:embarassed2:Habari ambazo nimezipata toka kwa kaka yangu anayehudhuria mafunzo ya kupandishwa cheo katika Chuo Cha Polisi Moshi (CCP). Ni kuwa siku ya jana chuoni hapo ilikuwa ni majonzi makubwa kwa askari wanaohudhuria course mbalimbali chuoni hapo. Majonzi hayo na vilio vilitawala pale mwili wa askari mwenzao aliyekuwa akihudhuria mafunzo ya ngazi ya corpolo kutokea mkoani Manyara. Askari huyo alifariki dunia kwa prssure na kisukari. Sasa basi kilichipelekea kuwepo na vilio vingi na lawama za hapa na pale ni kwamba: Askari huyo ambaye kwa sasa ni marehemu na mungu amlaze mahali pema, hakuhudhuria kipindi chuoni hapo kwa vile alikuwa na mapumziko aliyopewa na daktari wa Chuo ( ED ). Baada ya kutafutwa wasiohudhuri vipindi ikaonekana na yeye hakuhudhuria hivyo Afisa mmoja aliyetajwa kwa jina la JB IBRAHIM mwenye Cheo cha Mrakibu mwandamizi (ASP), na ambaye ni Adjutant hapo Chuoni. Afisa huyo bila hata kumsikiliza askari huyo na bila hata kuangalia cheti toka kwa daktari kama kweli amepewa mapumziko. Pamoja na kulalamika kuwa anayo ED bila huruma na bila ubinadamu na bila kutumia busara na bila kutumia akili kama afisa wa polisi mwenye cheo na madaraka makubwa kama hayo. Afisa huyo aliamuru askari huyo awekwe mahabusu kwa kosa hilo. Kitendo cha kuwekwa mahabusu askari huyo kilipelekea afya yake kubadilika ghafla na akiwa ndani ya mahabusu hiyo ni wenzake ambao walitoa taarifa kuwa kuna mgonjwa ndani amezidiwa na ndipo askari waliokuwa zamu wakatoa taarifa na kumkimbiza hospital ambako ndiko alikotwaliwa na Muumbaji na ikwa ndiyo mwisho wake.
Kutokana na hali hiyo wanafunzi waliopo Chuoni hapo wamehuzunika sana na baadhi yao wamesikika wakisema ni vyema mkuu wa jeshi afanye uchunguzi wa kina wa swala hilo. Inasemekana pia afisa huyo ameonyesha kutokuwa na uelewa wa maamuzi yake katika kila kona ya chuo hicho na kuonekana kama antafuta sifa au kujipendekeza kupandishwa cheo haraka. Pamoja na hayo wameomba kwamba mara mkuu wa polisi atakapofika chuoni hapo wiki hii kuhitimisha mafunzo ni vyema akaondoka na ofisa huyo na kwenda kumpa kazi nyingine huku akifanya uchunguzi wa jambo hilo. Kuendelea kuwepo hapo chuoni ni kuharibu nidhamu ya askari na jeshi zima la polisi. Kitendo cha kumuweka askari mwenzake mahabusu huku akiwa mgojwa na ugonjwa ambao tayari daktari amethibitisha ni kufundisha nini askari ambao watakwenda sasa kuwa karibu na wananchi na endapo watamkamata mwananchi ana kosa na ni mgonjwa je atasalimika. Naomba ndugu zangu hasa waandishi wa habari mlioko humu mnisaidie kupaza sauti ili tukomeshe tabia kama hizi. huyu ni kiongozi ambaye anatoa mafunzo kwa askari wa nchi nzima. je kuna haja ya ofisa huyo kuendelea kuwepo chuoni hapo? Tafadhalini tusaidiane.