua zile pesa zilirudi kule Zilipotoka.

Hao ni wafanyabiashara na wana jukumu la kuboresha huduma na kuondoa usumbufu to the maximum katika huduma zao.
 
Tigo pesa wahuni sana kuna siku walishanifanya nikae kigoma mwezi mzima nilikosea namba ya wakala, nilipiga cm mpk matusi yalitumika ndy. Mpk Leo mm na tigo pesa mbali mbali staki hata kuwasikia
 
Pole mkuu ila utaratibu ni lazima ufuatwe. Wasingeweza kukuamini kwa kusema tu hivyo wakurudishie hela fasta
 
uwe unazima data mkuu. Ni data tu hiyo kwa vyovyote
 
Sio kweli
 
mkuu unatakiwa uvute subira hasa mimi nilirudishiwa baada ya mwezi na wiki tatu nlifuatilia mpaka nkachoka kila ukiwauliza wanakwambia vuta subira
Mi nilishawahi kufatilia mwaka mzima kiasi chenyewe Tsh 50,000 tu baada ya kupata changu nilifanya jambo moja tu la busara nilivunja ile chip kwa amani sijawahi kuwaza tena kutumia Tigo tena
 
TIGO hawakuwa hivi kabla, haya matatizo na mimi yashanikuta. Tena sio mara moja. Zamani kukosea namba walikuwa wanakwambia ndani ya masaa 24 ila ukikata tu simu ela inarudishwa, siku hizi, utaambiwa ndani ya masaa 24, utasubiri hadi week, yani bila kwenda ofisini kwao ndio inaweza kula kwako mazima.

Customer care ni mbovu balaa, siamini kama waliowekwa hicho kitengo wamefika hata level ya diploma, yani usiombe apokee mdada, majibu ya hovyohovyo utapewa, hawajari matatizo ya mteja.
 
yani hilo sio tatizo kabisa, wanachotakiwa wao ni kumpigia simu muhusika. issue ni kwamba hawampigii simu muhusika.ishanitokea zaidi ya mara moja, wanasema tutampigia muhusika kabla ya kurudisha ela ila hawapigi, muda mwingine unamtumia mtu ela, unakuta kasahau password, hawezi kuitoa, hivyo unakuwa unajua mtu anayetakiwa kupigiwa simu, chakushangaza ukienda ofisini kwao watampigia ukiwepo na ela inarudishwa in few minutes, sasa ni wangapi wanaweza kwenda huko ofisini kwao?

-pia inatia mashaka kukosea kutuma hela kimakosa kwani process husika inatoa muda kuverifyy jina na number husika
Tumia akili kidogo tu ndugu, ukituma ela kwenda mtandano mwingine hakuna verification ya jina hadi umemaliza tuma ela, pia muda mwingine inakubidi kurudishwa ela kutokana na sababu mbali mbali, moja kukosea namba, mbili uliyemtumia kusahau password, tatu uliyemtumia kuomba umtumie hiyo ela kwa namna tofauti as huko alipokuwepo hawezi toa hizo ela, n.k

sasa uaminifu unaoutaka wewe ni upi labda?
 
kiukweli hawa jamaa mi siwaelewi kabisa..tarehe 17/11 nilituma pesa kimakosa kwenda kwa mtu wa voda 50,000/=, baada ya kugundua nimekosea hapo hapo nikampigia sim yule niliyemtumia akawa hapatikani niawema afadhali hapatikani atakua hajaitoa,nikapiga sim tigo hapo hapo wakasema wewasiliana na watu wa voda hela wameizuia huyo mtu hawez kutoa nisubiri masaa 72 pesa itarudi,nikasubiri zaidi ya masaa 72 nikawapigia wakasema nisubir tena masaa 72 kama huyo mtu atakua hajatoa pesa watarudisha,nnachoshangaa kivip huyo mtu awe katoa pesa wakati nili toa taarifa mda mchache baada ya kukosea na vip iwezekane atoe pesa wakati hapatikani mda wote(maana nilikua nampigia almost kila siku,na nilimtumia text incase akipatikana ntapata delivery report),nikasubir tena masaa 72 nilipowapigia wakaanza kuongwa kwa ukali,nikawapigia voda nao sikuwaelewa...hadi leo pesa yangu haijarudi na tule mtu haptikani mpaka leo..hivi TCRA hawahusiki na hizi kesi?
 
Pia wanatatizo la matumizi ya airtime na bundles.Unashangaa hujapigia mtu au kujiunga na ma caller tune au huduma yoyote ila salio limepungua.TIGO acheni mambo ya ajabu ajabu.

Pia ukinunua bundle la data muda mwingine linakua less than thamani ya pesa.
 
Baada ya kusoma comment za wenzangu nami niongee ya moyoni.
Kuna siku mama mmoja ninaye mfahamu alikuja kwangu akiwa na shida na nauli ila hela yake ilikuwa tigopesa akaniomba akisema naomba nikutumie hii hela kwenye simu yako halafu unipe hela keshi,baada ya kumtazama kwa makini na kwa vile anashida hasa ukizingatia ni mtu mzima ikabidi nikubali tu! Baada ya siku tatu yule mama alipiga simu tigopesa hela ikatolewa kwangu ikapelekwa kwa yule mama swali langu kivipi hela itolewe kwenye simu yangu bila kufanya mawasiliano namimi? Maana kama tigo wangenipigia ningewaambia ukweli ulivyokuwa sasa badala yake yule mama hela yangu alichukua naya kwake akairudisha ndugu zangu niliumia sana maana yule mama nilimfuata nikamwambia mbona umefanya hivi alikuwa mkali nakunitolea matusi je kama ningeamua kuchukua hatua mkononi hamuoni hapo tigopesa kwa kukosa umakini mnaweza kusababisha watu kuuana? Ushahidi wa sms zote ninazo sijafuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…