Kashfa: Nesi amchapa Mjamzito Viboko, Kitoto Chafariki

Kashfa: Nesi amchapa Mjamzito Viboko, Kitoto Chafariki

idoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2013
Posts
3,051
Reaction score
1,423
Ni wakati wa uchungu wa kujifungua, Mtoto afia tumboni, hali ya mama utata.
Dodoma-25April2015.jpg

Dodoma.

Muuguzi mmoja wa zahanati ya Muungano, Chamwino, mkoani hapa, amekumbwa na kashfa nzito baada ya kudaiwa kumchapa viboko mama mjamzito, wakati akiwa katika hali ya uchungu wa kujifungua na kusababisha mtoto aliyetaka kujifungua kufariki akiwa tumboni.

Aidha, mama huyo ambaye kwa sasa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, hali yake inaelezwa kuwa mbaya. Mwanamke huyo, Mariamu Maroda, anadaiwa kulazwa kwenye chumba hicho kwa zaidi ya wiki moja, ambapo pamoja na kufanyiwa upasuaji, hakufanikiwa kupata mtoto wake akiwa hai.

Akisimulia mkasa huo, mama mdogo wa Maroda, Joyce Charles, alisema Aprili 3, mwaka huu Saa 12:00 jioni, walimpeleka zahanati ya Muungano akiwa na dalili za kujifungua na kupokelewa na muuguzi aliyemfahamu kwa jina la Lucy. "Nilishuhudia Lucy akimchapa Maroda viboko kwenye mapaja na mgongoni, akisema ana uwezo wa kujifungua lakini anadeka tu, nilishindwa kuingilia nikihofia asimdhuru zaidi mwanangu, ila nilihuzunika sana," alisema.

Alisema muuguzi huyo alitumia fimbo tatu kumchapa mgonjwa wake, ambazo alikuwa akizitumia kila moja inapovunjika. Alisema fimbo hizo zilipomalizika, alianza kumfinya kwenye mapaja kwa kutumia rula.

"Kesho yake saa 12:00 alfajiri, huku hali ya mgonjwa ikiwa mbaya, walitupatia gari likatupeleka hospitali ya Mvumi Misheni, ambako walisema hali aliyokuwa nayo mgonjwa wasingeiweza na kutuelekeza tumpeleke hospitali ya rufaa, lakini walimpa mgonjwa chupa mbili za damu," alisema.

Alisema Maroda alifikishiwa chumba cha upasuaji na kisha alilazwa wodi namba 17, lakini miguu na tumbo vilianza kuvimba na alipochunguzwa ikabainika ana usaha tumboni, hivyo aliamriwa arudishwe kwenye chumba cha upasuaji. "Yaani ukimuona, mwilini ana alama za fimbo na kufinywa. Sasa walipomfanyia upasuaji kwa awamu ya pili, alipelekwa ICU mpaka hivi tunavyozungumza ni zaidi ya wiki moja," alieleza Charles.

Viongozi wa Hospitali ya Rufaa, wenye mamlaka ya kuzungumzia suala hilo walionekana ‘kurushiana mpira' walipotakiwa kuelezea suala hilo. Hata hivyo, Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anatoria Mkindo, alikiri kuwepo kwa mgonjwa huyo.

Awali Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Zainab Chaula, alisema hakuwa na taarifa za kina kuhusu Maroda.
Mkindo alisema walikuwa wameagiza Ofisi ya Mganga wa Wilaya wa Chamwino, kuwapelekea taarifa kuhusu suala hilo. Alisema pia wametaka Ofisi ya Mganga Mkuu wa mkoa, ifahamishwe hatua zilizochukuliwa dhidi ya mtumishi aliyedaiwa kumchapa viboko mjamzito huyo.

"Mimi sio msemaji, anayetakiwa kuwapa taarifa kamili ni RMO (Chaula) kwanini awalete kwangu, nilichowaeleza ni ambacho nafahamu lakini siyo msemaji, nashauri muende ofisini kwa matroni wa hospitali mtapata taarifa kamili," alisema.Afisa Muuguzi wa ICU, Christina Mlumba, alisema, Maroda alipelekwa ICU baada ya kufanyiwa upasuaji na kwamba hali yake inaendelea vizuri.

Mdogo wa Maroda, Silika Mkwawi alivieleza vyombo vya habari kuwa ingawa hakuingia kwenye chumba cha kujifu
ngulia katika zahanati ya muungano, dada yake alipotolewa nje, muuguzi alimueleza kuwa alimchapa fimbo mbili tu, kwa sababu ya kudeka kwake.

Chanzo:
Nipashe
 
Duh! Huu ni ukatili uliopitiza. Huyu mwuguzi kasomea chuo gani kinachowafundisha wajawazito kuwachapa badala ya kuwasaidia? Sheria ichukue mkondo wake ili iwe fundisho kwa watu wengine.
 
Huyo muuguzi yaonyesha hana chembe ya huruma wala ubinadamu mkuu. Ni vema viongozi husika wamchukulie hatua kali Muuguzi huyo kukomesha vitendo hivi vya kikatili na unyanyasaji visivyoendana na maadili ya kazi ya uuguzi.
 
Duh! Huu ni ukatili uliopitiza. Huyu mwuguzi kasomea chuo gani kinachowafundisha wajawazito kuwachapa badala ya kuwasaidia? Sheria ichukue mkondo wake ili iwe fundisho kwa watu wengine.
kuna mama kanambia ya kuwa viboko vinaruhusiwa (viwili tu, ila sio upande wa tumbo) maana shughuli ya kuzaa ni pevu, mama anaweza akagoma kabisa, so anachapwa ili afanye fasta. ila kwa huyo nesi atakuwa alizidisha ndiyo maana dogo akafia tumboni.

  • Mdogo wa Maroda, Silika Mkwawi alivieleza vyombo vya habari kuwa ingawa hakuingia kwenye chumba cha kujifungulia katika zahanati ya muungano, dada yake alipotolewa nje, muuguzi alimueleza kuwa alimchapa fimbo mbili tu, kwa sababu ya kudeka kwake.

Huyo muuguzi yaonyesha hana chembe ya huruma wala ubinadamu mkuu. Ni vema viongozi husika wamchukulie hatua kali Muuguzi huyo kukomesha vitendo hivi vya kikatili na unyanyasaji visivyoendana na maadili ya kazi ya uuguzi.

Huyo atakua hajawahi kuzaa na hana bwana...unaanzaje kumpiga mjamzito..tena anayelia uchungu...
 
Mtu umeamua kusomea fani ya kusaidia wagonjwa hiyo inadhihirisha ni mapendo yako kutaka kusaidia watu.
Lakini inashangaza nesi wanakuwa na roho mbaya kama ameona mhalifu pindi unapoingia hospital hata salam hawapokei I hate them kwa wanavyokuwa na nyodo.
Huyo nesi ningempeleka akamzalishe chui kwa fimbo
 
Hawanaga adabu hawa manesi sijui ni stress za maisha maana unamkuta kavuta mdomo. Na amuombe Mungu huyo mama apone. Inaonekana anatetewa na wakubwa wake mbona wanaficha hali halisi
 
Manesi ndivyo walivyo, binafsi nilishuhudia kwa macho yangu mwenzangu akipigwa makonde kisa eti anamchelewesha nesi anataka kwenda kulala japo na mimi nilikuwa nimesuswa kisa eti nililetwa Muhimbili nikitokea TMJ nilipokuwa nimelazwa hivyo wakawa wananiangalia pasipo hata kunihudumia huku wakinizodoa eti mnajifanya mna hela mnaenda TMJ mmeona huko yamewashinda ndiyo mnakuja huku. Waliniacha tokea usiku wa saa saba nikiwa na hali mbaya mpk kesho yake saa nane nilipoomba nipatiwe cm yangu na ku wapigia ndugu zangu nikiwaambia mimi nakufa taf nitafutieni Dr aje aniokoe. Walikuja ma dr watatu ndiyo walionizalisha na nilijifungua mtoto mfu. Ukweli huwa naumia sana, mpaka leo hii nikikumbuka huwa nalia sana! yaani manesi wamekuwa na roho mbaya sana utadhani hawana dini!!
 
Eeh Mungu saidia Mama zetu. Tazama pia roho za hawa wauguzi na roho zao Mbaya
 
juz tu serikali imelipa fidia kwa uzembe na kusabisha kilema\utasa.

naye huyu wapo tayari kumlipa ?.
 
Manesi ndivyo walivyo, binafsi nilishuhudia kwa macho yangu mwenzangu akipigwa makonde kisa eti anamchelewesha nesi anataka kwenda kulala japo na mimi nilikuwa nimesuswa kisa eti nililetwa Muhimbili nikitokea TMJ nilipokuwa nimelazwa hivyo wakawa wananiangalia pasipo hata kunihudumia huku wakinizodoa eti mnajifanya mna hela mnaenda TMJ mmeona huko yamewashinda ndiyo mnakuja huku. Waliniacha tokea usiku wa saa saba nikiwa na hali mbaya mpk kesho yake saa nane nilipoomba nipatiwe cm yangu na ku wapigia ndugu zangu nikiwaambia mimi nakufa taf nitafutieni Dr aje aniokoe. Walikuja ma dr watatu ndiyo walionizalisha na nilijifungua mtoto mfu. Ukweli huwa naumia sana, mpaka leo hii nikikumbuka huwa nalia sana! yaani manesi wamekuwa na roho mbaya sana utadhani hawana dini!!

Pole sana mamito, Mungu akupe faraja.
 
Kosa la nurse ni kumchelewesha mpaka akapata complications....viboko mgongoni na kwenye mapaja vitauaje mtoto au kusababisha usaha tumboni.

Kuna wauguzi visirani lakini kuna wagonjwa visirani pia
 
Manesi ndivyo walivyo, binafsi nilishuhudia kwa macho yangu mwenzangu akipigwa makonde kisa eti anamchelewesha nesi anataka kwenda kulala japo na mimi nilikuwa nimesuswa kisa eti nililetwa Muhimbili nikitokea TMJ nilipokuwa nimelazwa hivyo wakawa wananiangalia pasipo hata kunihudumia huku wakinizodoa eti mnajifanya mna hela mnaenda TMJ mmeona huko yamewashinda ndiyo mnakuja huku. Waliniacha tokea usiku wa saa saba nikiwa na hali mbaya mpk kesho yake saa nane nilipoomba nipatiwe cm yangu na ku wapigia ndugu zangu nikiwaambia mimi nakufa taf nitafutieni Dr aje aniokoe. Walikuja ma dr watatu ndiyo walionizalisha na nilijifungua mtoto mfu. Ukweli huwa naumia sana, mpaka leo hii nikikumbuka huwa nalia sana! yaani manesi wamekuwa na roho mbaya sana utadhani hawana dini!!

Pole sana ndugu yangu,nafurahi sana nikienda hospital nimkute mwanaume kuliko mwanamke hasa nikienda kujifungua,yaani unahudumiwa vizuri sana.
 
Tuache masihara huyu anatakiwa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu, kwanza amlipe fidia mgonjwa na kifungo juu, utakujaje kazini umepigwa au umetukanwa na mumeo hasira uziamishie kwa mgonjwa? anatakiwa apewe adhabu kali ili fundisho kwa wengine.
 
  • Thanks
Reactions: kui
upuuzi mtupu hakuna chochote hapa,uchunguzi ukifanyika utagundua na utaweka ukweli hapa.Watanzania wanapenda sana kupika majungu,
 
uchunguz wa nn ! wkt vyeti vikiwa vinaenda na hii hbr.. ni uthibitisho tosha mahakamani.
 
Kama alivyosema mdau mmoja, kuchapa viboko, maneno ya kejeli, au vibao nk, vinamfanya mama anayetaka kujifungua kuongeza juhudi za kusukuma mtoto. Lakini tatizo ni kuwa, siku hizi kuna vyuo uchwara vingi na havitoi elimu inayojitosheleza kwa wahudumu wa afya, hasa wa vijijinî.

Haiwezekani, kwa nesi aliyesomea afya ya uzazi akaona mwanamke ameshikwa uchungu kwa zaidi ya masaa 8 tangu afike kituoni, na ameshindwa kusukuma mtoto halafu yeye bado akabaki anashangaa tu. Over-contraction ya uterus kwa muda mrefu lazima itasababisha kifo cha mtoto au sometimes mama au wote kwa pamoja. Contraction ya uterus ni kwa ajili ya kumsukuma mtoto atoke, sasa utakuta wanawake wengine njia zao ni ndogo, au mtoto kakaa vibaya na hii inasababisha washindwe kumtoa mtoto hata km utampiga namna gani. Ukiona muda unaenda na ameshindwa peleka theater.

Kuendelea kumchelewesha, kunapelekea mtoto kukosa oxygen ya kutosha na atafariki. Hii ni kwa sababu contractions zinapunguza volume ya damu kutembea kwenye mishipa, hii huzuia wanawake kupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua. Sasa pia damu itapungua kwenda kwa mtoto na atakosa oxygen.

Wanawake wajawazito wanaweza kupata complications za hatari ikiwa huduma ni mbovu, uzembe kwa kucheleweshwa kupata huduma inayotakiwa, mfano: upasuaji nk
 
Pole sana ndugu yangu,nafurahi sana nikienda hospital nimkute mwanaume kuliko mwanamke hasa nikienda kujifungua,yaani unahudumiwa vizuri sana.

Unafikiri kwa nini inakuwa hivyo? Unasemaje kuhusu barmaid wa kike kuwacngamukia wateja wanaume kuliko wateja wanawake wenzao??
 
Back
Top Bottom