Kashfa Nyingine nne nzito Zinakuja

Kashfa Nyingine nne nzito Zinakuja

Mkapa aliibinafsisha NBC kwa amri ya IMF na WB... Rejea JK Nyerere alivyopambana hadi kwenda kwa Clinton na kusababisha Prof Stieglitz kujizulu nafasi yake kama mshauri wa uchumi wa Clinton...
 
Hyo aliyechukua pesa atakuwa mshiria wa MENGI , hawezi kuguswa
 
Mkapa aliibinafsisha NBC kwa amri ya IMF na WB... Rejea JK Nyerere alivyopambana hadi kwenda kwa Clinton na kusababisha Prof Stieglitz kujizulu nafasi yake kama mshauri wa uchumi wa Clinton...
una kumbukumbku sana wewe
 
Kwani wewe huna uchungu na hii nchi??

Halafu title ya thread!!! kama vile unawapa adhabu vile??? Chunguza wewe uanike hayo madudu unless unatuambia wewe sio mzalendo!
 
Zitto na PAC wawe makini sana kwani lolote linaweza kuwatokea... Utoaji wa Vibali vya sukari unamgusa Pinda Moja kwa moja. Halahala LIWALO NA LIWE PROGRAM lisiwakumbe ...

ZITTO+PX.jpg

Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto amesema baada ya kukamilisha shughuli ya ufisadi wa Akaunti ya Tegeta Escrow ambayo Sh306 bilioni zilichotwa, kamati yake sasa inaelekeza nguvu katika kashfa nyingine nne.

Zitto alisema kamati yake itatumia mwezi huu na Januari kupitia ripoti nne ambazo zina masilahi kwa Taifa, ikiwamo ya utoaji wa vibali vya kuagiza na kuingiza sukari nchini.

Alisema ufisadi katika utoaji wa vibali hivyo ni mkubwa kuliko sakata la escrow... "Hili linagusa moja kwa moja maisha ya wananchi, wamiliki wa viwanda na uzalishaji. Tayari tumewaita Bodi ya Sukari tujadiliane kwa kina kuhusu suala hili," alisema.

Mbali na suala la sukari, alizitaja ripoti nyingine kuwa ni ya uchunguzi wa ubinafsishaji wa Benki ya NBC, ripoti maalumu ya Bandari na mikataba ya gesi.

"Baada ya kazi ya PAC, tunapumzika, kwani kama unavyojua kazi ilikuwa ngumu, wiki mbili nilikuwa silali. Kwa kuwa tuna ratiba ya wiki mbili. Kwa Desemba na Januari tutaanza kuzifanyia kazi," alisema Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema).

Wiki iliyopita, Bunge lilijadili ripoti ya PAC kuhusu ufisadi katika Akaunti ya Tegeta Escrow na kuhitimishwa kwa kuweka maazimio manane yakiwamo ya kuitaka Serikali iwawajibishe baadhi ya mawaziri na watendaji wengine wakuu huku likitaka pia uchunguzi uendelee kwa wote waliotuhumiwa kupokea fedha hizo kwa njia moja au nyingine.

Kauli ya Zitto inakuja wiki moja baada ya wamiliki wa viwanda vya sukari vya Kagera, Mtibwa na Kilombero kutishia kuvifunga kutokana na kuviendesha kwa hasara.

Wamiliki hao walisema watafunga viwanda hivyo kutokana na Serikali kushindwa kuzuia uagizwaji wa sukari nchini kinyume cha taratibu.

Mkurugenzi wa Viwanda vya Kagera na Mtibwa, Seif Seif alisema uagizaji wa sukari kutoka nje unafanyika kwa ushirikiano wa wafanyabiashara wakubwa na vigogo serikalini kinyume cha makubaliano na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya viwanda.

"Tulikubaliana kwamba Serikali iwe inaagiza tani 100,000 kutoka nje lakini sukari inayoingizwa sokoni ni zaidi ya tani hizo. Sukari tunayozalisha katika viwanda vyetu ipo na haina pa kwenda," alisema Seif na kuongeza:

"Leo ukipita katika maduka utakutana na sukari ya kila aina, wafanyabiashara wanaoagiza wanawatumia vigogo serikalini kuingiza sukari wapendavyo, tena bila kulipa kodi," alisema Seif.

Kutokana na hali hiyo, Seif alisema wamelazimika kupunguza wafanyakazi 2,000 na kubakiwa na 5,000 katika Kiwanda cha Kagera, Kilombero imepunguza 3,000 na wamebaki 6,000 huku Mtibwa ikiondoa wafanyakazi 3,000.

"Hali ni mbaya, si kama Watanzania wanavyofikiri. Tukifunga kabisa Watanzania wengi watakosa ajira kama ambavyo mnaona wengine wamekosa, hatuwezi kuendelea kufanya biashara ya hasara ambayo Serikali inaihalalisha," alisema.

Mwenyekiti wa Bodi ya Kiwanda cha Sukari Kilombero, Balozi Ami Mpungwe alisema: "Hali ni mbaya, tunaona kuliko kuendelea na hali hii ni bora tusimame kuzalisha sukari.

"Serikali kama kweli ina dhamira ya kuvifufua na kuviendeleza viwanda vyetu vya ndani ni lazima kuvilinda na kupiga marufuku uagizwaji holela wa sukari kutoka nje."

Chanzo: Mwananchi Decemba 2, 2014
 
Shame to them, ripoti ya ESCROW wameilet ikiwa na loopholes nyingi pasipo mfano. Ile ripoti ni either ilipikwa na hao wajumbe ili kubalance serikali na washirika wake mambo yasiende sawa. Baadhi ya maswali ambayo yapo vichwani mwa wadau wengi wanaofuatilia mambo ni haya.

1. Kwa nini Simba trust haijapewa airtime ya kutosha kama ilivyo PAP ilihali ana hisa 50% sawa na PAP.?

2. How on earth Stanbic walitoa >73 Bil cash pasipo vyombo vya usalama kufahamu, inafahamika kuwa bank ya biashara haiwezi kuwa na kiasi hicho cha pesa katika vault yake, ilikuwaje stanbic wakawa na hiyo cash ya kugawa.? Kama sio imetoka BOT.! Kama sio PAC wamefanya kusema hivyo ili point yao ya kuwa waliojichotea pesa cash hawafahamiki na kuacha watu wafukuze kivuli.?

3. Yes tufanye bil 73 zilikuwepo cash pale Stanbic na zikachotwa, waliochota hizo pesa iweje wasitambulike ilihali kuna uwepo wa CCTV camera.? Ama walikuwa invicible katika CCTV.?

4. Why mwigulu akurupuke na kudai pesa zilizochotwa zilipiwe kodi.? Sote tunatambua serikali inapokea kodi tokana na pesa halali, iweje hizi pesa ambazo wanaaminisha raia kuwa hazijapatikana kihalali, waziri mwenye dhamana azidaie kodi na watu wamshabikie kuwa yupo strict.?

Inshort haya mambo tunachezewa filamu ambayo wengi wamekubali kuicheza.
 
kikwete alishasema mumuache mkapa apumzike jamani. ha haaaaa
Dar es Salaam.[/SIZE][/FONT][/B] Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto amesema baada ya kukamilisha shughuli ya ufisadi wa Akaunti ya Tegeta Escrow ambayo Sh306 bilioni zilichotwa, kamati yake sasa inaelekeza nguvu katika kashfa nyingine nne.
[/FONT]
Zitto alisema kamati yake itatumia mwezi huu na Januari kupitia ripoti nne ambazo zina masilahi kwa Taifa, ikiwamo ya utoaji wa vibali vya kuagiza na kuingiza sukari nchini.

Alisema ufisadi katika utoaji wa vibali hivyo ni mkubwa kuliko sakata la escrow... “Hili linagusa moja kwa moja maisha ya wananchi, wamiliki wa viwanda na uzalishaji. Tayari tumewaita Bodi ya Sukari tujadiliane kwa kina kuhusu suala hili,” alisema.

Mbali na suala la sukari, alizitaja ripoti nyingine kuwa ni ya uchunguzi wa ubinafsishaji wa Benki ya NBC, ripoti maalumu ya Bandari na mikataba ya gesi.

“Baada ya kazi ya PAC, tunapumzika, kwani kama unavyojua kazi ilikuwa ngumu, wiki mbili nilikuwa silali. Kwa kuwa tuna ratiba ya wiki mbili. Kwa Desemba na Januari tutaanza kuzifanyia kazi,” alisema Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema).

Wiki iliyopita, Bunge lilijadili ripoti ya PAC kuhusu ufisadi katika Akaunti ya Tegeta Escrow na kuhitimishwa kwa kuweka maazimio manane yakiwamo ya kuitaka Serikali iwawajibishe baadhi ya mawaziri na watendaji wengine wakuu huku likitaka pia uchunguzi uendelee kwa wote waliotuhumiwa kupokea fedha hizo kwa njia moja au nyingine.

Kauli ya Zitto inakuja wiki moja baada ya wamiliki wa viwanda vya sukari vya Kagera, Mtibwa na Kilombero kutishia kuvifunga kutokana na kuviendesha kwa hasara.

Wamiliki hao walisema watafunga viwanda hivyo kutokana na Serikali kushindwa kuzuia uagizwaji wa sukari nchini kinyume cha taratibu.

Mkurugenzi wa Viwanda vya Kagera na Mtibwa, Seif Seif alisema uagizaji wa sukari kutoka nje unafanyika kwa ushirikiano wa wafanyabiashara wakubwa na vigogo serikalini kinyume cha makubaliano na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya viwanda.

“Tulikubaliana kwamba Serikali iwe inaagiza tani 100,000 kutoka nje lakini sukari inayoingizwa sokoni ni zaidi ya tani hizo. Sukari tunayozalisha katika viwanda vyetu ipo na haina pa kwenda,” alisema Seif na kuongeza:

“Leo ukipita katika maduka utakutana na sukari ya kila aina, wafanyabiashara wanaoagiza wanawatumia vigogo serikalini kuingiza sukari wapendavyo, tena bila kulipa kodi,” alisema Seif.

Kutokana na hali hiyo, Seif alisema wamelazimika kupunguza wafanyakazi 2,000 na kubakiwa na 5,000 katika Kiwanda cha Kagera, Kilombero imepunguza 3,000 na wamebaki 6,000 huku Mtibwa ikiondoa wafanyakazi 3,000.

“Hali ni mbaya, si kama Watanzania wanavyofikiri. Tukifunga kabisa Watanzania wengi watakosa ajira kama ambavyo mnaona wengine wamekosa, hatuwezi kuendelea kufanya biashara ya hasara ambayo Serikali inaihalalisha,” alisema.

Mwenyekiti wa Bodi ya Kiwanda cha Sukari Kilombero, Balozi Ami Mpungwe alisema: “Hali ni mbaya, tunaona kuliko kuendelea na hali hii ni bora tusimame kuzalisha sukari.

“Serikali kama kweli ina dhamira ya kuvifufua na kuviendeleza viwanda vyetu vya ndani ni lazima kuvilinda na kupiga marufuku uagizwaji holela wa sukari kutoka nje.”[/COLOR]

Chanzo: Mwananchi Decemba 2, 2014
[/QUOTE]
 
Kama JK ni msikivu avunje Baraza LOOOOTE
Ajivunje na yeye pia kwani hafai. Wakati wa Richmond Mwakyembe alimfichia siri ili asitimuliwe matokeo yake madudu zaidi yanazidi kutokea. Tatizo ni udhaifu wa rais kwani hata hili la Escrow linamgusa. Wa kwanza kuwajibika anatakiwa kuwa rais. Hawa wengine ni makafala tu kama ilivyokuwa kwa Richmond ambapo Lowassa na wenzake walibeba mzigo. Ndio maana wakati wa mjadala wa Escrow Lilowassa lilikuwa limebana kimya likichekea moyoni kwasababu lilionewa!
 
Zitto na PAC wawe makini sana kwani lolote linaweza kuwatokea... Utoaji wa Vibali vya sukari unamgusa Pinda Moja kwa moja. Halahala LIWALO NA LIWE PROGRAM lisiwakumbe ...
wa kuwalinda ni watza wenye mapenzi na uchungu na nchi yao
 
Edo ndiye aliyevujisha siri so hata hili litaibuka tu najua
Ajivunje na yeye pia kwani hafai. Wakati wa Richmond Mwakyembe alimfichia siri ili asitimuliwe matokeo yake madudu zaidi yanazidi kutokea. Tatizo ni udhaifu wa rais kwani hata hili la Escrow linamgusa. Wa kwanza kuwajibika anatakiwa kuwa rais. Hawa wengine ni makafala tu kama ilivyokuwa kwa Richmond ambapo Lowassa na wenzake walibeba mzigo. Ndio maana wakati wa mjadala wa Escrow Lilowassa lilikuwa limebana kimya likichekea moyoni kwasababu lilionewa!
 
Kuna jamaa mmoja mwenye asili ya wale wale akina nanihiii, yeye huingiza sukari akidai kuwa ni raw materials kwa ajili ya kutengenezea juice zake na vitu vya namna hio (kumbuka raw materials nyingi hazina kodi) kwa hio huenda mahali fulani kwenye moja ya magodauni na viwanda vyake na kuipaki kama sukari kamili na kuiuza ....... jamaa anapiga pesa ahdi basi lusungo tpaul njooni na mimi nimeingia kwenye PAC ntakuja na report yangu na maazimio yangu

Mmoja wa wezi hao ni bwana Masaburi, anayepiga dili kupitia mgongo wa mkewe, Janet Masbauri....hawa wapuuzi ndio wanaiguguna nchi hii. Jitu linaingiza sukari kama raw materials lakini ikishaingia nchini linaigeuza inakuwa Consumer goods. What a shame! Hapa ndipo mafisadi hawa walipoifikisha nchi hii. Na kwa hali hii tutarajie maumivu zaidi kwa wakulima wa miwa na wafanyakazi kwenye viwanda vya sukari...ambao watakosa ajira baada ya kupunguzwa. Hivi nchi hii ni nani aliyeturoga?
 
Last edited by a moderator:
nafikiri wakati umefika kuwakomesha hawa mafisadi na serikali ya ccm.
badala ya kulalamika tu ! tujiandikishe kwa wingi na kura zetu tusiwape kabisa ....tu vote kwa kusema hapana kwa ccm...maana imetosha sasa
 
Back
Top Bottom